June 30, 2016

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameagiza wakuu wa wilaya na mikoa kufanya ziara katika maeneo yao hasa vijijini ili kujua matatizo ya wananchi wao kwa ukaribu na kuyapatia ufumbuzi

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameagiza wakuu wa wilaya na mikoa kufanya ziara katika maeneo yao hasa vijijini ili kujua matatizo ya wananchi wao kwa ukaribu na kuyapatia ufumbuzi. 

Mhe.Majaliwa ameyasema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wakuu wa wilaya na mikoa walipokuwa Ikulu wakila kiapo cha maadili ya viongozi kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa mikoa yao. 

Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa wakuu wa mikoa na wilaya waache kukaa maofisini mwao badala yake watembelee wananchi na hasa wale wa hali ya chini ili kujua matatizo yao ya Ardhi na kupatia ufumbuzi migogoro ya wafugaji na wakulima. 

Pia Mhe.Majaliwa amewasisitiza wakuu hao kutambua kwamba majukumu waliyonayo ni makubwa na wananchi wana mategemeo makubwa juu yao na hivyo ni budi wakatekeleza wajibu wao na kuhakikisha watanzania wanapata huduma zote za muhimu kwa kutumia elimu, uwezo, uadilifu, uaminifu na uwajibikaji walionao ili kufanikisha maendeleo kwa wananchi. 

Aliongeza kuwa wakuu hao wana jukumu kubwa la kusimamia pesa za serikali pesa za miradi zinakokwenda katika halmashauri za wilaya zao na kukazia kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kwa yeyote ambaye hatofanya kazi zake kikamilifu. 

Waziri mkuu amewaagiza wakuu wa Mikoa kushirikiana kwa karibu na wakuu wa Wilaya ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya maeneo yao kwani wananchi wana kiu ya maendeleo katika maeneo yao.
Na Daudi Manongi-Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 29 Juni, 2016 amewaapisha wakuu wa Mikoa watatu aliowateua Jumapili iliyopita tarehe 26 Juni, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 29 Juni, 2016 amewaapisha wakuu wa Mikoa watatu aliowateua Jumapili iliyopita tarehe 26 Juni, 2016. 

Wakuu wa Mikoa walioapishwa leo Ikulu Jijini Dar es salaam ni Dkt. Binilith Satano Mahenge ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Charles Ogesa Mlingwa ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mara na Bi. Zainab Rajab Telack ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. 

Hafla ya kuapishwa kwa wakuu hao wa Mikoa imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na wakuu wa wilaya wateule ambao waliteuliwa na Rais Magufuli Jumapili iliyopita tarehe 26 Juni, 2016. 

Aidha, miongoni mwa wakuu wa wilaya 139 walioteuliwa, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika wilaya tatu ambapo ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mteule Mhe. Fatma Hassan Toufiq na badala yake amemteua Bi. Agness Elias Hokororo kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, ametengua uteuzi wa Mkuu wa wilaya ya Serengeti Mteule Bw. Emile Yotham Ntakamulenga na badala yake amemteua Bw. Nurdin Hassan Babu kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo na ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mteule Bw. Fikiri Avias Said na badala yake amemteua Bw. Miraji Mtaturu kuwa Mkuu wa wilaya hiyo. 

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wakuu wa wilaya wateule kwenda kuchapa kazi na kutatua kero za wananchi katika wilaya zao huku wakizingatia kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu. 

Rais Magufuli pia amewataka kusimamia ukusanyaji mapato ya serikali na matumizi ya fedha na rasilimali nyingine za umma, kuhakikisha wananchi wapo salama na pia kuhakikisha wananchi wanafanya kazi za uzalishaji mali. 

“Katika kazi hizi wapo watakaowakejeli, katika kazi hizi wapo watakaowadhihaki, nyinyi kavumilieni na mmuweke Mungu mbele na mkawaweke watanzania mbele, mkafanye kazi kadiri Mungu atakavyokuwa amewaongoza. 

“Nataka kuwahakikishia tunawaunga mkono kwa nguvu zote, mkafanye kazi bila uwoga wowote, katembeeni kifua mbele, kwa sababu tumewaamini wala msiwe na wasiwasi, ukifanya kitu kizuri kwa dhamira yako iliyo njema kitazaa matunda mazuri, ukifanya kitu kwa unafiki hakitafanikiwa” Amesema Rais Magufuli 

Katika hafla hiyo, wakuu wa mikoa walioapishwa na wakuu wa wilaya wateule wamekula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma, zoezi ambalo limeongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda. 

Katika hatua nyingine, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya Mazungumzo na mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani Bi. Melinda Gates ambapo Rais Magufuli amemuhakikishia mwenyekiti mwenza huyo kuwa serikali ya awamu ya tano itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano wake na taasisi hiyo ambayo imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Afya, Uongozi na Kilimo. 

Kwa upande wake Bi. Melinda Gate amempongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya katika kukabiliana na rushwa na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali, na pia kwa nia yake thabiti ya kuinua sekta ya kilimo inayotegemewa na idadi kubwa ya watanzania na ameahidi kuwa taasisi ya Bill and Melinda Gates itaendelea kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano katika kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Fantasia - Sleeping With The One I Love

Msanii Fantasia ametoa video ya wimbo wake mpya unaitwa “Sleeping with the One I Love.”, wimbo huu upo kwenye album yake mpya ya “The Definition Of”, inatarajiwa kutoka July 29.

Mwandishi wa ''The Concubine'' afariki

Mwandishi wa ''The Concubine'' afariki

Image captionElechi Amadi
Mwandishi maarufu wa Nigeria Elechi Amadi amefariki akiwa na umri wa miaka 82.
Amadi ambaye aliandika vitabu maarufu kama vile The Concubine,Isiburu,Sunset in Biafra,Peppersoup na The Road to Ibadan alifariki siku ya Jumatano mwendo wa saa tisa,wiki moja moja baada ya kuripotiwa kuugua.
Duru zimearifu kuwa marehemu alitarajiwa kuhudhuria hafla ya kusoma vitabu katika bandari ya Hacourt lakini hakuweza kutokana na kuugua kwake.
Akiwa mzaliwa wa eneo la Aluu katika jimbo la Riverstate mwaka 1934,Elecchi Amadi alisoma katika taasis ya Umuahia,Oyo na chuo kikuu cha Ibadan ambapo alipata shahada yake katika somo la fizikia na hesabati.
Pia aliwahi kufanya kazi kama mpimaji wa mashamba.

watu kumi nane wa uwawa somalia

Image copyrightEPA
Image captionMlipuko wa bomu Somalia
Habari kutoka Somalia zinasema kuwa watu 18 wameuawa baada ya bomu kulipuka na kuharibu kabisa basi walimokuwa wakisafiria katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara lililipua gari lililokuwa limewabeba abiria. Wote waliouawa walikuwa raia.
Mashambulizi hayo yalitokea katika mji wa karibu wa Lafole.
Inadhaniwa kuwa washambuliaji hao walikuwa wakilenga gari la wanajeshi lililokuwa karibu.
Mara kwa mara wapiganaji wa Al Shaabab hulenga wanajeshi wa Serikali

ZAIDI ya Sh milioni 800 zinatarajiwa kukusanywa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) kwa ajili ya kusaidia waathirika wa Virus

ZAIDI ya Sh milioni 800 zinatarajiwa kukusanywa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) kwa ajili ya kusaidia waathirika wa Virusi Vya Ukimwi mwaka huu. 

Fedha hizo zitakusanywa kupitia kampeni maalumu ya kupanda mlima Kilimanjaro ijulikanayo kama Kill Challenge inayofanyika kwa mwaka wa 15, ambayo kwa mwaka huu wapanda mlima 100 wamejitokeza kushiriki.

“Mgodi wa Geita kwa kushirikiana na Tacaids unatarajia kupandisha watu 50 katika kilele cha mlima Kilimanjaro na kundi lingine la waendesha baiskeli 50 linataraji kuzunguka mlima huo kwa ajili ya kukusanya fedha hizo,” alisema Meneja Mawasiliano wa Mgodi wa GGM, Tenga Tenga. 

Tenga alisema kampeni hiyo ya Kili Challenge inaongozwa na Balozi wake, Mrisho Mpoto ambaye ni msanii wa kughani mashairi na upandaji huo wa mlima utafanyika Julai 16 na kumalizika Julai 22, mwaka huu. 

Alisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, ambaye ataanzisha safari hiyo huku mapokezi ya kuwapokea wapandaji hao akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadiki. 

Naye Mwakilishi wa Tacaids, Jackson Peter, alisema Kili Challenge ya mwaka huu imepata uzito wa kipekee kutokana na Umoja wa Mataifa (UN) kupitia Shirika lake la Maendeleo la (UNDP) kutoa wawakilishi wanane kushiriki upandaji mlima huo kwa ajili ya kusaidia watu walioathirika na Virusi Vya Ukimwi nchini. 

Balozi wa Kili Challenge, Mpoto aliwataka wananchi na jamii kwa ujumla kutambua mapambano dhidi ya Ukimwi ni ya jamii yote hivyo inapaswa kuunga mkono jitihada za serikali kwa ajili ya kupambana ili kufikia sifuri tatu. 

“Naamini kwamba jitihada zinazofanywa na mfuko huu zinahitaji kuungwa mkono na Watanzania wote na wadau wenye machungu na nchi hii, hivyo tuungane kila mmoja wetu ama kwa kuxchangia au kumuelisha mwenzake ili mapambano haya yalete mabadiliko,” alisema Mpoto. 

Tangu kuanza kwa kampeni hiyo miaka 15 iliyopita zaidi ya Dola za Marekani 8,000 zimekusanywa na kugawiwa katika asasi mbalimbali nchini zinazoshiriki katika mapambano na kusaidia waathirika wa Ukimwi.

Fedha hizo zimepelekwa katika kusaidia mapambano dhidi ya Ukimwi, ikiwamo kujenga vituo vya ushauri na upimaji wa Ukimwi, ambavyo baadhi yao ni vile vilivyopo mkoani Tanga, Manyoni mkoani Singida na Geita.

MWANDISHI WA HABARI HAWA MKUU WA WILAYA HANDENI MKOANI TANGA

Rais Dkt John Pombe Magufuli leo amewaapisha wakuu wapya wa wilaya 139 na wakuu wa mikoa wanne kwenye hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.

dc4
dc4
Rais Magufuli akiwa na baadhi ya wakuu wa wilaya kwenye picha ya pamoja Ikulu Jumatano hii
Miongoni mwa wakuu wa wilaya wapya ni mtangazaji nguli wa redio na TV, Godwin Gondwe. Gongwe sasa ni mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga.\

CmGt_XDWIAEKn6X
Akiongea kwenye hafla hiyo, Rais Magufuli anayefahamika kwa utani mwingine alimsifia Gondwe kuwa ni mtangazaji mzuri na kumtaka atumie uwezo huo kutangaza maendeleo.
“Gondwe najua unatangaza,sasa utakwenda kutangaza maendeleo unakokwenda,ufanye kama unatangaza tangaza tu,” alisema.
CmGt_XDWIAEKn6X
Double G kama anavyojulikana pia alikuwa mtangazaji maarufu wa habari kwenye kituo cha runinga cha ITV. Amewahi pia kufanya kazi kwenye vituo vya redio vya Radio Free Africa na Radio One. Lakini pia alikuwa mhadhiri wa chuo kikuu cha Tumaini jijini Dar es Salaam.

June 29, 2016

ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 29 Juni, 2016 amewaapisha wakuu wa Mikoa watatu