December 31, 2016

Everton yazidisha masaibu ya Leicester



Kevin Mirallas wa Everton akiifungia timu yake bao la kwanza dhidi ya LeicesterImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionKevin Mirallas wa Everton akiifungia timu yake bao la kwanza dhidi ya Leicester
Kevin Mirallas na Romelu Lukaku waliiweka Everton kifua mbele na kuipatia ushindi wake wa kwanza ugenini tangu mwezi Septemba huku mabingwa watetezi wa ligi wakishuka karibu na eneo la kushushwa daraja.
Winga wa Ubelgiji Mirallas alichukua fursa ya kuiweka mbele Everton baada ya safu ya ulinzi ya Leicester kufanya masikhara .
Daniel Amartey ,Leonardo Ulloa na Damarai Gray walilishambulia lango la Everton na kumpatia kazi ya ziada kipa Roble lakini Everton ikaongeza bao la pili kupitia Romelu Lukaku.
Pasi ndefu kutoka kwa Ross Barkley ilimpata Lukaku ,ambaye alionyesha umahiri wake kabla ya kupiga mkwaju uliomuacha kipa Kasper Schmeichel bila jibu.

December 30, 2016

Mamlaka nchini Ujerumani imewafungulia mashtaka vijana saba wakimbizi kwa jaribio la kutaka kumuua



Benchi alilokuwa amelala aliyetaka kuuawa, katika kituo cha treni
Mamlaka nchini Ujerumani imewafungulia mashtaka vijana saba wakimbizi kwa jaribio la kutaka kumuua mtu asiye na makazi kwa kumchoma moto, wakati wa sikukuu ya Krisimas.
Washukiwa sita ambao wana kati ya miaka 15 na 18, walijisalimisha wenyewe baada ya polisi kuonesha picha zilizorekodiwa katika kamera ya uchunguzi, kuhusiana na shambulio hilo lililofanywa katika treni za chini ya ardhi mjini Berlin.
Hata hivyo mtu huyo hakudhurika.
Mshukiwa wa saba wa shambulio hilo, mwenye umri wa miaka 21, ambao polisi wanadai kuwa ndio mshukiwa mkuu, alikamatwa karibu na nyumbani kwake.
Watuhumiwa sita kati ya hao wanatokea Syria, huku mmoja akitokea Libya.
Wote hao walikwenda Berlin Ujerumani kama watu wanaotafuta makaazi mwaka 2014 na 2015.

Ryan Giggs kuifunza Swansea?


Ryan Giggs kulia ameorodheshwa miongoni mwa watu ambao huenda wakamrithi mkufunzi wa Swansea aliyetimuliwa Bob Bradley
Image captionRyan Giggs kulia ameorodheshwa miongoni mwa watu ambao huenda wakamrithi mkufunzi wa Swansea aliyetimuliwa Bob Bradley
Kiungo wa zamani wa Manchester United anatarajiwa kumrithi mkufunzi aaliyekuwa mkufunzi wa Swansea Bob Bradley, aliyetimuliwa usiku wa kuamkia leo na Klabu ya Swansea.
Awali, Giggs, mwenye umri wa miaka 43, alihojiwa mara mbili na timu hiyo kabla ya nafasi hiyo kuchukuliwa na Bradley mwezi Oktoba.
Bradley aliachishwa kazi baada ya kuiongoza Swansea kwa siku 85 pekee na kuiacha katika nafasi ya 19 kwenye ligi.
Ingawa hana uzoefu mwingi, baada ya kustaafu, Giggs aliitumikia Manchester United chini ya David Moyes na kuwa naibu wa kocha, chini ya meneja wa zamani Louis van Gaal.
Nahodha huyo wa zamani wa Wales anadaiwa kufanya mazungumzo na wasimamizi wa Swansea, na mwenyekiti wa klabu hiyo, Huw Jenkins anadaiwa kuvutiwa na Giggs.
Naibu kocha wa Zamani wa United Rene Meulensteen, anaamini Giggs anatosha kuiongoza Swansea.
"Siamini kuwa Giggs hana uzoefu, alipata ujuzi akiwa naibu mkufunzi chini ya Manchester United." Rene Aliiambia BBC Radio 5 Live.
Mkufunzi wa Swansea aliyepigwa kalamu Bob Bradley
Image captionMkufunzi wa Swansea aliyepigwa kalamu Bob Bradley
Wengine wanaosakwa na klabu hiyo ni meneja wa Wales, Chris Coleman, mkufunzi wa zamani wa Leicester City Nigel Pearson na aliyekuwa mkufunzi wa Birmingham City manager Gary Rowett.
Hata hivyo, Mrithi wa Bradley anatarajiwa kuchukua usukani baada ya mechi yao ya nyumbani dhidi ya Bournemouth mwisho wa mwezi.
Kwa sasa, timu hiyo inayoongozwa na wakufunzi wa muda Alan Curtis na Paul Williams watainoa timu hiyo hadi uteuzi utakapofanywa.
Swansea ilipoteza mechi yake ya saba kati ya mechi 11 kwa kupata kichapo cha 4-1 dhidi ya West Ham ikiongozwa na Bradley
Timu hiyo ina alama 12 baada ya kukusanya pointi 8 pekee na kufungwa mabao

December 29, 2016

magazeti ya leo 29/12/2016

                                           magazeti ya leo 29/12/2016
img_20161229_054722
img_20161229_054741
img_20161229_054801
img_20161229_054821
img_20161229_054849
img_20161229_054906
img_20161229_054925
img_20161229_054947
img_20161229_055005
img_20161229_055028
img_20161229_055107
img_20161229_055124
img_20161229_055141
img_20161229_055158
img_20161229_055217
img_20161229_055231
img_20161229_055246
                                         chanzo millardayo

TUKIO la kushangaza lililohusishwa na kifo cha Denis Komba




TUKIO la kushangaza lililohusishwa na kifo cha Denis Komba (24) baada ya nyoka aliyekuwa naye kuuawa, limechukua sura mpya baada ya mambo kadhaa kuibuka.
Hayo ni pamoja na familia kudai mzoga wa nyoka na kwenda nao kuuzika nyumbani, jambo lililoendelea kuhusisha suala hilo na imani za kishirikina.
Imeelezwa kuwa familia ilielezwa na mganga wa kienyeji kuwa mwili uliohifadhiwa hospitali, si wa mtoto wao, jambo lililowafanya kuuchukua mzoga wa nyoka na kwenda kuuweka katika mfuko wa sarandusi (kiroba) na kuuzika.
Hata hivyo, mashuhuda walieleza kuwa, familia hiyo ilikikata kichwa cha nyoka na kukizika kivyake na kiwiliwili sehemu nyingine huku mwili wa Komba ambaye naye alizikwa jana, ukizikwa katika kaburi eneo lingine tofauti. Tukio hilo ni la juzi na lilimhusu Komba, mkazi wa Mateka, manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Nyumbani kwao ni kilometa tano kutoka katikati ya mji wa Songea. Kabla ya maziko, baadhi ya vijana waliokuwa wamebeba jeneza, walikuwa wakikimbia nalo mwendo wa mchakamchaka huku wakiimba “mkimbize mkimbize nyoka awahi asije kudhuru watu wengine”.
Katika maziko hayo, hakuna ndugu aliyeonekana kulia wala hakukuwa na ibada yoyote wakati jina la marehemu linadhihirisha kuwa ni wa imani ya Kikristo. Wakati hayo yakiendelea msibani, baadhi ya watu wake wa karibu walidai alikuwa na tabia ya kucheza na nyoka mara kwa mara.
Hata hivyo, baba mzazi alikana kumuona mwanawe na nyoka. Naye daktari aliyechunguza mwili, alisema kifo cha Komba kinatokana na kugongwa na nyoka mwenye sumu kali, lakini hakuna jeraha wala alama yoyote iliyoonekana katika mwili huo.
Familia yachukua mzoga wa nyoka
Habari zinaeleza kuwa juzi familia ilikwenda kuzungumza na watu wa Idara ya Maliasili, waliochukua mzoga wa nyoka kwa uchunguzi kama nyara ya serikali. Walikubaliana kuwa familia itakwenda kuufukia na ndipo Maliasili walimrudisha nyoka hadi eneo la tukio na familia kumchukua.
Ilielezwa kuwa hatua hiyo, inatokana na madai kuwa kuna mganga amehusisha mzoga wa nyoka huyo na mwili wa Komba.
Watu wa karibu wa familia hiyo, ambao hawakutaka kutaja majina yao gazetini wakiwemo mafundi seremala na majirani, walieleza kuwa familia wakiongozwa na baba mzazi Sevelin Komba, walirudi eneo la tukio baada ya kutoka kwa mganga wa kienyeji na kumchukua nyoka na kumpeleka nyumbani.
Habari zinaeleza kuwa familia baada ya tukio hilo, walikwenda kwa mtaalamu wa mambo ya asili (mganga wa kienyeji) ambaye hakufahamika mara moja na kuelezwa kwa nini wamekubali kumuacha mtoto wao akiteseka juani kwani mwili walioupeleka nyumbani kutoka hospitali si wa Denis (Komba).
Aidha familia baada ya kumchukua nyoka huyo eneo la tukio alikouawa, baada ya kufikishwa nyumbani alikatwa kichwa kwa makubaliano ya familia ya marehemu na kiwiliwili kuzikwa tofauti na kichwa katika mfuko wa sarandusi. Baba mzazi alikanusha suala hilo la kwenda kwa mganga.
Katika maziko hayo, hakukuwa na chakula wala matanga na watu wengi walijitokeza ili kushuhudia kitakachoendelea. Alizoea kutembea,kucheza na nyoka Kwa mujibu wa majirani hao ni kwamba kwa muda mrefu Komba alikuwa na vitendo vinavyoashiria mambo ya kishirikina.
Kwamba hata huyo nyoka, si mara yake ya kwanza kutembea naye, kwani alikuwa akionekana naye mara kwa mara hasa katika viwanja vya mpira, kwa kuwa marehemu alikuwa mpenzi mkubwa wa mchezo wa mpira wa miguu.
Walisema Komba (Denis) alikuwa na vitendo vya kishirikina na alifahamika sana kwa jina ‘Dogo Mzimu’, kutokana na kuwa na mambo makubwa ya yakishirikina tofauti na umri wake, jambo lililosababisha hata baadhi ya watu wengine mtaani kwake kumuogopa licha ya upole wake.
Baba mzazi azungumza
Baba mzazi wa Komba, Sevelin Komba akizungumzia maisha ya mtoto wake kabla ya tukio hilo, alisema ni mtoto wa kwanza kati ya watoto watano na kwa muda wote wa maisha yake alikuwa kijana mzuri, ambaye alikuwa anajishughulisha na kazi ya useremala, ujenzi wa nyumba pamoja na kilimo.
Alisema, wiki tatu zilizopita yeye na familia yake akiwemo Denis walikwenda shamba katika kijiji cha Mpitimbi Songea vijijini kwa ajili ya shughuli za kilimo kwani ni kawaida ya familia hiyo kila inapofika msimu wa kilimo wanakwenda kulima kwa ajili ya kupata chakula cha familia.
Lakini baada ya wiki moja, yeye kama kiongozi wa familia, alirudi nyumbani kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kupata mahitaji ikiwemo chakula na vitu mbalimbali pindi wanapoendelea na shughuli zao za kilimo na kuwaacha watoto wake wakiongozwa na Denis shambani.
Alisema hata hivyo, siku mbili kabla ya tukio hilo tarehe 25, Denis alirudi nyumbani kutoka kijijini kwa ajili ya kufuata mahitaji, ambayo baba yake tayari alishanunua na siku iliyofuata tarehe 26 asubuhi Denis alipewa mahitaji yote muhimu na kurudi shambani huku akiwa na baiskeli.
Hata hivyo, siku hiyo ya tarehe 26 majira ya saa 4 usiku, alipigiwa simu na watu waliojitambulisha kwamba ni wauguzi katika hospitali ya mkoa Ruvuma na kumtaarifu kwamba mtoto wake, Denis, yupo hospitali amepata matatizo hivyo anahitajika kufika haraka.
Komba alisema, mara baada ya kufika hospitali ya mkoa, alishangaa kuona kuna umati mkubwa wa watu wakiwemo askari polisi na waendesha boda boda, ambapo alielezwa kuhusu tukio la kifo cha Denis na alioneshwa mwili wa marehemu mtoto wake, lakini alishangaa kumuona mtoto wake Denis mwili ukiwa na tope.
Komba (baba) alieleza kuwa, wakati huo wote hakuambiwa chanzo cha kifo cha mwanawe hadi siku ya pili ambayo alipata taarifa kuwa kifo cha mtoto wake, kimesababishwa na kufa kwa nyoka aliyekuwa akimmiliki, ambaye alipigwa na wananchi kufuatia kutaka kugonga mwendesha boda boda.
Alisema, ilipofika siku ya pili majira ya mchana, alichukuliwa hadi kituo kikuu cha polisi mjini Songea na baadaye kupelekwa idara ya Maliasili, nje ya mji wa Songea na kuoneshwa nyoka aliyemgonga mtoto wake , ambaye bado alikuwa chini ya ulinzi wa maofisa maliasili Kanda ya Kusini.
Kwa mujibu wa baba huyo, jana saa 1 usiku baada ya kikao cha familia kilichofanyika mchana, walikubaliana waende eneo la tukio baada ya maofisa maliasili kumrudisha nyoka huyo akiwa ameshakufa hadi eneo hilo. Ndipo familia walipomchukua na kumpeleka nyumbani kwa Denis, ambaye katika uhai wake alikuwa na mke na mtoto mmoja.
Alisema, wakiwa katika maandalizi ya mazishi ya Denis baadhi ya majirani waliofika nyumbani kwa ajili ya kushiriki maandalizi ya mazishi, walitaka Denis azikwe kaburi moja na nyoka wake, jambo ambalo familia wamekataa, kwa kuwa yule ni binadamu na nyoka ni mnyama, ambaye ni adui kwa binadamu.
Baba amkata kichwa nyoka Hata hivyo, jambo la kushangaza baba wa marehemu amemkata kichwa nyoka na kusisitiza kwamba Denis atazikwa pekee yake, kiwiliwili cha nyoka kitazikwa peke yake na kichwa kifukiwe eneo lingine, kitendo kinachoaminika ni jambo la kishirikina.
Mafundi seremala, bodaboda wanena
Wakizungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina yao baadhi ya mafundi seremala, ambao marehemu Denis alifanya nao kazi kwa karibu walisema kuwa, Denis licha ya kuonesha vitendo vingi vilivyoashiria mambo ya kishirikina, lakini alikuwa kijana mpole na mwenye upendo mkubwa kwa wenzake.
Lakini, walisema hawaamini kama kifo cha Denis, kimetokana na kuumwa na nyoka, bali kimetokana na mambo ya kishirikina yaliyopelekea yeye kupoteza maisha kwa vile nyoka huyo alikuwa akimuongoza katika mambo mbalimbali.
“Sisi tunakuambia hivi huyu alikuwa anamtumia sana nyoka kwa imani za kishirikina kwani alikuwa naye mara kwa mara hata akiwa katika matembezi ya kawaida na alimtumia katika shughuli zake,”walisema.
Daktari azungumzia uchunguzi
Kwa mujibu wa daktari aliyemfanyia uchunguzi Denis, Dk Geofrey Mdede alisema kifo cha Denis kimetokana na kugongwa na nyoka mwenye sumu kali.
“Kwa utaratibu wa hospitali mgonjwa akishafariki kama ni kifo cha mashaka huwa tunamfanyia uchunguzi ili kubaini chanzo chake na tulipomfanyia Denis tukabaini amekufa baada ya kugongwa na nyoka,” alisema Dk Mdede.
“Lakini kwa bahati mbaya sana sikuona eneo aliloumwa na nyoka kwani meno ya nyoka ni madogo sana kama sindano na laiti marehemu angekuwa hai basi angeonesha eneo alilogongwa na nawaomba sana jamii iamini kwamba kifo cha Denis kimetokana na kugongwa na nyoka,”alisema.
Denis azikwa
Denis amezikwa jana katika makaburi ya Mateka huku umati mkubwa wa watu ukifurika kwa ajili ya kushuhudia na kushiriki maziko yake. Vijana waliobeba jeneza waliimba nyimbo mbalimbali na kulikimbiza jeneza kwa mtindo wa mchakamchaka wakisema mkimbize mkimbize nyoka awahi asije kudhuru watu wengine.
Dereva wa bodaboda aathirika kisaikolojia
Habari zilizopatikana ni kwamba dereva wa boda boda, Kassian Haule ambaye baada ya tukio hilo alilazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya uchunguzi zaidi, jana ameruhusiwa kutoka hospitali hapo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa madereva wenzake wa bodaboda, Haule ameanza kupoteza kumbukumbu ya mambo mbalimbali.
Maliasili wamzungumzia aina ya nyoka huyo
Mhifadhi wa Wanyamapori wa Hifadhi ya Taifa ya Selous Kanda ya Kusini, Msondi Simwanza, alisema aina ya nyoka aliyehusika katika tukio hilo ni ‘blackmamba’ na ni kati ya nyoka hatari duniani kwa sumu kali.
Simwanza alisema nyoka wa aina hiyo, hupenda kuishi kwenye mazingira yenye vichaka, hasa kwenye mashimo ya vichuguu au mengineyo. Juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji alithibitisha tukio hilo. Alisema mwili wa marehemu haukuwa na jeraha lolote.
Alisema nyoka aliyeuawa na wananchi alichukuliwa na idara ya mali ya asili. Pia alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini kiini cha tukio hilo la kuuawa kwa nyoka na kisha mmiliki wake naye kufa.

Darassa akifanya yake mbele ya wafanyabiashara wa Ilala.





Hit maker wa wimbo Muziki, Shariff Thabeet aka Darassa Jumatano hii alikutana na wafanyabiashara wa soko la Ilala Boma na kuonyesha baadhi ya vitu ambavyo ataenda kuvifanya Jumamosi hii kwenye Jukwaa la Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.

Darassa akifanya yake mbele ya wafanyabiashara wa Ilala.
Darassa na Roma, kwa pamoja watapanda katika Jukwaa la Dar Live kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya ili kumaliza ubishi wa nani mkali wa michano katika pambano la Nichane Nikuchane.
Akiwa kwenye Viwanja vya Karume jijini Dar, leo, Darassa aliisimamisha Ilala pale alipotoa burudani fupi ikiwa ni kionjo kabla ya shoo yenyewe kamili ya siku hiyo.
Akiongea na mashabiki wake, Darassa alisema amejipanga vizuri kuonyesha mambo mapya katika jukwaa hilo la burudani.
“Mashabiki zangu, siku hiyo ya Mkesha wa Mwaka Mpya mnachotakiwa kufanya ni kuja kwa wingi pale Dar Live kushuhudia miujiza nitakayoifanya kwani siku zote naamini huwa nafanya miujiza kila ninapopanda jukwaani.” alisema Darassa.
Naye Meneja wa Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers ambao ni waandaaji wa pambano hilo, Abdallah Mrisho, alisema: “Shoo hii inayoenda kufanyika ni ya tofauti, kama tujuavyo Roma na Darassa kwa sasa ndiyo habari ya mjini hasa kwenye muziki wa Hip Hop, hii ni mara ya kwanza kwa Darassa kupanda kwenye Jukwaa la Dar Live, hivyo mashabiki ni fursa yenu kujumuika naye siku hiyo.”
Katika hatua nyingine, Meneja wa Dar Live na mratibu wa mpambano huo, Juma Mbizo, alisema: “Kwa kiingilio cha Sh 5,000, mashabiki watapata fursa ya kuingia na kushuhudia mpambano huo mkali ambao rasmi utaanza saa 7 mchana mpaka majogoo.”
Mbali na wakali hao kupanda jukwaani siku hiyo, pia wengine watakaotoa burudani ni pamoja na Kundi la Muziki wa Taarab la Jahazi, Juma Nature, Makhirikhiri, MC Darada, Topido, ID Classic, H-Mbizo na wengine wengi.

VIDEO KALI ZA MWAKA 2016 KUTOKA KWA BAHATI BUKUKU

Image result for PICHA YA BAHATI BUKUKU


KUWA WAKWANZA KUPATA KITU UKIPENDACHO ,,,,,,,,,,,ANGALIA VIDEO ZA BAHATI BUKUKU


SONG TULIZA MAWIMBI






                                             SONG UMEZIDI WOTE

December 28, 2016

YANGA jana ilijiongezea pointi tatu




Image result for yanga fc
 YANGA jana ilijiongezea pointi tatu muhimu baada ya 
kuifunga Ndanda Fc mabao 4-0 katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Ushindi huo umekuja baada ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu kutoka sare ya bao 1-1 na African Lyon katika mechi iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita na hivyo kupunguzwa kasi ya kuelekea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, nafasi inayoshikiliwa na Simba.
Yanga sasa imefikisha pointi 40, ikiwa nyuma kwa pointi moja dhidi ya Simba, ikiombea Simba ipate sare ama ipoteze dhidi ya Ruvu Shooting leo ili shughuli ya kufukuzia kilele cha msimamo inoge vizuri.
Yanga ilianza mechi hiyo kwa kasi ilikishambulia lango la Ndanda na dakika ya tatu Donald Ngoma aliandika bao la kuongoza baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa kona wa Haruna Niyonzima.
Kuingia kwa bao hilo kuliifanya Ndanda kufurukuta kidogo ambapo katika dakika ya 12 nusura mchezaji wa zamani wa Yanga, Kigi Makasi aandike bao la kusawazisha kwa mkwaju mkali wa adhabu ndogo lakini uliishia mikononi mwa kipa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’.
Dakika ya 20, Ngoma aliiongezea Yanga bao la pili kwa kuunganisha krosi ya Juma Abdul kabla ya kuujaza mpira wavuni akiwaacha mabeki wa Ndanda wamezubaa wakidhani mfungaji ameotea.
Dakika tano baadae, Yanga ilipata bao la tatu lililofungwa mshambuliaji wake Amisi Tambwe baada ya kugongeana vema pasi na Ngoma kabla ya kumgeukia kipa wa Ndanda na kuujaza mpira wavuni. Baada ya bao hilo, mpira ulilazimika kusimama kwa dakika chache kutokana na kipa wa Ndanda Jeremiah Kisubi kuumia.
Mabingwa hao watetezi ambao jana walionyesha soka safi walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 3-0 kabla ya Vincent Bossou hajafunga bao la nne katika dakika 88 akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona iliyochongwa na Abdul.
Kwenye uwanja wa Manungu, Turiani wenyeji Mtibwa Sugar waliitambia Majimaji kwa kuifunga bao 1-0. Kwa matokeo hayo, Mtibwa imepanda mpaka nafasi ya tatu ikiwa na pointi 30 na Majimaji inabaki nafasi ya 14 na pointi zake 17.
Yanga: Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Vincent Bossou, Kelvin Yondan, Said Juma ‘Makapu’/ Justine Zulu, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Emmanuel Martin/ Geoffrey Mwashiuya.
Ndanda FC: Jeremiah Kisubi/, Kiggi Makassi, Bakari Mtama, Paul Ngalema, Hemed Khoja, Salvatory Ntebe/Ayoub Shaaban, Abuu Ubwa/Salum Minely, Nassor Kapaman, Salum Telela, Omar Mponda na Riffat Khamis.

Mwanasoka maarufu nchini Kenya, Joe Kadenge, amelazwa katika hospitali moja mjini Nairobi


Kadenge na mpira alazwa nchini Kenya

Mwanasoka maarufu nchini Kenya, Joe Kadenge, amelazwa katika hospitali moja mjini Nairobi baada ya kuugua.
Nyota huyo mstaafu aliyeiwakilisha klabu ya Afc Leopards na timu ya taifa ya Kenya, alikimbizwa hospitalini mapema wiki hii baada ya kuugua kisukari.
Wachezaji wenzake wa zamani, George Sunguti na Reginald Asibwa walimsaidia kumfikisha hospitalini baada ya kuzidiwa na maumivu.
Hata hivyo familia yake inasema kuwa Kadenge amepata nafuu na hali yake inaendelea kuimarika.
Ni mara ya pili shujaa huyo kuugua na kukimbizwa hospitalini .
Mwezi Oktoba, Kadenge alikimbizwa hadi hospitali ya Meridian mjini Nairobi alipokuwa akitazama mechi ya ligi ya soka ya taifa hilo.
"Amepata nafuu kwa sasa na mke wake amejiunga naye hospitalini kumsaidia," Sunguti ameliambia gazeti la Nation nchini Kenya.
Wapenzi wa soka nchini humo wamekuwa wakimtakia mzee huyo nafuu.
Mnamo mwezi Septemba Kenya ilimpoteza kocha na mchezaji maarufu James Sianga aliyefariki baada ya kuugua kwa kipindi kirefu magharibi mwa Kenya.

December 27, 2016

Gereza kuu la Kigali lateketea kwa moto

Gereza kuu la Kigali maarufu 1930
Gereza kuu la Kigali maarufu 1930 lateketea kwa moto. kufikia leo jioni moshi inaendelea kutanda. Kilichosababisha moto huo hakikajulikana.
Shughuli za kuzima moto bado zinaendelea huku vikosi vya Askari Jeshi na polisi vikionekana hapa na pale kando kando mwa jengo la gereza hilo.
 Hilo Ni gereza linalohifadhi wafungwa wa mchanganyiko wale wa kisiasa na wengine wa mauaji ya kimbari. Miongoni mwa wafungwa wa kisiasa Ni Victoire Ingabire aliyehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela miaka 4 iliyopita Kwa hatia ya kuchochea utengano wa kikabila na kuhatarisha usalama wa raia.
Viongozi kadhaa serikalini wamefika kwenye eneo la tukio wakiwemo mawaziri na wakuu wa jeshi na polisi.
Bado Ni mapema kujua athari zilizotokana na tukio hilo kwani waandishi wa habari hawajaruhusiwa kuingia katika jengo la gereza kuu ya Kigali.
Magari ya zima moto bado yanapishana na magari ya kubeba majeruhi huku wafungwa wakionekana nje ya gereza na ulinzi ukiwa umeimarishwa.

CHANZO BBC

Rose Muhando Mapenzi New Music 2016

Image result for PICHA ZA ROSE MUHANDO

                               SIKILIZA HAPA CHINI NAKUWA  WAKWANZA KUPATA HII


Anthony Lusekelo maarufu 'Mzee wa Upako awafukuza waandishi wa habari kanisani


Image result for PICHA YA MZEE WAUPAKO



MMCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo jijini Dar es Salaam, Anthony Lusekelo maarufu 'Mzee wa Upako, aliwagomea waandishi wa habari kusikiliza hotuba yake ya ibada na kutuma wasaidizi wake wawaondoe waandishi hao.
“Samahani tunaomba muondoke kwani Mchungaji amesema hataki kumuona mwandishi hivyo tunaomba muende kwenye makanisa mengine,” alisema msaidizi huyo na kuhakikisha waandishi wote wanaondoka eneo hilo majira ya saa sita kasoro mchana.
Lusekelo maarufu Mzee wa Upako hivi karibuni amekuwa akirushiana maneno na baadhi ya waandishi wa habari baada ya kuandikwa akituhumiwa kuwa mlevi na kutukana hadharani.
Desemba 25 ya kila mwaka, waumini wa dini ya Kikristo nchini huungana na wenzao duniani kuadhimisha sherehe za kuzaliwa kwa Bwana wao Yesu Kristo yapata miaka 2000 iliyopita.
Wakati huohuo waumini wa dini ya Kikristo nchini wametakiwa kudumisha upendo, utii na unyenyekevu ili kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Bwana na Mwokozi wao Yesu Kristo ikiwa ni pamoja na kuliombea amani taifa lao la Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ibada ya mkesha wa sikukuu hiyo, Dk Alex Malasusa, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, aliwataka waumini wa kanisa hilo, kuhakikisha wanakuwa mabalozi wa amani na upendo kwa wenzao.
Alisema siku ya Krismasi ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwana wa Mungu Yesu Kristo ambaye kutokana na upendo wake, aliwaunganisha watu na Mwenyezi Mungu.
“Tuuenzi upendo wake, lakini kubwa zaidi tukumbuke kuwa amani ndio msingi wa sikukuu hii. Hata alipokuja Yesu maneno yake ya kwanza yalikuwa ni amani,” alisisitiza. Askofu Malasusa, aliwataka wananchi katika kudumisha upendo huo, waliombee taifa pamoja na viongozi wake ili amani iliyopo iendelee kudumu.
“Ndio maana leo katika ibada yetu ya mkesha wa Krismasi tumeamua kupeana zawadi ikiwa ni ishara ya kuoneshana upendo na kudumisha amani miongoni mwetu,” alisema.
Mara baada ya ibada hiyo, waumini wa kanisa hilo, walibadilishana zawadi ambayo kila mtu alikuja nayo na kumpatia mwenzake huku Askofu Malasusa na viongozi wengine wa Kanisa hilo nao wakigawa zawadi zao kwa waumini hao.

maGAZETI YA LEO 27/12/2016


20161227_041800
20161227_041810
20161227_041823
20161227_041834
20161227_041844
20161227_041854
20161227_041915
20161227_041924
20161227_041938
20161227_041947
20161227_041957
20161227_042010
20161227_042021
20161227_042031
20161227_042041
20161227_042051
20161227_042102
20161227_042110
20161227_042124
20161227_042132
20161227_042147
20161227_042158
20161227_042209
20161227_042218
20161227_042229
20161227_042236
20161227_042311
20161227_042318
20161227_042345
20161227_042352


kuwa wakwanza kusikiliza  hii na kusikiliza