January 31, 2017

Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Ndembezi katika Wilaya ya Shinyanga Mjini imefanya usafi wa Mazingira

 Image result for picha ya ccm



Jumuiya ya vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Ndembezi katika Wilaya ya Shinyanga Mjini imefanya usafi wa Mazingira katika kituo cha afya cha Ngokolo Mjini Shinyanga,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka arobaini ya Chama hicho ambapo kilele chake ni Februari 05,mwaka huu.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana wa ccm-uvccm kata ya  Ndembezi DOTTO JOSHUA  amesema maadhimisho ya Chama hicho kwa mwaka huu 2017 yatafanyika kwa utaratibu wa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo usafi,badala ya mikutano,ngoma na Maandamano kama ilivyozoeleka.

Mwenyekiti huyo amesema Miaka arobaini tangu kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM, wananchi wameendelea kuwa na  imani na Chama hicho tawala ambacho kimepiga hatua mbalimbali za mafanikio.


Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM  wilaya ya Shinyanga mjini CHARLES SANGURA amesema kuelekea kilele cha maadhimisho hayo Chama na  Jumuiya zake,ikiwemo wazazi,UWT,na vijana  watafanya shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo utoaji wa Elimu, usafi wa mazingira, na upandaji wa miti.

Senegal na Liverpool, Salif Diao ameiambia timu yake ya zamani kwamba inapaswa kumsaidia Sadio Mane


Senegal
Image captionSadio Mane

Mchezaji wa zamani na kiungo wa timu za Senegal na Liverpool, Salif Diao ameiambia timu yake ya zamani kwamba inapaswa kumsaidia Sadio Mane kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya kukosa mkwaju wa adhabu ambao uliisababishia timu yake ya Senegal kuondolewa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon.
Mane alivunjika moyo baada ya kukosa penalti muhimu katika robo fainali dhidi ya mahasimu wao timu ya Cameroon.Diao amesema kwamba kuna haja ya kuwa na mtazamo chanya juu ya kushindwa kwa timu ya Senegal na siyo kumfanya Mane kuwa ndiye mchawi wao.
Ilikuwa ni huzuni kuu kwa kilichomtokea. Ni kawaida barani afrika kumtafuta mchawi lakini nadhani amecheza vizuri ukiondoa kasoro hiyo, pengine tulitarajia makubwa ziaidi kutoka kwake na timu nzima lakini nafikiri bado hajakomaa sawasawa.
Ingawa naamini akisalia na timu ya Liverpool kwa miaka miwili zaidi,anaweza kuwa bora zaidi na kubeba jahazi la timu, ameyasema hayo Diao ambaye alikuwa sehemu ya timu ya Senegal ambayo ilipoteza mchezo dhidi ya Cameroon katika michuano ya fainali za mwaka 2002 kombe la mataifa ya Afrika mtanange uliosambazwa nchini Mali.
Pamoja na kupoteza nafasi ya kusonga mbele katika michuano hiyo, Diao amemtetea na kocha wa timu yake ya taifa Aliou Cisse kusalia katika nafasi yake na kuiruhusu timu kupata nafasi ya kukua pamoja kwa michuano ijayo inayotarajiwa kufanyika nchini Cameroon wakiwania kufuzu michuano ya kombe la dunia.

WANANCHI WASHINYANGA KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA SHERIA




Image result for PICHA YA KITABU CHA sheria


Wakazi wa mji wa Shinyanga na maeneo yaliyopo Jirani wameombwa kushiriki kwenye maadhimisho ya wiki ya Sheria nchini ili waweze kujifunza na kupata ushauri  mbalimbali kuhusu masuala ya kisheria.

Akizindua wiki ya sheria kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Fadhiri Nkulu ambaye  pia ni mkuu wa wilaya ya Kahama amesema maadhimisho hayo ni fursa kwa wananchi kujua sheria,hivyo ni jukumu la wadau wa masuala ya kisheria ikiwemo mahakama kubainisha hatua zilizofikiwa katika uboreshaji wa huduma,hivyo Jamii inapaswa kuhudhuria ili kujifunza


Ameonya mahakimu wanaokiuka maadili ya kazi kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa,hivyo kuminya upatikanaji wa haki na kuchafua sifa ya mhimili wa mahakama,kwamba mamlaka husika hazitosita kuchukua hatua za kinidhamu.
Kwa upande wao Baadhi ya wananchi waliokuwa wamehudhuria katika uzinduzi wa wiki ya sheria wamesema hawana uelewa wa kutosha hivyo kuimba idara ya mahakama na wadau wengine kutoa elimu mara kwa mara kuhusu masuala ya kisheria,badala ya kusubiri maahimisho.

Kilele cha  wiki ya sheria ni Februari mbili,mwaka huu ambapo uzinduzi kimkoa umefanyika leo katika viwanja vya kikosi cha zimamoto,huku kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ikisema ‘’umuhimu wa utoaji haki kwa wakati,na kuwezesha ukuaji wa uchumi’’.


ANGLIA VIDEO YA HISTORIA YA SIMBA NA YANGA 

Magazeti ya Tanzania January 31, 2017 kuanzia, Udaku, Hardnews na michezo


Ulimiss hii EXCLUSIVE: Hamorapa aongea ukweli kuhusu undugu na Harmonize, Wolper wake je? tazama kwenye hii video hapa chini



MTUWANGU WANGUVU LEO JUMAANNE NIME KUSONGEZEA HII HISTORIA YA YANGA NA SIMBA


treni ya abiria ya Deluxe, iliyokuwa ikitoka mkoani Kigoma kwenda Dar es Salaam kuanguka mkoani Pwani.


WATU kadhaa wamejeruhiwa, mmoja akiwa ana hali mbaya baada ya mabehewa tisa ya treni ya abiria ya Deluxe, iliyokuwa ikitoka mkoani Kigoma kwenda Dar es Salaam kuanguka mkoani Pwani.
Katika mabehewa hayo, manne yameanguka, matatu yameacha njia na mawili yametenguka.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Boniventure Mushongi, mabehewa yaliyoanguka ni saba na kwamba wanaendelea kuwaokoa majeruhi.
Akizungumza kwa njia ya simu, Msemaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Midladjy Maez alisema ajali hiyo ilitokea saa 9:40 alasiri katika Kitongoji cha Kambini Ruvu Ngeta, Kata ya Kikongoa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani. Maez alisema mabehewa hayo yalianguka baada ya treni kuacha njia na kusababisha majeruhi kadhaa.
“Ni kweli ajali hiyo imetokea na kusababisha majeruhi na hadi wakati huo kulikuwa hakuna taarifa yoyote ya kifo kilichotokana na ajali hiyo, licha ya kwamba mtu mmoja ndiyo hali yake mbaya,” alisema Maez, bila kutaja sababu za ajali hiyo.
“...Imeripotiwa watu kadhaa wamejeruhiwa na mmoja amejeruhiwa sana, hizi ni taarifa za awali…baada ya kikosi cha uokoaji kumaliza kazi ya kuinua mabehewa ndio taarifa ya waathirika itakamilika,” alisema Maez katika taarifa yake.
Alisema treni hiyo ilitakiwa ifike Dar es Salaam saa 11 jioni, lakini ilipofika hapo mabehewa hayo yalianguka na kusababisha kushindwa kuendelea na safari.
“Kutokana na ajili hiyo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na Mkurugenzi Mkuu wa TRL wanaelekea eneo la tukio ili kuweza kujua kilichotokea,” aliongeza msemaji huyo wa TRL.



CHANZO HABARI LEO

Afumaniwa akizini na mke wa mtu


Image result for picha ya jeneza

WATU watatu wilayani Igunga mkoani Tabora wamekufa akiwemo mwanaume aliyeuawa na kundi la wananchi baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mtu. Watoto wawili wa familia moja wamepoteza maisha kwa kuzama kwenye shimo la maji.
Akizungumza jana mjini Tabora, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Kamishna Msaidizi Hamisi Selemani amesema katika tukio la Januari 28, mwaka huu katika Mtaa wa Stoo, Kata ya Igunga Mjini, mkazi wa Mtaa wa Masanga, Khalid Kassim (50) aliuawa na kundi la wananchi zaidi ya 100 ikidaiwa alifumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mtu.
Kamanda Selemani amefafanua kuwa Kassim alifumaniwa na mwenye mke, Muungano Isaack (44) mkazi wa Mtaa wa Stoo.
Amesema baada ya kumfumania, Isaack alipiga kelele kuomba msaada, ndipo wananchi walitoka kwa wingi na kumshambulia kwa kipigo Kassim.
Amebainisha kuwa polisi walipata taarifa na kufika katika mtaa huo na kukuta wananchi wakiwa wamekimbia, hivyo askari walimchukua mtuhumiwa na kumpeleka Hospitali ya Wilaya ya Igunga ambako aliaga dunia wakati akipatiwa matibabu.
Kamanda Selemani amesema katika tukio la pili lilitokea siku hiyo, katika Kijiji cha Mwazizi Kata ya Bukoko, watoto wawili wa familia moja, Gumba Ngasa (2) na Kija Ngasa (1) wote wa kike, walizama maji na kufariki dunia wakati wakivuka maji.
Kamanda amesema watu wawili, Muungano Isaack na Maria Joseph wanashikiliwa na Polisi huku wengine walioshiriki mauaji ya Kassim wanaendelea kutafutwa na jeshi hilo.
Ametoa mwito kwa wazazi kuwa makini na kipindi cha masika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Dk Godfrey Mgongo amesema uchunguzi wa awali unaonesha kifo cha Kassim kilisababishwa na kuvuja damu nyingi kichwani kutokana na majeraha aliyokuwa nayo.
Aidha, Dk Mgongo alibainisha kuwa vifo vya watoto wawili Gumba na Kija vilisababishwa na maji mengi waliyomeza baada ya kuzama.

Mcheza tenesi Roger Federer kutoka Switzerland, amefanikiwa kupata ushinda wa 18



Mcheza tenesi Roger Federer kutoka Switzerland,
 amefanikiwa kupata ushinda wa 18 wa Grand Slam kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano kwa kumshinda kwa seti tano mfululizo Rafael Nadal, katika fainali ya mashindano ya Australian Open.
Federer mwenye umri wa miaka 35 alishinda kwa seti 6-4 3-6 6-1 3-6 6-3 na kupata ushindi wake wa tano wa Melbourne.
Nadal mwenye umri wa miaka 30 yuko nafasi ya pili sawa na Pete Sampras.

Ushindi mkubwa wa mwisho wa Federer ulikuwa wa Wimbledon mwaka 2012.
“Nimekuwa nikija hapa kwa karibu miaka 20 sasa,”alisema. Nimekuwa nikifarahia na sasa familia yangu inafurahia pia.

watu mamilioni wako katika hatari ya kupoteza maisha



Umoja wa Mataifa umesema mamilioni ya watu wako katika hatari ya kupoteza maisha kutokana na athari za kiangazi na ukame nchini ETHIOPIA.

Mkuu wa Ofisi ya Msaada wa Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, STEPHEN O'BRIEN  amesema ukame huo umesababisha watu milioni 5.6 nchini ETHIOPIA kuhitaji msaada wa dharura

O'BRIEN amehadharisha kuwa iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa watu wengi watapoteza maisha kutokana na njaa kama ilivyokuwa mwaka jana.

Mkuu wa Kitengo cha Kukabiliana na Majanga nchini ETHIOPIA, MITIKU KASSA amesema nchi hiyo inahitaji msaada wa dola milioni 948 za Marekani ili iweze kukabiliana na hali ya ukame na baa la njaa.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Sudan imemuita mwanabalozi wa Marekani mjini Khartoum kupinga hatua ya Rais Donald Trump


Rais wa Sudan Omar Bashir

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Sudan imemuita mwanabalozi wa Marekani mjini Khartoum kupinga hatua ya Rais Donald Trump ya kuwapiga marufuku raia wa nchi hiyo kuingia Marekani.
Sudan inasema kuwa hatua hiyo ni ishara mbaya baada ya hatua nzuri za kuboresha uhusiano wa mataifa hayo mawili ikiwemo kupunguza vikwazo vya kiuchumi na ushirikiano katika vita dhidi ya Ugaidi.

Amri hiyo ya Trump ilitikiza mpango mzima ya wakimbizi wa Marekani baada ya kutangazwa marufuku ya siku 90 ya usafiri wa raia kutoka Somalia, Sudan, Libya, Syria, Iran, Iraq na Yemen

January 29, 2017

WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesisitiza kuwa suala la mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi limekwishatolewa taarifa


Image result for picha ya malawi

WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesisitiza kuwa suala la mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi limekwishatolewa taarifa na Wizara hivi karibuni na kwamba lipo chini ya Jopo la Usuluhishi linaloundwa na viongozi wastaafu wa Afrika kutoka nchi za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Wizara hiyo imefikia hatua ya kusisitiza hilo kutokana na baadhi ya vyombo vya habari hususani magazeti kupotosha lengo la mkutano wa wizara hiyo na waandishi wa habari uliofanyika Januari 26, mwaka huu.
Katika tarehe hiyo, wizara hiyo ilikutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa taarifa kwa umma kuhusu Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi ambao umepangwa kufanyika mjini Lilongwe, Malawi Febuari 3 hadi 5, mwaka huu.
Katika taarifa ya ufafanuzi jana, Wizara hiyo ilisema; “Hata hivyo, vyombo vingi vya habari hususan Magazeti ya tarehe 27 Januari, 2017 vimeandika kwamba Mkutano huo ni maalumu kwa ajili ya kujadili mgogoro wa Mpaka kati ya Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa pamoja na kesi ya Watanzania nane waliokamatwa kwa madai ya kuingia nchini Malawi bila kibali.
“Wizara inapenda kuchukua nafasi hii kutoa ufafanuzi kwamba, suala la mgogoro wa mpaka limekwishatolewa taarifa na Wizara hivi karibuni kwamba lipo chini ya Jopo la Usuluhishi linaloundwa na Viongozi Wastaafu. “Jopo hilo linaongozwa na Joachim Chissano, Rais Mstaafu wa Msumbiji akisaidiwa na Festus Mogae, Rais Mstaafu wa Botswana na Thabo Mbeki, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini.
“Aidha, kuhusu suala la Watanzania wanane waliokamatwa kwa madai ya kuingia nchini Malawi bila kibali lipo Mahakamani hivyo halitakuwa sehemu ya mazungumzo ya Mkutano wa Tume ya Pamoja.
Kwa mujibu wa Wizara hiyo, mantiki ya Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati Tanzania na Malawi ni njia mojawapo ya kuendelea kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Imesema mkutano huo ambao ni wa kawaida, una lengo la kujadili na kutathmini hatua zilizofikiwa katika utekelezwaji wa makubaliano yaliyofikiwa katika Mkutano wa Tatu wa JPCC uliofanyika nchini Juni 24 hadi 30, mwaka 2003.

Mwanamumenjia na kuendesha baiskeli siku 30


Image result for PICHA YA BAISKELI

Mwanamume mmoja nchini China ambaye alikuwa na matumaini ya kuendesha baiskeli hadi nyumbani kwao kusherehekea mwaka mpya, aligundua baada ya siku 30 kuwa alikuwa amepotea njia.
Mwanamume huyo alikuwa na matumaini ya kuwasil nyumbani kwao huko Qiqihar mkoa wa Heilongjian baada ya kuanzia safari yake huk Rizhao umbali wa kilomita 1,700.
Lakini alisimamishwa na polisi wa trafiki akiwa amepotea umbali wa kilomita 500 katika mkoa wa Anhui.
Wakati waligundua, polisi walimlipia tikiti ya treni ili arudi nyumbani.
Ripoti zinasema kwa mwanamume huyo alikuwa akilala maduka ya intaneti kwa sababu hakuwa na pesa.
Mwanamume huyo hakuwa na uwezo wa kusoma ramani na hivyo alikuwa akitegemea watu kumuelekeza.
Polisi walimsimamisha kwa sababu alikuwa akitumia barabara ambayo baiskeli haziruhisiwi kuitumia.
Baada ya kugundua makosa yake, polisi na watu wote waliokuwa kituoni ambapo alisimama walichanga pesa na kumnunulia tikiti ili asafiri nyumbani.