December 28, 2017

wemasepetu ampashavu paul makonda

Image result for picha ya wema sepetu na makonda

Wema na RC Makonda
Malkia wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu ameonyesha kuguswa na utendaji mzuri wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

Muigizaji huyo toka arejee Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitokea CHADEMA, amekuwa karibu zaidi na mkuu huyo wa mkoa.
Alhamisi hii Wema amepost picha ya mkuu huyo na kuandika ujumbe unaowataka wakazi wa Dar es salaam kujivunia mkuu huyo kutokana na utendaji wake wa kazi.
“Tanzania Kwanza. Katika vitu ambavyo Dar pia inatakiwa kujivunia ni kupata RC mwenye akili nyingi… Mungu akakutangulie katika kazi zako za lengo la kuijenga Tanzania yako izidi kuwa zaidi ya ilipo sasa,” aliandika Wema.
Aliongeza, “Ipo siku wataelewa tu, The Man Himself… Call Him Mr Dar-es-salaam… Viva RC wangu…. Viva Rais wangu…. #UzalendoKwanza … cc @paulmakonda May everything you wish well for your Nation Be…. We support you fully,”
Muigizaji huyo bado anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya baada ya kudaiwa kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake kupitia kampeni ya kupambana na dawa za kulevya iliyoanzishwa na RC Makonda.

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara klabu ya Yanga

Image result for PICHA YA YANGA

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara klabu ya Yanga, kupitia kwa msemaji wake Dismas Ten imekiri kuwa kupata matokeo dhidi ya Mbao FC imekuwa ni jambo mgumu lakini wamejipanga vyema kwa mchezo wa Jumapili.
Ten amekiri ugumu huo wakati akiongelea maandalizi ya Yanga kuelekea mchezo huo ambao utapigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
“Hatujawahi kupata matokeo dhidi ya Mbao FC, imekuwa ni mechi ngumu kila tunapokutana nao lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata hizo alama tatu kabla ya kwenda kwenye Kombe la Mapinduzi”, amesema Ten.
Yanga imekuwa ikipata wakati mgumu inapokutana na Mbao FC tangu ilipopanda daraja misimu miwili iliyopita ambapo katika mechi nne za ligi Yanga haijashinda hata mechi moja.
Yanga kwasasa inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 22 nyuma ya Simba SC na Azam FC zenye alama 23 kila mmoja. Ligi kuu itaendelea wikiendi hii kwa mechi za raundi ya 12 kupigwa. 

MMESSI AZIDI KUWA JEURI

Image result for PICHA YA MESSI

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema Lionel Messi ndio mtu anayeifanya Barcelona iwe timu yenye nafasi kubwa ya kutwaa Ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu.
Guardiola ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari ambaye alimuuliza kuhusu timu yake ya Man City kama ina nafasi kubwa ya kushinda ubingwa wa Ulaya msimu huu.
Pep alimjibu mwandishi kwa kumuuliza swali kuwa, “Ni timu gani anachezea Lionel Messi”, ? Baada ya mwandishi kujibu kuwa ni Barcelona ndipo Guardiola akamwambia kuwa ndio timu yenye nafasi ya kutwaa UEFA.
Guardiola alifafanua kuwa aina ya uchezaji wa Barcelona kwa sasa ni hatari zaidi kwani wanaanza kumiliki mpira kwenye eneo la ushambuliaji kwa kumtumia zaidi Messi.
“Hakuna asiyejua ubora wa Messi, na kama Barcelona inamtumia kwenye eneo la adui unategemea nini kama sio kukumaliza tu mpinzani”, ameeleza Guardiola.

Nawapongeza sana baadhi ya viongozi wa dini kama vile Askofu Kakobe, Askofu Gwajima,

Nawapongeza sana baadhi ya viongozi wa dini kama vile Askofu Kakobe, Askofu Gwajima, 
Image result for PICHA YA KAKOBE NA GWAJIMA
Mchungaji Msigwa ameweka wazi kuwa hicho kilikuwa kilio chake kikubwa kwa viongozi wa dini kwani Tanzania inapaswa kujengwa na watu wote na si wanasiasa tu 
"Nawapongeza sana baadhi ya viongozi wa dini kama vile Askofu Kakobe, Askofu Gwajima, Askofu Bagonza na Shayo ambao kwa namna moja kimekuwa kilio changu kikubwa pamoja na wananchi wengine kuona viongozi wa dini wanakuwa kimya wakati mambo hayaendi vizuri, Kwa kifupi niwapongeze sana kwa sababu nchi hii inajengwa na sisi sote na mali yetu sote" alisema Msigwa 
Aidha Mchungaji Msigwa aliendelea kusema kuwa yeye amesikitiswa na baadhi ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wanataka kulifanya Taifa la Tanzania lisiwe la watu wa kufikiri 
"Hoja alizotoa Askofu Kakobe zinafafanua vizuri na kuwafanya watu wafikiri na kujibu kwa hoja lakini watu wameanza kumshambulia kwa kejeli na maneno ambayo si ya kiugwana, hoja siku zote hujengwa kwa hoja hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria, Kakobe alimuomba Mhe. Magufuli akatubu kwamba anaiendesha nchi kama vile nchi ya chama kimoja" Alisisitiza Msigwa 

Iraq na Syria zimetangaza ushindi dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu

Iraq na Syria zimetangaza ushindi dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu
Syrien Rakka (Getty Images/D.Souleiman)

Iraq na Syria zimetangaza ushindi dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu katika wiki za karibuni, baada ya mwaka mmoja ulioshuhudia mataifa ya nchi hizo, washirika kadhaa wa kimataifa na vikosi mbalimbali vya ndani vikiwafurusha wapiganaji kutoka miji na vijiji vilivyounda himaya ya ukhalifa lililokuwa limejitangazia kundi hilo.
Marekani imeongoza muungano wa kijeshi wa kimataifa ulioendesha kampeshi ya mashambulizi ya ndege dhidi ya Dola la Kiislamu tangu 2014, wakati kundi hilo lilipoteka theluthi moja ya ardhi ya Iraq. Wanajeshi wa Marekani wametumika kama washauri kwa vikosi vya ardhini vya Iraq na makundi ya Kikurdi na Kiarabu nchini Syria.
Muungano huo umeliambia shirika la habari la reuters katika taarifa kwa njia ya barua pepe, kwamba kuna magaidi chini ya 1,000 wa IS katika eneo lao la pamoja la operesheni, ambapo wengi wao wanaendelea kusakwa katika maeneo ya jangwa mashariki mwa Syria na magharibi mwa Iraq. Idadi hiyo haihusishi maeneo ya magharibi mwa Syria yalio chini ya udhibiti wa serikali ya rais Bashar al-Assad na washirika wake.
Irak - Rawa vom IS befreit (Reuters/O. Waheeb)
Wanajeshi wa Iraq wakionyesha alama ya V kuashiria ushindi dhidi ya IS.
Mshirika mkuu wa Assad, Urusi nayo imetangaza leo kuwa vita kuu na Dola la Kiislamu vimekwisha. Waziri wa mambo ya kigeni Sergei Lavrov, alisema jukumu muhimu kwa sasa ni kuliangamiza kundi jengine la Kiislamu, la Nusra Front.
"Jeshi la Syria, pamoja na washirika wake na kwa msaada wetu, linapambana na wapiganaji wa Al-Nusra Front, lakini wanaweka upinzani, kutokana kwa sehemu, kwa mujibu wa taarifa tulizo nazo, na msaada wa kutoka nje," alisema Lavrov alipokutana na kiongozi wa upinzani kutoka Syria Ahmed Jarba mjini Moscow.
Muungano wa Marekani ulisema Desemba 5 kwamba kulikuwa na chini ya wapiganaji 3000 waliosalia. Iraq ilitangaza ushindi wa mwisho dhidi ya kundi hilo Desemba 9. Muungano huo umesema wengi wa wapiganaji hao ama waliuawa ua kutekwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Urusi yaituhumu Marekani kwa kuwapa mafunzo IS
Wakati huohuo, mkuu wa wa majeshi ya Urusi ameituhumu Marekani kwa kuwapa mafunzo wapiganaji wa zamani wa IS nchini Syria, ili kuivuruga nchi hiyo, madai yake yakijikita kwenye kituo cha kijeshi cha Marekani kilichopo kwenye eneo la kimkakati la Taf kwenye kivuko kati ya Syria na Iraq. Urusi inasema kituo hicho kipo kinyume na sheria na kwamba chenye pamoja na eneo linalokizunguka vimekuwa tundu jeusi ambamo wapiganaji wanaendesha shughuli zao bila kizuwizi.
Syrien Kampf um Rakka (Reuters/R. Said)
Mpiganaji wa kundi la SDF akionyesha alama ya V baada ya ushindi dhidi ya IS mjini Raqqa.
Na kwingineko shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema wapiganaji kutoka jamii ya Yazidi ya nchini Iraq, ambayo ilikandamizwa vibaya na Dola la Kiislamu, wamliwauwa raia 52 katika tukio linalodhihirika wazi kuwa la ulipizaji kisasi, baada ya kuteka maeneo kutpkakwa wapiganaji hao.
Human Rights Watch imesema katika ripoti yake kuwa ndugu wa wahanga hao waliiambia kuwa Juni 4, 2017, vikosi vya Yazidi viliwazuwia na kuwachinja wanaume, wanawake na watoto, kutoka familia nane za kabila la Wasunni la Al-Bu Metewut, ambao walikuwa wakikimbia mapingano kati ya IS na wapiganaji wanaoiunga mkono serikali kaskazini mwa mji wa Mosul.

Mwanajeshi apigwa risasi




Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kikosi cha Makambako (KJ 514) ambaye amefahamika kwa jina la Neema Masanja amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na mchumba wake ambaye ni askari wa Jeshi la Polisi Makambako mkoani Njombe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Prudensiana Protas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo mapema jana na kusema kuwa Askari wa jeshi la polisi Makambako mkoani Njombe ambaye anafahamika kwa jina la Zakayo Dotto alifanya tukio hilo la mauaji kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi. 
Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kumtafuta mtuhumiwa Zakayo Dotto ambaye baada ya kufanya tukio hilo la mauaji alikimbia kusikojulikana.