Dj Maphorisa na Wizkid wameungana tena kwenye wimbo wa pamoja, Good Love. Umetayarishwa na Nana Rouges huku video ikiongozwa na Sesan Film Factory.
November 29, 2016
Mgahawa mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani, Issa Kapande `Chef Issa', umefunguliwa nchini Sweden na kuvunja rekodi ya dunia.
Balozi Msechu alimpongeza Issa Kapande na mkewe kwa kufanikisha kuwapo kwa mgahawa huo ambao umeweka rekodi kuwa mgahawa mkubwa kuliko yote ya Kiafrika katika nchi za Ulaya.
Aidha, alimshukuru Torvald Brahm mwenyeji wa mji huo kwa kumuunga mkono Issa hadi kufanikisha ndoto yake ya kuwa na mgahawa wa kwanza wa Kiafrika katika mji wa Trollhattan utakatoa huduma ya chakula cha kitanzania.
Katika uzinduzi huo ambapo wenyeji wa manispaa hiyo akiwemo Meya na mwenyekiti wa Trollhattan, Paul Akerlund na msaidizi wake Peter Eriksson walikuwepo, balozi ambaye ndio kwanza ameanza kazi alielezea kufurahishwa na juhudi za Kapande.
Alisema Issa ameonesha njia kwamba inawezekana kwa watu waliopo Ughaibuni sio tu kuajiriwa, bali kujiajiri katika nyanja mbalimbali.Alisema hilo linawezekana kutokana na kufuatilia kwa karibu taratibu za wenyeji na kisha kutumia mafunzo yaliyopo kukamilisha ndoto.
"Ni dhahiri kuwa, Chef Issa kwa kupitia taaluma yake ya upishi amewezeshwa kumiliki mgahawa huu hapa Trollhattan,S weden kwa hilo, napenda tuishangilie na kuipigia makofi Sweden na Trollhattan."Alisema akimpongeza kijana huyo ambaye pia amewekeza mkoani Mtwara.
Katika mahojiano, Mpishi Mkuu Issa Kapande alisema mafanikio yake yanatokana na juhudi kubwa na nia aliyoiweka katika kujifunza na kufundisha wengine katika mitandao ya wapishi wakuu.
Alisema akiwa amefanyakazi katika nchi 17 na tayari akiwa na vitega uchumi nchini alianzia nia ya kuwekeza Sweden mwaka 2009 wakati alipohamia nchini humo akitokea Uswisi. Alisema alianza kwa kuomba vibali, lakini mchakato kamili ulianza mwaka 2013."Tulilazimika kufanya utafiti kidogo" alisema na kuongeza kuwa katika utafiti huo walihoji watu 300 na kujua mwelekeo hasa wa shughuli yao unastahili kuwaje.
Kapande ambaye ni mhitimu wa chuo kikuu cha Manchester Metropolitan na Chuo kikuu cha kimataifa cha menejimenti ya hoteli cha Uswis amesema amepambana vikali na mkewe hadi kufikia hatua ya kuanzisha mgahawa huo ambao upo katika eneo la ukubwa wa skwea mita 810.Kapande ambaye mwaka jana alitwaa tuzo ya dhahabu katika upishi akiwa na timu ya Sweden magharibi alisema kuna umuhimu mkubwa kwa wapishi wa nyumbani kukubali kubadilika na kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kujifunza na kufunza ili kuwa na aina nyingine ya mapishi katika kuendeleza sekta.
Ndani ya mgahawa huo pia watu mbalimbali watapatiwa taarifa za utalii Tanzania.
Katika kazi yake ya upishi, amebahatika kuwapikia watu mashuhuri duniani, baadhi wakiwa Andrew Young, Mchungaji Jesse Jackson, Robert Mugabe (Rais wa Zimbabwe), Paul Kagame (Rais wa Rwanda), Benjamini Mkapa (Rais mstaafu wa Tanzania), Raila Odinga (Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya), Daniel Arap Moi (Rais Mstaafu wa Kenya), Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi. Hillary Clinton na mumewe Bill Clinton, Mke wa Rais wa zamani wa Marekani Laura Bush.
Wengine ni Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, mwigizaji Chris Tucker, Rais wa zamani wa Afrika Kusini hayati Mzee Nelson Mandela, Koffie Olomide, Youssour ndour, Arsene Wenger (Kocha wa Arsenal ya England), Gianluca Vialli (nyota wa zamani wa Italia aliyewahi kuichezea na kuinoa Chelsea ya England), Rais wa Congo DRC, Joseph Kabila, Billy Gates na wengine wengine wanapenda kula chakula katika hoteli hiyo
mawaziri walioteuliwa na Rais John Magufuli si waoga na wanatekeleza wajibu
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina amesema mawaziri walioteuliwa na Rais John Magufuli si waoga na wanatekeleza wajibu wao ikiwa ni pamoja na kumshauri Rais katika masuala mbalimbali.
Mpina aliyasema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mwandoya wilayani Meatu mkoani Simiyu huku akisikitika kuwa maneno yanayotolewa dhidi ya mawaziri na manaibu na viongozi wa vyama vya upinzani kuwa wao ni waoga na hawamshauri Rais si sahihi.
Alisema baadhi ya viongozi hao wamekuwa wakibeza utendaji wa Baraza la Mawaziri na kuwaita waoga wasiomshauri Rais.
“Wapo wale wenzetu wa upande wa pili ambao ni wapinzani wamekuwa wakitubeza mawaziri tulioteuliwa na Rais Magufuli kuwa tumekuwa waoga na hivyo kushindwa kumshauri na kulifanya taifa kusinyaa, hii si kweli. Nyinyi ni mashahidi, mmeona jinsi tunavyochapa kazi,” alisema.
Katika kudhihirisha kuwa wanatekeleza wajibu na kumshauri Rais, Mpina alisema Serikali iliamua kumnyang’anya Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye shamba la hekta 33 kwa kushindwa kuliendeleza.
“Oktoba 28, mwaka huu, Rais John Magufuli alibatilisha hati ya kumiliki ardhi ya shamba namba 3074 lililopo Mabwepande, Dar es Salaam lililokuwa na hati namba 53086. Jina la mmiliki lililoandikwa katika hati ni Frankline Sumaye huu ni ushauri Rais alipewa na Waziri wa Ardhi na akachukua hatua,” alieleza Mpina.
Alisema wataendelea kuchukua hatua bila ubaguzi wa aina yoyote kwa wasiotaka kufanya kazi kwa kufuata utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akataza biashara barabarani
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo, amewataka wafanyabiashara wanaotumia maeneo ya waenda kwa miguu pembeni mwa barabara za Manispaa ya Dodoma, kuondoa biashara hizo mara moja na kwenda maeneo waliyopangiwa rasmi.
Jafo ametoa agizo hilo katika ziara yake fupi ya kutembelea ujenzi wa maeneo mbalimbali ya mjini wa Dodoma ikiwa pamoja barabara ya kuelekea soko la majengo na dampo la kisasa la chidaye nje kidogo ya mji.
Amesema wafanyabiashara hao wanatakiwa kuondolewa na kupewa nafasi katika masoko rasmi kwani upangaji huo wa bidhaa pembeni ya barabara ni uchafuzi na uharibifu wa barabara, wakati mwingine husababisha ajali kutokana na waenda kwa miguu kukosa sehemu ya kupita.
Kutokana na ujenzi wa barabara hiyo, wananchi pamoja na wafanyabiashara wa soko kuu majengo mkoani humo, wameanza kuondokana na adha ya muda mrefu ya ubovu wa miundombinu ya barabara kutokana na awali kutopitika na kutengeneza kwa kiwango cha lami, hali itakayosaidia kurahisisha usafiri wa abiria pamoja na mazao kuingia sokoni.
Mbali na ujenzi wa miundombinu ya barabara, lakini hivi sasa baadhi ya barabara za mji huo zinaendelea kukarabatiwa sambamba na ujengaji wa dampo la kisasa ikiwa ni maandalizi ya ujio wa makao makuu ya nchi.
Msanii wa Hip Hop nchini Young Killer amesema sababu zinazopelekea wasanii wa hip hop nchini kutokuwa na bifu

Msanii wa Hip Hop nchini Young Killer amesema sababu zinazopelekea wasanii wa hip hop nchini kutokuwa na bifu ni kutokana na mafanikio madogo wanayoyapata kupitia muziki.
Akiongea kupitia eNewz Killer amesema hakuna msanii wa hip hop mwenye mafanikio ya kupata show ya milioni 10 hivyo wanakosa cha kujitambia na ukizingatia bifu nyingi husababishwa na mafanikio makubwa japo bifu zao zipo moyoni.
Pia Killer amesema muziki wa sasa una changamoto nyingi na ili upate nafasi ni lazima uzungumziwe hivyo haoni tatizo la Young D kutupiwa dongo na Stamina kuwa hata mapaka kwa sasa wana'rap'.
Killer pia amesema anajipanga kurudi na kurekebisha kila kitu ambacho hakipo sawa.
Jumla ya wanafunzi 16,907 kati ya 25,413 wa shule za msingi katika mkoa wa Shinyanga wamechaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari
Jumla ya wanafunzi
16,907 kati ya 25,413 wa shule za msingi
katika mkoa wa Shinyanga wamechaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari kidato
cha kwanza kwa mwaka 2017,ufaulu ambao ni sawa na asilimia 66.53 ya waliofanya
mtihani,wa kuhitimu darasa la saba mwezi septemba mwaka huu
Akitangaza matokeo ya
uteuzi wa wanafunzi watakaojiunga na
kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2017,katibu tawala mkoa wa shinyanga
ALBERTH MSOVELA anesema matokeo na ufaulu huo umetokana na usimamizi,utendaji
na Jitihada baina ya walimu,watendaji na wanafunzi wenyewe.
Amesema matokeo hayo
yametoa fursa kwa mkoa kushika
nafasi ya 15 kati ya mikoa 26 iliyopo hapa nchini huku shule mbili zikiwa
kwenye kumi bora baada ya kushika nafasi ya kwanza na ya pili.
.jpg)
Diwani wa kata ya
kambarage katika manispaa ya Shinyanga Hassan Mwendapole,ni miongoni mwa wajumbe
waliohudhuria kwenye kikao cha kutangaza uteuzi wa wanafunzi, ambaye alitaka
kupata ufafanuzi wa mambo kadhaa ikiwemo mgawanyo wa nafasi za kwenda kusoma
shule za bweni
---
Akijibu hoja ya mheshimiwa
MWENDAPOLE afisa Elimu wa mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi amesema ushirikiano wa wazazi kufuatilia mwenendo
wa watoto,inahitaji kipaumbele na kwamba suala la kukariri lina taratibu zake
kwa kuwa lipo kisera.
Aidha wadau wote wa Elimu waliokuwa kwenye kikao
hicho wamesisitizwa kutumia nafazi zao
kuielimisha Jamii Juu ya umuhimu wa kupeleka watoto shuleni,kwani elimu ni kito
cha thamani,na daraja thabiti la kumvusha mwanadamu kutoka hatua moja ya chini
kwenda hatua nyingine ya mafanikio.
November 28, 2016
HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE,NOVEMBA 29,2016-
![]() |
Magazetini leo Jumanne,November 29 2016 |
TANZANIA
Mtuwangu wangu wanguvu enderea kuwa na mimi ili nikuongezea maarifa zaidi kupitia ukurasa wetu wa KALI ZOTE BLOG LIKE pegi yetu ya facebook SYLUS DENNISS ,ISTAGRAM SYLASS DENNISS NA TWETER SYLAS DENNISS,,,,,,,, tangaza biashara yako hapa kwenye mtandao unawafikia mamilioni ya watu wasiliana nasi kwa namba 0742692079
Msanii Di’Ja kutoka Record Label Supreme Mavin Dynasty (SMD) ya Nigeria inayomilikiwa na DonJazzy, ameachia video mpya ya wimbo unaitwa “Sowemo”.
video mpya ya mc koba song zawadi
Msanii wa
bongo freva kutoka nchini Tanzania mc koba baada ya ukimya wa miaka kadha hivi
ameamua kuachia ngoma kali inayo tamba tz kwa jina la
zawadi
Msani mc
koba wakati akizungumza na KALIZOTE BLOG ameelezea kwanini wa sanii wa bongo
freva nchini TZ kushindwa kuachia albam amesema sababu ya kwanza nia usabazaji ,

watanzania wengi wanapenda msanii ateo ngoma moja kwa mimi bado sijafikilia kutoa albam kwa sasa ila ngoma zipo za kutosha mda ukifika nitato na sikwamba akuna wa sanii ambao awatoe albam wapo
David Nkulila amejiuzuru nafasi ya ujumbe kwenye kamati ya Fedha na utawala kwa kile alichokieleza ameshindwa kukubaliana na baadhi ya mambo yanavyoamuliwa
Diwani wa kata ya
Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga David
Nkulila amejiuzuru nafasi ya ujumbe kwenye kamati ya Fedha na utawala kwa
kile alichokieleza ameshindwa kukubaliana na baadhi ya mambo yanavyoamuliwa
katika kamati na baraza.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari kwenye kikao maalumu
kilichofanyika kwenye klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Shinyanga mjini
hapa.
Mheshimiwa Nkulila
amesema hatua ya kujiuzuru kwake katika nafasi hiyo ni ishara ya kutokubaliana
na na baadhi ya mambo ambayo yanakiuka sheria,kanuni na taratibu.
Ameyataja baadhi ya
mambo yaliyosababisha yeye kujiuzuru katika kamati hiyo ya Fedha na utawala
kuwa ni Pamoja na udanganyifu uliofanyika ambapo baraza la madiwani la manispaa
ya Shinyanga liliandaa bajeti na kuiwasilisha wizarani,kutotekelezeka kwa
sheria ya ujenzi wa nyumba za ghorofa kutokana na mianya ya rushwa,lakini
mgogoro wa greda,hoja za barabara za lami ambapo ambapo zimekuwa zikitajwa
kilometa nyingi tofauti na uhalisia.
Diwani nkulila
amesema amefikia uamuzi wa kujiuzuru katika nafasi hiyo ya ujumbe wa kamati ya
fedha na utawala, baada ya kutafakari kwa kina Juu ya utata kuhusu mambo kadhaa
yanayojitokeza katika Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga ambayo ni kinyume na
matarajio lakini pia yana athari kwa
wananchi ambao walimwamini na kumpa
dhamana ya uongozi.
Mheshimiwa Nkulila akizungumza na waandishi wa habari