April 30, 2018

Amuuwa mpenzi wake kwa kumnyonga




Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia kijana aliyefahamika kwa jina la Nicholas Light (25) mkazi wa Mtaa wa Mahama Ilemela kwa kunyonga mpenzi wake Victoria Swai (26).
Inadaiwa kijana huyo alifanya mauaji hayo kwa kumkaba shingo mpenzi wake huyo hali iliyopelekea kukosa hewa na baadae kufariki dunia.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kudai tukio hilo limetokea katika jengo la Ekacliff ofisi ya Kilimanjaro Avitaion.
Katika tukio hilo polisi walifanya uchunguzi katika nyumba alipokuwa akiishi marehemu na mpenzi wake na kumkuta mtuhumiwa akiwa amejificha juu ya dari ya nyumba.
Chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa kuwa ni  wivu wa kimapenzi ambapo mtuhumiwa huyo  alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa alikuwa akimsaliti kimapenzi ambapo  mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi, pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

Hatujaridhika kwa kumfunga Yanga........ ANGALIA SYLAS TV









Manara ametoa kauli hiyo mara baada ya 'Kariakoo Derby' kumalizika katika uwanja vya Taifa Jijini Dar es Salaam huku timu yake ikiwa imetoka na ushindi wa bao 1 lililofungwa mnamo mwa dakika 38 kupitia Erasto Nyoni kwa kutumia kichwa akiunganisha krosi ya Kichuya.

"Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumepata matokeo ila hatujaridhika bado mpaka tuwe mabingwa, 'perfomance' yetu kwa ujumla ilikuwa nzuri ndio maana hata 'corner' moja wenzetu hawakuweza kupata lakini sisi vilevile tulicheza kwa heshima", amesema Manara.
Pamoja na hayo, Manara ameendelea kwa kusema "kipindi cha kwanza kilipomalizika nilishuka chini nikazungumza na wachezaji wangu kuwa waende wakawafunge Yanga kwa heshima kwasababu wao ni mabingwa watetezi na msiende kuwafunga kwa dharau kwa hiyo niliwapa maelekezo madhuri vinginevyo tungewadharaulisha kwa kuwafunga mabao 5, 6 kwa hiyo tumewafunga kwa heshima kutokana ni wakubwa wenzetu".
Kutoka na ushindi walioupata jana Simba sasa wamekuwa wamefikisha alama 62 kwenye mechi 26 huku ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja kwenye ligi kuu msimu huu. Simba inabakiza alama 4 pekee ili iweze kuwa bingwa msimu huu.

    Hatujaridhika kwa kumfunga Yanga

                                                 ANGALIA HAPA SYLAS TV



April 29, 2018

Msafara wa JPM wasimamishwa


Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, umesimamishwa na wananchi wa eneo la Migori mkoani Iringa ili kutoa kero zao zinazowakabili, kwa kiongozi huyo mkubwa wa nchi.
Msafara huo ambao ulikuwa ukipita kuelekea mkoani Irnga kwa ajili ya tukio la uzinduzi wa barabara ya Iringa Migori  yenye urefu wa km 189, umelalamikiwa kero mbali mbali zinazowakabili wananchi wa eneo hilo pamoja na changamoto zinazoikabili shule ya sekondari Nyerere iliyopo mkoani Iringa, na kutoa fedha taslim shilingi milioni 5 ili kusaidia ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu.
Baada ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Walend Manga kuelezea hatua walizofikia za ujenzi wa nyumba za walimu wanazojenga kwa nguvu yao na wananchi, pamoja na kumshukuru Rais Magufuli kwa fedha zinazopelekwa mashuleni, Rais Magufuli alisikika akisema ..."Ahsante sana Mwalimu Mkuu, shule yenu ina jina zuri, jina la Nyerere, na mimi nitawaongezea milioni 5, sina milioni tano hapa!!? Hebu nisaidie hapa hapa kabisa, bahati nzuri nina milioni 5 hapa, nakupa hapa hapa, kazitumie vizuri, mimi huwa nafuatilia, siku moja nitapita hapa nicheki hizi milioni tano zimetumika wapi.
Sambamba na hilo Rais Magufuli amemtaka Mkandarasi aliyepewa jukumu la kusambaza miundombinu ya umeme kwenyye eneo hilo kukamilisha mapema, ili kuwaletea wananchi maendeleo.
CCM MKOA WA TABORA YA JIVUNIA 
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ANGALIA 
VIDEO SYLAS TV

Zimbabwe yaruhusu bangi kutumika






Nchi ya Zimbabwe imehalalisha uzalishaji wa bagi kwa matumizi ya kiafya na kisayansi.
Zimbabwe itakuwa nchi  pili kufanya hivyo barani Afrika baada ya Lesotho, ambayo ilitoa leseni yake ya kwanza kwa kilimo cha mmea huo mwaka uliopita.
Waziri wa afya David Parirenyatwa amechapisha sheria zinazowaruhusu watu na kampuni kupewa leseni ya kufanya kilimo cha bangi ambayo hufahamika nchini humo kama mbanje, na kwamba watu wa nchi hiyo sasa wanaweza kutuma maombi ya kulima bangi, na leseni yake itakuwa inaombwa upya kila baada ya miaka mitano, na itawaruhusu wakulima kumiliki, kusafirisha na kuuza bangi.
Watuma maombi watatakiwa kueleza ni wapi watafanyia kilimo chao, kiwango ambacho wataweza kuzalisha na kuuza na wakati wa kuzalisha bangi hiyo.
Nchini Zimbabwe ilikuwa ni haramu kupanda, kumiliki au kutumia mmea huo nchini Humo, na iwapo mtu atapatikana na makosa hayo anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 12 jela.
MARUFUKU POLISI KUKATA BANGI 
ANGALIA VIDEO SYLAS TV


wasanii wa tanzania kufaidika



Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeumizwa vikali na baadhi ya makampuni yanayowatumia vibaya wasanii wa muziki na waigizaji wa filamu kwenye matangazo yao kwa kuingia nao mikataba mibovu ambayo haina faida kwa watu hao.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe juzi bungeni wakati akihitimisha mjadala wa makadirio ya bajeti ya wizara yake.
Waziri Mwakyembe amesema amechukizwa na kitendo cha Mzee Majuto kuomba achangiwe fedha kwa ajili ya matibabu ile hali anaonekana karibia nusu ya mabango yote ya matangazo hapa nchini na kutangaza kiama kwa makampuni na taasisi zinazonyonya wasanii.
Kwa kweli dhuluma kwa wasanii ilikuwapo kubwa sana kwa kutumia ‘middle men’ (watu wa kati), watu wenye fedha wamechezea sana wasanii wetu. Hili limeanza kubadilika tumeanza kuwa-empower (kuwawezesha) wasanii wetu kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wasitumie middle men,“ameeleza Waziri Mwakyembe.
Kwa mfano vijana wetu wazuri kama kina Kanumba, amefariki kila mtu anajua ni milionea, hapana.. waliotajirika ni wengine. Leo hii mwanasanaa mzuri mzee majuto anaumwa, anaomba fedha, mimi nachanga kutoka mfuko kwangu, maisha yenyewe unayaelewa waheshimiwa.. lakini nusu ya mabango ya biashara ni ya Mzee Majuto.“amesema Mwakyembe.
Hata hivyo, Waziri Mwakyembe tayari ameshateua kamati maalumu ya wanasheria ambayo itapitia upya mikataba yote ya wasanii na waigizaji kwa kuanzia na Makampuni yaliyowahi kufanya kazi na Mzee Majuto na Marehemu Steven Kanumba.
Naomba sasa nitumie nafasi hii kueleza kwamba nimeunda Kamati ya wanasheria, tunaanza na kesi ya Mzee Majuto, Mashirika yote na makampuni yote yaliyoingia mikataba na Mzee Majuto tutaipitia upya mikataba hiyo, kama ameonewa ni lazima ilipwe familia yake, tumeshachoka. Na tukishamaliza tunarudi kwa Kanumba na msanii yeyote ambaye anaona aliingia mkataba wa kipumbavu aje atuone.“amemaliza Waziri Mwakyembe.
Familia ya Mzee Majuto Jumatano Aprili 25, 2018 ilijitokeza kuomba msaada wa hali na mali kwa Watanzania ili aweze kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Tanzania yaomba ufadhili wa mradi tiegler Gorge kutoka AfDB

Image result for tanzania

Tanzania imeiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kufadhili mradi wake wa kuzalisha umeme wa maji wa megawati 2,100 katika maporomoko ya Mto Rufiji.

Taifa hilo la Afrika Mashariki linauangalia mradi huo wa Stiegler Gorge katika Hifadhi ya Mbuga ya Selous inayotambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu na Utamaduni (UNESCO) kama urithi wa dunia kuwa muhimu katika kukomesha tatizo sugu la uhaba wa umeme nchini humo. Wizara ya Fedha ya Tanzania imesema katika taarifa yake ya jana Jumamosi kwamba Rais John Magufuli,

ambaye anahusika moja kwa moja katika mradi huo uliozorota kwa muda mrefu, aliwasilisha ombi hilo la fedha kwa Rais Akinwumi Adesina wa Benki ya AfDB wakati wa mazungumzo nchini Tanzania katika mji mkuu wa Dodoma 
mwishoni mwa wiki. AfDB imethibitisha kwamba imelipitia 
ombi la Magufuli lakini halikutaja gharama za mradi huo. Lakini wakosoaji wanasema kupata ufadhili wa mradi huo itakuwa vigumu kwa sababu ujenzi wa bwawa la maji katika mto unaopita katika hifadhi ya Selous utaathiri wanyama pori na makaazi yao.

AIBU YA KUMBA NANDI ANGALIA SYLAS TV 
hapachini

MBUNGE MSUKUMA awasha moto na makonda


Image result for makonda na msukuma

mbunge msukuma amtaka makonda kufanya  kazi ambazo zina muhusu asiingilie bunge kwani amesha itia hasala serikali 
angalia hapa alicho kisema MSUKUMA KUHUSU MAKONDA

ANGALIA HAPA SYLAS TV



mpoki aitabilia yanga kushindwa mechi zidi ya simba ........angalia hapa sylas tv alicho kisema mpoki


Image result for yanga



simba ni timuu kubwa kama iliweza kuwa ambia mashabiki wake wa halibu viti basi kwa umoja huo wata wa ambia wakaibe kombe simba wanaumoja


Image result for mpoki




angalia hapa chini alicho kisema mpoki

TIMU ya Jang’ombe Boys ya Zanzibar imetwaa ubingwa

Image result for TIMU ya Jang’ombe Boys

TIMU ya Jang’ombe Boys ya Zanzibar imetwaa ubingwa wa mashindano ya Muungano baada ya kuifunga Karume Market ya Dar es Salaam kwa penalti 6-5 katika mchezo uliochezwa juzi Uwanja wa Bandari, Temeke.
Karume Market ambao ni mabingwa wa Mkoa wa Dar es Salaam walianza kupata bao lililofungwa na Eddy Ngalambe na kudumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko ambapo Jang’ombe Boys ilianza kuliandama lango la Karume Market huku wakipigiana pasi moja moja na kupata bao kwa mkwaju wa penalti lililofungwa na Mustafa Hassan na kufanya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 1-1 na kulazimika kupigiana penalti.
Karume Market ilipiga penalti saba na kupata tano na Jang’ombe walipiga sita na kukosa moja na kufanya waibuke mabingwa kwa penalti 6-5.
Akizungumza kabla ya kukabidhi kombe Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Almas Kasongo alisema mashindano ya Muungano ni mwanzo wa kuendeleza mahusiano ya kisoka kwa Zanzibar na Mkoa wa Dar es Salaam.
“Mapema mwaka huu tumekubaliana na ZFA kuwa na mashindano ya Muungano na leo hii tumeanza utekelezaji wake na lengo la mashindano ni kuendeleza mahusiano ya kisoka na wenzetu wa Zanzibar ndio maana hapo unawaona viongozi wa ZFA,” alisema Kasongo.
Fainali hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwepo wenyeviti vya vyama vya soka Ubungo, Temeke, Ilala pamoja na wajumbe wa kamati mbalimbali za DRFA na wengine toka Zanzibar.

TIMU ya Jang’ombe Boys ya Zanzibar imetwaa ubingwa wa mashindano ya Muungano baada ya kuifunga Karume Market ya Dar es Salaam kwa penalti 6-5 katika mchezo uliochezwa juzi Uwanja wa Bandari, Temeke.
Karume Market ambao ni mabingwa wa Mkoa wa Dar es Salaam walianza kupata bao lililofungwa na Eddy Ngalambe na kudumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko ambapo Jang’ombe Boys ilianza kuliandama lango la Karume Market huku wakipigiana pasi moja moja na kupata bao kwa mkwaju wa penalti lililofungwa na Mustafa Hassan na kufanya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 1-1 na kulazimika kupigiana penalti.
Karume Market ilipiga penalti saba na kupata tano na Jang’ombe walipiga sita na kukosa moja na kufanya waibuke mabingwa kwa penalti 6-5.
Akizungumza kabla ya kukabidhi kombe Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Almas Kasongo alisema mashindano ya Muungano ni mwanzo wa kuendeleza mahusiano ya kisoka kwa Zanzibar na Mkoa wa Dar es Salaam.
“Mapema mwaka huu tumekubaliana na ZFA kuwa na mashindano ya Muungano na leo hii tumeanza utekelezaji wake na lengo la mashindano ni kuendeleza mahusiano ya kisoka na wenzetu wa Zanzibar ndio maana hapo unawaona viongozi wa ZFA,” alisema Kasongo.
Fainali hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwepo wenyeviti vya vyama vya soka Ubungo, Temeke, Ilala pamoja na wajumbe wa kamati mbalimbali za DRFA na wengine toka Zanzibar.

baraza huru la habari


VYOMBO vya habari nchini vimetakiwa kuanza mchakato mara moja wa kuanzishwa kwa Bodi ya Ithibati na Baraza Huru la Habari ambalo litawatambua wanahabari kama wanataaluma, lakini pia kusimamia haki na maslahi yao.
Baada ya kuanza kutumika rasmi kwa Kanuni za Maudhui mitandaoni, redioni na kwenye runinga, tayari maombi 86 ya blogu, majukwaa ya kimtandao, redio na televisheni za mitandaoni zinazotaka kujisajili yametumwa kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe aliyasema hayo bungeni Dodoma wakati akihitimisha hoja ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/19.
Dk Mwakyembe alisema kutokana na ukosefu wa chombo hicho ambacho kiko kwa mujibu wa Kanuni zilizo chini ya Sheria ya Huduma za Habari Namba 12 ya Mwaka 2016, kwa sasa kazi ya uandishi wa habari haitambuliki kama taaluma na wanahabari wengi wanafanya kazi kwa katika mazingira magumu kimaslahi.
“Watu wa kuwaonea huruma ni waandishi wa vyombo vya habari binafsi, kuna waandishi wanapata mshahara wa kitumwa yaani upo hata chini ya kiwango cha kima cha chini…”
“…Hakuna mkataba wa kazi, kwa kweli vijana wangu wanachezewa sana, hawawekewi hata bima wala kuingiziwa kwenye mifuko ya hifadhi. Undeni Media Council (Baraza la Habari) yenu tutawasaidia, chini ya sheria hii mtakuwa na ajira inayowalinda wengi,” amesisitiza.
Amesema katika majadiliano ya kupitisha bajeti hiyo, wabunge wengi ikiwemo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, walihoji kwa nini mpaka sasa serikali haijaliunda baraza hilo wakati sheria na kanuni zilishatoka na kuanza kutumika.
Alisema pamoja na kwamba katika bajeti ya mwaka 2018/19 wizara yake imeomba fedha za uanzishwaji wa chombo hicho cha Bodi ya Ithibati na Baraza Huru la Habari, mchakato mzima wa uanzishwaji wake unavihusu zaidi vyombo vyenyewe vya habari.
“Kwa sababu serikali ikianzisha yenyewe, yataanza maneno kwamba chombo hiki hakiko huru, naomba vyombo vya habari vijitokeze tuunde hii bodi. Lengo kubwa la serikali ni hivi vyombo vijiendeshe vyenyewe,” alisema.
Akizungumzia kanuni mpya zilizo chini ya Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta ya mwaka 2010, alisema tayari watumiaji wa blogu, majukwaa ya mitandao, redio na televisheni za mitandaoni wameanza utekelezaji wa kanuni hizo na 86 wametuma maombi ya kusajiliwa.
Alisema sababu hasa za serikali kuanzisha kanuni hizo ni kutokana na ukweli kuwa vyombo hivyo, hivi sasa duniani vinabeba nafasi sawa na vyombo rasmi vya habari katika kuhabarisha.
“Naamini ndani ya miaka mitatu vitakuwa vikubwa kuliko vile rasmi. Redio na runinga za mitandaoni na majukwaa mitandaoni vimeanza kuwa muhimu katika kuhabarishana, tatizo havina utambulisho rasmi kwamba ni wanahabari, hawana miiko ya uandishi wa habari, hawabanwi na maadili yoyote, hawalipi kodi pamoja na kwamba wanashindana na vyombo rasmi hii si fair (haki),” alisisitiza.
Alisema kutokana na matumizi makubwa ya vyombo hivyo vya habari kupitia mitandaoni, siku hizi mtu anaweza asisome gazeti hata kwa wiki nzima, lakini akiendelea kupata habari zote kupitia majukwaa hayo ya mtandaoni, blogu, redio na runinga za mtandaoni.
Alieleza kuwa kuwekwa kwa kanuni hizo kunalenga kuvidhibiti vyombo hivyo kimaadili na kuvitambua kitaaluma kwa kuwa uendeshaji wake wa sasa una changamoto kubwa ya ukosefu wa maadili na miiko ya taaluma ya uandishi wa habari.
“Hivi vyombo vina changamoto kubwa, lazima viwe na maadili na miiko. Tatizo la vyombo vya mitandaoni vimejaa fake news, wapotoshaji na waongo. Kuna nchi zimekaribia kwenda vitani kwa ajili ya vyombo hivi,” alifafanua.
Alieleza kuwa asilimia 75 ya nchi duniani zimechukua hatua kudhibiti maudhui kwenye mitandao.


Alitaja baadhi ya nchi zilizoweka udhibiti wa maudhui ya mtandaoni kuwa ni Marekani, Australia, Uingereza, Canada na India ambapo sasa Tanzania nayo imeona wajibu wa kulinda maudhi hayo ya mitandao. Bunge liliidhinisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/19 ya Sh bilioni 33.3 ambapo kati ya fedha hizo mishahara ni Sh bilioni 12.2, matumizi mengine ni Sh bilioni 9.3 na miradi ya maendeleo ni Sh bilioni 8.7.

Yanga yatangaza mbinu zake za kuikarisha Simba


Yakiwa yamebakia masaa kadhaa kuelekea katika mtanange wa kukata na shoka 'Kariakoo derby', klabu ya Yanga imeibuka na kudai hawana shaka yeyote kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Simba kwani wao wanachosubiri ni dakika 90 za uwanjani nasio kitu kingine.

Hayo yamebainisha na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga Dismas Ten na kusema kuwa maandaalizi ya mechi hiyo yamekamilika kwa asilimia 100.
"Mazoezi ya siku nane yamefanyika kwa umakini mkubwa  kwa upande wa timu na kwa upande wa uongozi maanadalizi yote muhimu yamekwisha fanyika na kinachosubiriwa sasa ni dakika 90 za uwanjani. Hali ya wachezaji ipo vizuri kabisa kasoro Ngoma pekee bado yuko nje ya kikosi kwa majeraha. Suala la nani ataanza au kutocheza tumewaachia benchi la ufundi kuona nani wanaweza kumtumia kulingana na ‘game plan’ waliyokuwa nayo", amesema Dismas.
Katika hatua nyingine Kocha Zahera Mwinyi amesema ameridhishwa na uwezo wa wachezaji waliopo kwenye kikosi cha Yanga,anachohitaji ni muda wa kukaa nao ili aendelee kuwajenga na kuwaimarisha zaidi tayari kwa michezo ya kimataifa.
makonda na msukuma ulingoni
angalia hapa chini

Wanajihadi waua zaidi ya watu 30

Image result for Zaidi ya watu 30 wa kabila la Tuareg wameuliwa


Zaidi ya watu 30 wa kabila la Tuareg wameuliwa na wapiganaji wa kijihadi nchini Mali katika eneo la kaskazini-mashariki linalopakana na Niger. 

Kundi la zamani la waasi wa Tuareg la MSA pamoja na viongozi wa makabila wamesema, shambulio hilo limetokea siku moja baada ya washambuliaji waliokuwa katika pikipiki kuwauwa watu 12 karibu na eneo la Anderamboukane. 

Katika wiki za hivi karibuni, kumezuka vurugu upya katika taifa hilo la Afrika. Mapema mwezi huu, kambi ya Umoja wa Mataifa katika mji wa Timbuktu ilishambuliwa kwa mabomu ya roketi na mabomu yaliyotegwa ndani ya magari, na kuua askari mmoja wa kulinda amani na kujeruhi wengine saba. Umoja wa Mataifa umeonya mwezi uliopita kwamba usalama unazidi kuzorota nchini Mali, na vurugu zinasambaa hadi nchi jirani. 

 msukuma na makonda ulingoni
angalia video sylas denniss


April 27, 2018

mpango wa ndege za kivita Ujerumani na Ufaransa



ILA Air Show in Berlin 2018 | Florence Parly & Ursula von der Leyen (Reuters/)


Ujerumani na Ufaransa zimekubaliana kuhusu mahitaji makuu kwa ajili ya ndege mpya ya kivita kuchukuwa nafasi ya Typhoon ya Eurofighter na Rafale kuanzia 2040, kulingana na duru za wizara ya ulinzi ya Ujeurmani
Hatua hii itaanzisha mradi uliozinduliwa kwa mara ya kwanza Julai mwaka jana na maafisa kutoka mataifa yote mawili watasaini waraka wa uainishaji kandoni mwa maonyesho ya ndege za kivita ya Berlin ILA, yaliofunguliwa na kansela Angelea Merkel siku ya Jumatano. 
Pamoja na kuwa na uwezo wa kufanyakazi kivyake, au kuongoza kundi lingine la ndege zikiwemo zisizo na rubani, ndege hiyo itahitaji pia kuwa na uwezo wa kuendesha operesheni za mashambulizi na kujihami, walisema maafisa wa wizara ya ulinzi ya Ujerumani.
Ilikuwa haijaamuliwa bado iwapo ndege hiyo mpya itakuwa inaendeshwa tu na rubani au itakuwa pia na toleo la isiyokuwa na rubani. Lengo ni kuanza kuzitumia ndege hizo mpya, zikiwa na uwezo wenye mipaka, kuanzia mwaka 2040.

sikiliza hapa chini sylas tv


April 26, 2018

KOCHA Mkuu wa timu ya Majimaji FC ya Songea mkoani Ruvuma, Peter Mhina ameahidi ushindi


Image result for majimaji fc



KOCHA Mkuu wa timu ya Majimaji FC ya Songea mkoani Ruvuma, Peter Mhina ameahidi ushindi kuelekea mchezo wake wa wikiendi hii dhidi ya Ruvu Shooting katika Uwanja wa CCM mjini Songea.
Akizungumza na gazeti hili, Mhina alisema timu yake imekuwa ikijiandaa vyema na mchezo huo tokea irejee kutoka mkoani Mwanza ilipocheza na Mbao FC na kutoka sare ya 2-2.
Alisema wamefanya mazoezi vya kutosha, ambapo katika mazoezi hayo alisema wamefanikiwa kurekebisha makosa yao yaliopelekea kupata sare dhidi ya Mbao FC.
Mhina alisema amewajenga vyema vijana wake kisaikolojia ili kuhakikisha wanapambana na kushinda dhidi ya Ruvu Shooting.
Alisema ana imani kubwa sana na timu yake itapambana na kuweza kuibuka na ushindi.
Mchezaji huyo wa zamani wa timu za African Sports na Maji Maji FC alisema atahakikisha wanashinda na mechi zao zote zilizobakia dhidi ya Azam FC, Singida United, Mtibwa Sugar na Simba SC.
Katika msimamo wa Ligi Kuu, Majimaji ina alama 20 ipo katika nafasi ya 15. Timu hiyo imeshinda mechi 3, sare 11 na kupoteza mechi 11.

Polisi Tanzania yatishia kuwapiga waandamanaji


Tanzania imesambaza askari polisi katika miji mikubwa nchini humo Jumatano, katika juhudi za kuzuwia maandamanao ya kuipinga serikali yalioitishwa mwanaharakati Mtanzania anaeishi Marekani.
Tansania Polizei auf Straße (DW/Ericky Boniphace)
Maandamao hayo yaliyopigwa marufuku - ambayo yalipangwa kufanyika Alhamisi katika maadhimisho ya muungano kati Tanganyika na Zanzibar, yaliitishwa na mwanaharakati aliejipeleka uhamishoni nchini Marekani Mange Kimambi.
"Wanaopanga kuandamana kesho watakiona cha moto, watapigwa kama mbwa koko." Alisema Gilles Muroto kamanda wa jeshi la polisi wa mji mkuu wa utawala wa Dodoma wakati akiongea na waandishi wa habari siku ya Jumatano.
Hofu ya kurudi Tanzania
Katika mji wa kaskazini mwa Tanzania wa Arusha, ambao ni ngome ya upinzani polisi iliwakamata Jumanne watu saba ikiwatuhumu kwa kuwahamasisha Watanzania kushiriki katika maandamano hayo yaliopigwa marufuku.

Tansania Polizei Verstärkung in Ohio (DW/E.Boniphace )

Anasema kuwa anaogopa kurudi Tanzania kwa kuhofia kunyanyaswa na serikali kwa sababu ya kuwakosoa viongozi wenye mamlaka. Picha za kwenye televisheni zinaonesha askari polisi walio na silaha wakiwa katika miji kadhaa mikubwa ya Tanzania na kuwonya wanachi wasishiriki maandamano ambayo yamepigwa marufuku na serikali.Mange Kimambi anayeishi Los Angeles nchini Marekani, anawafuasi milioni 1.8 katika mtandao wa kijamii wa Instagram ambako anajipambanua kama mwanaharakati wa demokrasia, Mtanzania mwenye fahari."
Hofu ya kuutia doa utawala wa Magufuli
Maandamano nchi Tanzania hata kwa kiwango kidogo, yanatazamiwa kutia dosari kwa uongozi wa Rais John Pombe Magufuli anaedaiwa kuua upinzani na uhuru wa kujieleza tangu alipoingia madarakani rasmi mwaka 2015.
Magufuli alionya juma lililopita kuwa mtu yeyote anayepanga kuandamana, atakutana na mkono wa sheria na kusema kuwa kamwe serikali yake haitaruhusu mageuzi ya kiuchumi yaliofanyika kuharibiwa na waandamanaji wachache wasiotii sheria.
.

Lakini Kimambi alisisitiza katika mitandao ya kijamii kuhusu watu kuandamana Aprili 26, kushinikiza Magufuli aachie madaraka. Maandamano kama haya yaliwahi kuitisha tena na chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema mwaka 2016 lakini hayakufanikiwa kutokana na upinzani kutoka kwa serikali iliyopo madarakani.
Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulitoa tahadhari juu ya uwezekano wa kutokea vurugu kwa waandamanaji. Maria Sarungi Tsehai aliebobea katika masuala ya mawasiliano na mtu maarufu nchini Tanzania, mwezi huu aliandika katika blogu kuwa "Nguvu kubwa inayotumiwa na serikali kuzuia maandamano, inatosha kuonesha ushawishi alionao Mange Kimambi kwa vijana".
Aidha iliongeza kuwa, "kama mwanamke aliepo Los Agelea anaweza kuhamasisha watanzania kudai haki zao kupitia maandamano na kuitaka serikali iwajibike na viongozi wakubwa wa serikali wanatoa vitisho kuhusu hayo maandamano hiyo inadhihirisha kwamba athari za Mange Kimambi kwa serikali ni kubwa." Aliandika Tsehai.

Nani atatamba kati ya Bayern Munich na Real Madrid?

Nani atatamba kati ya Bayern Munich na Real Madrid?

Bayern Munich kuchuana na Real Madrid uwanjani Allianz Arena katika mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa
25.04.2018 Champions League: Bayern München gegen Real Madrid
25.04.2018 Fussball Champions League/ Hinspiel FC Bayern Muenchen gegen Real Madrid (picture-alliance/S. Simon)
Mtanange wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Bayern Munich na Real Madrid utakuwa mchuano wa kupigania pia ubabe wa soka la Ulaya. Kidumbwedumbwe hicho cha kwanza kati ya timu hizo mbili ni leo katika uga wa Allianz Arena.
Hii itakuwa mara ya 25 kwa timu hizo mbili kukutana katika soka la Ulaya, huku kila timu ikiwa imeshinda mara 11 na kutoka sare mara mbili. Leo usiku itakuwa mara ya saba kwa vilabu hivi kukutana katika nusu fainali. Katika mapambano yao yote, Real Madrid imefunga jumla ya mabao 37, Bayern mabao 36. 
Kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes amesema Real Madrid inapaswa kuwa na wasiwasi kuhusu Robert Lewandowski kama vile ambavyo Bayern Munich itakuwa inalenga kumdhibiti Cristiano Ronaldo.
Mabingwa hao wa Ujerumani wanawaalika Real katika mechi kali ya miamba ya Ulaya wakilenga kutwaa mataji matatu msimu huu. Bayern imethibitisha kuwa David Alaba hatashiriki mechi ya leo kutokana na jeraha la paja.
Macho wa Cristiano Ronaldo
Ronaldo amefunga mabao 42 katika mechi 39
Ronaldo amefunga mabao 42 katika mechi 39
Ronaldo amefunga mabao 42 katika mechi 39 wakati Lewandoswki ametikisa wavu mara 39 katika mechi 43. Mechi ya marudio ya nusu fainali kati ya timu hizo mbili itakuwa Mei mosi mjini Madrid.
Uchambuzi wa awali hasa umemlenga mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ambaye amefunga bao katika kila mechi zote 10 za Madrid katika Ligi ya Mabingwa msimu huu.
Amefunga mabao 9 katika mechi sita dhidi ya Bayern Munich.
Hata hivyo kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane ameonya kuwa Bayern Munich wako imara wakati huu kuliko walipowabandua nje ya kinyang'anyiro hicho msimu uliopita.
Zidane amesema kuwa watahitaji kuonyesha uchezaji wa kiwango cha juu dhidi ya Bayern, huku akiongeza kuwa suala kuwa waliwaondoa katika robo fainali msimu uliopita halijalishi lolote wakati huu.
Hapo jana, Liverpool iliwachabanga Roma mabao matano kwa mawili katika mechi ya kusisimua iliyochezwa uwanjani Anfield. Nyota wa Liverpool Mohamed Salah alifungia timu yake mabao mawili miongoni mwa mabao hayo matano na kuonesha umahiri wake

Kocha Bayern asema Real AMdris wanapigika

Bayern Munich ilipoteza nafasi kadhaa katika kipigo chao cha magoli 2-1 nyumbani dhidi ya Real Madrid katika duru ya kwanza ya nusu fainali ya Champions League, lakini Kocha Jupp Heynckes amesema bado wana matumaini.
Fußball Bundesliga FC Augsburg - FC Bayern (picture-alliance/dpa/A. Gebert)
Bayern walipaswa kuongoza kwa magoli kadhaa katika kipindi cha kwanza kutokana na fursa walizokuwa nazo Thomas Mueller, Robert Lewandowski, Mats Himmel na Franl Ribery.
Lakini Wajerumani hao waliangushwa na umalizaji mbaya isivyo kawaida, uliowaruhusu mabingwa watetezi Real Madrid kuchomoka na ushindi na kuwaacha Bayern katika hatari ya kuondolewa mashindanoni na klabu ya Uhispania kwa msimu wa tano mfululizo.
"Hatukati tamaa," alisema Heynckes, aliyeiongoza Bayern katika ushindi wa mataji matatu mwaka 2013. " Unapotengezena nafasi nyingi dhidi ya timu kama Real basi hii ni ishara pia kwamba hasimu wako anapigika."
"Hatuna cha kupoteza na tutacheza kwa uhuru. Pengine zaidi ya tulivyocheza katika duru ya kwanza kwa sababu mchezo wetu haukuwa imara kama ambavyo tungependa."
UEFA Champions League Halbfinale | FC Bayern München - Real Madrid | TOR Madrid (Reuters/M. Rehle)
Real Madrid wakifunga goli lao la kwanza kupitia kwa Marcelo, katika uwanja wa Alllianz Arena mjini Munich, Aprili 25,2018.
Majeraha ya mapema yawaponza
Bayern ilipata matatizo ya mapema kutokana na majeraha kwa Arjen Robben na Jerome Boateng lakini waliendelea kupenya ngome ya Real kwa urahisi katika dakika 45 za kwanza, huku walinzi wa klabu hiyo ya Uhispania wakipambana na kasi ya Ribery na Lewandowski.
Lakini badala ya kuongezea kwenye goli la ufunguzi la Joshua Kimmich alilolipachika wavuni katika dakika ya 28, walikubali goli la kusawazisha dakika ya 44 kupitia mkwaju uliopigwa kwa ustadi na Marcelo, baada ya Dani Carvajal kuupiga mpira kwa kichwa na kuangukia karibu na eneo alilokuwa Marcelo.
Baadaye kosa la kiulinzi lililofanywa na Rafinha liliwaruhusu real kufunga bao la ushindi na kuiacha Bayern ikihitaji ushindi mjini Madrid wiki ijayo ili kusonga mbele katika hatua ya fainali.
"Simlaumu yeyote lakini operesheni zetu za ulinzi katika magoli yote zilikuwa mbaya," alisema Heynckes. Umalizaji wetu pia haukuwa mzuri. Hatukuwa na umakini kama kawaida 

waandishi habari 14 wa tupwa gerezani


Image result for gerezani


Mahakama ya nchini Uturuki imetoa adhabu ya kifungo gerezani kwa waandishi habari 14 wa gazeti kuu la upinzani la nchini humo "Cumhuriyet" kwa makosa ya kuyaunga mkono makundi ya kigaidi.

 Mashirika ya kutetea haki za binadamu ikiwa pamoja na la Amnesty International na la waandishi wa habari wasio na mipaka wamelaumu vikali mashtaka dhidi ya waandishi hao huku kukiwa na wasiwasi mkubwa juu ya kubanwa uhuru wa vyombo vya habari nchini Uturuki.

 Kati waandishi 17 wa gazeti hilo waliofikishwa mahakamani watatu waliachiwa huru. Mhariri mkuu wa gazeti hilo Murat Sabuncu amepewa adhabu ya kifungo cha miaka 7 na nusu jela. Hata hivyo waandishi hao wanatazamiwa kukata rufaa.

simba ya zidi kutamba 
angalia hapa chini maneno ya mpoki




April 25, 2018

Uingereza yawatahadharisha raia wake maandamano

Bendera ya Uingereza
ikiwa wewe ni raia wa Uingereza na unapanga kusafiri kuelekea Tanzania wiki hii unatakiwa kuwa mwangalifu ili kuhakikisha kuwa haujipati katika maandamano ya kisiasa yanayopangwa kufanyika tarehe 26 Aprili .
Katika tahadhari ya usafiri iliotolewa na ubalozi wa Uingereza, wasafiri wameonywa kwamba ijapokuwa safari za kuelekea taifa hilo hazina matatizo yoyote, wageni wanaoingia nchini humo siku hiyo wanafaa kuwa makini kwani iwapo kutakuwa na maandano kunaweza kuwa na 'maafa'.
Kulingana na gazeti la The Citizen Tanzania, tahadhari hiyo ilitolewa kufuatia wito wa kufanyika kwa maandano dhidi ya serikali na mwanaharakati wa mtandaoni anayeishi nchini Marekani Mange Kimambi.
Anadai kwamba maandamano hayo ni ya kupinga ukandamizaji wa uhuru wa kisiasa na unyanyasaji wa haki za kibinaadamu.

Barua ilioandikwa na ubalozi wa Uingereza
Image captionBarua ilioandikwa na ubalozi wa Uingereza kwa vyombo vya habari nchini Tanzania

Serikali tayari imepinga madai hayo na kusema kuwa maandamano hayo yatakuwa kinyume na sheria.
Rais John Magufuli amesisitiza kuwa maafisa wa usalama watakabiliana na wale watakaoshiriki katika maandamano hayo.
''Kutokana na uzoefu wa hapo mbeleniu balozi wa Uingereza nchini Tanzania umeonya kwamba maafisa wa usalama nchini Tanzania huenda wakatumia vitoa machozi na hata risasi kukabiliana na mandamano yoyote haramu''.
''Kuweni makini mulipo na epukeni makundi makubwa ya watu ama maandamano ya umma'', ilisema taarifa hiyo.
Takriban raia 75,000 wa Uingereza hutembelea Tanzania kila mwaka.

Wamiliki wa mitandao ya kijamii Tanzania waanza kusajiliwa


YouTube Gewalt Symbolbild (picture-alliance/dpa/N. Armer)
Mamlaka  ya  Mawasiliano nchini  Tanzania  imetoa  muda wa  mwisho  wa  wiki  mbili  kwa  wamiliki wa blogu kuandikisha  mitandao yao  chini  ya  sheria  kali  za maudhui  ya  mitandao  ya  kijamii.

Mamlaka  ya  Mawasiliano nchini  Tanzania  imetoa  muda wa  mwisho  wa  wiki  mbili  kwa  wamiliki wa blogu kuandikisha  mitandao yao  chini  ya  sheria  kali  za maudhui  ya  mitandao  ya  kijamii, huku  kukiwa  na  wasi wasi  kwamba  serikali inabana  uhuru  wa  watumiaji  wa mtandao  wa  intaneti.
Sheria  iliyopitishwa  mwezi  Machi  inafanya  kuwa  lazima kwa  wenye  blogu  na  wamiliki  wa  majukwaa  ya mtandaoni  kama   televisheni  za  mtandao  wa  Youtube kujiandikisha  katika  serikali  na  kulipa  kiasi  cha  dola 900 sawa  na  zaidi  ya  shilingi  za  Tanzania  milioni 2  ili kupata  leseni. 
Wanaharakati  wa  kidijitali  wanasema  hatua  hiyo  ni sehemu nyengine ya ukandamizaji  wa  serikali  dhidi  ya upinzani  na  uhuru  wa  kutoa  maoni  unaofanywa  na serikali  ya  Rais  John Pombe  Magufuli, ambaye alichaguliwa  mwaka  2015 na  kuahidi  kuharakisha  ukuaji wa  uchumi  na  maendeleo.
Waombaji  wanatakiwa  kutoa  maelezo  ya  wadau, mtaji, uraia  wa  mmiliki, ujuzi wa  wafanyakazi na  mipango  ya mafunzo, pamoja  na  hati  ya malipo  ya  kodi.

angalia hapa video hapa 
sylas tv