November 18, 2017

China na Korea Kaskazini zafanya mazungumzo

Kiongozi wa China akutana na mwenzake wa Korea Kaskazini


Kitengo cha taifa cha habari nchini Korea Kaskazini kimeripoti kwamba mjumbe maalum wa China Song Tao amefanya mazungumzo na Choe Ryong-Hae , ambaye ni mshauri wa karibu wa rais wa Korea Kaskazini Kim Jong un .
Ziara hiyo ambayo ni ya kwanza kuwahi kufanywa na afisa mwanadimizi wa China katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja inajiri wakati ambapo kuna hali ya wasiwasi mwingi kati ya washirika hao wawili na inafuatia ziara ya rais Trump katika eneo hilo.
Trump amekuwa akiishinikiza China kuiwekea vikwazo vya Umoja wa mataifa Korea Kaskazini
China haijatoa maelezo ya ziara hiyo, lakini vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vimesema kwamba bwana Song alisisitiza kuhusu mpango wa Bejing wa kuimarisha urafiki wa miaka mingi uliokuwepo kati ya mataifa hayo mawili.

Serena Williams amefunga ndoa

Siku ya jana kulivuja tetesi kuwa mcheza tensi namba moja kwa ubora duniani, Serena Williams amefunga na mpenzi wake Alexis Ohanian huko Contemporary Arts Center, New Orleans nchini Marekani.
Wawili hao ambao wamebahatika kupata mtoto mmoja walifunga pingu za maisha huku mrembo huyo akitinga magauni matatu tofauti katika sherehe hiyo iliyoudhuliwa na watu wake wa karibu.

Chanongo amerejea dimbani





Kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa ligi kuu bara mara mbili Mtibwa Sugar, Haruna Chanongo amerejea dimbani baada ya kupona majeraha  na ameanza mazoezi ya pamoja na wenzie.
Chanongo aliyekuwa anasumbuliwa na majeraha ya goti kwa muda mrefu baada ya kukaa nje kwa takribani miezi 6, ameanza mazoezi peke yake aliyopangiwa na jopo la madaktari wa klabu ya Mtibwa Sugar na sasa madaktari wamemruhusu kutumika katika michezo ya kimashindano baada ya kufanya vipimo vya mwisho nakuonekana yupo fiti .
Meneja wa kikosi cha Mtibwa Sugar, Sidy Ibrahim ameuambia mtandao rasmi wa klabu kuwa repoti iliyotolewa na jopo la madakatari wa timu wakiongozwa na Dk.Mussa Juma wamemruhusu Chanongo kucheza
“Chanongo ameruhusiwa kucheza hata michezo ya kimashindano baada ya kufaulu vipimo vya mwisho hivyo hana tatizo lolote .” Amesema Sidy.
Sidy Ibrahim ameongeza “Kafanya mazoezi na wenzake na anaonekana kuwa fiti hivyo hata mchezo ujao dhidi ya Kagera anaweza kutumika kulingana na mahitaji ya kocha.”
Nyota huyo hadi anaumia alikuwa na kiwango bora katika klabu ya Mtibwa Sugar  huku akifunga magoli 7 katika michezo ya ligi kuu aliyokuwa amecheza hadi anaumia katika msimu uliopita.
Kurejea kwa Chanongo kunafanya nyota waliopona majeraha ya muda mrefu kufikia wawili kipindi hiki baada ya Hassan Isihaka kupona na hivyo kuzidi kuimarisha  kikosi  cha wana tam tam.
Wachezaji ambao wanaweza kuukosa mchezo ujao dhidi ya Kagera Sugar siku ya Jumapili kutokana na majeraha ni Henry Joseph Shindika , Salum Kanoni , Shaban Kado, Salum Kihimbwa na Mohamed Issa ataukosa kutokana na kutumikia kadi tatu za njano.

fiesta ya obwa







Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahamud ametumia kongamano la Fursa iliyoandaliawa na Clouds Media Group kuomba tamasha kubwa la muziki la Fiesta lifike kisiwani hapo.
Hayo yamebainishwa leo na RC Ayoub katika kongamano la fursa linalofanyika Kisiwani Zanzibar katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, huku siku ya kesho tarehe 19 mwezi huu likitarajiwa kuhamia katika ukumbi wa Golden Tulip kisiwani humo.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Fursa wameandika maneno yanayoashiria Mkuu wa mkoa huyo anahitaji uwepo wa tamasha la muziki la Fiesta lililokuwa likifanyika kwa muda mrefu nchini basi lifike pia katika kisiwa hicho.
Nafahamu ndugu yangu @MutahabaRuge ana nia ya dhati kuinua Zanzibar nimemuomba kwa kua Fiesta nayo ni Fursa naomba ije hapa Zanzibar na amekubali Fiesta itakuja Zanzibar. Mhe. RC Ayoub Mohamed #Zanzibar #AnziaSokoni


VIDEOSNew Video: Mr P – For My Head






Baada ya kuachia ngoma yake ya  ‘Cool It Down’ Peter Okoye (Mr P) ameachia video ya ngoma yake nyingine iitwayo ‘For My Head’ video hiyo imeongozwa na Unlimited L.A.  Hii ni ngoma yake ya pili toka amejitoa katika kundi la P-Square.


50 Cent ameachia audio ya ngoma yake mpya iitwayo ‘Still Think I’m Nothing


50_cent




Rapper 50 Cent ameachia audio ya ngoma yake mpya iitwayo ‘Still Think I’m Nothing’ aliyomshirikisha Jeremih. Kwa sasa 50 amekuwa akijikita zaidi katika tamhilia yake ya ‘Power’.


mjue Kaa (mnyama)


Kaa kijiwe


Kaa ni wanyama wa faila Arithropodioda Decapoda na oda ya chini Brachyura(brakhys = fupi, oura = mkia) ambao kwa kawaida wana mkia mfupi mno au fumbatio lao limejificha ndani ya kifua. Wanyama wengine wafananao na kaa, kama wanamezi (hermit crabs), kaa-mfalme (king crabs) na kaangao (horseshoe crabs), sio kaa wa kweli. Kaa wamefunikwa na kiunzi cha nje na wana miguu kumi(jozi tano) kama Decapoda wote. Jozi ya kwanza inabeba magando (kucha za kaa).
Kaa wanapatikana katika bahari zote duniani, lakini kaa wengi wanaishi kwenye maji baridi na nchi kavu, hata kwenye sehemu za kitropiki. Kaa wana ukubwa mbalimbali kwa mfano kuanzia pea crab mwenye urefu wa milimita kadhaa, mpaka kwa kaa wa Kijapani (Japanese spider crab wenye mpaka jumla ya urefu (pamoja na miguu yake) wa mita 4. [1]

Mabadiliko na uainishaji

Oda ya chini ya Brachyura ina jumla ya spishi 6793 katika familia 93[2], idadi sawa na mabaki ya oda Decapoda[3]. Mabadiliko ya vizazi ya kaa yanajumuisha kuongezeka kwa mwili wenye msuru na kupungua kwa fumbatio. Japokuwa makundi mengine nayo yanapitia mabadiliko hayohayo, kaa wameonekana kuimarika zaidi. Kaa wanafahamika kwa kuhudumia chakula na kulinda familia zao, na wakati wa kujamiiana hutafuta sehemu mzuri ya kaajike kutoa mayai yake.[4]
Kiasi cha spishi 850 [5] za kaa wanaishi kwe maji baridi, au nchi kavu na majini na wanapatikana maeneo mbalimbali hasa maeneo ya kitropiki na nusu tropiki, walionekana kuwa wanauhusiano na wanaunda familia iliyokubwa na karibu sana, lakini sasa inaaminika wanaunda makundi makubwa tofauti mawili, wale wa Dunia Mpya na Dunia ya Kale.

Tabia[hariri | hariri chanzo]

Kaa ni wanyama waliochangamka na wenye tabia tata. Huwasiliana kwa kugonga au kupunga koleo zao. Kaa huchukiana wao kwa wao,na mara nyingi dume huchukiana kuwapata kaa jike. [6] Kwenye fukwe kwenye miamba, ambako mapango na nyufa zimejaa, kaa hupigania pia kupata nafasi.

Chakula[hariri | hariri chanzo]

Kaa hula nyama na majani lakini hasa hula algi [7] na hula chakula kingi chochote kama vile moluski, minyoo, fungi, bacteria, na hata jamii nyingine za crustaceans, kutokana na upatikanaji wao na pia spishi ya kaa husika, kwa kaa wengi, mchanganyiko wa mlo wenye nyama na mimea hupendelea kukua haraka nawenye nguvu htabiti[8][9]

Mapishi ya kaa

Kaa huandaliwa na kuliwa katika namna mbalimbali sehemu tofauti tofauti za dunia.Baadhi ya spishi wanaliwa wote hata gamba lake, kama vile kaa mwenye gamba laini. Spishi nyingine huliwa miguu yake na koleo lake tu. Hiki ni kitu cha kawaida kwa kaa wa kuliwa kama vile snow crab.
Katika maeneo mbalimbali duniani viungo kadhaa huongezwa kuberesha ladha ya kaa mfano huko Asiai, kaa- masala na kaa- pilipili ni chakula chenye viungo vingi sana.
Kwa Uingereza nyama ya kaa na hupikwa huandaliwa ndani ya magamba ya kaa tena namna mojawapo ya kuandaa kaa wanyama ni kumwondoa na kumwandaa na kumchanganya na unga kutengeneza keki ya kaa.
Kwa kawaida kaa huchemshwa wakiwa hai, wana sayansi wa Norwei walidhihirisha suala hili kwa kusema kuwa kaa hawaumii wala kuhisi maumivu pindi wanapopikwa hivyo. [11], hata hivyo hapo baadae wana sayansi walitambua na kusema kuwa kaa nao huhisi maumivu na kuyakumbuka, japo hili si suala kubwa wakati wa kupika.

Waziri Mkuu ahimiza utunzaji wa mazingira


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema, serikali imeandaaa mikakti mbalimbali ya kudhibiti na kukabiliana na changamoto ya uharibifu wa mazingira, hususan uharibifu wa vyanzo vya maji, matumizi yasiyo endelevu ya ya ardhi, misitu na bioanuai nyingine.

Waziri Majaliwa ameyasema hayo wakati wa kuahirisha mkutano wa Bunge, mjini Dodoma ambapo amesema, mikakati hiyo ambayo inatekelezwa na sekta zote ni pamoja na Mkakati wa Taifa wa kukabliana na Mabadliko ya Tabia Nchi, Mkakati wa Taifa wa hatua za haraka za kuhifadhi mazingira ya pwani, bahari, mito na mabwawa.
“Mikakat mingine ni Mkakati wa Taifa wa kupanda na kutunza miti, Mkakati na Mpango kazi wa Taifa wa Hfadhi ya Bioanuai na Programu ya kukabiliana na kuenea kwa hai ya jangwa na ukame,” amesema Waziri Mkuu
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, mwishoni mwa wiki iliyopita ilicheza na Benin katika mchezo wa kimataifa wa kirafi ki uliopo katika kalenda ya Fifa, Shirikisho la Kimataifa la Soka.
Mechi hizo zilizomo katika kalenda ya Fifa ni muhimu sana, kwani zinasaidia kujua timu ya taifa husika iko katika nafasi gani katika viwango vya ubora vya shirikisho hilo, ambavyo hutolewa kila mwezi.
Tanzania, yaani Taifa Stars ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na Benin ugenini na sare hiyo inaweza kuipandisha kidogo Taifa Stars, ambayo iko katika nafasi ya 136 katika viwango vya mwezi uliopita, ambavyo vilitolewa Oktoba 16.
Katika viwango hivyo vya Oktoba, wenzetu Benin wenyewe wako katika nafasi ya 79 na inaonekana kuwa waliipata nafasi hiyo baada ya kupanda kwa nafasi tisa. Tanzania yenyewe ilipata nafasi hiyo ya 136 baada ya kuporoma kwa nafasi 19.
Hongera Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kujitahidi kuipatia Taifa Stars mechi za kimataifa za kirafi ki na hii itasaidia siyo tu kujua nafasi yetu katika viwango vya Fifa, ila pia itawawezesha wachezaji wetu kupata uzoefu wa mechi za kimataifa.
Nchi yetu ina vipaji vingi katika michezo mbalimbali na hasa soka, lakini kinachokosekana ni kutoibuliwa au kuendelezwa tofauti na wenzetu wanavyofanya. Mechi hizo za kimataifa za mara kwa mara zitawasaidia sana wachezaji wetu kutokuwa wageni na vitu au wachezaji mbalimbali wakubwa watakapokuwa wakishiriki mashindano fulani makubwa Afrika na dunia kwa ujumla.
Huko nyuma tuliona wachezaji wetu baadhi yao walikuwa wakishangaa hata viwanja vya wenzetu jinsi vilivyo vikubwa na vizuri, lakini kwa sasa hilo halipo tena, kwani hata sisi tuna uwanja unaofanana na vile vya Ulaya kwa ubora wa sehemu ya kuchezea na mahali pa kukaa watazamaji.
Hivyo kwa upande wa kuipatia Taifa Stars mechi za kimataifa za kirafi ki, TFF wanastahili pongezi kubwa kwa kuipatia Taifa Stars mechi hizo karibu kila mwezi. Hata hivyo, sasa wakati umefi ka kwa TFF kuhakikisha kila tunapocheza na timu, basi iwe iko juu yetu katika kiwango cha kimataifa ili tuweze kujifunza kitu kutoka kwa wenzetu hata kama tutafungwa.
Muhimu ni kuiandaa vizuri timu yetu kwa ajili ya kucheza na timu zenye uwezo zaidi yetu ili tuweze kuambulia kitu fulani na siyo kucheza na timu zilizopo chini yetu. Mchezo dhidi ya Benin angalau tulicheza na wenzetu waliopo juu yetu, hivyo hapo tunaweza kupanda kidogo licha ya kutoka sare.
Inajulikana kuwa wakati fulani ni ngumu kucheza na timu zenye viwango vya juu kwani nazo zimekuwa zikilinga kucheza na timu ndogo na kutaka kucheza na wakubwa wenzao ili wafaidike na mechi hizo kwa kupata ushindani na kujifunza kitu kutoka kwa wapinzani wao hao.
Hata hivyo, hilo lisiwakatishe tamaa TFF mnachotakiwa kufanya ni bora mkaingia gharama kwa kuzigharamia timu hizo kubwa mradi zikubali kucheza nazo ili timu yetu ifaidike na kitu fulani.
Taifa Stars iandaliwe vizuri kwa ajili ya mashindano yajayo ya kimataifa ili siku moja Tanzania iweze kushiriki fainali za Kombe la Dunia na lile la Mataifa ya Afrika (Afcon). Kwa mara ya mwisho Tanzania ilishiriki mashindano ya Afcon mwaka 1980 nchini Nigeria na tangu wakati huo tumekuwa tukiishia katika hatua ya kufuzu tu na kushindwa kucheza mashindano hayo au fainali za Kombe la Dunia. TFF jitahidini na msichoke kuiandaa timu hiyo pamoja na zingine za taifa ili Tanzania iweze kurejea katika mashindano ya kimataifa.

Sheria ya dawa za kulevya kung’ata zaidi

         Sheria ya dawa za kulevya kung’ata zaidi



SERIKALI imefanya marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini kwa kuwabana zaidi wafanyabiashara na watumiaji wa dawa hizo pamoja na kuwapa nguvu maofi sa wa mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa hizo ambapo sasa watatumia silaha kupambana na wanaouza dawa hizo.
Kibano hicho kimewekwa kwenye marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya ya Mwaka 2017 yaliyowasilishwa na kupitishwa jana bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama.

Kibano kwa wafanyabiashara wa dawa hizo ni pamoja na kuwekwa katazo na mtu atakayebainika kuwezesha au kusababisha mtu kuwekwa rehani ili kufanikisha biashara ya dawa za kulevya atakabiliwa na adhabu ya kifungo cha maisha.
Pia sheria hiyo sasa imeongeza makosa yatakayokosa dhamana kuwa ni kumiliki mitambo ya kutegeneza dawa za kulevya, kufadhili biashara ya dawa za kulevya na kuwaingiza watoto kwenye biashara na matumizi ya dawa hizo.
“Msingi wa hili ni kudhibiti ongezeko la wafanyabiashara wakubwa kupunguza viwango vya utunzaji na usambazaji wa dawa za kulevya nchini, mfano kokeni na heroini na kutohofia kuendelea kufanya biashara ya bangi na mirungi kwa sababu uwezekano wa kupata dhamana ni mkubwa kutokana na viwango vya uzito uliopo kwenye sheria kwa sasa ni vikubwa ambavyo ndivyo vigezo vya utoaji dhamana,” alisema.
Wafanyabiashara hao wanabanwa kwenye mali zao ambapo sasa badala ya mali za mtuhumiwa kutaifishwa za miaka mitano nyuma, zitataifishwa za miaka 10 nyuma tangu tarehe ya kushtakiwa.
Jenista alisema sasa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Dawa za Kulevya amepewa uwezo wa kushikilia akaunti za benki za watuhumiwa wa dawa hizo kwa muda ili kurahisisha, kuimarisha na kuboresha taratibu za uchunguzi na kuweka uhakika wa fedha haramu kutotoroshwa kwa urahisi au uchunguzi kutoharibiwa.
Alisema serikali itakuwa na mamlaka ya kutaifisha mali zilizo nje ya nchi za mtu aliyetiwa hatiani chini ya sheria hii ya kupambana na dawa za kulevya, kwa mujibu wa taratibu za kimataifa kati ya serikali ya Tanzania na nchi husika.
Marekebisho hayo pia yamewezesha uchukuaji wa maelezo ya watuhumiwa au mashahidi kwa njia za kisasa kama vile rekoda, video na vifaa vya dijitali. Jenista alisema Mahakama za chini zinapewa mamlaka ya kushughulikia makosa ya usafirishaji wa kiasi kidogo cha dawa za kulevya na kemikali bashirifu na hivyo kupunguza msongamano wa kesi Mahakama Kuu.
Kwa sasa mashauri yote ya dawa hizo zenye uzito unaozidi gramu mbili kwa kokeni na heroini, gramu 50 kwa bangi na kilo mbili kwa mirungi hupelekwa Mahakama Kuu.
Waziri huyo alisema sheria hiyo sasa inawapa nguvu maofisa wa mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya kumiliki na kutumia silaha inapobidi na kufafanua “wafanyabiashara kutokana na nguvu ya pesa wanamiliki silaha na kujiwekea kinga ya kiulinzi wakati wote hivyo kufanya mazingira ya kiutendaji ya mamlaka kuwa hatarishi wakati wa ukamataji.”
Kwa upande wa watumiaji wa dawa hizo, faini imetoka Sh milioni 20 au kifungo kisichopungua miaka 20 au vyote kwa pamoja na kuwa faini isiyopungua Sh milioni 50 au kifungo kisichozidi miaka 30 au vyote kwa pamoja.
Akisoma maoni ya Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Mwenyekiti wake Dk Jasmine Tiisekwa alisema wakati wa kutunga kanuni za utekelezaji wa sheria hiyo, serikali ione umuhimu wa kuongeza pombe aina ya viroba na dawa nyingine za binadamu ambazo zinaweza kutumiwa kama dawa za kulevya ili ziwe sehemu ya orodha ya dawa za kulevya ili kudhibiti mbinu mpya za kuzalisha dawa hizo nchini.
Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Masoud Abdallah Salim alisema upinzani unapingana na ofisa wa mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya kuruhusiwa kutumia silaha kwani hawana mafunzo ya kipolisi na wanaweza kutumia silaha vibaya.

Muuaji wa tembo atiwa mbaroni




POLISI mkoani Kigoma inamshikilia Maneno Tanu (26) kwa tuhuma za mauaji ya tembo na kuhusika kwenye shughuli za ujangili.

Meneja wa Kanda wa Pori la Akiba la Muyowosi Kigosi, Aloyce Mganga alisema kuwa mtuhumiwa alikamatwa majira ya saa 11 alfajiri jana katika kijiji cha Kagera Nkanda Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.

Mganga alisema kuwa awali mtuhumiwa alikamatwa katika msako ulioendeshwa kwa pamoja na polisi na shirika linalojihusisha na kampeni ya kuzuia ujangili la Friedkin Anti Poaching na kufanikiwa kumkatamata mtuhumiwa akiwa na bunduki moja aina ya SMG yenye risasi 98, magazini moja na mtambo wa kutengeneza gobore.

Alisema kuwa kwa wiki mbili walikuwa kwenye msako wa kumtafuta mtu huyo na baada ya kupata fununu yupo kijiji cha Kagera Nkanda walitengeneza mtego kwa kushirikiana na polisi na kufanikiwa kumkamata.

Aidha Meneja huyo alisema kuwa wakati anakamatwa mtuhumiwa hakuwa na nyara yeyote ya serikali lakini baada ya mahojiano alikiri kuhusika na mauaji ya tembo wawili katika pori hilo karibu wiki tatu zilizopita lakini pia alikiri kuwinda wanyama na kuuza nyama bila kuwa na vibali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martini Otieno hakutaka kukiri wala kukanusha habari hiyo badala yake alisema kuwa yuko kwenye ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Yussuf Masauni na kwamba atatoa taarifa baada ya kumaliza shughuli za ziara hiyo.

x

Maelfu ya watu waandamana kumshinikiza Mugabe kujiuzulu

Maelfu ya Wazimbabwe leo wameandamana katika mitaa ya mji mkuu, Harare, kuunga mkono hatua ya jeshi kuchukua udhibiti wa mamlaka na kumhimiza Rais Robert Mugabe, ambaye amewekwa katika kizuizi cha nyumbani, kujiuzulu. Waandamanaji hao waliojawa furaha huku wengine wakivalia bendera ya Zimbabwe, wamebeba mabango yenye maandishi:


 "Sharti Mugabe aondoke", au "Bob si mjomba wako." Wanaharakati wa Zimbabwe wameunga mkono mkutano huo wa kumshinikiza Mugabe kuondoka madarakani.
 Wengine ambao wameunga mkono wito huo ni Chama cha Maveterani wa Vita pamoja na chama kikuu cha upinzani, Movement for Democratic Change.


 Jeshi limeliambia shirika la habari linalomilikiwa na serikali kuwa mkutano huo umeruhusiwa kufanyika na kutaka uwe wa amani. Jeshi la Zimbabwe lilichukua udhibiti wa mamlaka mnamo Jumatano kwa njia ya amani na bila umwagikaji damu na kumweka Mugabe, mwenye umri wa miaka 93, katika kizuizi cha nyumbani na kuwakamata baadhi ya washirika wake. Rais Mugabe amekuwa madarakani kwa miongo minne


chanzo dw kiswahili

New Music: Nandy – Kivuruge


New Music: Nandy – Kivuruge





Msanii Nandy ambaye siku chache zilizopita ameshinda tuzo ya AFRIMA za nchini Nigeria, ameachia wimbo wake mpya uitwao ‘Kivuruge’. Wimbo umetayarishwa na Kenny Ringtone.

Watu 2 wauawa katika makaribisho ya Raila

Watu 2 wauawa katika makaribisho ya Raila 

Msafara wa kiongozi wa upinzani nchini Raila Odinga baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kutoka Marekani

Takriban watu wawili wameuawa katika mji mkuu wa Nairobi huku maafisa wa polisi wakikabiliana na wafuasi wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga .
Gari moja la maafisa wa polisi pia lilichomwa .
Makundi ya watu yalikusanyika katika uwanja wa ndege kumkaribisha kiongozi huyo amabye alikuwa amerejea kutoka mataifa Marekani.
Raila Odinga alisusia marejeleo ya uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.
Kulikuwa na ripoti za maafisa wa polisi waliorusha vitoa machozi katika gari la Raila Odinga alipokuwa akielekea mjini.
Siku ya Jumatatau Mahakama ya juu nchini Kenya inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu uhalali wa uchaguzi wa tarehe 26 Oktoba ambao rais Uhuru Kenyatta alibuka mshindi.

Rais wa Zimbabwe's Robert Mugabe amewatunuku shahada zaidi ya wanafunzi 3,300

Rais wa Zimbabwe's Robert Mugabe amewatunuku shahada zaidi ya wanafunzi 3,300 katika chuo kikuu cha Zimbabwe

Rais wa Zimbabwe's Robert Mugabe amewatunuku shahada zaidi ya wanafunzi 3,300 katika chuo kikuu cha Zimbabwe, akiwemo mke wa jenerali aliyemzuia siku ya Jumatano.
Marry Chiwenga alipata shahada ya MBA kulingana na shirika la habari la Zimbabwe.
Awali Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu jeshi la nchi hiyo lichukue madaraka siku ya Jumatano.
Alihudhuria sherehe za kuhitimu kwa mahafala kwenye mji mkuu Harare.
Bwana Mugabe amekuwa chini ya kuzuizi cha nyumbani kwa siku kadhaa huku kukiwa na mvutano kuhusu ni nani atamrithi.
Jeshi lilisema Ijumaa kuwa lilikuwa kwenye mazungumzo na Mugabe na litaujulisha umma kuhusu matokeo ya mazunngumoz hayo haraka iwezekanavyo.
Mtu moja aliyeshuhudia alinukuliwa na Reuters akisema kuwa Mugabe alishangiliwa wakati wa sherehe baada ya kuzungumza.
Jeshi lilichukua madaraka baada ya Mugabe kmfuta kazi makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita, na kuashiria kuwa alimpendelea mkewe kuweza kuchukua ungonizi wa Zanu-PF na urais.

Darleen ameachia wimbo mpya ‘Touch’, producer wa wimbo ni Laizer

Msanii wa muziki Bongo kutoka label ya WCB, Queen Darleen ameachia wimbo mpya ‘Touch’, producer wa wimbo ni Laizer.

MAGAZETI MATATU YA PEWA ONYO NA BUNGE LA TANZANIA

   
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limetoa onyo kali kwa magazeti na Wahariri wa gazeti la MtanzaniaMwananchi na Nipashe kwa kosa la kuchapisha na kusambaza mwenendo wa shauri lililokuwa likifanyiwa kazi na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge