May 31, 2018

Zitto atangaza kuungana na CHADEMA




Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ametangaza nia ya kushirikiana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Aikael Mbowe katika kupigania jimbo la Buyungu lililoachwa na Marehemu Mwalimu Kasuku Bilago.
Kupitia mtandao wake Zitto ameyaweka wazi hayo ambapo amesema kuwa kwa heshima ya Mwalimu Bilago yeye na Mbowe wamekubaliana kuwa watashawishi kuwepo na a Democratic Front Katika Jimbo la Buyungu. 
"ACT Wazalendo itaunga mkono mgombea wa CHADEMA au CHADEMA itaunga mkono mgombea wa ACT Wazalendo. Tunataka kuweka mgombea mmoja anayekubalika na Wananchi wa Buyungu na kufanya kampeni kwa pamoja mpaka ushindi" .
"Huu ni mwanzo wa harakati za kuwa na United Democratic Front dhidi ukandamizaji wa Demokrasia nchini na dhidi ya hali mbaya ya maisha ya watu wetu. Umoja wa zaidi ya vyama vya siasa ukihusisha vyama vya Wafanyakazi, vyama vya wakulima, vyama vya wafanyabiashara na wananchi wengine," Zitto.
Uchaguzi wa Buyungu utafanyika baadaye mwaka huu baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Kasuku Bilago kufariki dunia Mei 26, 2018.

BIBI ALITAKA KUNITOA SADAKA KWA WACHAWI

Mbunge auweka 'rehani' Urais wa JPM






Mbunge wa  Moshi Vijijini Antony Kalisti Komu ameamua kuweka nadhiri ya kuachana na siasa na kurudi kijijini kulima kwa kudai kuwa endapo katika uchaguzi mkuu wa 2020 watashindwa kumtoa rais Magufuli madarakani.
Nadhiri hiyo ya Komu imewekwa wazi na Katibu wa Itikadi na Uenezi ACT, Ado Shaibu ambaye amesema kwamba Mh. Komu ameyatoa hayo ya moyoni mbele yake na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe wakati wakiwa njiani kuelekea Kakonko kuupumzisha mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Kasuku Bilago.
"Miaka ya tisini tulikuwa na kizingiti cha kukabiliana na Nyerere. Yes, Nyerere campaigned against us, nchi nzima. Sasa hawana Nyerere. CCM imevurugwa maradufu na inaendelea kuvurugwa. CCM ya sasa si ile ya tisini au miaka iliyopita. Ni CCM mbovu iliyosheheni wageni na kuwaweka kando wabobezi na wakongwe" Komu.
Ameongeza "CCM ina-survive kwa nguvu ya dola na si nguvu ya hoja. Tukijipanga vizuri, tukawa well organised, tukawa focused kwenye kusimamia masuala yao na kuyaongoza vyema maeneo tunayoyaongoza, mambo yatabadilika. Jambo la msingi hasa nyinyi vijana ambao mnafuatwa na mnarubuniwa rubuniwa ni kusimama imara"
Mh. Komu amesisitiza "Kwa kweli mimi Magufuli tukimshindwa safari hii (2020) nitaachana na mageuzi na kurudi kwetu kijijini kulima". 
Mbali na hayo Mbunge huyo amewataka wabunge wa upinzani kujipanga na kujua kutumia fursa ndani ya utawala wa rais magufuli ili watanzania pasipo kujali vyama vyao waweze kuwaunga mkono

amber lulu  na nuh mziwanda wanyonyana sehem za siri

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 31.05.2018

Mourinho anamfuatilia Marko Arnautovic, Chelsea macho yao kwa Robert Lewandowski

Marko Arnautovic

Manchester United wanataka kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya mashambulizi wa kikosi cha West Ham Marko Arnautovic. The Hammers wananaweza kutaka malipo ya pauni £50m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Australia. (Sky Sports)
Lakini West Ham inasema hawataki kumuuza mshambuliaji huyo msimu huu. (Evening Standard)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alionekana katika mchezo wa kirafiki Jumatano baina ya Austria na Urusi , mchezo ambao aliucheza Arnautovic. (Vivaro News)
Chelsea wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji kutoka Poland Robert Lewandowski mwenye umri wa miaka 29 baada ya kutangaza kuwa anataka kuondoka Bayern Munich. (Mirror)
Meneja wa Manchester Jose MourinhoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMeneja wa Manchester United Jose Mourinho alionekana kwenye mechi iliyomuhusisha Arnautovic, huku kukiwa na fununu kwamba anamtaka kikosini
Liverpool inataka kumuuza mshambuliaji wao Mfaransa Nabil Fekir mwenye umri wa miaka 24 kwa Lyon kwa euro milioni 60m (Le Parisien)
Na Liverpool wanaye mlinda lango wa Barcelona Jasper Cillessen raia wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 29 kwenye orodha yake ya wachezaji wanaotaka kununua. (Mundo Deportivo)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Italia Jorginho, mwenye umri wa miaka 26, yuko tayari kujiunga na kikosi cha Manchester City kutoka Napoli baada ya kununuliwa kwa euro milioni hamsini baada ya kukubali mkataba wa miaka mitano na Man City. (La Gazzetta dello Sport)
Antoine GriezmannHaki miliki ya pichaAFP
Image captionAntoine Griezmann ameshauriwa asiondoke Atletico Madrid
Kocha wa timu ya Ufaransa Didier Deschamps amemshauri mshambuliaji wa safu ya mbele Antoine Griezmann, mwenye umri wa miaka 27, aendelee kubaki Atletico Madrid badala ya kujiunga na Barcelona. (RMC Sport)
Arsenal wamekamilisha mipango ya kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati ya Ufaransa Yacine Adli mwenye umri wa miaka 17 kutoka kikosi cha Paris St-Germain. (Mirror)
Aleksandar Mitrovic akiwa uwanjaniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionFulham watatakiwa kulipa karibu pauni milioni £20m kusaini mkataba na Mserbia Aleksandar Mitrovic anayeichezea Newcastler
Mshindi wa Kombe la Dunia akiwa na Brazil Ronaldo anataka kununua klabu ya Uhispania Real Valladolidkwa euro milioni 30. (O Globo)
Everton wanaweza kufufua tena azma yao ya kumtaka Mholanzi Patrick Van Aanholt, mwenye umri wa miaka 27 anayecheza katika safu ya ulinzi ya Crystal Palace (Daily Mail)
Newcastle wamepewa fursa ya kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati Joe Allen anayeichezea Stoke City akiwa na umri wa miaka 28. Anatokea Wales
Patrick Van AanholtHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEverton wanaweza kufufua tena azma yao ya kumtaka Mdochi Patrick Van Aanholt, anayechezea Crystal kwa sasa
Fulham watatakiwa kulipa karibu pauni milioni £20m kusaini mkataba na Mserbia Aleksandar Mitrovic anayeichezea Newcastle.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alikuwa akicheza kwa mkopo katika Craven Cottage msimu uliopita na aliisaidia klabu hiyo kupanda daraja na kuingia Ligi ya Premia. (Evening Standard)
Justin Kluivert -mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa timu ya Uholanzi Patrick Kluivert - anaweza kubakia katika Ajax licha ya fununu kwamba anapanga kuhama. Kluivert mwenye umri wa miaka 19 winga wa Uholanzi amekuwa akihusishwa na timu za Manchester United na Tottenham. (Fox Sports - in Dutch)
Kluivert amekubali mkataba wa Roma, lakini bado hawajaafikiana juu ya malipo na wenzao wa Uholanzi juu ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi . (Gianluca di Marzio - in Italian)
Mchezaji wa safu ya ulinzi Michael Dawson, mwenye umri wa miaka 34, amekubali kurejea Nottingham Forest kwa mkataba wa miaka miwili baada ya mkataba wake na Hull kumalizika. (Daily Mail)
Justin KluivertHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJustin Kluivert amekubali mkataba wa Roma
Southampton na Aston Villa wanamtaka mlinzi wa timu ya Ujerumani Tobias Pachonik.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa sasa yuko huru kwani bado hajasaini mkataba mpya na Carpi FC iliyopo katika Ligi ya pili ya Italia . (Turkish Football)

Mahakama yapingana na Rais





Mahakama Kuu ya nchini Kenya imezuia matumizi ya vifungu kadhaa vya Sheria ya mtandao iliyopitishwa na kusainiwa na Rais Kenyatta wiki mbili zilizopita nchini humo.
Mahakama imevizuia vifungu 26 vya Sheria hiyo mpaka hapo shauri litakaposikilizwa, hatua hii inafikiwa baada vya chama cha Wanahabari na waendeshaji wa Blogu kufungua pingamizi.
Akitoa uamuzi huo Jaji wa Mahakama Kuu, Chacha Mwita amesema kuwa sheria hiyo ni kandamizi kwa haki za binadamu ikiwemo uhuru wa kujieleza.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 18 mwaka huu ambapo itasikilizwa tena.


NILIANGUKA NA UNGO WA KICHAWI  KANISANI

Wito umetolewa kwa wanawake mkoani tabora kujitoa katika kumtumikia mungu



Wito umetolewa kwa wanawake mkoani tabora kujitoa katika
kumtumikia mungu na kumfanya wakwanza katika maisha yao 

Hayo yameelezwa na akina mama waliohudhulia katika siku ya
mwisho ya ya kongamano la watumishi wa mungu lililofanyika kwa siku tatu
mfululizo katika kanisa la effeso baptist lililopo bomba mzinga  ambapo muitikio wa wanawake umeonekana kuwa
mdogo ukilinganishwa na wanaume

Aidha vijana wote wametakiwa kujitoa kwa kazi ya mungu ili
kutengeneza taifa linalomcha mungu kwani kundi hilo linakubwa na changamoto
nyingi zinazowatenga na mapenzi ya mungu

Kwaupande wao wachungaji waliohudhuria kongamano hilo
wamewataka watumishi wote wa mungu kuitikia wito popote pale ambapo wataombwa
kuwepo ili kuweza kujifunza zaidi kwani mungu hupitia kwa mwanadam kufikisha
kile alichokusudia 
Hata hivyo wameshukuru ujio wa wageni walioongoza kongamano
hilo kwa siku tatu ambao ni pastor herb monroe, raymond clark barry na lynn
monroe wote kutoka nchini marekani kwa kusema kuwa wamebarikiwa sana.

Kongamano hilo liliandaliwa na kanisa la effeso baptist kwa
kushirikiana na radio uhai fm likiwa na lengo la kuwakutanisha watumishi wa
mungu katika kuimarishana kiimani



NILIANGUKA NA UNGO WA KICHAWI  KANISANI 

May 30, 2018

Mbwana Samatta atua Mecca kufanya Umrah..KUIJI


Mchezaji huyo baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Ubelgiji ametua mjini Mecca nchini Saudia Arabia kwa ajili ya kufanya ibada ya Umrah.






Mbwana Samatta (kushoto) akiwa na mchezaji mwenzake wa Genk, Omar Colley
Kwenye ziara hiyo, Samatta ameambatana na mchezaji mwenzake wa Genk, Omar Colley ambaye ni raia wa nchini Gambia.
Samatta anatarajiwa kurejea hapa nchini muda sio mrefu kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa hisani wa kuchangia elimu kati yake na timu ya Alikiba kwenye mchezo ambao unatarajiwa kuchezwa Juni 9, mwaka huu.
TABORA YA VAMIWA

MZEE WA UPAKO ADAI MTANZANIA KUFA MASKINI NI UFALA


Image result for Mzee wa Upako 

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu kama ‘Mzee wa Upako’ bado amedai kuamini kuwa Mtanzania kufa masikini ni ujinga na ufala, hii ni kutokana na rasilimali zilizopo ndani ya nchi. 

Mzee wa Upako amesema Tanzania tuna mbuga za wanyama, madini ya Tanzanite, ardhi yenye rutuba hivyo haiwezekani mtu kufa masikini. 


“Kufa masikini sio ujinga tuu ni ufala, sasa ufe masikini si fala tuu, halafu ukute ulipata nafasi na fursa mbalimbali huko,“amesema Mzee wa Upako kwenye kipindi cha Maisha Mseto cha Times FM na kusisitiza. 


“Tuna mbuga za wanyama , tuna Tanzanite, tuna almasi, tuna ardhi bora, Tanzania ni nchi ya pili katika Afrika kuwa na mifugo mingi, halafu bado sisi ni masikini? mimi akili haikubali.“amesema Mzee wa Upako na kutoa mfano. 

“Kuna nchi moja Singapore wanaendesha nchi yako kwa bandari tu lakini matajiri wanaikimbilia Japan, kwa hiyo mimi siamini Katika umasikini, sisi sio wazima tumerogwa.” amemaliza Mzee wa Upako

NIMELALA NA WANAMKE K ICHAWI 20000

Wanaotaka kustaafu wapewa onyo



Katibu wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Bi. Winifrida Rutahindurwa amewaonya waalimu wanaofanya udanganyifu katika taarifa zao za kiutumishi kwa lengo la kujiongezea muda wa kuwepo katika utumishi wa umma licha ya kuwa umri wao wa kustaafu kwa mujibu wa sheria kufika.
Bi. Rutahindurwa ametoa kauli hiyo Mei 29, 2018 mjini Bagamoyo alipokutana na waalimu wakuu na wakuu wa shule za umma kutoka wilaya za Bagamoyo na Chalinze kwa lengo la kutoa elimu juu ya wajibu wao na kusema kuwa  kuna wakati walimu walitakiwa kupeleka taarifa zao za kiutumishi kwa waajiri wao lakini baadhi yao walipeleka taarifa tofauti na zile walizojaza kwenye mikataba ya kazi wakati wa kuanza ajira.
"Kuna baadhi ya waalimu wanajifanya hawakumbuki walizaliwa mwaka gani wakati walijaza mikataba wakati wanaanza ajira na wengi wao wamebadilisha taarifa zao na kujipunguzia umri jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria", amesema Bi. Rutahindurwa.
Aidha, Bi. Rutahindurwa amefafanua kuwa mwalimu atakapoandikiwa kibali cha kustaafu, TSC pamoja na mfuko wamifuko ya hifadhi ya jamii wanajikita zaidi kuangalia taarifa za mwalimu alizojaza awali wakati anaanza ajira yake na sio kutegemea taarifa za stakabadhi ya mishahara peke yake.
"Naomba muwaeleze walimu wote katika shule zenu kuwa utakapoandikiwa kibali cha kustaafu sisi tunaangalia zaidi taarifa zako ulizojaza wakati unaajiriwa na ukibainika umedanganya utachukuliwa hatua kwa kuwa umemwibia mwajiri", amesisitiza Bi. Rutahindurwa.
Kwa upande wao waalimu walionesha kupokea maelekezo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuondoa usumbufu kwa mwalimu pale anafuatilia masuala yake ya mafao mara baada ya kustaafu.

WENYE VITI WA MTAA MARUFUKU KUJIUSICHA NA KUUZA ARIDHI

Wabunge hawafuati utaratibu"- Pius Msekwa



Sakata la matibabu ya Wabunge, Spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pius Msekwa amesema kuwa Wabunge hawafuati utaratibu kwa kufanya maamuzi yao binafsi.

Msekwa amefunguka hayo wakati akizungumza na eatv.tv na kusema kuwa kuna taratibu za matibabu kwa Wabunge na hairuhusiwi kutibiwa hospitali yoyote kwa uamuzi binafsi lakini wanashindwa kufuata miongozo hiyo na kuibua migogoro.
“Mbunge akiugua huwa anapelekwa hospitali ya serikali na endapo akitakiwa kuhamishwa hospitali atapewa rufaa na lazima bunge liwe na taarifa hakuna anayefanya maamuzi yake binafsi alafu anahitaji kulipwa”, amesema Msekwa.
Aidha, Msekwa ameongeza kuwa hakuna upendeleo kama ambavyo Kambi ya Upinzani Bungeni inavyodai na imekuwa hivyo tangu mwanzo kwa kuwa fedha zinazotumika ni za umma na zinataratibu zake.
Hayo yamejiri baadaya kuwepo kwa madai kuwa Wabunge wa upinzani hawapewi kipaumbele pindi wanapotakiwa kupatiwa matibabu.


mtaa wa mabatini uchafu umekidhili

Simba ya shindwa kufuta rekodi ya Yanga






Baada ya klabu ya Simba kutwaa ubingwa wa msimu huu, huku wakimaliza ligi wakiwa na alama 69, rekodi zinaonesha wameshindwa kuvunja rekodi za Yanga katika msimu wa 2015/16.

Msimu huu Simba imeshinda mechi 20 pekee kati ya 30 ambazo ndio mechi za msimu mzima, ambapo Yanga katika msimu wa 2015/16 ilishinda mechi 22 kati ya 30 za msimu huo.
Simba pia imetoa jumla ya sare 9 msimu huu lakini wapinzani wao wa Jadi Yanga walifanikiwa kutoa sare 7 pekee kwenye msimu wao wa 2015/16 ambapo waliibuka mabingwa wa ligi. 
Kwa upande wa mabao ya kufunga Simba pia washindwa kufikia mabao 70 ya Yanga wakiishia mabao 62 pekee msimu huu. Kwenye mabao ya kufungwa Simba wamefanya vizuri ambapo wameruhusu mabao 15 tu lakini Yanga walikubali mabao 20.
Kwa upande wa alama Simba wameshindwa kufikia alama 73 za Yanga msimu huo wakiishia alama 69 pekee katika michezo yao 30. Msimu huu timu pekee iliyovunja rekodi ya alama ni Manchester City ambayo ilifikisha alama 100 na kuvunja rekodi ya alama 95 iliyowekwa na Chelsea msimu wa 2004/05. 

TABORA  YA OMBEWA MAFANIKIO


Mkuu wa Mkoa kutumia Jeshi la Polisi kufunga mtaa




Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amesema atalazimika kutumia Jeshi la Polisi kusimamia zoezi la usafi na ujenzi wa vyoo salama katika Kijiji cha Namasinzi, baada ya wananchi hao kushindwa kujenga vyoo hivyo mbali na elimu ya umuhimu wa vyoo waliyopewa kwa muda mrefu.
Wangabo ametoa kauli hiyo wakati yupo katika Mkutano wa hadhara alioufanya kwenye kijiji cha Namasinzi, Kata ya Kapenta, Wilayani Sumbawanga, kijiji ambacho wananchi watatu wamefariki kwa ugonjwa wa kipindupindu na wengine wakiendelea kupatiwa huduma. 
Aidha, Wangabo amesema kuwa ikifikia hatua hiyo Kijiji hicho kitafungiwa na hakuna atakayetoka wala kuingia na hatimaye kusitisha shughuli za kiuchumi za Kijiji hicho ambacho ni maarufu kwa kilimo cha mpunga hali itakayopelekea maisha magumu kwa wananchi hao jambo ambalo asingependa litokee.
Katika kuhakikisha hali hiyo haitokei Mh. Wangabo alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule na timu yake ya usafi ya halmashauri kuhakikisha wanapita kaya kwa kaya ili kuzibaini kaya zisizopenda usafi na zisizokuwa na vyoo na kuzichukulia hatua za kisheria kwani kwa kushindwa kufanya hivyo kipindupindu hakitamalizika katika bonde hilo.
"Sasa tutatumia nguvu ya dola, ili kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi katika maisha ya usafi wala sio uchafu na kila mtu ahakikishe kwamba anakuwa na kiboko fulani ambacho ni kigumu amuone mtu anachemsha maji, anayaweka maji yake yanapoa akienda shambani anakwenda na maji mbayo yamekwisha poa, lakini mkilea lea hivi, waswahili wanasema ukicheka na nyani unavuna mabua, mabua ambayo tunayavuna ni vifo",amesema Wangabo.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa halmshauri ya Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Fani Musa ameendelea kuishukuru serikali kwa kuendelea kupeleka misaada katika bonde hilo ili kuhakikisha wanakabiliana na ugonjwa huo na kusisitiza kuwa wataendelea kutoa elimu bila ya kuchoka akiamini kuwa wananchi hao wataelewa wakiendelea kusimamiwa.



NIMELALA NA WANAMKE KICHAWI 20000

Mkurugenzi mtendaji wa maji safi tabora kumsimamisha kazi

Image result for Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya sikonge Mkoani Tabora


Baraza la madiwani
wa  halmashauri ya wilaya ya sikonge
Mkoani Tabora limemwagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo kumsimamisha
kazi Meneja wa mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira (SUWASA)  Eginia Benjamini Briton kwa tuhuma za ubadhifu
wa fedha za umma na Matumizi mabaya ya ofisi.

Maagizo hayo
yametolewa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mwalim Peter Nzalalila katika
kikao cha baraza la madiwani
kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha maendeleo ya jamii FDC Wilayani
humo.

Amesema kuwa
baraza hilo limeazimia kwa kauli moja
kumsima
misha kazi   meneja huyo
kutokana na kuwepo kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma pamoja na matumizi
mabaya ya ofisi hali ambayo imekuwa ikipelekea hali ya upatikanaji wa maji
wilayani humo kuwa wakusuasua.
Akipokea maagizo
hayo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Daktari Simoni Ngatunga amesema
kuwa atatekeleza agizo hilo kwa kutumia kanuni,sheria na Taratibu kwa kuwa hana
mamlaka ya kutengua uteuzi wa bodi ya maji ambayo inateuliwa na Wizara ya maji
na Umwagiliaji

Nao baadhi ya
madiwani wa halmashauri  hiyo Mbaruku
ally Mgaywa na Lucas Kiberenge wamesema kuwa wamefikia maazimio  hayo baada ya kuona kuwa ofisi ya mkurugenzi
mtendaji inashindwa kumuwajibisha meneja
huyo licha kuoneka wazi wazi kuwa kuna ubadhilifu wa fedha za umma zaidi
ya milioni 600
Meneja wa mamlaka
ya maji Safi na Usafi wa mazingira SUWASA Wilayani humo Enginia Benjamini
Briton amesema kuwa amesikitishwa na maamuzi yaliyotolewa katika kikao cha
baraza hilo kwani hakupewa nafasi ya kujibu chochote wala kujitetea kwa
chochote.
Kwa upande wake
mkuu wa wilaya ya sikonge bwana Peres Magiri amesema kuwa serikali ya wilaya
hiyo haiwezi kumvumlia mtumishi yeyote mzembe
ambae atabainika kula fedha za umma na huku akipongeza maamuzi yaliyotolewa
na baraza hilo.
Hata hivyo baraza
hilo la madiwani limeazimia kumsimamisha kazi Meneja huyo kwa muda
usiojulikana  huku likimuomba mkaguzi wa
ndani kuanza kufanya ukaguzi ili kuweza kubaini upotevu wa fedha zaidi ndani ya
mamlaka hiyo.



TABORA  YA OMBEWA MAFANIKIO