April 30, 2017

Aliyekuwa na uzani wa kilo 500 apungua hadi kilo 174

Eman Abd El Aty adaiwa kupunguza uzani kutoka kilo 500 hadi 174 na sasa atasafrishwa hadi UAE

 


Mwanamke aliyekuwa na uzani mzito zaidi duniani atasafirishwa hadi katika milki za kiarabu UAE baada ya mzozo kuhusu uzani wake katika hospitali ya India ambapo alikuwa akipatiwa matibabu.
Hospitali ya Saifee mjini Mumbai ilisema kuwa Eman Abd El Aty alifanyiwa upasuaji wa kupunguza uzani na sasa alikuwa huru kuondoka kwa sababu ana uzani wa kilo 172 kutoka kilo 500 alizokuwa nazo awali.
Lakini dadake alimshutumu daktari wa upasuaji huo kwa kudanganya na kumuomba amruhusu dadake aendelee kukaa katika hospitali hiyo.
Kwa sasa ataelekea katika hospitali ya Burjeel huko Abu Dhabi.
Taarifa iliotolewa na daktari wa bi Abd El Aty imesema kuwa atapatiwa matibabu muhimu kwa kuwa hospitali hiyo iko karibu na nyumbani.

Hospitali ya Saifee imeongezea kwamba ilikuwa fahari kwa juhudi zilizofanywa na kundi la madaktari wake ikidai kuwa mgonjwa huyo aliwasili kupitia ndege ya kubebea mizigo na sasa anarudi kama abiri katika ndege ya watu.

Mapema hospitali hiyo ilikuwa imepinga madai kwamba dadake El Aty, Shaimaa Selim ambaye alitoa kanda fupi ya video katika mitandao ya kijamii akidai kwamba dadake aliyekuwa hawezi kuzungumza ama hata kutembea hajapunguza uzani mkubwa kama hospitali hiyo inavyodai.
Daktari wa upasuaji wa watu walionenepa kupitia kiasi Muffi Lakdawala pia alikana madai hayo katika mtandao wa Twitter.

Ujerumani, Poland na England zajiimarisha


Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Löw alikamilisha kazi yake baada ya mabingwa hao wa dunia kupata ushindi wa tano kwenye mechi tano katika Kundi lao la kufuzu Kombe la Dunia.

Ushindi wao wa 4-1 dhidi ya Azerbaijan mjini Baku ulikuwa suala rahisi tu kwa Wajerumani ambao walifungwa bao lao la kwanza kabisa katika Kundi C. Ujerumani wanaongoza kileleni na pengo la pointi tano dhidi ya Ireland ya Kaskazini ambayo iliizaba Norway 2-0. Nayo Jamhuri ya Czech iliizaba San Marino 6-0. Kocha Löw alielezea kuridhika kwake na matokeo hayo
Kundi F
Fußball WM-Qualifikationsspiel Polen vs. Dänemark in Warschau (Reuters/Agencja K. Atys) Poland wako katika nafasi nzuri ya kufuzu
Uwanjani Wembley, England ilipambana na kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Lithuania. Ni mechi ambayo mshambuliaji Jermain Defoe mwenye umri wa miaka 34 alirejeshwa kikosini na akafunga bao lake la 20 la kimataifa. England sasa imejiimarisha kileleni mwa Kundi F. Vijana hao wa kocha Garry Southgate sasa ndio timu pekee ya Ulaya ambayo haijafungwa bao hata moja kufikia sasa. England wana pointi 13, nne mbele ya Slovakia ambao walisonga katika nafasi ya pili ya kundi hilo kwa kupata ushindi wa 3-1 dhidi ya Malta. Scotland wako nyuma na pengo la pointi sita baada ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Slovenia.
Katika Kundi E, nahodha wa Poland Robert Lewandowski alifunga bao katika mechi ya kumi mfululizo na kuiweka kileleni timu yake kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Montenegro. Montenegro sasa iko na pointi saba sawa na Denmark baada ya Wadenmark kutoka sare tasa na Romania, ambayo ina pointi sawa na Armenia. Armenia iliifunga Kazakhstan 2-0 na kuyaweka hai matumaini ya kucheza mechi za mchujo.

Kocha wa uholanzi atimuliwa
Fußball UEFA EURO 2016 Qualifikation Türkei - Niederlande Danny Blind (picture-alliance/dpa/T. Bozoglu) Danny Blind amepigwa kalamu baada ya kichapo dhidi ya Bulgaria
Wakati huo huo, Kocha wa Uholanzi Danny Blind ameüigwa kalamu, ikiwa ni chini ya saa 24 tu baada ya kichapo cha 2-0 dhidi ya Bulgaria kuiacha timu yake katika nafasi ya nne ya Kundi A la kufuzu katika dimba la Kombe la Dunia. Shirikisho la kandanda la Uholanzi lilitangaza uamuzi huo kupitia taarifa baada ya Blind, kuitwa kwa ajili ya mazungumzo ya dharura.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 amelalamikia uamuzi huo akisema kuwa timu yake ilikuwa kwenye mkondo sahihi na kichapo cha Bulgaria kilikuwa ni pigo. Timu ya taifa ya Uholanzi imekuwa ikiyumba tangu ilipokosa kushiriki dimba la Ubingwa wa Ulaya 2016 hasa ikizingatiwa kuwa miaka miwili kabla, ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye dimba la Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil. Jean Paul Decossau ni mkurugenzi wa shirikisho la soka la Uholanzi na hapa anaelezea kilichojiri

Kichapo hicho kimeiacha Uholanzi ikikabiliwa na mtihani mkubwa wa kumaliza katika mojawapo ya nafasi mbili za kwanza za kufuzu katika Kundi A. Ina pointi saba baada ya kucheza mechi tano na wako nyuma ya vinara Ufaransa ambao wana pointi 13, Sweden ina 10 na Bulgaria ina 9. Kocha msaidizi  Fred Grim atachukua usukani katika mchuano wa kirafiki kesho dhidi ya Italia mjini Amsterdam wakati kocha mpya akitafutwa.

Kuondoka kwa Zuma, kutaleta mabadiliko Afrika Kusini?


Maelfu ya raia wa Afrika Kusini wamekuwa wakiandamana kwa lengo moja: kumuondoa madarakani Rais Jacob Zuma. Lakini kuondolewa kwa Zuma kweli kunaweza kutatua matataizo yote ya nchini humo
Maelfu ya raia wa Afrika Kusini wakiwa wanaandamani kumshinikiza Rais Jacob Zuma kuachia madaraka, inaleta picha kama vile Zuma ndiyo kikwazo pekee kinacholizuia taifa hilo kusonga mbele.
"Zuma lazima aanguke" umekuwa wito maarufu tokea kulipoanza maandamano dhidi ya rushwa na ukosefu wa ajira mwaka 2015. Hata wanachama wengi wa chama chake cha African National Congress (ANC) wamembandilikia Zuma.

Kumuondoa Zuma hata hivyo, huenda lisiwe suluhisho la matatizo yote yanayolikabili taifa hilo kwa mujibu wa wachambuzi.
Chama cha ANC kimejaa wanasiasa wenye mitazamo sawa na Zuma, na matatizo ya kiuchumi ya Afrika Kusini yameingiliana sana na ukosefu wa usawa uliorithiwa tokea wakati wa ubaguzi wa rangi, kiasi ya kwamba hata Zuma akiondolewa madarakani, huenda hatua hiyo isilete mabadiliko makubwa nchini humo.
Sifa ya Zuma imechafuka kutokana na msururu wa kashfa za rushwa, ikiwa ni pamoja na ile inayohusu utumiaji wa fedha za kodi ya umma kuifanyika marekebisho nyumba yake binafsi, na mafungamano ya karibu na familia ya kibiashara na yenye ushawishi mkubwa.

Wakati huo huo mamilioni ya Waafrika Kusini wanaishi makaazi yasiyo halali, na bila ya huduma za msingi, huku ukuaji wa uchumi ukiwa unazorota hadi kufikia asilimia 0.3 mwaka jana na zaidi ya robo ya idadi yote ya watu nchini humo imekosa ajira.

Ongezeko la vimbunga kanda ya Sahar


Kanda ya jangwa la Sahel barani Afrika imeshuhudia ongezeko la mara tatu la vimbunga vya mvua vinanoleta taabu na uharibifu mkubwa badala ya kuleta manufaa tangu 1982.
Kanda ya jangwa la Sahel barani Afrika imeshuhudia ongezeko la mara tatu la vimbunga vya mvua vinanoleta taabu na uharibifu mkubwa badala ya kuleta manufaa tangu 1982. Hayo ni kwa mujibu wa utafiti juu ya mabadiliko ya tabia nchi uliotangazwa hapo siku ya Jumatano 26.04.2017. Wataalamu waliofanya utafiti huo wamesema iwapo hali ya kuongezeka kwa joto duniani haitatafutiwa ufumbuzi basi maeneo mengi katika kanda ya jangwa la Sahel yatakabiliwa na mvua kubwa kupita kiasi na mara kwa mara maeneo hayo yatakumbwa na mafuriko. Christopher Taylor mtaalamu wa maswala ya hali ya  hewa amesema nchi ambazo zina upungufu wa miundombinu hazitaweza kupambana na athari hiyo. Taylor na timu yake walifanya uchunguzi wa mawingu  kwa kutumia mitambo ya satellite mnamo mwaka wa1982-2016 ambapo walifuatilia  mageuzi ya ruwaza ya dhoruba katika eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara, ikiwa ni pamoja maeneo ya, Mauritania, Mali, Burkina Faso, Niger, Nigeria, Chad, Sudan na Senegal.

April 29, 2017

Bayern yapaa juu, Leipzig yayumba



Tunaanza na Bundesliga ambapo Bayern Munich waliupanua uongozi wao kileleni mwa ligi kuu hadi pointi tatu baada ya Thomas Muller kufunga goli pekee katika ushindi wao wa 1-0 dhidi ya wenyeji Borussia Moenchengladbach

Ni ushindi wa sita mfululizo kwa Bayern katika mashindano yote ambapo walionekana kuutawala mchezo kwa asilimia 70. Lilikuwa bao la pili la Muller msimu huu na lake la kwanza tangu desemba mwaka jana lakini amegeuka kuwa mtoa pasi 11 zilizopelekea kufungwa mabao. Huyu hapa Mueller "Inafuahisha sana kwamba tumeshinda. Pia nimeweza kufunga bao, hiyo bila shaka inafurahisha. Tumeburudika. Ulikuwa mchuano mkali. Kwa hivyo leo jumapili jioni ntakuwa hoi. Watu wengine watakuwa katika hali ya kutulia. Bila shaka lazima tukutane".
Wenyeji Gladbach, wameteremka hadi nafasi ya 10 baada ya kichapo hicho. Mapema jana, Schalke 04 ilipanda nafasi mbili juu hadi ya tisa baada ya kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Mainz. Sead Kolasinac alipachika wavuni bao hilo la ushindi. "Tulijitahidi sana kusogea nafasi za Europa League na kushinda mechi ya Bundesliga kabla ya kujiunga na timu ya taifa. Sasa tunaweza kujiunga na timu ya taifa kwa mechi za kimataifa bila shinikizo kabla ya kuendelea katika wiki mbili zijazo".
Deutschland Borussia Mönchengladbach v Bayern München (Reuters/T. Schmuelgen) Thomas Müller alifunga bao lake la pili msimu huu
Nambari mbili kwenye ligi RB Leipzig waliendelea kusambaratika baada ya kufungwa 3-0 na Werder Bremen siku ya Jumamosi. Kocha Ralph Hassenhtul amesema ni vyema kukitumia kipindi kinachoanza wiki hii cha michezo ya kimataifa kujinoa makali kabla ya kuanza kupambana katika mkondo wa mwisho wa ligi. Kichapo hicho kimewaacha katika nafasi ya pili na pointi 49, ikiwa na tofauti ya pointi tatu mbele ya Dortmund
Wakati huo huo Cologne waliimarisha nafasi zao za kucheza kandanda la Ulaya msimu ujao baada ya kuwamiminia mabao manne kwa mawili Hertha Berlin wanaoshikilia nafasi ya pili. Peter Stöger ni kocha wa Köln "Nna furaha kubwa sana kwamba tumecheza vizuri sana dhidi ya mpinzani mkali kabisa ambaye kila mara alikuwa hatari sana. Tulikuwa na nafasi ambazo tungeweza kufunga mabao zaid. Tumeona tulichotaka, kuwa wajasiri na matumaini ndani yetu na kushiriki kikamilifu katika mchezo huo na kujaribu kujikinga. Tulitekeleza vyema kile tulichozungumza".
Mambo hayawaendei vyema vijana wa Leipzig
Ni mechi iliyokuwa muhimu sana kwa mshambuliaji Anthony Modeste aliyetikisa nyavu mara tatu.
Modeste sasa ana mabao 22 nyuma ya Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang ambaye alifunga bao lake la 23 katika ushindi wao wa Ijumaa usiku wa 1-0 dhidi ya Ingolstadt. Robert Lewandowski ni wa tatu akiwa na mabao 21.
Wolfsburg waliwafunga washika mkia Darmstadt 1-0 wakati nambari nne Hoffenheim walipata ushindi wa 1-0 na sasa wako nyuma ya nambari tatu Borussia Dortmund na tofauti ya pointi moja pekee. Julian Nagelsmann ni kocha wa Hoffenheim "Leverkusen ina timu nziri sana, yenye wachezaji wa bei ghali na hivyo bado hawajatimiza matarajio yao. Lakini bado ni timu kubwa katika Bundesliga. Na hilo pia nimewaambia wachezaji wangu na mtu anaweza kuona. Katika kipindi cha kwanza tulikuwa ovyo  na mchezo wetu haukuwa sawa. Katika kipindi cha pili, tulijipanga vyema na tukapata bao safi"

Vita vya juu ya eneo la kushushwa ngazi vimepamba moto ambapo timu nne zina pointi 29. Timu hizi ni Mainz, Werder, Augsburg na Wolfsburg. Hamburg ni ya tatu kutoka nafasi ya mkia. Ingosltadt na Darmstadt  sasa zinakodolea macho shoka la kushushwa ngazi huku zikiwa zimesalia mechi 9 msimu kukamilika.

Kocha wa Bayern Münich Carlo Ancelotti amesisitiza ameweka fahamu zake katika kumaliza kazi ya kushinda taji la Bundesliga,


Kocha wa Bayern Münich Carlo Ancelotti amesisitiza ameweka fahamu zake katika kumaliza kazi ya kushinda taji la Bundesliga, kabla kuangalia ufanisi wa jumla alioupata katika msimu wake wa kwanza katika klabu hiyo



Hii ni kufuatia kule kushindwa nyumbani kwao Allianz Arena katika nusu fainali ya kombe la Ujerumani na mahasimu wao Borussia Dortmund BVB usiku wa Jumatano.
Mabingwa hao wa Ujerumani walikuwa kifua mbele 2-1 kabla Dortmund kuwashangaza kwa kutoka nyuma na kutwaa ushindi wa 3-2. Haya yote yanakuja wiki moja tu baada ya hao the Bavarias, kubanduliwa kutoka kwenye ligi ya mabingwa barani Ulaya na Real Madrid.
Bayern lakini bado wanaweza kulishinda taji la ligi kuu ya Ujerumani, Bundesliga, kwa mara ya tano mfululizo na ndilo jambo lililomfanya Ancelotti kukataa kuzungumzia ufanisi wake msimu huu, kwa sababu bado kuna mechi nne za ligi zilizosalia na wamebakisha pointi tano waweze kutawazwa mabingwa.
Hakuna wasiwasi wa kuachishwa kazi Ancelotti
"Ni mapema sana kwa hilo," alisema Ancelotti. "Tunastahili kuweka mambo wazi katika ligi kuu sasa haraka iwezekanavyo."
Deutschland DFB-Pokal Halbfinale Bayern München vs. Borussia Dortmund (Reuters/K. Pfaffenbach) Javi Martinez baada ya kuwafungia Bayern Munich goli la kusawazisha
Kwa sasa hakuna wasiwasi wa kuachishwa kazi kwa Ancelotti, ingawa hajapata ufanisi mkubwa katika msimu wake wa kwanza, akilinganishwa na mtangulizi wake Pep Guardiola aliyehamia Manchester City. Guardiola aliifikisha Bayern Munich katika nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya na akashinda Bundesliga na kombe la shirikisho la Ujerumani, DFB Pokal, katika msimu wake wa kwanza.
Javi Martinez na Mats Hummels walikuwa wamefunga magoli mawili katika kipindi cha kwanza na kulifuta lile la mapema lililowapa Dortmund uongozi na ambalo lilitiwa kimyani na Marco Reus.
Dortmund walizinduka kipindi cha pili na kupata ushindi
Lakini katika kipindi cha pili, BVB walizinduka kutoka kwenye kile kichapo cha 4-1 walichopewa na hao wapinzani wao hapo Allianz Arena wiki tatu zilizopita katika mechi ya ligi. Pierre-Emerick Aubameyang alifunga goli lake la 35 la msimu baada ya kuandaliwa na Ousmane Dembele, kabla chipukizi huyo kutoka Ufaransa, kufunga goli la tatu na la ushindi la Dortmund, dakika 16 kabla mechi kukamilika.
Deutschland DFB-Pokal Halbfinale FC Bayern München - Borussia Dortmund (Reuters/M. Dalder) Ousmane Dembele baada ya kufunga goli la tatu la Borussia Dortmund
Nahodha wa Bayern Philip Lahm atakayestaafu msimu utakapofikia kikomo alisema, "Tumeshushwa mabega pakubwa, tulitaka kufika fainali. Tunapokuwa tunaongoza mechi, inastahili kuwa vigumu kutushinda."

Bayern wanaweza kushinda taji la Bundesliga, iwapo Leipzig watashindwa kuwalaza FC Ingolstadt wanaoshikilia nafasi ya 17 na ambao wanapambana wasishushwe daraja. Ingolstadt ilikuwa timu ya kwanza kuifunga Leipzig katika mkumbo wa kwanza wa ligi kuu ya Ujerumani msimu huu na kiungo wao Alfredo Morales ameuambia wavuti wa klabu hiyo kwamba, iwapo wanataka kuwafunga tena, ni sharti wajizatiti sana.

vita vya Korea Kaskazini vyanukia


Marekani ikiionya Korea Kaskazini kutoijaribu Kijeshi,utawala wa Korea Kaskazini nao unajibu mapigo kwa jeuri kubwa

Kuongezwa kwa wanajeshi, majibizano ya maneno ya vitisho na kitisho cha vita vya kinyuklia yanazidi kuongeza wasiwasi kaskazini mashariki mwa Asia.
Marekani, kwa upande mmoja, inaimarisha juhudi zake katika eneo la kimkakati na Korea Kaskazini haionekani kusalimu amri wakati diplomasia na juhudi za kuzuia shambulio la nyuklia zikigongana. Kimsingi kunashuhudiwa wingu zito limeifunika rasi hiyo ya Korea.
Ikiwa ni kauli za jeuri na  kujiamini zinazotolewa na serikali ya Korea Kaskazini au upepo wa kishindo unaovuma upande wa Trump au majaribio ya kawaida ya makombora na mazoezi ya kijeshi, yote yanasababisha wasiwasi kote ulimwenguni huku hali ikionesha dalili za mambo kuelekea kufikia katika kiwango kibaya.
Ubabe wa Marekani unapojaribiwa
Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence, alitowa hotuba yake wiki iliyopita akiwa katika ndege ya USS ambayo ilitumiwa na Ronald Reagan huko Japan na kusema kwamba upanga umeshawekwa tayari.
Kauli hiyo imeonekana moja kwa moja kulenga kuionya Korea Kaskazini kutothubutu kuijaribu Marekani kijeshi akiongeza kusema kwamba "Marekani itajibu kwa kutumia nguvu kubwa ikiwa itashambuliwa."
Siku chache baadaye, katika hatua za kujibu mazoezi ya kijeshi ya wanamaji kati ya Marekani na Japan, gazeti rasmi la serikali Korea Kaskazini la Rodong Sinmun likaandika kwamba vikosi vya kimapinduzi viko tayari kuizamisha meli ya kubeba ndege za kijeshi za Marekani inayoendeshwa kwa nguvu za kyuklia kwa kombora moja tu.
Na hiyo ni baada ya kuripotiwa kwamba meli hiyo ya Marekani ya kundi la USS Carl Vinson itatia nanga  katika bahari ya pwani ya Rasi ya Korea, Korea Kaskazini ilijibu kwa kusema kwamba kupelekwa kwa zana hizo ni kitendo cha hatari kabisa kinachofanywa na wale wanaopanga kuanzisha vita vya nyuklia.
Kikosi hicho cha Vinson kitaungana na USS Michigan, nyambizi iliyosheheni makombora aina ya 144 Tomahawk ambayo ilishawasili katika bandari ya Korea Kusini ya Busan tangu Jumanne wiki hii.
Hali isiyoweza kupuuzwa
Hata hivyo, hadi wakati huu wasiwasi uliopo haujafikia kiwango cha kubadili mambo yalivyo ingawa kuna kitisho kinachozidi kuongezeka katika kanda hiyo ambacho hakiwezi kupuuzwa.
Uwezo wa jeshi la Korea Kaskazini unazidi kuimarika na hakuna ishara yoyote inayoonesha kwamba utawala huo utabadili msimamo wake wa jazba na mabavu, ambao kimsingi unauona ni muhimu kwao na unaostahili kuwepo kwa ajili ya kuuwezesha  kuendelea kuwepo.
Wiki hii pia, nchi hiyo ilionesha nguvu zake za kijeshi wakati ikiadhimisha miaka 85 tangu kuasisiwa jeshi la nchi hiyo ambapo zana nzito nzito zilioneshwa.

Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini, KCNA, hilo lilikuwa ni tukio kubwa kuwahi kufanyika la maonesho ya nguvu za kijeshi likihusisha mizinga na makombora ya masafa marefu 300 pamoja na nyambizi zinazoweza kutumiwa katika kushambulia meli za kivita.

KCNA halikuishia hapo tu, bali lilikwenda mbali zaidi na kuandika kwamba mazoezi hayo ya kijeshi yameonesha ni kwa jinsi gani Korea Kaskazini ina uwezo wa kuwamiminia mvua ya makombora bila hesabu wale lililowaita ''mabeberu'' yaani Marekani na "wafuasi wao wachafu."
Mwandishi:Saumu Mwasimba/DW English
Mhariri: Mohammed Khelef

Korea kaskazini yaendelea na ukaidi yafyatua kombora jingine

Korea kaskazini yaendelea na ukaidi yafyatua kombora jingine

Korea kaskazini imefanya jaribio la kombora leo Jumamosi(29.04.2017)Korea ya kusini na jeshi la Marekani zimesema,ikikaidi onyo la Marekani na,China, zilizojaribu kwa miaka kadhaa kudhibiti mpango wa silaha wa nchi hiyo.
Nordkorea provoziert mit weiterem Raketentest (Getty Images/AFP/Str.) Makombora ya Korea kaskazini yakifyatuliwa
Jaribio  hilo  lililofanywa  katika  eneo kaskazini mwa  mji  mkuu  wa Korea  kaskazini , Pyongyang, linaonekana  kuwa  limeshindwa, maafisa  wa  Marekani  na  Korea  kusini wamesema, katika  kile ambacho  ni jaribio  la  nne  mfululizo  la  Korea  kaskazini kushindwa  tangu  mwezi  Machi.
Jaribio  hilo linakuja  wakati  waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Marekani Rex Tillerson amelionya baraza  la  Usalama  la  Umoja  wa  Mataifa  kwamba  kushindwa  kuudhibiti mpango  wa  kinyuklia  na  makombora  wa  Korea  kaskazini  kunaweza  kusababisha "matokeo  mabaya".
UN Sicherheitsrat - US-Außenminister Rex Tillerson zu Nordkorea (Reuters/L. Jackson) Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Rex Tillerson
Maafisa  wa  Marekani , wakizungumza  kwa  masharti ya  kutotajwa majina, wamesema kombora  hilo huenda  ni  la  masafa  ya  kati  linalofahamika  kama KN-17 na  linaonekana kuwa liliripuka  na  kuvunjika  katika  muda  wa  dakika  chache  tangu  pale lilipofyatuliwa.
Korea kusini  imesema nchi  hiyo  ya  kaskazini  inacheza  na  moto  na  kuionya  kwamba itakabiliwa  na  vikwazo  vikali  zaidi  ya  Umoja  wa  Mataifa.
Ukiukaji wa maazimio ya Umoja wa Mataifa
Jeshi  la  Korea  kusini  limesema  kwamba  kombora  hilo , lililofyatuliwa  kutoka  katika jimbo  la  Pukchang  katika  mwelekeo wa  kaskazini  mashariki, lilifikia  umbali  hewani  wa kilometa 71  kabla  ya  kuvunjika vunjika  dakika  chache  wakati  likiruka. Limesema kurushwa  kwa  kombora  hilo  ni  ukiukaji  wa  wazi  wa  maazimio  ya  Umoja  wa  Mataifa na kuionya  Korea  kaskazini kutochukua  hatua  bila  kufikiria.
US Navy Destroyer USS Mason - DDG 87 (picture-alliance/dpa/A. Delgado) Moja kati ya meli za kivita za Marekani USS Mason - DDG 87
Utawala  wa  rais  wa Marekani  Donald Trump  unaweza  kuchukua  hatua  dhidi  ya  jaribio hilo  la  kombora  la  Korea  kaskazini  kwa  kuharakisha  mipango  yake kwa  ajili  ya vikwazo  vipya  vya  Marekani  dhidi  ya  Pyongyang, ikiwa  ni  pamoja  na  uwezekano  wa hatua  dhidi  ya maeneo  mahususi  ya  Korea kaskazini  na  China, afisa  wa  Marekani ameliambia  shirika  la  habari  la  Reuters jana.
Wakati Korea  kaskazini  inachukua  hatua kwa  kukaidi  mbinyo  kutoka  Marekani  na mshirika  wake  mkubwa  China, Marekani  inaweza  kufanya  luteka mpya  ya  jeshi  la  majini na  kuweka  meli  zaidi  za  kijeshi  na  ndege  katika  eneo  hilo  kwa  nia  ya  kuonesha uwezo  wa  nguvu  zake , afisa  huyo  amesema , kwa  masharti  ya  kutotajwa  jina.
US Flugzeugträger USS Carl Vinson (Reuters/U.S. Navy photo/M. Castellano) Meli iliyobeba ndege za kivita za Marekani USS carl Vinson
Vikwazo vipya
Afisa  huyo  amesema  vikwazo vyovyote  vipya  vinaweza  kuwekwa  katika  siku  chache zijazo na  vinaweza  kulenga  idadi  kadhaa  ya  maeneo  ambayo  tayari  yametathminiwa  na serikali  ya  Marekani  kwa  ajili  ya  hatua  kama  hizo, wakati  utawala  huo  wa  Marekani unaendelea  kutayarisha  mpango  mkubwa  zaidi  wa  vikwazo.
Maeneo  lengwa  ya vikwazo hivyo , afisa  huyo  amesema , yanaweza  kuwa  taasisi  za  kifedha  na  makampuni  muhimu ya  Korea kaskazini  pamoja  na  China, hatua  ambayo  huenda  ikaikasirisha  China.
USA Präsident Donald Trump bei der NRA - National Rifle Association (Reuters/J. Ernst) Rais wa Marekani Donald Trump
Wakati  rais  Trump  amemsifu  rais  wa  China Xi Jinping kwa  kuashiria ongezeko  la ushirikiano kuhusiana  na  suala  la  Korea kaskazini , afisa  huyo  amesema  Beijing  bado "inahitajika  kuchora  aina  fulani  ya  msitari mchangani" na  Pyongyang kuhusiana  na mpango  wake  wa  kinyuklia.

Papa Francis aanza ziara nchini Misri


Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis ameanza ziara nchini Misri, katika juhudi za kuhimiza maelewano kati ya Wakristu na Waislamu na kuepusha ghasia zinazofanywa kwa kutumia jina la Mungu.
Ägypten Papst Franziskus in Kairo | mit Abdel Fattah al-Sisi (Reuters/The Egyptian Presidency) Papa Francis akisalimiana na Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri mjini Cairo
Mara tu baada ya kuwasili mjini Cairo mchana wa leo, Papa Francis amepokelewa na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi kwa heshima za kijeshi, huku makasisi wakijipanga mstari kumsalimia. Baadaye ametembelea chuo kikuu maarufu cha Kiislamu cha Al-Azhar, ambako amefanya mazungumzo na Mufti Mkuu Ahmed al-Tayeb, yaliyoelezewa kama yenye kukamilisha mchakato wa kuboresha mahusiano kati ya Wakatoliki na Waislamu wa madhehebu ya Sunni. Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya ndege kabla ya kutua mjini Cairo, Papa Francis amesema ziara yake ya masaa 27 itakuwa ya kusajiisha umoja na udugu. Ujumbe huo pia ndio alioutoa kwa watu wa Misri, kabla ya kufunga safari kuizuru nchi yao.
''Kwa moyo wenye furaha na shukrani nitaitembelea nchi yenu, ambayo ni kitovu cha ustaarabu na zawadi wa Mto Nile, nchi ya jua na ukaribu, ambako maaskofu na manabii waliishi, na ambako Mungu mwenye rehema na uwezo, aliitoa sauti yake'', alisema Papa Francis na kuongeza, ''Ninayo furaha ya kweli kuja kama rafiki, na kama mjumbe wa amani katika nchi ambayo miaka 2000 iliyopita, iliipa hifadhi familia takatifu iliyokuwa ikikimbia kitisho cha mfalme Herod.''
Mjadala kati ya waislamu na wakristo
Ägypten Besuch vom Papst Franziskus in Kairo (Reuters/Egypt TV/A. Abdallah Dalsh) Ulinzi uliimarishwa mjini Cairo wakati wa ziara ya Papa
Katika ziara yake hiyo fupi, Papa Francis atakutana kwa pamoja na viongozi wa Kiislamu na wa Kikristu, kabla ya kulitembelea kanisa lililoshambuliwa kwa mabomu mwezi Desemba mwaka jana. Watu 29 walipoteza maisha katika shambulio hilo. Shambulio jingine kwenye kanisa la Koptiki mwezi huu wa Aprili liliuwa waumini 45.
Makanisa yote nchini Misri yamewekewa ulinzi wa ziada, kwa hofu kuwa mashambulizi mengine yanaweza kufanywa wakati huu wa ziara ya Papa Francis. Licha ya wasiwasi kuhusu usalama lakini, Papa Francis anatarajiwa  kutumia gari la kawaida tu katika shughuli zake.
Wakati ya ziara yake hii nchini Misri, Papa Francis atahutubia mkutano wa kimataifa kuhusu amani ambao umeandaliwa na chuo cha al-Azhar, ambacho ni kituo cha maarufu cha elimu kwa zaidi ya miaka 1000, chenye msikiti wenye historia ya fahari kubwa.
Kukosoa makosa ya Papa Benedikt wa XVI

Francis ni Papa wa kwanza kuitembelea Misri tangu ziara nyingine ya kihistoria iliyofanywa nchini humo na Papa John Paul wa II mwaka 2000. Uhusiano kati ya Misri na makao makuu ya Kanisa Katoliki uliingia doa enzi za Papa Benedikt wa 16, ambaye kufuatia shambulizi jingine kwenye kanisa la Koptik mwaka 2006 alitoa kauli iliyochukuliwa kama yenye kuunganishi dini ya Islamu na ghasia, kauli iliyokosolewa na chuo cha Al-Azhar kama uingiliaji wa mambo ya ndani ya Misri.

Wakristu wa madhehebu ya Koptik ni asilimia kumi ya wakazi wote milioni 92 wa Misri, na wamekuwa wakilengwa na mashambulizi ya mara kwa mara. Rais wa sasa wa Misri, japo anachukuliwa kama mtu anayetawala kwa mkono wa chuma amekuwa rafiki wa wakristu walio wachache nchini humo, na mwaka 2015 alikuwa rais wa kwanza wa Misri kushiriki katika ibada ya Krismasi.

April 26, 2017

Picha ya Rihanna na Lupita Nyong'o imezua mjadala kwamba huenda wawili hao wanapanga kubuni filamu

Baadhi ya mashabiki waliopendekeza wazo la filamu ya nyota hao wawili



Picha ya Rihanna na Lupita Nyong'o imezua mjadala kwamba huenda wawili hao wanapanga kubuni filamu hatua ambayo imewashinikiza nyota hao kujitokeza na kusema ndio wana mpango huo.
Picha ya Rihanna na Lupita yazua mjadala wa kutengezwa kwa filamu

Picha hiyo ya 2014 ya mitindo ilisambazwa na mashabiki wengi na sasa Rihana amesema kuwa ana mpango kama huo katika mtandao wake wa Twitter.
Mashabiki wamependa sana wazo hilo.
Lupita naye alijibu katika mtandao wa Twitter akisema mimi naunga mkono pendekezo hilo iwapo umeunga mkono.
Zaidi ya mashabiki 200,000 walilipenda chapisho hilo la Twitter na mapema siku ya Jumatatu Rihanna alijibu ''I'm Pit'z''-jina la utani katika filamu yake ya Star Wars.


 Baadhi ya mashabiki waliopendekeza wazo la filamu ya nyota hao wawili

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Maoni ya mashabiki kuhusu picha hiyo katika Twitter
Watu wengine 99,000 walilipenda chapisho hilo na sasa nyota hao sasa wameunga mkono pendekezo hilo .
Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Baadhi ya mashabiki waliopendekeza wazo la filamu ya nyota hao wawili
Wazo la filamu kutokana na picha hiyo lilionekana katika mtandao wa Tumblr wakati picha hiyo ilipochapishwa kwa mara ya kwanza ,lakini sasa wawili hao wamejumuika na sasa inaonekana kwamba mtandao wa Twitter ulitengeza filamu.
Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Rihanna alijibu kwa kusema kuwa inawezekana
Lakini huku mashabiki wakichangia ni nani anayefaa kupata sifa hizo kwa wazo hilo na kupata faida.
Mashabiki wengi wa Twitter hatahivyo wanegependa wazo hilo kufanikiwa.


Marekani imechukua hatua isiyo ya kawaida na kuwaita Maseneta wote kwa kikao cha kupashwa habari kuhusu Korea Kaskazini katika ikulu ya White House.
Washington imeendelea kueleza wasiwasi wake kuhusu mpango wa Korea Kaskazini kuendelea kufanya majaribio ya makombora na silaha za nyuklia, na vitisho vyake kwa majirani zake na Marekani.
Kikao hicho, ambacho kitashirikisha maseneta 100 pamoja na waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson na Waziri wa Ulinzi James Mattis kitafanyika Jumatano.
China, mshirika mkuu wa Korea Kaskazini, imehimiza pande zote kuwa na uvumilivu.

Rais wa China Xi Jinping alitoa wito huo alipozungumza kwa simu na Rais Donald Trump Jumapili.
Bw Xi alihimiza pande zote mbili "kuvumiliana na kujiepusha na vitendo ambavyo vinaweza vikaongeza wasiwasi zaidi", kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya China.
Kwa upande wake, bw Trump amesema Korea Kaskazini inahatarisha uthabiti katika rasi ya Korea kwa kuendelea na msimamo wake mkali.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwenyekiti wa Jopo la Wakuu wa Majeshi ya Marekani Joseph Dunford atakuwa miongoni mwa watakaowapasha habari Maseneta.
Maafisa wa Ikulu ya White House mara kwa mara huwapasha habari wabunge kuhusu masuala ya usalama, lakini ni nadra sana kwa bunge lote la Seneti kwenda White House.
Pamoja na Bw Tillerson na Jenerali Mattis, kutakuwepo pia na Mkuu wa Taifa wa Ujasusi Dan Coats na Jenerali Joseph Dunford, Mwenyekiti wa Jopo la Wakuu wa Majeshi ya Marekani.
Msemaji wa ikulu ya White House Sean Spicer alipoulizwa maswali kuhusu kikao hicho aliwaomba wanahabari waelekeze maswali yao kwa kiongozi wa wengi katika bunge la Seneti, Mitch McConnell.
Wasaidizi wakuu wa Rais Trump ambao walihojiwa na Reuters, walisema Bunge la Wawakilishi pia linataka kuandaliwe kikao sawa na hicho cha maseneta kuhusu Korea kaskazini.
Washington imesema kundi la meli za kivita, likiongozwa na meli kubwa yenye uwezo wa kubeba ndege USS Carl Vinson, linatarajiwa kufika rasi ya Korea siku chache zijazo.
Hii ni licha yakuwepo na habari za utata kuhusu zilikokuwa zinaelekea meli hizo awali.
Meli hizo za kivita vilikuwa zimedaiwa kuwa njiani kuelekea rasi ya Korea zikitokea Australia lakini baadaye zikaelekea hadi mlango wa kuingia Bahari ya Hindi.
Lakini sasa maafisa wa jeshi la wanamaji la Marekani wamethibitisha kwamba meli hizo zinaelekea rasi ya Korea.
Bw Trump pia ameambia mabalozi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwenye mkutano White House kwamba Umoja wa Mataifa ni sharti uiwekee Korea Kaskazini vikwazo vipya.

Gazeti la chama tawala cha Workers' Party Rodong Sinmun alieleza meli hiyo kuwa "mnayama".
Korea Kaskazini imeahidi kuendelea na majaribio yake ya makombora licha ya onyo la Bw Trump na wataalamu wanasema kwamba taifa hilo linajiandaa kufanya jaribio jingine la silaha ya nyuklia.
Washington ina wasiwasi kwamba Pyongyang inaweza kupata uwezo wa kuweka bomu la nyuklia kwenye kombora linaloweza kuifikia Marekani.
China inahofia uwezekano wa kuzuka kwa vita kamili rasi ya Korea, ambavyo vinaweza kusababisha kusambaratika kwa utawala wa Kim Jong-un.
China ina wasiwasi kwamba tukio kama hilo linaweza kupelekea wakimbizi wengi kukimbilia usalama China. Aidha, uwepo wa Wamarekani Korea Kaskazini utaifanya Marekani kuwa na udhibiti wa eneo linalopakana na China.

April 25, 2017

Mshike mshike wa kuwania ubingwa ligi kuu ya England utaendelea tena leo


Chelsea

Mshike mshike wa kuwania ubingwa ligi kuu ya England utaendelea tena leo kwa mchezo mmoja kupigwa vinara wa ligi hiyo Chelsea watakua katika uwanja wao wa nyumbani kuwaalika watakatifu wa Southampton.

Nahodha wa Chelsea Gary Cahill anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi baada ya kurejea mazoezi baada ya kupona tatizo la tumbo .
Diego Costa na Eden Hazard wanatarajiwa kuanza katika mchezo huu baada ya kuanzia bechi katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Tottenham wikiendi iliyopita

Diamond amefunguka kwa mara ya kwanza sababu za kumshirikisha Young Killer katika wimbo wake mpya ambao bado haujatoka.





Diamond amefunguka kwa mara ya kwanza sababu za kumshirikisha Young Killer katika wimbo wake mpya ambao bado haujatoka.
Ni mara nyingi hitmaker huyo wa Marry You, ameonekana kushindwa kuzizuia hisia zake za kumkubali Msodoki huku mara kadhaa akionekana kutumia mistari ya rapper huyo katika kuandika katika mitandao yake ya kijamii.

Akiongea na kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatatu hii, Diamond amesema,”Nilimuita Young Killer kuja studio, nikamwambia sijawahi kumshirikisha mtu katika muziki kipindi hiki na nikimshirikisha mtu ni wa WCB, kuna nyimbo yangu nataka nikushirikishe tufanye. Kwanza alipata shock kidogo, alipagawa kidogo” 

“Nikamwambia usipagawe, hii nyimbo ukifanya verse mbovu nakufuta na hapa katika ofisi mimi ndio nimekupigania hili swala uingize verse kwa sababu kila mtu anashangaa kwanini Young Killer? Ile verse imeandikwa ndani ya siku hizi tatu, akanambia hii nyimbo angekuwa mtu mwingine ningeshamaliza. Katika intro ya kutafuta kuingilia alitafuta karibuni hata masaa sita, lakini mwisho wa siku amefanya verse kali sana sana, imeshaisha bado kushoot video ngoma itoke,” ameongeza.

Bosi huyo wa WCB amesisitiza, “Young Killer mtu ambaye masikini ya Mungu anajitahidi sana sana kufight na mtu ambaye anaandika, mimi napenda mtu anavyandika. Nikajua kwanza nikimchukua Young Killer, nitawaempower vijana wengine wengi wenye ndoto ya kufanya muziki kuona kwamba kumbe na sisi tunawezekana. Kwasababu wangejua Diamond angefanya ngoma labda na Fid Q na Joh, wao wanajua hizo ndio atafanya nao, lakini nimeonyesha kuwa yoyote ninaweza nikafanya naye nyimbo. Na Young Killer kiukweli anachokifanya ni kitu kikubwa na video tutashoot hapa hapa Tanzania na ngoma ni kali na yakinyamwezi.”

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro amezungumzia vurugu zilizotokea hivi karibuni katika mkutano

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro amezungumzia vurugu zilizotokea hivi karibuni katika mkutano uliotakiwa kufanyike na maeneo ya Mabibo na Chama cha wananchi CUF. Kamanda huyo amesema kuwa suala hilo na wale waliojeruhiwa upelelezi utasema kama hao watu ndiyo waliokuja kuvamia au la. 

Kamanda Sirro amezungumza na wanahabari na kusema kuwa, mikutano ya ndani inaruhusiwa hata bila kutoa taarifa Polisi, lakini kwa waliojeruhiwa amedai kuwa upelelezi utaweka wazi mengi zaidi.
“Kuna hili tukio lililotokea tarehe 22 mwezi wa 4, 2017 majira ya saa tano karibu na nusu kwenye hotel moja inaitwa Vina Hotel, hii hotel iko maeneo ya Mabibo kuna wanachama wa Chama cha CUF maana yake Chama kile kina kundi A na kundi B inaonekana kundi A walikuwa wanafanya mkutano wao ndani ya ukumbi kwahiyo baadhi ya watu ambao tunafuatilia wakiwa na magari yapatayo mawili walivamia mkutano huo na wakafanya fujo, kwahiyo kukawa na vurugu kubwa sana na baadhi ya watu wameumia lakini huyu bwana Juma Shaban Nkumbi huyu Mwenyekiti wa CUF wanasema wa Kinondoni alikuwa ameita mkutano kwahiyo kwenye vurugu hizo kuna baadhi ya watu wameumia suala kubwa ni kujua kwa wale waliokuja kuvamia walikuja kufanya nini ni suala la upelelezi kwasababu mtu kaumia kakatwa na kitu chenye ncha kali,” alisema Kamanda Sirro.
“Amefungua jalada lake akieleza kuwa amepigwa mtu fulani na huyo mtu ndo kamjeruhi kwahiyo je, ni wale waliovamia ni jambo la upelelezi kwahiyo upelelezi utatuambia kama ni wao waliovamia, nilikuwa nawaambia pale hata kama wamevamia je kuna uhalali wa kumkata na mapanga? ni suala la upelelezi kwahiyo kimsingi niseme tu kwamba wale waliokamatwa nikutokana na yale malalamiko dhidi yao ambapo watu wameandika maelezo yao wamewatambua wamewataja kwahiyo ndiyo kesi imefunguliwa na hili la wao kutujulisha ni suala ambalo kwa kawaida wanamjulisha OCD,” alifafanua Kamanda Sirro.
“OCD wetu ndiyo anaweza kujua hilo lakini nafikiri katika busara ya kawaida mikutano ya ndani mara nyingi huwa siyo lazima tutoe kibali kwa hiyo unaweza kuta vyama vingine vya siasa au madhehebu mbalimbali wanaweza hata wasitupe taarifa kwasababu ni mikutano ya ndani lakini nafikiri kama walifanya busara zaidi watakuwa walimjulisha OCD kama mkutano wa namna hiyo ulikuwa unaendelea

Korea Kaskazini imefanya zoezi kubwa la kijeshi ambapo ufyatuaji wa risasi ulifanyika ili kuadhimisha miaka 85 tangu uzinduzi wa jeshi lake.

Korea Kaskazini imefanya zoezi kubwa la kijeshi ambapo ufyatuaji wa risasi ulifanyika ili kuadhimisha miaka 85 tangu uzinduzi wa jeshi lake.
I
Korea Kaskazini imefanya zoezi kubwa la kijeshi ambapo ufyatuaji wa risasi ulifanyika ili kuadhimisha miaka 85 tangu uzinduzi wa jeshi lake.

Mamlaka ya Korea Kusini imesema kuwa idadi kubwa ya vifaa vyake vya kijeshi vimepelekwa katika eneo la Wonsan kwa zoezi la kijeshi.

Korea Kusini pia imesema kuwa wanamaji wake wamekuwa wakifanya mazoezi ya pamoja na meli za kijeshi za Marekani.
Wajumbe kutoka Korea Kusini, Marekani na Japan wanafanya mazungumzo mjini Tokyo.

Mapema mjini Washington rais Trump alisema kuwa Korea Ksakzini ni tisho la ulimwengu.
Amewaalika maseneta wote 100 kwa mkutano katika ikulu ya Whitehouse siku ya Jumatano kuhusu hali ilivyo Korea Kaskazini.






Kupitia mtandao wa Instagram, Manara ameamua kuandika ujumbe mzito ambao unaashiria kutoridhishwa na adhabu aliyopewa na kamati hiyo.
Salaam… Namshukuru Mungu kwa sasa masuala yangu binafsi ya kifamilia nimeyamaliza.

na naweza sema kitu, kwanza niwape pole nyie kwa haya yaliyonitokea, mm c mtu ninayeamini uonevu c mtu ninayeweza kunyamaza nikiona haki inaporwa, c mtu mwenye moyo dhaifu wa kuogopa kukosoa pale

panapopaswa kurekebishwa, na always ntabaki hvyo, Juzi Ijumaa jioni niliambiwa na ofisi yangu imekuja barua toka TFF, ikiniarifu kuna wito wa kunitaka nifike Karume kusikiliza mashtaka dhidi yangu jpili ya jana asubuhi, wakati huo nikiwa zbar kwa masuala yangu ya kifamilia, na ofisi ikaiandikia Tff barua ya kuomba kusogezwa mbele kwa shauri hili hadi jnne ya kesho kwa kuwa ntakuwa nipo Dar.

barua iliwafikia na bnafsi nikaongea na Afred lucas msemaji wao na akanijibu ameipokea yy na imegongwa muhuri na katibu mkuu wa TFF keshaipata, kumbuka hyo ni jioni ya Ijumaaa , Jmosi nikampigia Alfred kuulizia kikao hcho cha kamati kimepangwa lini,akanijibu jtatu ya leo atanijibu, jana tena mkasikia mliyosikia,ni uharaka upi ilionao tff wa kushindwa kunipa haki ya kusikilizwa? natural justice nchi hii haitambuliki!!wahaini na wauaji nao pia husikilizwa,,iweje kwa mtuhumiwa ambae anapigia kelele haki ya mwajiri wake?

kuna hoja dhaifu inajengwa kuwa nilipaswa nijibu bnafsi barua ya Tff , hv ningewezaje kuijibu barua wakati sikuwepo Dar na sikuwa nimeiona na vp klabu yangu isiwe na haki ya kunijibia barua, wakati leo imepokwa haki ya kutokuwa na msemaji? na hv Tff hawajui kuwa mm nilikuwa naongea kwa niaba ya ofisi na klabu yangu?

nikija sababu za kunifungia nimejiuliza ni kaka yangu huyu msemwa aliyekuwa anasoma hii hukumu?

nimemuona kwa Millard Ayo, anasoma hukumu ilio kinyume na hati ya mashtaka, hati yao ina makosa mengine na hukumu pia nyingine, ni aina ya hukumu katili zaid kwa vwango vya mpira wetu, ila nawaambia Tff Haji hajawahi kuwa dhaifu wa moyo, anaweza kuwa dhaifu wa kiwiliwili, lakini nna moyo wa Simba,

ntapambana kwa kiwango cha juu sana, ntadai haki yangu na ya mwajiri wangu kwa viwango, na ntaziomba kamati zao zipokee rufaa yangu na kukaa kwa uharaka huu walionifanyia, na nipewe haki ya kusikilizwa,nisihukumiwe kishabiki wala kwa chuki, na nawahakikishia kikao kitakachokaa

Serikali ya Tanzania imeliagiza shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo (UNDP) kumuondoa mkurugenzi mkuu

  • Serikali ya Tanzania imeliagiza shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo (UNDP) kumuondoa mkurugenzi mkuu mwakilishi wa shirika hilo Tanzania kumuondoa kutoka nchini humo.
  • Tanzania imesema Bi Awa Dabo hajakuwa na maelewano mazuri na baadhi ya watumishi wenzake pamoja na wasimamizi wa shirika hilo.
  •  
  • Taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje ya Tanzania imesema hilo limechangia "kuzorotesha utendaji wa shirika hilo nchini (Tanzania) na kupunguza kasi ya kuleta maendeleo kwa Watanzania endapo hatua za haraka hazingechukuliwa."
  •  
  • Magufuli: Mwacheni Kikwete apumzike
  • Mwanamke akatiza kwa ghafla mkutano wa Magufuli
  • Serikali ya Tanzania kupitia wizara hiyo imetoa wito kwa UNDP kuwakumbusha watumishi wake kuwa "kipaumbele chao ni kufanya kazi na Serikali ili kufikia maendeleo yaliyoainishwa kwenye Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano na Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo yamefafanuliwa katika Agenda ya mwaka 2030."