May 20, 2017

jinsi ya Chui kula windo lake akiwa juu ya mti?


Ikiwa Chui hatompandisha mnyama huyo mtini basi ako kwenye hatari ya kumpoteza kwa fisi na simba.

Wanyama wengi wakiwemo wanyama wakubwa watano wa Afrika, hurandaranda katika mbuga ya wanyama pori ya Sabi Sand nchini Afrika Kusini.
Wakati mwingine wanyama hawa hupatikana maeneo wasiyotarajiwa, kama twiga mdogo ambaye waelekezi walimpata juu ya mti akiwa amekufa.
Chui mkubwa alimuua twiga huyo kisha akampandisha mita kadha juu ya mti. Alisherehekea chakula hicho kwa siku chache na kuacha tu mifupa, ngozi na nyama nyama zikiwa zimetapakaa.
Twiga huyo alikuwa na uzito wa kila 300 karibu na uzito mara tano zaidi ya Chui.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ikiwa Chui hatompandisha mnyama huyo mtini basi ako kwenye hatari ya kumpoteza kwa fisi na simba.
Ni kitu ambacho kinaeleweka kuwa kisicho cha kawaida kufanyika lakini Chui ana sababu nzuri ya kuweza kufanya hivyo.
Ikiwa Chui hatompandisha mnyama huyo mtini basi ako kwenye hatari ya kumpoteza kwa fisi na simba.
Kumpandisha juu ya mtu humsadia Chui kuzuia chakula chake kuibiwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwezi Februari mwaka 2017.
Utafiti uliofanywa na shirika moja lisilokuwa la serikali uligundua kuwa chui katika mbuga ya Sabi Sands huwawinda karibu familia 40 ya wanyama
Haki miliki ya picha Villiers Steyn, Panthera
Image caption Ikiwa Chui hatompandisha mnyama huyo mtini basi ako kwenye hatari ya kumpoteza kwa fisi na simba.
Chui hupandisha mtini nusu ya wanyama anaowawinda. Pia hupoteza moja ya mawindo yake kati ya matano kwa wanyama wengine kama fisi, simba na hata chui wa kiume.
Ikiwa chui ataamua kupandisha mtini windo lake na kisha kugundua hakuna mshindani karibu anawez kumburura kutafuta mti unaofaa ulio karibu
Mara chuo anapokaribia mti hupanda hadi umbali wa mita10 juu kutafuta eneo lililo salama kuning'inisha windo lake.
Hata hivyo wakati mwingine hali huwa ni ya dharura. Kama fisi yuko karibu Chui mara moja anaweza kupanda mti wowote ulio karibu kuzuia chakula chake kuibwa.

May 18, 2017

Msichana wa miaka 10 anayetaka kutoa mimba nchin india

Maandamano dhidi ya ubakaji wa watoto


Haki miliki ya picha Getty Images
Jopo la madaktari linakutana India kuamua iwapo mtoto wa miaka 10 aliyebakwa na babake wa kambo anaweza kuruhusiwa kutoa mimba.

Msichana huyo alibakwa mara kadhaa na babake wa kambo na anatarajiwa kujifungua katika kipindi cha miezi minne ijayo
Sheria ya India haikubali utoaji mimba baada ya wiki 20, ila tu ikiwa maisha ya mwanamke mja mzito yamo hataraini.
Sheria hii kali ilipitishwa ili kuwezesha usawa wa jinsia zote, kiume na kike. 

Kumekuwa na mila na desturi India ambapo wanawake wengi wamekua wakitoa mimba punde wanapogundua wanabeba mimba ya mtoto msichana. 

Katika miezi ya karibuni, Mahakama ya Juu ilipokea maombi ya wanawake kadhaa waliodai kupata mimba baada ya kubakwa.
Wanawake hao walitaka kutoa mimba zilizopita wiki 20.

Mahakama imekua ikituma maombi haya kwa jopo la wataalamu wa afya. 

Kesi ya sasa kutoka jimbo la Haryana, madaktari wanakutana kuamua ombi la familia ambayo inataka mtoto wao wa miaka kumi kutoa mimba. 

Habari za mimba hii zilitolewa na mamake msichana huyo ambaYe alimpeleka mwanawe hospitalini baada ya kulalamika maumivu ya mwili.

Duru zinasema msichana huyo amekua akiishi nyumbani wakati mamake akiwa kazini ambapo ni kijakazi.

Nani alihusika katika shambulio la kirusi cha mtandaoni


Kompyuta


 
Nani alihusika katika shambulio la kirusi cha mtandaoni ambacho kiliathiri kompyuta katika zaidi ya mataifa 150 duniani, zikiwemo Kenya na Tanzania? Kumeibuka madai kwamba huenda wadukuzi walitoka Korea Kaskazini.
Lakini kufikia sasa, hakuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha hilo.
Huenda hujawahi kusikia kuhusu kundi linaloitwa Lazarus Group, lakini pengine unafahamu baadhi ya matokeo ya shughuli zake. Kundi hili lilihusika katika kudukua mfumo wa kompyuta wa Sony Pictures mwaka 2014 na tena wakadukua benki moja ya Bangladesh mwaka 2016.
Inasadikika kwamba wadukuzi hao wa Lazarus Group walifanyia kazi yao China lakini kwa niaba ya Korea Kaskazini.
Wataalamu wa usalama mtandaoni sasa wanahusisha shambulio la kirusi cha WannaCry na kundi hilo baada ya ugunduzi uliofanywa na mtaalamu wa usalama wa kompyuta wa Google Neel Mehta.
Mehta aligundua kwamba maelezo ya kutunga programu ya kompyuta ya kirusi cha WannaCry yanafanana na maelezo ya programu zilizowahi kutumiwa na Lazarus Group awali.

Huenda ikawa labda ni sadfa tu, lakini kuna viashiria vingine.
Kutofautisha maelezo ya kompyuta
Prof Alan Woodward, mtaalamu wa usalama wa mifumo ya kompyuta, anasema ujumbe wa kuitisha kikombozi unatumia lugha inayoonekana kana kwamba aliyetafsiri alitumia kompyuta kuufanya kuwa wa Kiingereza, na ujumbe ulioandikwa kwa Kichina unaonekana kuandikwa na Mchina asilia.
"Mnavyoona uhusiano ni mdogo sana na labda ni sadfa tu," Prof Woodward anasema.
"Hata hivyo, uchunguzi zaidi unahitajika.
"Ugunduzi wa Neel Mehta ndio kiashiria muhimu zaidi kufikia sasa kuhusu chanzo cha WannaCry," kampuni ya usalama wa kompyuta ya Urusi, Kaspersky, inasema.
Hata hivyo, maafisa hao wanasema habari zaidi zinahitajika kuhusu aina za awali za WannCry kabla ya uamuzi kamili kufanywa.
Haki miliki ya picha EPA
Image caption WannaCry hutishia kufuta data kwenye kompyuta mtu asipolipa kikombozi
"Tunaamini kwamba ni muhimu watafiti wengine maeneo mengine ya dunia wachunguze kuhusu kufanana huku na wajaribu kuchimba zaidi kupata maelezo zaidi kuhusu asili ya WannaCry," kampuni hiyo ilisema.
"Ukiangalia shambulio la udukuzi la benki hiyo ya Bangladesh, siku za mwanzo, hakukuwa na maelezo mengi ya kulihusisha na kundi la Lazarus Group.
"Baadaye, ushahidi zaidi ulitokea na kutuwezesha, pamoja na wengine, kuhusisha kundi hilo na shambulio hilo kwa imani zaidi. Utafiti zaidi unaweza kuwa muhimu sana katika kubainisha ukweli."
Huwa vigumu sana kubaini nani amehusika katika shambulio la mtandao - na mara nyingi hutegemea maafikiano badala ya uthibitisho.
Kwa mfano, Korea kaskazini haijawahi kukiri kuhusika katika udukuzi wa Sony Pictures - na ingawa watafiti, na serikali ya Marekani, wanaamini kwamba ni Korea Kaskazini iliyohusika, hakuna anayeweza kupuuzilia mbali uwezekano kwamba madai hayo si ya kweli.
Wadukuzi walio na utaalamu wa juu wanaweza kuifanya ionekane kwamba shambulio hilo lilitoka Korea Kaskazini kwa kutumia mbinu mbalimbali.
'Ushahidi hauwezi kujisimamia'
Kuhusu WannaCry, kuna uwezekano kwamba wadukuzi walinakili tu maelezo ya kompyuta yaliyotumiwa awali na Lazarus Group.
Lakini Kaspersky wanasema dalili za kupotosha katika maelezo ya WannaCry zinaweza kuwepo lakini ni vigumu kiasi, kwani katika toleo la baadaye la kirusi hicho, maelezo yaliyokuwa yanafanana nay a Lazarus Group yaliondolewa.

May 17, 2017

Mzozo mpya umeibuka kati ya tume huru ya uchaguzi nchini Kenya,


Viongozi wa Nasa
Mzozo mpya umeibuka kati ya tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, na vinara wa mrengo wa upinzani wa NASA kuhusu utangazaji wa matokeo rasmi ya kura za Urais.
IEBC imeijibu mrengo wa upinzani wa Nasa kufuatia vitisho vyake vya kususia uchaguzi iwapo tume hiyo itafaulu kwenye rufaa iliyowasilisha mahakamani dhidi ya uamuzi wa mahakama ulioruhusu matokeo ya kura za Urais kutangazwa katika kituo cha kupigia kura.
Hii ni baada ya viongozi wa upinzani kuishauri IEBC dhidi ya kusaka njia za kubadili mipango hiyo ili kutangaza matokeo ya kura za Urais katika kituo cha kitaifa jinsi ilivyokuwa matokeo ya miaka iliyopita.
Tume hiyo kupita mwenyekiti wake Wafula Chebukati, imeeleza kuwa haitobadili msimamo wake wa kukata rufaa na kuwaambia viongozi wa upinzani kuheshimu mahakama na kutumia njia za kisheria kutatua malalamiko yao.

Viongozi wa mrengo wa upinzani wakiongozwa na Mgombea wa Urais, Raila Odinga, walitishia kususia uchaguzi iwapo tume hiyo itakata rufaa na kuruhusu matokeo ya Urais kutoka kila kituo kutangzwa kitaifa.
''Kuitishia IEBC kuhusu uamuzi wake wa kukata rufaa, ni kutishia uhuru wake, na wasioridishwa na hatua hiyo, wajiunge kwenye kesi wasake suluhisho za kisheria,'' alisema Chebukati.
Taifa la Kenya linatarajiwa kuandaa uchaguzi mkuu wa Urais baadaye mwaka huu huku ushindani mkali ukitarajiwa kati ya Rais Uhuru Kenyatta anayewania kiti hicho kupitia mrengo wake wa Jubilee na Raila Odinga, anayebeba bendera ya mrengo wa Upinzani wa Nasa.
Takriban wagombea kumi na wanane wa Urais wamejitokeza.

Tahadhari dhidi ya Ebola

Image result for ebola virus patients

Shambulio la mtandaoni duniani ambalo limesababisha kutekwa kwa mafaili katika kompyuta linaonekana kupungua kuanzia jana Jumatatu wakati maafisa wanafanyakazi kuwakamata watu 

wanaohusika. Miongoni mwa waliyogundua ni uwezekano wa uhusiano kati ya kirusi kinachofahamika kama "ransomware", kinachotambulika kama WannaCry na wadukuzi ambao 

wanahusiana na Korea kaskazini. Ugunduzi huo bado ni wa muda , kampuni moja ikiueleza kuwa ni njama lakini bado ni dhaifu. 

Kampuni ya usalama wa mtandaoni Kaspersky Lab imesema kwamba sehemu ya programu ya WannaCry inatumia mfumo wa kanuni kama malware ambayo ilisambazwa hapo kabla na kundi la Lazarus, kundi la wadukuzi ambao walihusika na kudukua mafaili ya kampuni ya Sony ambalo Korea kaskazini ililaumiwa.


 Wakati huo huo rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kwamba Urusi haihusiki kwa lolote na shambulio hilo la mtandaoni.

Donald Trump amefichua taarifa za siri

Image result for picha ya trump

Gazeti la Washington Post limeripoti kwamba rais Donald Trump amefichua taarifa za siri kuhusiana na wanamgambo wa Dola la Kiislamu kwa maafisa wa Urusi wakati wa mkutano wao wiki 

iliyopita, na kusababisha shutuma kali kutoka kwa Wademocrats na Warepublican. Mshauri wa usalama wa taifa McMaster alizungumza na waandishi habari kukana taarifa hizo.

"Hakuna kitu ambacho rais anakichukulia kwa dhati kabisa kama usalama wa watu wa Marekani. Taarifa hiyo imekuja usiku, kama ilivyoripotiwa, ni uongo. Rais na waziri wa mambo ya kigeni

 wameangalia vitisho kadhaa kwa nchi zetu mbili ikiwa ni pamoja na kitisho kwa usafiri wa anga. Hakuna wakati vyanzo vya 

upelelezi ama mbinu vilijadiliwa."Gazeti hilo la Washington Post limesema mshirika wa upelelezi hakutoa ruhusa kwa Marekani kutoa taarifa hizo kwa maafisa wa Urusi. Shirika la ujasusi la Marekani CIA na ofisi ya mkurugenzi wa idara ya upelelezi ya taifa walikataa kusema lolote jana.


chanzo dw

May 16, 2017

dunia ya kia mwisho

Mwanamke ajioa baada ya kukosa mchumba

Q May Chen mwanamke mwenye saratni ya matiti aliyejioa




Mwanamke mmoja ambaye anaugua saratani ya matiti amejioa mwenyewe baada ya kusubiri mchumba kwa muda mrefu.
May Chen mwenye umri wa miaka 28 kutoka Taiwan ameambia BBC kwamba anaugua ugonjwa huo lakini hajakubali sababu hiyo kuhujumu ndoto yake ya kuolewa.
''Nimekuwa nikisubiri mtu kujitokeza na kusema kwamba angependa kufunga ndoa nami mbali na kupiga picha za harusi nami aliambia BBC .

 Q May Chen Anasema kwamba ameamua kuafikia ndoto yake kupitia kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne na vito alivyovaa
Anasema kwamba wakati unapohisi kwamba huna miaka mingi ya kuishi huna budi kujifanyia maswala ambayo yamekuwa ndoto yako.
Anasema kwamba ameamua kuafikia ndoto yake kupitia kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne na vito alivyovaa.

Anasema kuwa wapiga picha walimshauri kupiga picha katika studio lakini yeye akawaambia kwamba anataka picha sawa na zile za harusi.
Hivyobasi alikodisha gari na kwenda kupiga picha hizo katika maandhari ya harusi.
''Nilipovalia rinda la harusi nilijawa na hisia mpaka nikahisi kulia''.
Anasema kwamba alihisi kana kwamba ameafikia ndoto yake ya miaka mingi.
Kwa sababu yeye huugua saratani ya matiti hulazimika kwenda hospitali mara tatu kwa wiki ili kudungwa sindano mbali na kutibiwa kwa kutumia kemikali.
Anaongezea kwamba kwa muda mrefu hakuweza kusimama kwa miguu miwili na kuvaa suruali ndefu, ''nilikuwa nikitembea kwa kiti cha magurudumo''.
Anasema kwamba hakuweza kutembea na kwamba nywele alizo nazo sio nywele zake asilia.
Habari ya mwanamke huo imewagusa watu wengi ulimwenguni.


Anasema kwamba anatumia habari yake kuwapa moyo wanaougua kwamba maisha sio mabaya sana.
''Mbali na maisha na kifo mambo mengine yote ni madogo''.
Anasema kwamba watu wengi wanaougua huwa na wasiwasi wataishi kwa muda gani na lini watafariki ama iwapo matibabu wanayopata yanafanya kazi.
''Lakini mimi nawashauri kwamba usiwe na wasiwasi kwa sababu hujui, kwa hivyo kwa nini usijiliwaze''?

Marekani yaituhumu Syria kwa kuchoma wafungwa gerezani


Sehemu inayosemekana kuwa wafungwa huchomewa
  1. Marekani imeituhumu serikali ya Syria kwa kujenga sehemu ya kuchoma maiti katika jela ya kijeshi iliyopo karibu na Damascus ili kuficha mauaji ya halaiki ya wanaoshikiliwa na serikali.
  2.  
  3. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeonyesha picha zilizopigwa kupitia njia ya Satelite ambazo imesema ni sehemu ya kuchoma maiti katika gereza lililopo Sednaya ambapo Umoja wa Mataifa na mashirika ya kutetea haki za binadamu yamesema maelfu ya wafungwa wameteshwa na kunyongwa.
  4. Image caption Sehemu inayosemekana kuwa wafungwa huchomewa
  5. Mwanadiplomasia mwandamizi wa Marekani anayehusika na masuala ya Mashariki ya kati, Stuart Jones, amesema kwa siku wafungwa takriban hamsini wanauawa katika gereza la Sednaya.
  6. Ameongeza kusema kuwa, mauaji hayo yanafanyika kutokana Syria kuungwa mkono na Urusi na Iran.

Mtandao wa kijamii wa Facebook bado unatumika nchini Thailand, licha ya muda wa mwisho kukamilika


Wathailand ni kati ya watumiaji wakubwa zaidi wa Facebook barani Asia,
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Utawala unafuatilia habari kuhusu mfalme mpya Vajiralongkorn
Mtandao wa kijamii wa Facebook bado unatumika nchini Thailand, licha ya muda wa mwisho kukamilika wa kuitaka Facebook, kuondoa taarifa ambazo utawala wa nchi hiyo umezitaka kuwa potovu kwake.
Facebook ilikuwa imepewa muda wa hadi 10:00 (04:00 GMT) kuondoa kurasa 131 ambazo Thailand ilisema zinakiuka sheria zake kali za lese-majeste 

Zaidi ya watu 100 wamefunguliwa mashtaka chini ya sheria hiyo tangu yafanyike mapinduzi ya kijeshi miaka mitatu iliyopita.
Utawala ulitishia kuchukua hatua za kisheria na kuufunga kabisa mtandao wa Facebook.

Baada ya muda uliotangazwa kupita katibu katika kampuni inayosimamia mawasiliano nchini Thailanda, aliwaambia waandishi wa habari kuwa amri za mahakama zimetolewa kwa kurasa 34, na utawala huo ulikuwa ukitafuta amri zingine kwa kusara zingine 97.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wathailand ni kati ya watumiaji wakubwa zaidi wa Facebook barani Asia
Wathailand ni kati ya watumiaji wakubwa zaidi wa Facebook barani Asia, huku maelfu ya biashara ndogo zikiutegemea mtandao huo kama chomo kikuu cha mauzo.
Ikiwa serikali itatekeleza vitisho vyake na kuwalazimisha watoa huduma za mitandao kuifunga, kutakuwa na malalamiko makubwa nchini humo.

Hata hivyo serikali ina matumaini ya kuhakikisha kuwa hakuna taarifa zinazotajwa kuwa mbaya, zitaruhusiwa kuonekana nchini Thailand licha ya kuwepo changamoto z

wajua kifua kikuu kina uwa



Kifua Kikuu (Tuberculosis) ni ugonjwa wa kuambukiza, ambao mara nyingi hushambulia mapafu. Ugonjwa huu unachukua nafasi ya pili ya magonjwa yanayosababisha vifo duniani.
Mwaka 2015, watu wapatao milioni 1.8 wanakadiriwa kufa kwa ugonjwa huu, huku idadi ya watu milioni 10.4 wakiwa wanaugua kifua kikuu. Kufuatia ugunduzi wa Robert Koch uliofanyika mwaka 1882, ugunduzi na utumiaji wa chanjo na dawa za kuponya kifua kikuu ulileta imani kuwa ugonjwa huu ungetokomezwa. Shirika la Umoja Wa Mataifa liliwahi kubashiri kuwa ugonjwa huu utakuwa umetokomezwa kufikia 2025.
Kifua Kikuu husababishwa na:
Ugonjwa wa kifua kikuu ama TB, husababishwa na bakteria aitwaye Mycobacterium tuberculosis. Bakteria huyu husambaa kwa njia ya hewa wakati mtu mwenye TB (ambaye mapafu yake yameshambuliwa) akikohoa,akipiga chafya,akitema mate,akicheka ,au akizungumza.
TB huambukizwa lakini siyo rahisi kuipata. Uwezekano wa kupata TB kutoka kwa mtu anayeishi au kufanya kazi naye ni mkubwa kuliko kutoka kwa mgeni. Watu wengi ambao tayari wamaeanza tiba sahihi angalau kwa wiki 2 hawaambukizi.
Toka antibiotics zilipoanza kutumika kutibu TB, baadhi ya aina ya bakteria hao wamegeuka sugu kwa dawa. Multidrug-resistant TB (MDR-TB) ni hali ambapo dawa haziwezi tena kuwaua bakteria wote, hivyo wale wanaosalia wanajijengea usugu wa dawa hiyo na dawa nyngine pia kwa wakati mmoja.
Multidrug-resistant TB (MDR-TB) inatibika kwa kutumia dawa za kipekee (very specific anti-TB drugs) ambazo ni chache na hazipatikani kirahisi. Katika mwaka 2012, karibu watu 450,000 walipata MDR-TB.
Watu wenye upungufu wa kinga za mwili huwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata active TB. HIV hudhoofisha kinga za mwili, na kuufanya mwili kupata shida ya kudhibiti bakteria wa TB. Watu wenye mchanganyiko wa HIV na TB wana uwezekano wa kupata active TB kwa kiwango cha ailimia 20-30 ukilinganisha na wale ambao hawana HIV.
Matumizi ya tumbaku yamedhihirika kuongeza uwezekano wa kupata active TB. Aslimia 20 ya TB duniani huhusishwa na matumizi ya tumbaku.
Dalili za manzo za Kifua Kikuu:
. Kukohoa, wakati mwingine kukiwa na makohozi au damu
. Kusikia baridi
. Uchovu
. Homa
. Kukonda kwa mwili
. Kukosa hamu ya kula
. Kutoa jasho usiku
Dalili za kifua kikuu:
Kifua kikuu huathiri hasa mapafu, lakini kinaweza kuathiri vile vile sehemu nyingine za mwili. Wakati TB imeathiri sehemu tofauti ya mwili, dalili zinaweza kubadilika. Bila kupata tiba, TB huweza kusambaa kwenye sehemu nyingine za mwili kupitia mfumo wa damu.
. Tb ikishambulia mifupa inaweza kuleta maumivu ya uti wa mgongo na kuharibu maungio ya mifupa
. TB ikishambulia ubongo husababisha meningitis
. TB ikishambulia maini na figo huweza kusababisha damu ndani ya mkojo
. TB ikishambulia moyo inaweza kuathiri uwezo wa moyo wa kusukuma damu na kusababisha cardiac tamponade ambayo inaweza kuua.
Tiba ya Kifua Kikuu
Wagonjwa wengi wa TB wanaweza kupona kama dawa stahiki itakuwepo na kutolewa inavyopaswa. Aina ya dawa na urefu wa muda wa matumizi vitategemea umri wa mgonjwa, hali yake ya afya kwa ujumla, usugu wa mwili wake kwa dawa, kama TB in latent au active, sehemu yake ya mwili iliyoathirika (i.e mapafu, ubongo, figo).
Watu wenye latent TB wanaweza kuhitaji aina moja tu ya dawa, wakati watu wenye active TB (na hasa MDR-TB) watahitaji mchanganyiko wa dawa.
Ni muhimu kwa mgonjwa kuhakikisha kuwa anamaliza dawa, hata kama dalili za TB zitakuwa zimeondoka. Bakteria waliosalia na kuvumilia tiba iliyotolewa wanaweza kugeuka sugu kwa tiba hiyo na kupelekea kupata MDR-TB hapo baadaye.

Majaji wawili wa Mahakama Kuu waacha kazi

Majaji wawili wa Mahakama Kuu waacha kazi

  • Rais Magufuli ameridhia maombi ya watatu hao kutaka kuacha kazi
Haki miliki ya picha Ikulu, Tanzania
Image caption Rais Magufuli ameridhia maombi ya watatu hao kutaka kuacha kazi
Majaji wawili wa Mahakama Kuu nchini Tanzania wameacha kazi, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
Taarifa hiyo inasema majaji Aloysius Kibuuka Mujulizi na Upendo Hillary Msuya wamewasilisha maombi ya kuacha kazi kwa rais, ambayo yamekubaliwa.
Jaji Mujulizi alikuwa pia mwenyekiti wa tume ya kurekebisha sheria Tanzania.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Saidi Meck Sadiki pia ameacha kazi.
Taarifa ya ikulu haijaeleza sababu iliyowafanya maafisa hao watatu kuamua kuomba kuacha kazi.

Mchezaji wa akiba Cesc Fabregas alifunga goli katika dakika ya 88



Mchezaji wa akiba Cesc Fabregas alifunga goli katika dakika ya 88 wakati mabingwa wapya wa ligi kuu ya England, Chelsea, walipowalaza Watford 4-3 usiku wa Jumatatu.
England Chelsea Meister Jubel (Reuters/Sibley Livepic) Kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas

Mechi hiyo ya ligi iliyochezwa katika uga wa Stamford Bridge ilikuwa na mbwembwe chungu nzima.
Nahodha wa the blues John Terry alicheza mechi yake ya 716 na akatia kimyani bao la kwanza ila alifanya makosa na kumpelekea Etienne Capoue kusawazisha. Cesar Azpilicueta na Mitchy Batshuayi walifunga baadaen na kuwaweka Chelsea juu 3-1, lakini Stefano Okaka alifunga goli la kusawazisha baada ya Daryl Janmaat kuwafungia Watford la pili.

Lakini Cesc Fabregas alipachika wavuni goli la nne na kuwapa mabingwa hao wapya ushindi na kuwaweka katika nafasi ya kuwa timu ya kwanza kushinda mechi 30 katika ligi hiyo yenye mechi 38 kwa kila timu, lakini hilo litafanyika iwapo watashinda mechi yao ya mwisho mnamo wikendi, kwani kwa sasa wameshinda mechi 29.
"Kuna uwezekano wa kushinda mechi 30 na ni lazima tujaribu kulifikia lengo hilo sasa," alisema kocha wa Chelsea Antonia Conte baada ya mechi hiyo.

Naye mkufunzi wa Watford, Walter Mazzarri alisema, "kulikua na mazuri na ambayo si mazuri katika mechi hiyo, lakini zaidi ya yote ninajivunia timu yangu."
Leo hii kutakuwa na mechi zengine katika ligi hiyo ambapo Arsenal watakuwa wanakwaana na Sunderland walioshushwa daraja tayari, mechi hiyo ikipigwa uwanjani Emirates, halafu Manchester City wavae njuga kucheza na West Bromwich Albion.

ALIYEKUWA Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, ametishiwa kufyatuliwa risasi na askari polisi.


ALIYEKUWA Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, ametishiwa kufyatuliwa risasi na askari polisi.

Hili ni tukio la pili kutokea baada ya aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, kutishiwa bastola hadharani.
Katika video iliyoanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii jana, linaonekana gari aina ya Land Cruiser lenye namba T 296 ATW, ambalo liliegeshwa pembeni kisha wakashuka askari wawili – mmoja wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na mwingine polisi wa kawaida.
Askari huyo wa FFU baada ya kushuka kwenye gari hilo, alinyanyua bunduki na kufyatua risasi hewani kabla mwenzake kumfwata na kumshika kifuani na kutaka kumrudisha katika gari.
Kisha alimfuata Malima na kuzungumza naye na wakati wakiendelea, yule askari aliyefyatua risasi naye alikuja na kumsukuma mara mbili waziri huyo wa zamani, kisha akanyanyua bunduki juu.
Askari huyo alisikika akitamka: “Kwanini hamuheshimu, kwanini hamuheshimu Serikali nyie, mzee heshimu Serikali, mimi nimewekwa kuitumikia Serikali, siwezi kudharaulika.”
Mtu mwingine wa pembeni ambaye hakuonekana katika video hiyo, alisikika akisema: “Huna mamlaka, huna mamlaka ya kutishia.”
Wakati wote huo, Malima alionekana akiwa ameweka mikono mfukoni mwa suruali yake.
Baada ya majibizano, mmoja wa askari alionekana akimsihi mwenzake waende katika gari, huku akitamka “Poti, Poti, Poti ee.” 
CHANZO CHA TUKIO
Taarifa za ndani zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea katika eneo la Masaki jijini Dar es Salaam jirani na Hoteli ya Double Tree, ambako dereva wa Malima aliegesha gari vibaya.
Hatua hiyo ilisababisha kutokea kwa majibizano kati ya maofisa wa Kampuni ya Udalali ya Majembe kabla polisi kuingilia kati na kufyatua risasi juu.
Inaelezwa kuwa Malima alifika akiwa kwenye gari jingine na kukuta mzozo unaendelea.
KAULI YA POLISI
Akizungumza na MTANZANIA, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda, alisema ufafanuzi kuhusu tukio hilo utatolewa leo.
Pia alisema wanaendelea kumhoji Malima katika Kituo cha Polisi Oysterbay.
“Polisi walikuwa wanafanya ukamataji, lakini tukio litatolewa ufafanuzi kesho (leo)… kuna mambo mawili, kuna kumshikilia na kumhoji, sisi tunamuhoji,” alisema Kaganda.
WAZIRI MWIGULU
MTANZANIA lilipomtafuta kwa simu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kuzungumzia tukio hilo, aliomba atumiwe ujumbe mfupi na hata alipotumiwa hakujibu.
LEMA AONYA
Akizungumza na MTANZANIA, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Godbless Lema, alisema roho za visasi zinaendelea kujengwa kati ya raia na polisi na hivyo taifa linakoelekea ni kubaya kwani litapoteza dira na amani.
“Nimesikitika na nampa pole Malima, matukio ya aina hii yako mengi. Kama imefika mahali tunatoleana SMG hadharani, hakuna mtu ambaye yuko salama katika nchi hii,” alisema.
Lema alikwenda mbali na kugusia matukio yaliyowahi kutokea, likiwamo lile la aliyekuwa Waziri wa Habari, Nape na kusema kuwa hata aliyemtishia bastola hajakamatwa.
“Kama kusipokuwa na udhibiti watu watauana hadharani, tukio la kubishania parking (maegesho) si la kurushiana risasi, ni suala la maelewano tu,” alisema.
TUKIO LA NAPE
Machi 23, mwaka huu, Nape alitishiwa bastola akiwa nje ya Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam, alipotaka kuzungumza na waandishi wa habari.
Tukio hilo lilitokea saa chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kumvua uwaziri.
Nape alipanga kuzungumza na vyombo vya habari, lakini harakati zake zilitiwa dosari, ikiwamo kuzuiwa kufanya mkutano ndani ya Hoteli ya Protea na kuamua kuzungumza nje ya hoteli hiyo.
Hata hivyo, kabla ya kushuka katika gari kuzungumza na vyombo vya habari, alifuatwa na watu wawili waliodaiwa kuwa ni askari na kutaka kumzuia asishuke.

WANAWAKE wawili wameuawa



WANAWAKE wawili wameuawa kikatili kwa kushambuliwa na mashoka na waume zao wa ndoa katika matukio mawili tofauti yaliyotokea mkoa wa Rukwa.
 Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Polycarp Urio amethibitisha kutokea kwa matukio hayo akisema chanzo ni wivu wa kimapenzi wa waume zao.
Wanawake waliouawa ni Theresia Baltazar ambaye wakati wa uhai wake alijulikana kwa jina lingine la Selemani (49) mkazi wa kijii cha Msia kilichopo Bonde la Ziwa Rukwa, Sumbawanga. Theresia aliuawa kikatili kwa kukatwa na shoka kichwani na shingoni na mumewe wa ndoa, Patrick Kipesa(39). Kwa mujibu wa Kamanda Urio, tukio hilo lilitokea Mei 14 mwaka huu saa 1.30 asubuhi kijiji cha Msia kata ya Milepa, tarafa ya Mtowisa, Sumbawanga.
“Baada ya mwanaume huyo kumuua mkewe kikatili naye alijiua kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani sebuleni kwake,” alisema. 
Inadaiwa chanzo cha kufanya mauaji hayo na yeye kujiua ni wivu wa kimapenzi baada ya kuhisi mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine ambaye hajafahamika kwa majina. 
Mwingine aliyeuawa ni Fatma Yusuph (22) mkazi wa Mtaa wa Sengetela Manispaa ya Sumbawanga.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda, Urio Fatuma ameuawa kwa kukatwa panga shingoni na mzazi mwenzake aliyetoroka baada ya kutenda uhalifu huo na jitihada za kumsaka sheria iweze kuchukua mkondo wake zinaendelea.
“Marehemu (Fatuma) alifika kituo cha Polisi kutoa taarifa ya kujeruhiwa akiwa na hali mbaya ambapo alipewa PF3 ili akatibiwe ndipo mauti ilimkuta akitibiwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga” alieleza Kamanda Urio.
Naye kikongwe Abel Sikazwe (90) aliyekuwa mgane kwa muda mrefu akiishi peke yake kwenye nyumba yake, aliuawa kwa kupigwa kichwani na kitu chenye ncha kali kisha kuvunjwa mkono na mguu kwa imani za kishirikina. 
Taarifa za uhakika kutoka kijiji cha Muzi zinaeleza kuwa tangu enzi za uhai wake marehemu Sikazwe alikuwa akihusishwa na ushirikina.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Polycarp Urio amethibitisha kutokea kwa matukio yote hayo ambapo alisema mtuhumiwa mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano akihusishwa na mauaji ya kikongwe Sikazwe. 
Alisema marehemu Sikazwe aliuawa juzi akiwa amelala peke yake nyumbani kwake ambapo watu hao baada ya kumuua, waliutelekeza mwili wake mbele ya nyumba yake na kutokomea kusikojulikana.
Kaimu Ofisa Tarafa, Peter Mankambila alithibitisha kuwa kikongwe huyo alikuwa akiishi peke yake baada ya kufiwa na mkewe miaka kadhaa iliyopita.
 “Mwili wa marehemu huyo uligunduliwa na mjukuu wake wa kike wakati alipofika nyumbani kwake alfajiri kumsalimia. Ndugu wa marehemu waliutaarifu uongozi wa kijiji,” alieleza.
 Kamanda Urio alisema miili ya marehemu imekabidhiwa kwa ndugu zao kwa ajili ya maziko.

Merkel, Macron waazimia kuimarisha ushirikiano


Angela Merkel Emmanuel Macron Berlin (Reuters/P.Kopczynski) Rais Emmanuel Macron na Kansela Angela Merkel mjini Berlin
Ziara ya Rais Emmanuel Macron  mjini Berlin jana jioni ilikuwa ya kwanza kwake kama rais wa Ufaransa nje ya nchi, baada ya 
kukabidhiwa rasmi madaraka juzi Jumapili. Alilakiwa na umati wa watu waliokusanyika karibu na ofisi ya Kansela Angela Merkel, 

baadhi wakipeperusha bendera ya Umoja wa Ulaya. Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, Merkel na Macron waliojawa na tabasamu, walisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa nchi zao kwa manufaa ya Ulaya nzima. Kansela Merkel alisema anaunga mkono Ufaransa yenye nguvu.

''Kila mmoja wetu anasimamia maslahi ya nchi yake, lakini, kijadi maslahi ya Ujerumani yamefungamana na maslahi ya Ufaransa'', alisema Bi Merkel, na kuongeza kuwa. Ujerumani inaweza kufanikiwa tu, ikiwa mambo yanakwenda vizuri Ulaya, na mambo yatakwenda vizuri Ulaya, ikiwa kuna Ufaransa yenye nguvu.
Msukumo mpya kwa Ulaya
Emmanuel Macron und Angela Merkel Berlin (Reuters/F.Bensch) Macron na Merkel waunga mkono msukumo mpya kwa Umoja wa Ulaya
Aidha, Kansela Merkel alieleza kuwa yeye na mgeni wake wamekubaliana juu ya mipango kadhaa ya kuupa msukumo mpya uhusiano kati ya Ufaransa na Ujerumani, ukiwemo wa mikutano ya mawaziri mwezi Julai baada ya Ufaransa kukamilisha uchaguzi wa bunge.
Viongozi hao wawili hali kadhalika walizungumzia utayarifu wao wa kukubali mabadiliko katika muundo wa Umoja wa Ulaya, kwa madhumuni ya kuufanya umoja huo kuwa wenye ufanisi zaidi. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema yeye hataogopa kuyaleta mezani masuala ambayo siku za nyuma yalikuwa yakinyamaziwa.
Alisema, ''Aghalabu, suala la mabadiliko katika mkataba wa Ulaya limekuwa mwiko nchini Ufaransa. Kwangu haitakuwa hivyo. Matarajio yangu ni kwamba mwelekeo wa pamoja wa Ulaya uwe wa kurejesha ufanisi katika kanda inayotumia sarafu ya yuro, na katika Umoja wa Ulaya. Na ikiwa mchakato huo utahitaji mabadiliko ya kitaasisi, sisi tuko tayari''. 
Hofu kuhusu sera ya deni la pamoja
Deutschland Neuer 50-Euro-Schein soll sicherer gegen Fälschungen sein | Mario Draghi (Reuters/K. Pfaffenbach) Rais Macron anataka mabadiliko katika sera kadhaa za kifedha katika kanda ya sarafu ya Euro

Rais Emmanuel Macron pia alitumia mkutano wa jana kutuliza hofu za wanasiasa wa nchini Ujerumani, kuhusu pendekezo lake la awali la kuwepo bajeti ya pamoja kwa nchi 19 zinazotumia sarafu ya yuro, kwa madhumuni ya kushughulikia vyema zaidi mzozo wa kifedha. Baadhi ya wanasiasa wa Ujerumani walilichukulia pendekezo hilo kama njia ya kuwatwisha mzigo zaidi walipa kodi wa Ujerumani, mnamo wakati uchaguzi muhimu ukikaribia.

Macron alifafanua kuwa pendekezo lake hilo halilengi kuugawa mzigo wa madeni ya siku za nyuma miongoni mwa wanachama wa kanda ya sarafu ya yuro, akisema badala yake anataka mpango wa pamoja wa siku za usoni katika masuala ya uwekezaji.

Mkutano kati ya viongozi hao wa nchi mbili ambazo zinachukuliwa kama mihimili ya Umoja wa Ulaya, umefanyika wakati umoja huo ukikabiliwa na changamoto kadhaa, zikiwemo kujiondoa kwa Uingereza katika mchakato ambao unajulikana kama Brexit, na kukua kwa hisia za kuutilia mashaka umoja huo miongoni mwa raia wa nchi zinazouunda.

Ujerumani huenda ikaondoa wanajeshi wake

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema Ujerumani inaweza kuondoa wanajeshi wake waliopo Uturuki iwapo Uturuki itaendelea kusisitiza kuwanyima ruhusa wabunge wa Ujerumani kuwatembelea wanajeshi hao.

Takriban wanajeshi 250 wa Kijerumani wapo katika kambi ya jeshi la anga ya Incirlik nchini Uturuki, ukiwa ni mchango wa Ujerumani katika ujumbe wa kijeshi unaoongozwa na Marekani unaopambana na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS katika nchi jirani ya Syria.
Duru za wizara ya mambo ya nje ya Uturuki zimeliambia shirika la habari la Reuters, kwamba ziara ya wabunge wa Kijerumani katika kambi hiyo haitakuwa hatua sahihi kwa sasa bila ya kutoa maelezo zaidi.
"Hii ni bahati mbaya sana, na tumelisema hilo kwa njia tofauti. Tutaendelea na mazungumzo na Uturuki lakini wakati huo huo tutalazimika kutafuta njia nyingine za kutimiza lengo letu kwa sababu tumeshawahi kuwa na tatizo hili la kuzuiwa ziara, kabla. Na hilo linamaanisha kutafuta njia mbadala kwa kambi hii ya Incirlik na suluhu moja miongoni mwa nyingine ni Jordan," amesema  Kansela Angela Merkel, akiwa katika mkutano na waandishi habari hapo jana, alipoulizwa juu ya uamuzi wa serikali ya Uturuki wa kuwazuia wabunge wa Ujerumani kuwatembelea wanajeshi wao katika kambi hiyo ya jeshi la anga ya Incirlik.
Timu ya utafiti wa kijeshi ya Ujerumani itaizuru Jordan katika siku za karibuni kuangalia uwezekano wa kupata kambi ya kijeshi nchini humo. Hayo ni kulingana na duru za serikali ya Ujerumani.
Kutokana na sababu za kihistoria na kama njia ya kuzuia matumizi mabaya ya madaraka, jeshi la Ujerumani Bundeswehr linadhibitiwa na bunge la Ujerumani, na sio serikali, hili linamaanisha kwamba wabunge wana haki ya kukagua shughuli za jeshi la Ujerumani, ikiwa ni pamoja na vikosi vya kijeshi vilivyotumwa nje ya nchi.
Uhusiano kati ya Uturuki na Ujerumani uliporomoka kwa kasi kubwa kuelekea uchaguzi wa kura ya maoni wa Aprili 16 wa nchini Uturuki wa kupanua madaraka ya Rais wa nchi hiyo Tayyip Erdogan.
Ujerumani na washirika wengine wa nchi za Magharini wameonesha wasi wasi kuhusu kile wanachokitaja kuwa ni kuelekea utawala wa kimabavu nchini Uturuki.
Mwaka jana Uturuki iliwaekea marufuku wabunge wa Ujerumani kutembelea kambi hiyo kwa miezi kadhaa ikiwa kama jawabu la azimio la bunge la Ujerumani la kutangaza mauaji ya Waarmenia yaliyofanywa na vikosi vya utawala wa Ottoman mwaka 1915 kuwa ni ya kimbari, matamshi yaliyokataliwa na Uturuki
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani amaesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Sigmar Gabriel  atalizungumzia suala hilo la kambi ya Incirlik na wenzake ambao pia ni wanachama wa NATO mjini Washington Marekani leo hii.

May 13, 2017

Juventus yatinga fainali Monaco

Wachezaji wa klabu ya Itali Juventus wakisheherekea ushindi wao dhidi ya Monaco


 
Klabu ya Juventus kwa mara ya pili imefuzu katika fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya baada ya kuishinda Monaco kwa jumla ya mabao.
Wakiwa wanaongoza 2-0 katika awamu ya kwanza ya mechi ,timu hiyo ya Itali iliongeza jumla ya mabao wakati mshambuliaji wao Mario Mandzukic alipofunga .
Dani Alvez aliongeza bao la pili baada ya kipa Danijel Sabusics kuupangua mpira ulioanguka mbele yake.
Kylie Mbappe alifunga krosi iliopigwa katika kimo cha nyoka ya Joao Moutinho ili kufunga bao la kufutia machozi, lakini klabu hiyo ya ligi ya daraja la kwanza haikuweza kufunga zaidi ya bao moja.
Juventus ambao hawajashinda kombe hilo tangu 1996 na waliopoteza katika fainali ya mwaka 2015 dhidi ya Barcelona watakabiliana na Real Madrid au Atletico Madrid katika uwanja wa Cardiff mnamo tarehe 3 mwezi Juni.

May 12, 2017

Uhuru wa vyombo vya habari haujakmatukioomaa


Kila mwaka, tarehe 3 Machi, dunia inaadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari. DW inaangalia hatua zilizopigwa na changamoto zilizopo katika sekta ya habari barani Afrika kama vile wanasiasa kuingilia sekta hiyo.
 
Sikiliza sauti 09:44

Mahojiano na Deodatus Balile, Jukwaa la Wahariri Tanzania

Huku dunia ikiadhimisha siku ya uhuru wa habari , waandishi habari nchini Uganda wanazidi kukabiliwa na mazingira magumu ya kazi kutokana na sheria kandamizi zinazobuniwa kila kukicha. Aidha makabiliano na vyombo vya usalama hasa polisi na vitisho vya mara kwa mara kutoka kwa wanasiasa na hata waajiri wao vimeshudiwa mara kwa mara. Haya ni licha ya madai ya utawala nchini humo kwamba unalinda kwa dhati uhuru wa habari.

May 11, 2017

“Professa Jay” ameitaka timu yake ya Simba kuweka nguvu zaidi katika fainali ya kombe la shirikisho kuliku kombe la ligi.






Legendari wa Muziki wa kizazi kipya nchini na Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ,
      Legendari wa Muziki wa kizazi kipya , Joseph Haule , “Professa Jay”.

Simba SC ipo katika nafasi ya pili katika ligi kuu soka Tanzania Bara ikiwa na alama 62 sawa na klabu ya Yanga inayoongoza kwa tofauti ya Mabao, pia ikiwa na michezo mitatu mkononi.
Professa Jay licha ya kuiombea timu yake kutwaa Ubingwa wa ligi kuu, amesema Simba ina nafasi ya kuutwaa Ubingwa wa kombe la shirikisho watakapocheza fainali dhidi ya Mbao FC kwenye uwanja Wa Jamhuri mjini Dodoma  May  28.
Professa Jay ambaye ni Mbunge wa Chadema kupitia jimbo la Mikumi, alisema ubingwa wa Ligi Kuu kwa Simba utatagemeana na mechi za Yanga, kama watashinda mechi zao 3 zilizobaki watajihakikishia ubingwa huo tofauti na Simba yenye mechi mbili itakuwa ni kazi bure hivyo ni vyema zaidi kujipanga kwa fainali ya FA.
Furaha yangu ni kuona Simba Sc inachukua ubingwa wa ligi kuu bara na ubingwa wa shirikisho, kutokana na ubora wa kikosi cha timu yetu hivyo tutashinda mechi zilizobaki na kutwaa ubingwa, japo imani yangu kubwa zaidi ipo kwenye kombe la shirikisho. “alisema Professa Jay”.

Baraza la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeidhinisha uamuzi wa kulipatia bara la Afrika nafasi tisa timu

Hatua ya nyongeza ya timu hizo inatajwa kama sababu mojawapo ya kuonekana kwa nchi ambazo zilikuwa hazipati nafasi

Mmoja wa wasichana wa Chibok waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria ameamua kusalia na mumewe badala ya kuachiliwa huru

Wasichana wa Chibok baada ya kupokewa na serikali
Mmoja wa wasichana wa Chibok waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria ameamua kusalia na mumewe badala ya kuachiliwa huru kulingana na msemaji wa rais wa Nigeria.
Alitarajiwa kuwa miongoni mwa kundi la wasichana walioachiliwa siku ya Jumamosi.

Garba Shehu aliambia runinga moja kwamba wasichana 83 walitarajiwa kuachiliwa huru lakini mmoja wao akasema : hapana nafurahi nilipo, nimepata mume.
Wasichana 82 waliachiliwa huru ikiwa ni kati ya mazungumzo yalioafikiwa na shirika la ICRC.
Serikali ilikubali kuwaachilia huru wanachama wanne wa Boko haram kubadilishana na uhuru wa wasichana hao duru ziliambia BBC.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wasichana wa Chibok baada ya kupokewa na serikali
Wapganaji hao wanadaiwa kuwazuilia zaidi ya wasichana 100 kati ya 276 waliowateka katika eneo la Chibok miaka mitatu iliopita.

Trump amfuta kazi James Comey



Ikulu ya Marekani ya White House imetangaza jana kwamba rais Donald Trump amemfuta kazi mkurugenzi wa shirika la uchunguzi wa makosa ya jinai FBI James Comey kuhusiana na jinsi 

anavyoshughulikia uchunguzi kuhusiana na barua pepe za Hillary Clinton. Barua kutoka Ikulu ya White House imemfahamisha Comey kwamba kufukuzwa kwake kazi kunaanza mara moja. 

Comey amekuwa akiongoza uchunguzi kuhusu mawasiliano kati ya wasaidizi wa kampeni ya Trump na maafisa wa Urusi kabla ya uchaguzi wa rais mwaka 2016. Mkurugenzi huyo wa FBI 

alikosolewa vikali pale alipotangaza kwamba shirika lake linafungua upya uchunguzi kuhusiana na jinsi Clinton alivyozihifadhi taarifa nyeti kiasi siku chache kabla ya uchaguzi. Trump alisema katika barua yake kwamba Ikulu ya White House tayari inatafuta mtu wa kuchukua nafasi yake.


chanzo dw

May 10, 2017

Msanii wa muziki, Rama Dee amedai kauli yake “Hanscana ni muongozaji mkali wa video kuliko Adam Juma” siyo kama alimkosea heshima muongozajii huyo mkongwe wa video za muziki.


Muimbaji Rama Dee
Muimbaji huyo amedai alitaka kumwambia ukweli muongozaji huyo ili kama anaweza kubadilka abadilike.
“Sikujenga beef na Adam Juma, nilisema kitu ambacho nakiona,” Rama Dee alimjibu mmoja  kati ya mashabiki wake ndani ya Kikaangoni EATV.  “Kwanini nimwambie kwa siri, hakuna cha siri, mtu akizungua unamwambia moja kwa moja,”
Aliongeza, “Mimi sina beef na mtu, mimi nafikiri mtu akiambiwa ukweli anatakiwa kutulia siyo na wewe unanza kutafuta namna ya kujitetea,”
Muimbaji huyo amedai hataki kuzungumzia zaidi mahusiano yake na Adam Juma kwa kuwa tayari ameshamalizana naye.
Hata hivyo kauli hiyo ya ‘Hanscana ni mkali kuliko Adam Juma’, ilipingwa na wadau mbalimbali katika mitandao ya kijamii wakidai muimbaji huyo amemkosea heshima Adam Juma.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha ( RPC ), Charles Mkumbo amesema wanamshikilia mmiliki wa basi dogo aina ya Coaster ambayo ilipata ajali na kusababisha vifo kwa wanafunzi, walimu na dereva wa shule ya siku ya Lucky Vincent Jumamosi huko Karatu, Arusha.

RPC Mkumbo amedai wanamshikilia mmiliki wa shule hiyo kwa kuruhusu gari yake hiyo kubeba abiria wengi zaidi kuliko uwezo wa gari.
"Siku ya tukio walikuwepo abiria 38 kwenye gari katika uchunguzi baada ya kubaini hilo tumeshachukua hatua kwa mtu aliyewezesha gari hilo kupakia hao watu, tumeshamkamata mmiliki wa gari ambaye ndiye mwenye shule hii, sasa hivi tunaendelea na uchunguzi na utakapokamilika atafikishwa mahakamani" alisema RPC wa Arusha.
Kwa mujibu wa Mkumbo anasema gari hiyo ilikuwa na kibali cha kubeba watu 30 lakini gari hiyo siku ya ajali ilikuwa na watu zaidi ya 30.

Monaco ina kibarua kigumu dhidi ya Juve



Ni timu zipi zitaelekea Cardiff kwa fainali ya Champions League barani Ulaya, swali  hilo linaanza kupatiwa jibu leo wakati  mkondo wa pili wa mchezo wa nusu fainali kati ya Juventus, na AS Monaco utakapofanyika.
UEFA Champions League Halbfinale AS Monaco - Juventus (picture-alliance/Zumapress/M. Ciambelli) Washambuliaji hatari wa AS Monaco Kylian Mbappe na Radamel Falcao
Monaco  pamoja  na  Atletico  Madrid  zinakabiliwa  na  majukumu ambayo  yanaonekana  kuwa  karibu  ya  kutowezekana  katikati  ya wiki  hii  katika  michezo  ya  mkondo  wa  pili wa  nusu  fainali  ya kombe  la  ligi  ya  mabingwa ,  Champions League  barani  Ulaya, ambapo  wapinzani  wao  Juventus  na  Real Madrid  wapo  katika ukingo wa  kukutana  mjini  Cardiff  katika  fainali  ya  mwaka  huu 2017.
Fußball AS Monaco v Juventus Turin - UEFA Champions League Juventus' Gonzalo Higuain celebrates scoring their second goal with Miralem Pjanic (Reuters/E. Gaillard) Gonzalo Higuain akikumbatiwa na mchezaji mwenzake Miralem Pyanic baada ya kufunga bao
Hata  kocha  wa  Monaco Leonardo  Jardim  anaukadiria  mchezo huo  kwa  kiwango  cha  nafasi  moja  tu  katika  20 zilizopo. Na wengi  wangesema  kwamba huo ni  msimamo wa  matumaini  kwa nafasi  ilizonazo  kikosi  chache  chenye  wachezaji  wachanga kuweza  kubadilisha  matokeo  ya  awali  ya  mabao 2-0 dhidi  ya Juventus  Turin.
Mabingwa  hao  watarajiwa  wa  ligi  ya  Ufaransa  ambao  hupachika mabao  bila  shida  katika  ligi  ya  nyumbani , wamepachika  mabao 3 mara  27  msimu  huu. Lakini  hakuna  timu  iliyokwisha  fanya hivyo  dhidi  ya  ngome  ya  Juventus  ambayo  imeruhusu  mabo mawili , mara  tano  tu  katika  michezo  51  katika  kampeni  ya mwaka  huu, haijashindwa  nyumbani  katika  muda  wa  miezi 20  na ngome  yake  imevujisha  mabao  mawili  tu  katika  michezo  11  ya Champions League.
Fußball AS Monaco v Juventus Turin - UEFA Champions League (Reuters/E. Gaillard) Mpambano kati ya Monaco na Juventus Turin wa nusu fainali mjini Monaco
Takwimu  hizi  zinatoa  nguvu  zaidi  kwa  Bibi Kizee, wakati  timu hiyo  ikiwa  na  uwezo  wake  wote  wa  wachezaji, kama  ilivyokuwa wakati  walipofanikiwa  kutuliza  mzuka  wa  washambuliaji  hatari  wa Monaco  katika  mji wa  kitalii  wa  Monaco wiki  iliyopita, ama wakati  Leo Messi  na  wenzake   wa  Barcelona walipopigwa sindano  ya  ganzi  na  kuendeshwa  mchakamchaka  mjini  Turin.
Kutokana  na  hilo, kocha  wa  Monaco Jardim  alisema  jukumu  lake la  kwanza  lilikuwa  kuingiza  imani  katika  kikosi  chake kwamba hawapambani  na  dude lililokufa.
"ni  wajibu  wetu  kufanya  kitu  tofauti. Iwapo unashindwa  nyumbani kwa   mabao 2-0 ni  wazi kwamba  unapaswa  kuja  na  kitu cha ziada," Jardim  alisema  katika  mkesha  wa  kuamkia  mchezo  huo.
"Mjini  Monaco  tulipata  kipigo kutokana  na uzoefu: mikwaju yetu kuelekea  golini  ilikuwa  sawa  na  Juventus. Tofauti  ilikuwa kiwango  cha  mafanikio  yao  kilikuwa  asilimia  100, kwa  upande wetu  ilikuwa  ziro."  Ameongeza  Jardim.
Inter Mailand AC Mailand 2010 (AP) Kocha wa Juve Massimiliano Allegri
Kocha  wa  Juve Massimiliano Allegri  alicheka  baada  ya kuambiwa  kwamba  matokeo yamekamilika  na  timu  yake  tayari  ni mshindi. "Huwezi  kujua  kile  kitakachotokea  katika  mchezo. Monaco huenda  wakaingia  katika  mchezo  huo  katika  mtindo tofauti kabisa na  kufanya  hali  kuwa  ngumu na  wana  wachezaji wenye  uwezo  mkubwa, vipaji  vya  juu  kabisa," amesema.
"Tunapaswa  kuanza  mwanzo  kabisa , tuhakikishe  tunacheza  kwa nguvu  katika  mchezo  huo  na  matumaini  ni  kwamba  tutakuwa bora  kiufundi  kuliko  tulivyokuwa  kule  Monaco, ambako  tulipata fursa  nyingi  na  kutengeneza  mazingira  yaliyoleta  hatari na  mara nyingi  tulifanya  makosa.
Mwandishi : Sekione  Kitojo / afpe / dpae