September 24, 2016

magazeti 24/9/2016

Magazetini leo Jumamosi,Septemba 24,2016




















 

September 23, 2016

MTOTO Dominica Matenya (3) amefariki dunia kwa kudaiwa amenyweshwa dawa za miti shamba

MTOTO Dominica Matenya (3) amefariki dunia kwa kudaiwa amenyweshwa dawa za miti shamba

Image result for pich ya kibuyu 
MTOTO Dominica Matenya (3) amefariki dunia kwa kudaiwa amenyweshwa dawa za miti shamba na jirani yake, Leah John katika Kitongoji cha Danduhu, Kijiji cha Didia kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. 

Mtendaji wa kijiji hicho, Waziri Shimba alisema tukio hilo lilitokea jana saa sita mchana ambapo alieleza kuwa alipata taarifa hiyo kutoka kwa majirani na kuanza kufuatilia. 

Shimba alisema mtoto huyo alidaiwa kusumbuliwa na maradhi ya kuharisha na mwili kuwa na mabaka, ambapo jirani yao, Leah walikubaliana na mzazi wa mtoto kumpatia dawa za miti shamba, lengo likiwa ni kuondoa mabaka ya mwili. 

Diwani wa Viti Maalumu, Mengi Charles alisema walielezwa mtoto huyo aliamka akiwa hajazidiwa ila mwili wake ulikuwa na mabaka na ndio jirani yake akampatia dawa ya miti shamba ili kumwondolea mabaka ya mwili aliyokuwa nayo. 

Mama wa mtoto, Thereza Omari, alisema kuwa mtoto wake alipoamka asubuhi alianza kuharisha kidogo huku akiwa na mabaka mwilini na jirani huyo alimueleza kuwa anayo dawa ya miti shamba itakayoweza kumtibu mabaka na akaamua kutompeleka hospitali.
Na Kareny Masasy-Habarileo Shinyanga

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa, jana amewasili Bukoba mkoani Kagera kuwatembelea

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa, jana amewasili Bukoba mkoani Kagera kuwatembelea



Tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba mkoani Kagera Septemba 10 lilisababisha vifo vya watu 19 huku wengine zaidi ya 250 wakiachwa na maejeraha mbalimbali. 


Alipofikika katika uwanja wa ndege wa Bukoba, Edward Lowassa aliyeambatana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema , Sheikh Katimba, Khamis Mgeja na Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare waliongozana hadi eneo la Hamugembe na Kashai kujionea madhara ya tetemeko la ardhi. 

Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa maeneo hayo, Lowassa aliwapa pole sana kwa yote yaliowafika na kusisitiza kwamba anaamini serikali itachukua jukumu la kuwasaidia. 


Aidha, amesema kuwa msaada wake yeye atampatia Mkuu wa Mkoa, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu ili uweze kuwasaidia wananchi wa Kagera.




Kama Una Habari,Picha,Tangazo n.k Wasiliana Nasi 

New Video: Abela Music ft Izzo Bizness – Balaa





Katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, Abela Music ameachia wimbo aliomshirikisha member mwenzake wa kundi la The Amazing, Izzo Bizness. Wimbo unaitwa Balaa na video imeongozwa na Extra Films.









Video: J.Martins Ft. Ferre Gola song Ekelebe


Don Family Music Group Presents J.Martins With his new Visuals Dubbed ‘Ekelebe’ Which he Teams up with the Sensational DR Congo singer Ferre Gola



katika viwanja mbalimbali ambapo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Simba SC ataikaribisha Majimaji ya mjini Songea.

Michuano ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea kesho katika mzunguko wa sita kwa kupigwa michezo mitano katika viwanja mbalimbali ambapo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Simba SC ataikaribisha Majimaji ya mjini Songea.




Afisa Habari wa Simba SC Haji Manara amesema, wanaupa umuhimu mkubwa mchezo huo na hawawezi kuidharau Majimaji kwani kila timu inaingia Uwanjani kwa ajili ya kutafuta pointi tatu.
Kwa upande wake Meneja wa Majimaji Godfrey Mvula amesema, wamejiandaa ili kuhakikisha wanapata pointi tatu kwani wameshapoteza michezo mitano iliyopita hivyo watahakikisha wanapambana kwa ajili ya kujihakikishia ushindi huku wakiahidi kuendeleza ushirikiano na Kocha Kali Ongala ambaye anatarajia kurejea ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kuendelea kukifundisha.
Mechi nyingine zitakazopigwa hapo kesho katika muendelezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ni Mbeya City akiwa ugenini dhidi ya JKT Ruvu katika Uwanja wa Mabatini Mkoani Pwani, Ndanda FC akiikaribisha Azam FC kwa Uwanja wa Nangwanda sijaona Mkoani Mtwara, Tanzania Prisons akiikaribisha Mwadui FC Uwanja wa Sokoine Mkoani Mbeya na Mtibwa Sugar akiikaribisha Mbao FC katika Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
Wakati huohuo, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfred Lucas amevitaka vilabu vya ligi daraja la kwanza vinavyoanza ligi kesho kujifunza kupitia mashindano yaliyopita ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo za kushushwa daraja.

Vikosi vya ulinzi na usalama vimefungua mafunzo ya pamoja ya utendaji kivita kwenye maeneo ya fukwe na visiwa

Vikosi vya ulinzi na usalama vimefungua mafunzo ya pamoja ya utendaji kivita kwenye maeneo ya fukwe na visiwa vilivyopo ndani ya bahari kwa lengo la kukabiliana na maovu yatendekayo ndani ya bahari na kuimarisha ulinzi.


Mafunzo hayo ya pamoja ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ yameshirikisha vikosi vya Anga, Nchini Kavu na Baharini, JKT na Wanamgambo kwa lengo la kuwajengea uwezo kivita na huku ikielezwa kuwa Jeshi la Tanzania ni miongoni mwa majeshi bora dunia.
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Venance Mabeyo amesema jeshi limekuwa imara katika kuhakikisha linakabiliana na vitendo vya uharamia, ugaidi, uvuvi haramu na uingizwaji wa madawa ya kulevya na uhalifu wowote unaoweza kutokana na fukwe zetu.

Mafunzo hayo yatahitimishwa Wilayani Bagamoyo Septemba 30 na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli huku Kaimu Mkuu wa Kamandi ya Wanamaji akiwataka watanzania kutambua kuwa Jeshi lao lipo imara katika kulinda mipaka yao.

Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 25 ametangazwa kuwa chifu wa mji Argungu wa kazkazini magharibi mwa Nigeria


Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 25 ametangazwa kuwa chifu wa mji Argungu wa kazkazini magharibi mwa Nigeria


Msichana Hindatu Umar
Image captionChifu wa mji wa Argungu ulioko kazkazini magharibi mwa Nigeria, Hindatu Umar aliye na umri wa miaka 25

Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 25 ametangazwa kuwa chifu wa mji Argungu wa kazkazini magharibi mwa Nigeria, ikiwa ni mara ya kwanza wanamke kushika wadha huo.
Hindatu Umar pia anakuwa chifu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuwa chifu wa mji huo katika jimbo la Kebbi lenye wakaazi wengi waislamu.
Baadhi ya wakaazi wa eneo hilo wamelalamika wakidai hana ujuzi wa kutosha na si mkakamavu.
Lakini ukweli ni kwamba amekuwa akihudumu kama naibu wa chifu kwa mda sasa ndiposa akapandishwa cheo baada ya mda wa aliyekuwa chifu kumalizika.
 anasema wengi wameshangazwa na hatua hiyo kwa sababu ni nadra kwa wanawake kushika nyadhfa za kiutawala na kisiasa katika maeneo yaliyo na waakaazi wengi waislamu huko kazkazini mwa Nigeria

Imebainika kuwa video ya ile ngoma ya KAZI KAZI ya Profesa Jay na Sholo Mwamba ilitawaliwa na mabalaa makubwa na ya aina yake.

Imebainika kuwa video ya ile ngoma ya KAZI KAZI ya Profesa Jay na Sholo Mwamba ilitawaliwa na mabalaa makubwa na ya aina yake.






Video hiyo ilifanyika katika maeneo ya Uwanja wa Fisi na balaa lilianza baada ya kuanza ku'shoot', imeelezwa kuwa kulimiminika mamia ya watu, kitendo kilichompa presha Profesa kujiuliza kama atatikiwa kuwalipa watu wote wale au itakuwaje! maana walionesha kujishughulisha mno na video hiyo.
Kwa upande wake Sholo Mwamba alisema "Watu waliojaa kwenye ile video walikuja tu kwa mapenzi yao kwangu na Prof. Jay, lakini Profesa Jay alistuka sana baada ya kuona watu wanaanza kucheza na mapanga na zile silaha nyingine nyingi unazoziona".
Pia akaongeza "Sehemu nyingine iliyoleta ugumu zaidi, ni pale unapoona watu wanacheza kamari, kulitokea vurugu kubwa, wahuni walipigana sana".
Akizungumza na eNewz, Sholo Mwamba aliomba wadau wa muziki waendelee kutoa support kubwa kuukuza muziki wa Singeli.
Pia akatumia nafasi hiyo kuweka wazi kwamba kwa sasa anafanya kazi chini ya usimamizi Endless Fame ya Wema Sepetu.

Dereva wa Tz aliyetekwa nyara DRC aachiwa huru


Dereva wa Tz aliyetekwa nyara DRC aachiwa huru



Dereva wa Tz aliyetekwa nyara DRC asimulia masaibu

  •  
Mmoja kati ya madereva nane wa Tanzania waliotekwa na wapiganaji wa Mai mai Jamuhuri ya demokrasia ya Congo,Asman Fadhil amesema kuwa  kutekwa kwao, na namna walivyookolewa na jeshi la nchi hiyo pamoja na maisha walioisha wakiwa mateka.

Msanii mkongwe wa vichekesho nchini maarufu kwa jina la Senga wachekeshaj

Msanii mkongwe wa vichekesho nchini maarufu kwa jina la Senga,
 amepiga stori na eNewz na kufunguka kuhusu sanaa na
   kufunguka kuhusu sanaa ya vichekesho nchini na kusema kuwa Bongo kwa sasa
 wachekeshaji ni
wachekeshaji ni wachache sana, na kwamba wengi ni waigizaji.

Image result for picha ya senga

Senga alisema wengi wanaojita wachekeshaji kwa sasa ni watu ambao si comedians, 
bali ni waigizaji wa kawaida wanaolazimisha tu kuchekesha.
Senga alishauri akisema "Wachekeshaji wanapaswa kujifunza kutumia vitendo zaidi katika maigizo yao ili kazi zao ziwe za kimataifa".
Senga alimalizia kwa kusema kiswahili ni lugha inayoeleweka nchi chache tu, hasa Tanzania hivyo kutumia maneno mengi kwenye ucheshi ni kujifungia milango ya kupata soko la kimataifa.

Dully Skyes amesema wamekuwa wakiishia kumuita Braza D tu ila Diamond Platnumz, Mr Blue pamoja na Queen Darlin ndiyo wasanii pekee ambao wamekuwa wakilipa fadhila kwake

Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva Dully Skyes amefunguka na kusema kuwa katika wasanii wote ambao aliwasaidia katika muzuki mpaka wametoboa ni wasanii watatu tu ambao wamekuwa wakilipa fadhila kwake na ambao wamekuwa wakimpigania.

Image result for pich Dully Sykes


Dully Skyes alisema hayo kwenye kipindi cha Planet bongo na kusema kuwa amewasaidia wasanii wengi lakini wengi wao wamekuwa wakiishia kumuita Braza D tu ila Diamond Platnumz, Mr Blue pamoja na Queen Darlin ndiyo wasanii pekee ambao wamekuwa wakilipa fadhila kwake pamoja na kumpigania.


"Watu ambao nimewasaidia wananipa heshima ni wawili tu, wengine wanaishia kuniita braza D tu, lakini Diamond Platnumz, Mr Blue pamoja na Queen Darlin ndiyo wananipa ile heshima kabisa na wanauchungu na mimi kwamba huyu kaka yetu kwa hiyo katika wale watoto ambao nimewatoa kwenye muziki wakiwa wadogo na wananisaidia ni hao watatu" alisema Dully Skyes

Msanii Timbulo alisema haya baada ya kuzinguliwa na msanii Vanessa Mdee pamoja na Malaika


Msanii wa muziki wa bongo fleva Timbulo amefunguka na kusema kuwa asilimia kubwa ya wanawake wamezoea kupata kidogo katika maisha yao ya kila siku ndiyo maana inapotokea wamepata kikubwa wanawehuka na kuvurugika.
Image result for picha ya timbulo
Timbulo
Timbulo alisema hayo kupitia kipindi cha eNewz ya EATV na kusema kuwa kuna baadhi ya wanawake wakipata fedha au mafanikio katika maisha yao wanabadilika na kuwa na mashauzi na kwamba wanajisahau walipotoka na kuanza kuonesha dharau.
"Watoto wa kike wamezoea kupata kidogo wakipata kikubwa wanawehuka, wanabadilika wanajiona wasichana wazuri, na ikishatokea akaanza kuonekana kwenye TV vichwa vyao vina vurugika akili, wanashindwa kutambua nafasi walizopata, mimi naamini ukipata nafasi ya kufanya kazi na msanii yoyote anayefanya vizuri ni nafasi nzuri kwa msanii wa kike na yeye kufanya vizuri" alisema Timbulo
Msanii Timbulo alisema haya baada ya kuzinguliwa na msanii Vanessa Mdee pamoja na Malaika