February 18, 2017

Hii ni kazi mpya ya TID akimshirikisha Fid Q iliyorekodiwa TID mwaka 2007.


Hii ni kazi mpya ya TID akimshirikisha Fid Q iliyorekodiwa TID mwaka 2007.
Wimbo huo ulirekodiwa mwaka 2007, siku tatu tu baada ya muimbaji huyo kutoka jela. Kutoka jela kwa muimbaji huyo kulitokana msamaha wa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete siku ya Uhuru.
Maisha ya Jela unazungumzia msoto ambao muimbaji huyo aliupata baada ya kufungwa jela. “TID ameelezea maumivu, maumivu ya moyo, kuchanganyikiwa, na bila kusahau mateso ya kiakili aliyoyapata akiwa jela kutokana na adhabu kali alizozipata baada ya hukumu hiyo,” yanasema maelezo.
Fid Q alikuwa mtu wa karibu na TID wakati wa kifungo na baada ya kutoka na alimwelezea namna wananchi walivyochukulia kufungwa kwake hivyo alikuwa mtu sahihi kushirikishwa kwenye wimbo huo ambao ulikuwa wazo na CEO wa Tongwe Records, J-Murder.
Hata hivyo licha ya wimbo huo kumalizika, haukuweza kutoka kipindi hicho kwasababu walitaka kwanza TID awe kwenye hali ya kawaida baada ya kutoka kifungon

Msanii Alikiba baada ya kufanya vizuri na wimbo wa “Aje”, ameachia rasmi Video mpya ya wimbo wa “Aje Remix

Msanii Alikiba baada ya kufanya vizuri na wimbo wa “Aje”, ameachia rasmi Video mpya ya wimbo wa “Aje Remix”, akiwa amemshirikisha msanii M.I kutoka Nigeria. Tazama hapa chini alafu toa komenti yako.

MKUU wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akishirikiana na kamati yake ya Ulinzi na Usalama wamefanikiwa kukamata kete 88 za dawa





MKUU wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akishirikiana na kamati yake ya Ulinzi na Usalama wamefanikiwa kukamata kete 88 za dawa za kulevya aina ya mirungi zilizokuwa zimefungwa kwa mtindo wa vifurushi kwa kutumia kamba za migomba.
Tukio hilo la kukamata dawa hizo limetokea katika kijiji cha Mzeri, kata ya Misima ambapo Gondwe alibainisha kuwa wilaya hiyo ina matumizi makubwa ya mirungi na bangi.
Imeelezwa kuwa dawa hizo zilikua zikisafirishwa kutoka Korogwe na kwamba mtuhumiwa alifanikiwa kuwatoroka polisi na jitihada za kumtafuta ili kumfikisha kwenye vyombo vya sheria zinaendelea.
“Vijana wetu wa upelelezi wamegundua utumiaji wa dawa hizo na tutahakikisha tunawafikisha kwenye vyombo vya sheria wauzaji na watumiaji wa dawa hizo,” alisema.
Aliongeza kuwa polisi inashirikiana na zimamoto na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kudhibiti kabisa biashara hiyo.
“Tumeunda timu ambayo mwenyekiti wake ni OCD itakayokuwa inafanya doria usiku na mchana ili kuhakikisha vijana wetu wanabaki salama na kukomesha kabisa biashara ya dawa za kulevya,” alisema.
Mkuu huyo wa wilaya alitoa wito kwa watumiaji na wauzaji wa dawa hizo kuacha mara moja badala yake wajikite kwenye shughuli nyingine halali zitakazoweza kuwainua kiuchumi.
“Jeshi la polisi halitaacha kuwafuatilia na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kwani Serikali wilayani Handeni haitakuwa tayari kuona nguvu kazi ya vijana inateketea,” alisema.
Baadhi ya vijana wilayani humo wameunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kupambana na dawa za kulevya na wamesema kuwa nguvu kazi ya vijana wengi imekuwa ikiteketea kutokana na utumiaji wa dawa hizo

SERIKALI imesema sekta ya habari inakabiliwa na changamoto katika uwasilishaji wa taarifa kwa umma




SERIKALI imesema sekta ya habari inakabiliwa na changamoto katika uwasilishaji wa taarifa kwa umma kunakotokana na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia hivyo kuwataka wadau kujitahidi kwenda na wakati hasa kwa upande wa redio ili wasipitwe na wakati.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mwanzoni mwa wiki katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya habari nchini.
Alisema kuwa wakati umefika kwa wadau wa sekta ya habari kufikiri kwa kina namna ya kuhabarisha umma kwa kuangalia namna ya uwasilishaji ambapo kwa sasa changamoto kubwa ni kasi ya ukuaji wa teknolojia ya habari na namna ambapo redio zinaweza kushindana na vyombo vingine.
Alisema kwa wanahabari wanapaswa kuwa makini na taarifa wazitoazo kwa jamii kwani kumekuwa na mazoea ya baadhi yao kuripoti habari bila kufanya uchuinguzi wa kina huku wakitumia chanzo kimoja cha habari badala ya kujiuliza maswali mengi ili kupata taarifa sahihi.
Akizungumzia urasimu wa upatikanaiji wa habari mikoani, wilayani na wizarani alisema kuwa Sheria ya Habari imempa nguvu Mkurugenzi wa Habari Maelezo amabaye ndiye msemaji mkuu wa serikali awajibike kutoa habari za serikali.
Alisema kuwa kwa kipindi cha nyuma maofisa habari walikuwa hawahudhurii kwenye vikao muhimu vya maamuzi, hivyo kutokuwa na taarifa sahihi. Alisema kuwa kama waziri mwenye dhamana na wizara hiyo lengo la serikali ni kuhakikisha kunakuwa na mazingira wezeshi kwa ukuaji wa tasnia ya habari hata kama ni kwa kubadilisha sheria inayobana uhuru wa habari.
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania-COMNETA, Prosper Kwizige alisema kuwa ipo changamoto kwa baadhi ya maafisa habari mikoani na wilayani kuleta urasimu mkubwa katika utoaji wa taarifa zinazohitajika kwa waandishi wa habari hivyo kukwamisha upatikanaji wa habri kwa umma.
Kwa upande wake, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dk Edefonce Nfuka alisema kuwa maadhimisho hayo yamekuwa jukwaa muafaka kwa wadau wa sekta hiyo kutoa mrejesho wa wahitimu kutoka kwenye vyuo hapa nchini na hivyo kusaidia katika uboreshaji wa mitaala ili kuwa na wahitimu mahiri kwenye sekta hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk Ayubu Rioba alisema kuwa kwa siku za nyuma redio ilikuwa ni chombo cha kuaminika katika utoaji wa habari hivyo kujijengea umaarufu na kuaminika zaidi tofauti na ilivyo sasa ambapo kun

Baadhi ya wafanyabiashara wadogowadogo wamachinga walioko maeneo ya ya makoroboi mkoani mwanza leo wameleta mzozo

Image result for PICHA YA MACHINGA MKOANI MWANZA                                           
 Baadhi ya wafanyabiashara  wadogowadogo wamachinga walioko maeneo ya  ya makoroboi mkoani mwanza leo  wameleta mzozo mkubwa baada  ya  kupanga bidhaa zao mbele ya maduka  ya wafanyabiashara    

Hayo yametokea leo mkoani mwanza  baada ya mgambo kuwafukuza wamachinga ambao hawatakiwi  wanaofanya biashara zao  pembezoni mwa barabara  na kuwaamuru waende maeneo ambayo ni makoroboi, Tanganyika basi na sahara.



Wakizungumza na wakati wa ufukuzwaji wa wafanyabiashara hao,  baadhi ya wafanyabiashara wa maduka wamesema wamevamiwa maeneo yao  hivyo kuziba njia na wateja  huku awali gari la matangazo lilipita kuwapa taarifa wamachinga watoke kwenye maeneo ambayo hayatakiwi
wafanyabiashara wa maduka…

Nao wamanchinga hawakuwa nyuma  wamesema  hawakubainisha   maeneo ambayo wanatakiwa kwende   richa yakuwa taarifa walipewa kwa njia  ya tangazo
Cast……wamanchinga…..14/2/2017…ed……

Aidha mwenyekiti wa wamanchinga mkoani mwanza said tyembo amesema kuhusu zoezi hilo la kuondolewa kwa baadhi ya wamanchi  awali  walikaaa kikao na uongonzi wa halimashauri ya jiji 4/1/2017 na kupendekeza barabara mbili zifungwe  kwaajiri kuwaweka  wamachinga hao  lakini taarifa hiyo hazikupitishwa rasmi

Cast … mwenyekit….14/2/2017 

imeandikwa na mwandishi wa KALI ZOTE Na James Timber KUTOKA Mwanza 

ZIFAHAMU FAIDA 5 ZA KUNUNIANA NA MPENZI WAKO


Image result for faida ya kuwa na mpenzi

Mapenzi yana wigo mpana mno ambao mtu anapaswa kuuangalia kwa jicho pana na akili pembuzi kabla ya kuingia, namaanisha kwamba ni lazima kuchunguza kina cha maji kabla ya kuzamia. Sasa basi, zifuatazo ni faida tano utakazozipata ukiwa umenuniana na mpenzi wako. 


HUSAIDIA KUPUNGUZA MIGOGORO

Image result for faida ya kuwa na mpenzi



Ni ukweli usiopingika kuwa, katika hali ya kawaida, ukiwa mbali na mtu fulani katika jamii unayoishi ni vigumu sana kujikuta umekwaruzana naye. Hii ni kwasababu utakuwa hauingiliani naye katika mizunguko yako, vivyo hivyo kwa wapenzi walionuniana. 

Hali hii hupunguza kabisa migogoro ya hapa na pale, kwani hiki ni kipindi ambacho mtakuwa mbalimbali jambo ambalo huepusha maudhi ya kibinadamu. 

Mfano, yawezakana katika kipindi mlichonuniana na mpenzi wako, uliingia ujumbe wa mapenzi kwenye simu yake kutoka kwa mtu aliyekosea namba. Kwa kuwa hauko naye karibu jambo hili halitakuumiza maana hutaelewa nini kimeendelea tofauti na kama ungelikuwa naye karibu. 

Kwa hiyo kuna baadhi ya maumivu na maudhi ambayo utaepukana nayo kwa kipindi cha kununiana kwenu. Ni kweli kabisa kwamba hupunguza migogoro na mitafaruku ya hapa na pale, umeelewa mpenzi msomaji wangu? Haya twende kwenye faida ya pili. 

KUBAINI TABIA X ZA MWENZAKO
Image result for faida ya kuwa na mpenzi


Hiki ni kipindi ambacho sasa kitakusaidia wewe kubaini tabia na mienendo mibaya ya mwenzi wako. Hii ni kwa kuwa utakuwa mbali naye hivyo naye hujiona kuwa yuko huru kufanya jambo lolote analoona kuwa linafaa bila kujali uwepo wako kwani kila mtu hana ‘time’ na mwenzake. 

Kama kuna asili ya maisha yake ambayo aliiacha baada ya kuingia katika uhusiano na wewe, ambayo ni mbaya zaidi sasa hapa ataanza kuirudia kwa kujiona kuwa hana mtu wa kumzuia na kumbana. 

Kama ni mlevi kupindukia, mchafu, muongo na tabia nyingine mbaya za kufanana na hizi basi ataanza kuzionesha katika kipindi ambacho mmenuniana. 

KUPATA MUDA WA KUTAFAKARI ZAIDI

Image result for faida ya kuwa na mpenzi



Hapa naomba nieleweke vizuri kabisa kwamba, ninapoongelea suala la kutafakari zaidi katika kipindi ambacho wewe hauna maelewano mazuri na mwenzi wako, namaanisha kuwa utapata muda mzuri zaidi wa kutafakari penzi lenu kwa ujumla. 

Ni kipindi kitachokuongoza wewe kuwa na uelewa wa ni aina gani ya mpenzi uliyenaye. Kivipi? Ni kwamba, katika muda huu mara nyingi utataka kupata suluhu ya kununiana kwenu, lakini pia katika kutafuta suluhu hiyo utapata fursa ya kutafakari kwa kina juu ya penzi lenu huku ukimpima mwezi wako kwa mtazamo chanya. 

KUFAHAMU AINA YA MARAFIKI ZAKE

Image result for faida ya kuwa na mpenzi



Si kila rafiki wa mwenza wako ana nia nzuri na uhusiano wenu au anafurahia penzi lenu. Mathalani, labda wewe ni msichana na pengine miongoni mwa rafiki zake kuna mmoja au wawili ambao hutamani sana kupata penzi lako. 

Sasa katika kipindi ambacho utakuwa umenuniana na mpenzi wako basi itakuwa ni nafasi nzuri kwao kuitumia kunyunyizia sumu ya kumponda huku wakikutamkia maneno ya kukushawishi, hivyo utakuwa umeelewa ni aina gani ya marafiki alionao mwenzi wako. 

Hii si kwa msichana tu, hata kwa wanamume kwani huenda kati ya rafiki wa ‘girlfriend’ wako, kuna wanaokutamani, sasa wakiona huna uhusiano mzuri na mpenzi wako, watatumia nafasi hii kukuambia maneno ya uongo juu yake na kukuonesha kila dalili za kukutaka.

Hivyo utakuwa umefahamu ni aina gani ya rafiki ambao mpenzi wako anao. Tambua kwamba, marafiki wengi wana tabia zinazofanana. 

KUBAINI AINA YA PENZI ALILONALO KWAKO


Image result for faida ya kuwa na mpenzi



Katika kipindi hiki, utaweza kuelewa ni aina gani ya penzi alilonalo huyo mtu wako juu yako. Kwa mpenzi aliye na hisia za dhati kabisa kwako, katika kipindi hiki atakuwa ni mtu wa kutafuta njia ya kupata suluhu ya tatizo lenu. 

Pamoja na kwamba wewe utakuwa umenuna, bado yeye ataonesha kukujali kama kawaida, atakupigia simu za hapa na pale yaani ilimradi tu asikie angalau sauti yako, lengo lake likiwa ni kutaka kurejesha ukaribu ambao sasa anaona kama akiupoteza itakuwa ni maumivu kwake. 

Kwa mantiki hiyo basi, utagundua ni kwa jinsi gani anathamini penzi lenu na ni aina gani ya penzi alilonalo kwako. Yote haya utabahatika kuyajua kupitia kipindi cha kununiana kwenu. 

Hata hivyo, niwatahadharishe kwamba, kuandika haya isiwe ni tiketi ya wewe sasa kuanza kununiana na mpenzi wako eti kwa kigezo kwamba utapata nafasi ya kumfahamu, la hasha!
Siku zote katika uhusiano wako epuka maudhi na migogoro isiyokuwa ya lazima

madawa ya kulevya yagunduliwa mpakani Marekani

Manati
Maafisa wa Marekani wanaoshika doria mpakani, wamegundua manati kubwa ambayo ilikuwa imefungamanishwa na ua ulio kwenye mpaka wa taifa hilo na Mexico.
Manati hiyo inaonekana kuundwa mahsusi kwa ajili ya kurusha dawa za kulevya hadi Marekani.
Marekani imekuwa ikikabiliana sana na walanguzi wa mihadarati kutoka Mexico pamoja na wahamiaji.
Rais Donald Trump ameahidi kujenga ukuta mrefu sana kuzuia hilo.
Manati hiyo kubwa iligunduliwa na maafisa kusini mashariki mwa Tucson, Arizona, wiki iliyopita.
Wanasema waliwaona wanaume kadha wakitawanyika na kutoroka walipogundua kwamba maafisa hao walikuwa wanafika.
Maafisa hao walipokagua eneo hilo, waligundua vifurushi viwili vya bangi, vilivyokuwa na bangi ya jumla ya kilo 21.
Vifurushi hivyo vilikuwa bado havijarushwa.
Manati hiyo ambayo ilikuwa imejengwa upande wa Mexico wa ua ilibomolewa.
Hakuna aliyekamatwa kuhusiana na kisa hicho.

ManatiHaki miliki ya pichaUSBP
Image captionManati hiyo ilikuwa imeunganishwa na ua

Takriban umbali wa maili 650 kati ya maili 1,100 (1,770km) za mpaka wa Mexico na Marekani tayari kumejengwa ua au ukuta.
Trump ameahidi kujenga ukuta mrefu lakini walanguzi wamekuwa wakitumia ubunifu katika kutumia njia za kufikisha madawa Marekani.
Miongoni mwa njia hizi ni kutumia ndege ndogo zisizo na marubani na wakati mwingine kuchimba njia za chini kwa chini zinazofika hadi Marekani.
Mwezi Machi, maafisa waligundua njia ya chini kwa chini ya umbali wa mita 380 ambayo ilikuwa imetoka kwenye mgahawa mmoja Mexico hadi kwenye jumba moja California.

chanzo bbc

huenda simu muundo wa Nokia 3310 zikazinduliwa upya na kuanza kuuzwa tena baadaye mwezi huu.

Nokia 5110
Kuna taarifa kwamba huenda simu muundo wa Nokia 3310 zikazinduliwa upya na kuanza kuuzwa tena baadaye mwezi huu.
Kampuni ya HMD Global Oy ya Finland, ambayo ina haki za kuunda bidhaa za nembo ya Nokia ndiyo inayodaiwa kuwa na mipango hiyo.
Simu hizo inaarifiwa zitazinduliwa wakati wa Kongamano la Simu za Rununu Duniani baadaye mwezi huu.
Kampuni ya Nokia ilinunuliwa na Microsoft mwaka 2013.
Simu asilia za Nokia 3310 zilipata umaarufu kutokana na uthabiti wake.
Nokia 3310/3330, zilizinduliwa 2000, na ni miongoni mwa simu zilizouzwa sana duniani. Jumla ya simu 126 milioni za aina hiyo zilitengenezwa na Nokia.
Una kumbukumbu za simu hiyo?
Dave Mitchell nchini Uingereza anaamini kwamba anamiliki moja ya simu za zamani zaidi aina ya Nokia 3310 nchini Uingereza.
Alinunua simu hiyo mwaka 2000 na anasema amekuwa akiitumia tangu wakati huo - bila natatizo yoyote.
Mwanajeshi huyo wa zamani anasema simu hiyo imewahi kufuliwa pamoja na nguo kwenye mashine, ikakanyagwa na hata kutumbukia kwenye mchuzi.
Anasema huwa inamhitaji kuweka chaji baada ya siku kumi.
Bado ina betri yake asili.
"Nilinunua simu hii zaidi ya miaka 17 iliyopita na sijawahi kubadilisha chochote. Sijui ni watu wangapi wenye simu za kisasa wanaweza kusema hayo."

Historia ya simu za Nokia


Nokia 1011Haki miliki ya pichaNOKIA
Image captionSimu hii ya Nokia 1011 iliyozinduliwa mwaka 1992 iliyokuwa na uzani wa nusu kilo (gramu 495/1.1lb), ilikuwa ya kwanza ya GSM kuuzwa sana
Nokia 5110Haki miliki ya pichaNOKIA
Image captionNokia aina ya 5110 ambazo ungebadilisha sehemu ya juu
Nokia 8210Haki miliki ya pichaNOKIA
Image captionNokia 8210 ambayo ilikuwa nyepesi zaidi mwaka 1990. Ilikuwa na uzani wa gramu 79
3330 Nokia phoneHaki miliki ya pichaNOKIA
Image captionNokia 3310/3330, zilizinduliwa 2000, na ni miongoni mwa simu zilizouzwa sana duniani. Jumla ya simu 126 milioni za aina hiyo zilitengenezwa na Nokia.
Nokia 3650Haki miliki ya pichaNOKIA
Image captionMajaribio ya kwanza kabisa ya simu aina ya smartphone ilikuwa Nokia 3650 iliyozinduliwa 2002. Ilitumia mfumo endeshi wa Symbian Series 60, lakini haikuvuma sana kutokana na kipadi yake
Nokia 7600Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMoja ya simu za kwanza za Nokia za 3G, Nokia 7600 ilizinduliwa 2003. Ilikuwa sehemu ya msururu wa simu za "Mitindo". Haikuvutia watu wengi.
Nokia N-GageHaki miliki ya pichaNOKIA
Image captionNokia ilizindua pia N-Gage mwaka 2003, ambayo ni mashine ya kucheza michezo ya kompyuta na simu. Haikuvutia watu wengi.

Magazeti ya Tanzania February 18, 2017 kuanzia, Udaku, Hardnews na michezo



MAGAZETI

on
Good Morning mtu wa nguvu, leo ni February 18 2017 na kama ilivyo kawaida yangu ya kila siku alfajiri nimekusogezea habari kubwa kwenye Magazeti kurasa za mwanzo na mwisho kuanzia ya UdakuHardnews na Michezo ili uje kinachoendelea Mtu wangu usiache kukaa karibu yangu kwenye Facebook, Twitter na Instagrams sylas denniss ili niwe nakutumia kila kinachonifikia