July 28, 2016

Al-Shabab washambulia mtambo wa mawasiliano Kenya

Shabab


Image copyright AFP
Image caption Wanamgambo wa al-Shabab wamekuwa wakishambulia Kenya mara kwa mara
Washukiwa wa kundi la Al-Shabaab mapema leo Alhamisi wameshambulia na kulipua mtambo wa mawasiliano ulioko katika mji wa Fino, Lafey katika kaunti ndogo ya Mandera nchini Kenya.
Afisa mkuu wa Polisi huko Lafey, Bosita Omukolongolo, amesema kuwa kisa hicho kilitokea saa nane usiku.
Afisa huyo wa Polisi anasema kuwa walikabiliana vikali na wanamgambo hao, lakini hakuna maafa yaliyoripotiwa upande wa polisi waliokuwa wakiulinda mlingoti huo wenye vifaa vya kupeperusha mawasiliano.
Kundi la Al- Shaabab, ambalo lina makao yake nchini Somalia, limehusika na mashambulizi ya mara kwa mara pamoja na mauaji nchini Kenya na mataifa kadhaa ya Afrika Mashariki na upembe wa Afrika.

July 25, 2016

Mechi ya kirafiki kati ya miamba wa Uingereza, Manchester City na Manchester United, imefutiliwa mbali kutokana na mvua kubwa


ManchesterImage copyrightGETTY
Image captionManchester United watarejea Manchester baadaye leo
Mechi ya kirafiki kati ya miamba wa Uingereza, Manchester City na Manchester United, imefutiliwa mbali kutokana na mvua kubwa.
Mechi hiyo ilikuwa imepangiwa kuchezewa uwanja waBirds Nest, Uchina na ingekuwa ya kwanza kwa mameneja wapya Pep Guardiola na Jose Mourinho.
Jumapili, Mourinho alikuwa amedokeza kwamba hali katika uwanja huo ilikuwa mbaya.
CityImage copyrightGETTY
Image captionCity watakutana na Borussia Alhamisi
Hata kabla ya mechi kuahirishwa rasmi, Guardiola alikuwa amesema matumaini yake ni kwamba wachezaji wake wasiumie.
City na United wamesema “waandalizi wa mchuano huu pamoja na klabu zote mbili” wameamua kuahirisha mechi hiyo iliyopangiwa kuchezewa uwanja uliotumiwa kuandaa michezo ya Olimpiki 2008.
GuardiolaImage copyrightAFP
Image captionGuardiola na Mourinho walishindana vikali La Liva
Mvua kubwa ilinyesha Jumapili na watabiri wa hali ya hewa walisema mvua zaidi ingenyesha Jumatatu.
United watarejea Manchester baadaye leo nao City wasafiri hadi Shenzhen Jumanne kwa mechi dhidi ya Borussia Dortmund ya Ujerumani siku ya Alhamisi

Riek Machar ''apinduliwa'' Sudan Kusini

Image captionTaban Deng Gai
Maafisa wa serikali ya Sudan Kusini wameiambia BBC kwamba wanamtambua waziri wa madini Taban Deng Gai kuwa makamu wa kwanza wa rais akichukua mahala pake Riek Machar ambaye alitoroka mji mkuu wa Juba baada ya mapigano makali mapema mwezi huu.
Hatahivyo msemaji wa Machar amesema kuwa wameukataa uteuzi wa Bwana Deng.
Bwana Deng alikuwa mpatanishi mkuu wa Machar na hatua yake ya kuchukua wadhfa huo unaonyesha kuwa wametofautiana, hivyobasi kuweka mgawanyiko katika upinzani ambao unazidi kutatiza juhudi za kupata amani nchini Sudan Kusini ,kulingana na wachanganuzi.
Image copyrightREUTERS
Image captionWananchi wa Sudan Kusini wakiangalia runinga
Takriban watu 300 walifariki katika mapigano mapema mwezi huu katika mji mkuu wa Juba,kati ya vikosi vilivyo vitiifu kwa Machar na mpinzani wake rais Salva Kiiir.
SORCE BBC

KUZALIWA KWA JOHN RAMBO [Sylvester Gardenzio StallonE

Sylvester Gardenzio Stallone[(amezaliwa tar. 6 Julai 1946), amepewa jina la utani kama Sly Stallone,[] ni mshindi wa Tuzo za Academy - akiwa kama mwigizaji, mwongozaji na mwindishi-skrini bora wa filamu wa Kimarekani.
Image result for john rambo
Huyu ni mmoja kati wa watu walioingiza fedha nyingi sana katika sanduku la ofisi kwa miaka ya 1970 na 1990. Sylvester Stallone, ni kioo na shujaa wa filamu za mapigano. Amecheza nyusika mbili ambazo ni mashuhuri sana: Rocky Balboa, mwana-masumbwi mmoja aliyeshinda mashindano kwa kupigana kwa upenzi na imani, na John Rambo, askari shupavu aliyefanya kazi za hatari vitani.


Image result for john rambo

Image result for john rambo costume

maisha ya na storia Arnold Schwarzenegge

Arnold Schwarzenegger (amezaliwa tar. 30 Julai 1947 nchini Austria) ni mwigizaji wa filamu na mwanasiasa aliyekuwa gavana wa jimbo la California nchini Marekani tangu 2003 hadi Januari 2011. Arnold anaishi mjini Los AngelesCalifornia.

Image result for historia ya anord


Image result for historia ya anord

Schwarzenegger alielekea nchi Marekani mnamo mwaka wa 1968 na kisha baadaye akawa mwigizaji wa filamu. Ameigiza filamu nyingi tu, ikiwemo ile ya The Terminator na nyingine nyingi tu. Mnamo mwaka wa 2003, pale Bw. Gray Davis alipoondoka madarakani, Schwarzenegger akashinda kiti cha kuwa Gavana wa California akarudishwa mwaka 2007.


Image result for historia ya anord

Schwarzenegger ameoana na Bi. Maria Shriver.
Kabla ya kuwa mwigizaji, kwanza alikuwa Mnyanyua Vyuma. Kwa kigezo hicho akafanikiwa kushinda mashindano ya Mr. Universum kwa takriban mara saba.

Image result for historia ya anord

Watoto wengi wameuwawa Afghanistan 2016, yasema UN

Idadi ya watoto waliouwawa katika machafuko ya Afghanistan katika nusu ya kwanza mwaka huu, imeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Afghanistan UNAMA.

Afghanistan UNAMA Symbolbild
Idadi ya watoto wanaouwawa Afghanistan imeongezeka
Idadi hiyo imekuja katika ripoti ya katikati ya mwaka, iliyotolewa siku chache tu baada ya shambulio baya zaidi la bomu kuwahi kuikumba Kabul tangu uvamizi wa mwaka 2001, ulioongozwa na Marekani na kuufurusha utawala wa Taliban.
Jumamosi watu wasiopungua 80 waliuwawa na wengine 231 kujeruhiwa katika shambulio la kujitoa muhanga, wakati wa maandamano ya amani ya waafghanistan wa jamii ya wachache wa Hazara, ambao ni waumini wa Kishia. Wengi wa waliouwawa ni raia wa kawaida.
Kundi la dola ya kiislamu IS lilikiri kuhusika, jambo lililozua wasiwasi kwamba kundi hilo ambalo limekuwa katika maeneo ya mpakani ya mashariki mwa nchi hiyo karibu na Pakistan kwa mwaka mmoja uliopita, linapanga kustawisha uwepo wake Afghanistan, baada ya kupoteza maeneo mengi nchini Syria na Iraq.
Idadi hiyo ya watu waliouwawa Jumamosi haikuwepo kwenye ripoti hiyo ya UNAMA, kwani ripoti hiyo inaangazia wahanga wa kuanzia Januari 1 hadi Juni 30 mwaka huu. Inasema kwamba theluthi moja ya wahanga katika hiyo miezi 6 walikuwa watoto, huku 388 wakiuwawa na 1,121 wakijeruhiwa, hiyo ikiwa ni asilimia 18 zaidi ya nusu ya kwanza ya mwaka 2015.
Ripoti hiyo imetaja makabiliano baina ya wanamgambo na vikosi vya Afghanistan vinayoungwa mkono na NATO kama chanzo kikuu cha mauaji hayo. Idadi ya waliojeruhiwa imefikia kiwango cha juu zaidi tangu Umoja wa Mataifa uanze kutoa ripoti zake mwaka wa 2009, na umoja huo umeitaja idadi hiyo kama jambo la kushtusha na la aibu.
Taliban Afghanistan Friedensprogramm
Taliban wamechangia mno mauaji
Takwimu hizi ni ishara ya ongezeko la ukosefu wa usalama unaoendelea kuikumba Afghanistan wakati ambapo kundi la Taliban linaeneza mashambulizi yake nchi nzima.
"Kila muhanga aliyenukuliwa kwenye ripoti hii, kutoka wale waliouwawa wakiwa wanasali, waliouwawa kazini, wakisoma, wakiteka maji, wakitibiwa hospitalini, kila mmoja anawakilisha kushindwa kwa dhamira, na huu unapaswa kuwa wito kwa pande zote zinazohusika katika mzozo huu kuchukua hatua zinazohitajika ili kupunguza mateso kwa raia," alisema mkuu wa UNAMA Tadamichi Yamamoto.
Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imesema kwamba makundi yanayoipinga serikali kama Taliban yamechangia kwa asilimia 60 ya wahanga. Vikosi vya Afghanistan vimehusika kwa asilimia 22 ya majeruhi wote, na vikosi vya kimataifa vilivyosalia nchini humo vimesababisha asilimia 2 ya wahanga, huku asilimia 17 ikiwa haiwezi kutambulika iwapo ilisababishwa na pande moja ua mwengine.
Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanasema pande zote mbili zilisema zinajitolea kwa kiasi kikubwa, ingawa ni hatua chache mno zilizochukuliwa kuwalinda raia.
Majeruhi kutokana na mabomu yaliyotegwa barabarani yalipungua pakubwa kwa asilimia 21, jambo ambalo Umoja wa Mataifa unasema limetokana na kubadilika kwa mfumo wa machafuko hayo na pia mfumo mzuri wa serikali wa kufahamu palipo na mabomu.

Mhamiaji wa Syria ahusika na shambulio la Ansbach

Mhamiaji wa Syria aliyekataliwa hifadhi ya ukimbizi Ujerumani mwaka mmoja uliopita amekufa baada ya kuripuwa bomu karibu na tamasha la muziki mkoani Bavaria ambalo limemuuwa yeye mwenyewe na kujeruhi watu wengine kadhaa.

Polisi imesema watu 12 wamejeruhiwa watatu kati yao wakiwa mahatuti katika shambulio hilo lililofanyika katika mji wa Ansbach mji wenye wakaazi 40,000 ulioko kusini magharibi mwa Nuremberg ambapo ndiko pia kuliko kambi ya jeshi la Marekani.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 27 inasemekana alikuwa akipatiwa matibabu ya akili baada ya kujaribu kujiuwa mara mbili na kwa mujibu wa polisi alikuwa amekusudia kushambulia tamasha hilo la muziki lakini alikataliwa kuingia ndani kwa sababu alikuwa hana tiketi na ndipo aliporipuwa bomu hilo nje ya mkahawa ulioko karibu.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa kwa haraka Jumatatu (25.07.2016) waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la Bavaria Joachim Herrmann hakufuta uwezekano wa shambulio hilo kuwa na uhusiano na kundi la Dola la Kiislamu.
Hermmannn) amesema "Mripuko huo ulikuwa ni kifurushi kilichokuwa kimejazwa vipande vya vyuma ambao ungeliweza kujeruhi au kuuwa watu wengi zaidi mambo yanayosababisha kuwepo kwa tuhuma kwamba hili ni shambulio la Waislamu wa itikadi kali. Hata hivyo tunatakiwa kufanya uchunguzi wa kina kuyakinisha hilo. Tunataraji kutowa maelezo kwa wananchi hivi karibun."
Jaza ya kufadhiliwa
Waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la Bavaria Joachim Herrmann.
Waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la Bavaria Joachim Herrmann.
Herrmann amesema inatisha kwamba mtu aliyekuja katika nchi yao kutafuta hifadhi ametenda tendo hilo la kinyama na kujeruhi idadi kubwa ya watu baadhi yao wakiwa katika hali mahatuti.
Tukio hilo litazidi kupalilia mashaka ya wananchi yanayozidi kuongezeka kuhusu sera ya Kansela Angela Merkel ya kuwacha milango wazi kwa wakimbizi ambapo kwayo zaidi ya wahamiaji milioni moja wameingia nchini Ujerumani katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita wengi wao wakikimbia vita nchini Syria, Iraq na Afghanistan.
Akizungumzia tukio hilo naibu mkuu wa polisi wa mji Ansbach Roman Fertinger ametilia mkazo kujumuishwa kwa vipande vya chuma katika bomu hilo.
Naibu mkuu huyo wa polisi amesema "Baadhi ya vipande vya chuma vilipatikana vimezagaa.Vipande vya aina hii kwa kawaida hutumika kwa shughuli za mbao.Itabidi tuchunguze kubaini iwapo vilitumika katika bomu hilo."
Mashambulizi yaliyoikumba Ujerumani hivi karibuni yanazusha masuala mazito kuhusu sera ya kuwapa hifadhi wakimbizi na usalama nchini kote hilo likiwa ni shambulio la nne la matumizi ya nguvu nchini katika kipindi kisichozidi wiki moja likiwemo lile la mauaji ya watu tisa yaliyofanwa na Mjerumani mwenye asili ya Iran Ijumaa iliopita.
Sera ya Merkel lawamani tena
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.
Stephan Meyer mbunge kutoka chama cha kihafidhina cha Kansela Angela Merkel amesisitiza kwamba ni kosa kabisa kumlaumu Angela Merkel na sera yake ya wakimbizi kwa mfululizo wa matumizi ya nguvu katika kipindi cha moja lililopita.
Mayer ameliambia shirika la utangazaji la Uingereza BBC kwamba wahamiaji na wakimbizi milioni moja nukta moja walioingia nchini mwaka jana ni changamoto kwa wasimamizi ya sheria juu ya kwamba wimbi hilo la wakimbizi limepunguwa katika miezi ya hivi karibuni.
Mayer ambaye ni msemaji wa masuala ya ndani wa chama cha Christian Social Union cha jimbo la Bavaria ambacho ni chama ndugu cha chama Merkel cha CDU amesema hawawezi kusajili na kudhibiti wahamiaji wote wanaovuka mpaka na kuingia Ujerumani.

Koffi Olomide atimuliwa Kenya kwa kumpiga teke dancer wake (Video)


Mwanamuziki mkongwe wa DRC, Koffi Olomide ametimuliwa nchini Kenya, Ijumaa hii na kurudishwa kwao Kinshasa, baada ya asubuhi ya jana kuonekana akimpiga teke dancer wake wakati akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, jijini Nairobi.
Olomide alionekana kwenye video akimshambulia mmoja wa dancers wake na kujikuta akibebwa mzobe mzobe jana jioni baada ya kuhojiwa kwenye kituo cha runinga cha Citizen TV.
Staa huyo alikuwa atumbuize Jumamosi hii kwenye viwanja vya Bomas of Kenya.
Hatua hiyo ilikuja baada ya kamanda mkuu wa jeshi la polisi jijini Nairobi Japheth Koome kudai kuwa polisi walikuwa wakifanyia uchunguzi tukio hilo.
Kuna hatihati kuwa Olomide akapigwa marufuku kabisa kukanyaga nchini Kenya.

Video: Gucci Mane – Waybach


In celebration of his new album Everybody Looking, Gucci Mane jumps in his “Waybach” and rides out in style. With Mike WiLL Made-It alongside him, he gets chauffeured through East Atlanta in his white Maybach (a gift from his girlfriend Keyshia Ka’oir) while flashing his jewelry and stacks of cash. The fit and now sober rapper also gives us a peek at his lavish Atlanta mansion.


Kiongozi wa upinzani afungwa jela C Brazaville


Image copyrightAMNESTY INTERNATIONAL
Image captionPaulin Makaya
Mahakama moja nchini Congo Brazaville imemfunga kiongozi mmoja wa upinzani kifungo cha miaka miwili jela kwa kuchochea ghasia kulingana na shirika la habari la AFP.
Mashtaka yake yanatokana na maandamano yaliokatazwa ambayo kiongozi huyo Paulin Makaya aliyapanga mwaka 2015.
Maandamano hayo yalifanywa kupinga kura ya maoni iliomaliza kipindi cha awamu mbili za kuwa raia na kumruhusu rais aliye mamlakani Denis Sassou Nguesso kupigania awamu ya pili mnamo mwezi Machi mwaka huu.
Makaya alisema kuwa ataka rufaa dhidi ya hatia hiyo huku wakili wake akiutaja uamuzi huo kuwa usio wa haki na haramu.