Ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imezuiliwa nchini Canada muda wowote itatatua nchini baada ya kuachiwa.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa asubuhi ya leo kupitia ukurasa wake wa twitter.
“Ndege yetu aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imezuiliwa nchini Canada ilikwishaondoka Canada kuja Tanzania. Aidha, ndege kubwa nyingine 3 (2 Bombardier CS300 kutoka Canada & 1 Boeing 787-8 Dreamliner kutoka Marekani) zitawasili baadaye mwaka huu,” amesema Msingwa.
No comments:
Post a Comment