Header Ads

Guardiola: Nimeleta tiki-taka Uingereza

Image copyrightGETTY
Image captionPep Guradiola
Mkufunzi mpya wa Manchester City Pep Guardiola anasema kuwa alienda nchini Uingereza kuthibitisha kuwa inawezekana kucheza mchezo mzuri katika ligi ya Uingereza.
Gurdiola mwenye umri wa miaka 45 ambaye ametia kandarasi ya miaka mitatu ,amesema kuwa alipendelea kusalia kuifunza Bayern Munich ,lakini alitaka mtihani mwengine katika ukufunzi wake.
Raia huyo wa Uhispania amekiri kwamba alikuwa na kila alichohitaji wakati alipokuwa Barcelona ,lakini akakana kuwa huenda anakabiliwa na kibarua kigumu katika klabu ya Manchester City.
''Niko hapa kuthibitisha kuwa ninaweza kuchezesha soka nzuri vilevile nimekuwa nikicheza'',alisema.
Image copyrightAP
Image captionManchester City
Alipoulizwa iwapo anaweza kuanzisha mtindo mzuri wa tiki-taka kama ule wa Barcelona ,alisema Guardiola:''Hiyo ndio sababu niko hapa''.
Aliongezea:''Sijawahi kucheza wakati wa siku kuu ya Boxing Dei.Sijawahi kuwa katika uwanja wakati ambapo kuna upepo mkali na baridi na uwanja sio mzuri.Ni lengo langu.Nataka kuwathibitishia''.

No comments