Ripoti iliyotolewa na kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania imebainisha kwamba kuna ongezeko kubwa la ukatili dhidi ya watoto kwa kipindi cha miezi sita ya kwanza katika mwaka 2018.
Ongezeko kubwa la matukio ya ubakaji wa watoto ni mara tatu zaidi ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2017, kutoka 12 kwa mwaka hadi 533 kwa mwaka 2018.
Hivyo ni wastani wa watoto 394 wamebakwa kila mwezi katika maeneo mbalimbali ya Tanzania bara kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2018
Mwanamke mmoja nchini Japan amefuzu kuwa rubani wa kwanza wa ndege za kivita nchini humo, Luteni Misa Matsushima, mwenye umri wa miaka 26, ameanza majukumu yake leo baada ya kumaliza mafunzo ya kurusha ndege ya kivita aina ya F 15, jeshi la Japan limetangaza.
Luteni Misa amewaambia wanahabari kwamba, kwa kuwa rubani wa kwanza mwanamke atafungua fursa kwa wanawake wengine kuingia kwenye fani hiyo.
“Tangu nilipoangalia sinema ya Top Gun, wakati nikiwa shule ya msingi basi nikatokea kuwapenda sana marubani wa ndege za kivita,” anasisitiza Misa.
Japan ina viwango vya juu vya ukosefu wa usawa wa kijinsia, ambapo wanawake wengi wanatarajiwa kuwa mama wa nyumbani badala ya kuajiriwa, lakini kutokana na kukabiliwa na changamoto ya kuwa na wazee wengi, mnamo mwaka 2013 Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Shinzo Abe, aliahidi kuwawezesha zaidi wanawake katika ajira.
Jeshi la Japan lilianza kuajiri wanawake kwa mara ya kwanza mwaka 1993 isipokuwa kwa marubani, ambapo iliondoa amrufuku hiyo mwaka 2015, ambapo kwa sasa wanawake wengine watatu wamejiunga kwenye mafunzo ya kuwa marubani wa ndege za kivita.
Uamuzi mgumu wa Rais John Magufuli wa kuboresha usafiri wa anga nchini kwa kununua ndege kubwa ya Boeing 787-8 Dreamliner, umemkimbiza Diwani wa Chadema katika kata ya Ndumeti, Wilaya ya Siha, Jackson Rabo kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kwa mujibu wa diwani huyo moja ya sababu iliyomvutia kujiunga na CCM baada ya uamuzi wa Rais John Magufuli kuhamishia ofisi zote za serikali mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Valerian Juwal amethibitisha kuwa Diwani Jackson Rabo anakuwa Diwani wa tano katika wilaya hiyo kujiuzulu mwaka huu.
EBOLA ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ambavyo uishi katika miili ya binadamu na wanyama. Kwa mara ya kwanza ugonjwa huu ulitokea mwaka 1972 katika milipuko miwili iliyotokea kwa pamoja katika sehemu ya Nzara nchini Sudan na Yambuku nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo karibu na mto Ebola ambapo jina la ugonjwa huu lilipatikana. Toka kipindi hicho kumekuwa na muendelezo wa milipuko mbalimbali katika nchi tofauti za Afrika katika miaka tofautitofauti.
Mlipuko wa sasa wa ugonjwa wa Ebola umetokea katika nchi zilizopo magharibi mwa Afrika ,kesi ya kwanza iligunduliwa mwezi Machi,2014. Mlipuko wa sasa ni mkubwa zaidi kuwahi kutokea toka virusi wasababishao ugonjwa huu ulipogunduliwa mwaka 1976 ukiwa umesababisha vifo vingi zaidi kuliko milipuko yote ya miaka ya nyuma kwa pamoja.Mlipuko wa sasa umeathiri nchi nyingi zaidi,miongoni mwa nchi zilizoathrika sana ni Guinnea,Sierra Leone na Liberia.Kutokana na mlipuko wa sasa kuwa na athari kubwa na kuathiri nchi Zaidi mnamo Agusti 8,2014 shirika la afya ulimwenguni (WHO) lilitanganza mlipuko huu kuwa ni dharura ambayo nchi zote duniani zilitakiwa zishiriki katika harakati za kuudhibiti.
DALILI ZA UGONJWA WA EBOLA
Dalili za ugonjwa wa Ebola huaanza kuoneekana siku 2 mpaka 5 tangu mtu apate maambukizi ila kwa wastani ni siku 8 mpaka 10.
Zifuatazo ni dalili kuu za ugonjwa wa Ebola;
Homa
Maumivu makali ya kichwa
Maumivu ya misuli
Kufa ganzi
Kuharisha
Kutapika
Maumivu ya tumbo
Kutokwa damu pasipo sababu sehemu mbalimbali za mwili
Unapoona dalili moja au zaidi kati ya hizi unatakiwa uwahi mara moja katika kituo cha afya kwa uchunguzi Zaidi na matibabu itakapohitajika.
NJIA ZA MAAMBUKIZI YA EBOLA
Ugonjwa wa Ebola usambazwa kwa njia ya kugusa majimaji ya mwili wa mgonjwa au mnyama aliyeathiriwa na ugonjwa huu. Majimaji yatokanayo na damu,kinyesi na matapishi yanasababisha maambukizi kwa kiasi kikubwa.
Virusi vya Ebola pia hupatikana katika maziwa ya mama,mkojo na shahawa.Virusi huendelea kupatikana kwa siku 70 hadi 90 kwenye shahawa za mwanaumme aliye na ugonjwa huu.
Machozi na mate pia yanaweza kuwa na virusi vya ugonjwa huu
Virusi vya Ebola pia vinaweza kusambazwa kwa njia ya kugusa sehemu na vitu kama meza,vitinda na kadhalika ambavyo vina virusi tayari.
Virusi vya Ebola mara nyingi havisambazwi kwa njia ya hewa ila vinaweza kusambaa kwa njia ya matone ya majimaji yanayotoka kinywani au puani pale mgonjwa anapokohoa au kupiga cha fya.
NJIA ZA KUJIKINGA NA EBOLA
Hakikisha usafi wa mwili wako, kwa mfano osha mikono yako kwa maji safi na sabuni na epuka kugusa damu au majimaji ya mtu yeyote.
Usiguse vitu kama nguo,shuka,vifaa vya matibabu na kadhalika ambavyo vimeguswa na damu au majimaji ya mgonjwa wa Ebola
Epuka kushiriki mazishi ambayo yanahusisha kugusa mwili wa mtu aliyefariki.
Epuka kugusana na popo na wanyama jamii ya sokwe au majimaji,damu na nyama zao .
Epuka kusogelea sehemu zilizotengwa kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa wa Ebola
Baada ya kutoka eneo lenye mlipuko wa ugonjwa huu fuatilia kwa umakini afya yako kwa kipindi cha siku 21 na ukiona dalili zozote za ugonjwa huu nenda kituo cha afya mara moja.
NJIA ZA KUJIKINGA KWA WATOA HUDUMA ZA AFYA
Wahudumu wa afya ni miongoni mwa watu walio katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya ugonjwa huu kutokana na ukaribu walionao na wagonjwa.Kutokana na hali hiyo Wahudumu wa afya wanatakiwa kuwa makini sana wanapotoa huduma kwa wagonjwa.
Vaa nguo zinazotakiwa za kujikinga na maambukizi
Tenga wagonjwa wa Ebola na wagonjwa wengine
Epuka kugusa moja kwa moja bila kinga miili ya watu waliofariki kutokana na Ebola
Ikitokea umegusa moja kwa moja majimaji,damu,mkojo,machozi au shahawa za mgonjwa wa Ebola toa taarifa haraka kwa afisa wa afya.
Aliyekua rais wa Uruguay Jose Mujica, aliyejulikana kama rais maskini zaidi duniani amesema hatachukua malipo yake ya uzeeni tangu aanze kuhudumu kama seneta.
Mujica aliacha kazi ya useneta mnano Jumanne, kiti ambacho amekua akishikilia tangu muda wake wa kuhudumua kama raisi ukamilika mwaka wa 2015.
Alidai kuwa amechoka na hangeweza kuendelea na kazi hadi mwaka wa 2020. Muasi huyo wa zamani wa mrengo wa kushoto ana miaka 83.
Mujica aliwasilisha barua ya kuacha kazi kwa mkuu wa seneti. Alisema ya kwamba fikra ya kuacha kazi ni ya kibinasfi huku akiongeza kuwa ni uchovu wa safari ndefu.
Hata hivyo aliongeza kua ataendelea kuchangia hoja kwa sababu bado akili yake inafanya inafanya kazi.
Mujica anayejulikana kwa matamshi yake ya kichesi aliomba msamaha kwa wenzake kwa uamuzi huo.
Mwaka 2016, alidai rais wa Venezuela Nicolás Maduro ni mwendazimu kama mbuzi.
Umaarufu wake ulienea kutokana na maisha yake ya chini ya kukataa kuishi kwenye ikulu ya rais.
Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini (CHADEMA), Anthony Komu.
Akizungumza na East Africa BreakFast ya East Africa Radio amesema kuwa hawezi kuondoka CHADEMA na hajawahi kufanya mazungumzo na Waitara kuhusu suala hilo kwani yeye ndio muasisi wa upinzani na anajivunia historia hiyo .
“Mimi sio sehemu ya mpango huo na sielewi Waitara katoa wapi taarifa hiyo naomba wananchi wangu watambue kuwa mimi sio mpinzani wa kuunga unga mimi ni miongoni mwa waasisi wa upinzani”, amesema Komu.
Jumamosi ya Agosti 11, 2018 kupitia Weekend BreakFast ya East Africa Radio Waitara aliwataja wabunge watano kutoka CHADEMA wanaotaraji kujiunga na CCM akiwemo Anthony Komu.
Meli ya mizigo ijulikanayo kama LCT Rahimu imewaka moto mapema leo ikiwa katika bandari ya Bagamoyo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Fatuma Latu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutaja chanzo chake kuwa ni hitilafu ya umeme wakati mafundi wakijaribu kuchomelea mlango wa meli hiyo kwa kutumia umeme wa jenereta iliyokuwa ndani yake.
Amesema vyombo vya zimamoto na uokoaji vimefanikiwa kuzima moto huo na kwamba nahodha kwa sasa anahojiwa na vyombo vya usalama ili kupata maelezo zaidi.
Inadaiwa kuwa meli hiyo imetokea visiwani Zanzibar na ilikuwa bandarini hapo ikisubiri shehena ya kokoto kwa ajili ya kuipeleka Zanzibar.
Paris St-Germain wanaandaa pauni milioni 100 kwa ofa ya mchezaji wa Tottenham mwenye miaka 26 raia wa Denmark Christian Eriksen. (Express)
Schalke wana nia ya kumasaini mchezaji mwenye miaka 22 raia wa England Reuben Loftus-Cheek kwa mkopo lakini Chelsea haunda wasiruhusu kuondoka kwake. (Telegraph)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMatteo Darmian
Beki wa Manchester United Matteo Darmian anataka kuondoka Old Trafford na Juventus, Napoli na Internazionale wanamwinda mchezaji huyo mwenye miaka 28 raia wa Italia. (Manchester Evening News)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho aliachanganyikiwa kufuatia madai ya Paul Pogba ya kuwepo uhusiano mbaya kati yao siku ya Ijumaa. (Telegraph)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMarcus Bettinelli
Kipa Marcus Bettinelli, 26, anaweza akaamua kuondoka Fulham baada ya kuachwa nje ya kikosi kilichocheza mechi ya kwanza ya msimu. (Mail)
Liverpool watasikiliza ofa kwa mchezaji wa maiaka 32 mlinzi rauia wa Estonia Ragnar Klavan. (Liverpool Echo)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionLee Cattermole
Kiungo wa kati wa Sunderland mwenye miaka 30 Lee Cattermole huenda akahamia Bordeaux, ambapo aliyekuwa meneja wa zamani wa Black Cats sasa ndiye meneja. (Teamtalk)
Wale wanaolengwa kuchukua nafasi ya mkurugenzi mpya wa Manchester United ni pamoja na kipa Edwin van der Sar, mkurugenzi wa Juventus Fabio Paratici na Monchi, mkurugenzi wa zamaniawa Sevilla na sasa Roma. (Independent)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionWilfried Zaha
Mshambuliaji Wilfried Zaha anasema bado anazungumza na Crystal Palace kuhusu kuongezwa mkataba wake huko Selhurst Park. (Mail)
Meneja wa zamani wa Argentina Jorge Sampaoli anataka kurudi kwenye usimamizi na Mexico. (Goal)
Paris St-Germain na Monaco wanataka kiungo wa kati wa Sevilla mwenye miaka 29 Mfaransa Steven Nzonzi. (France Football)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMaxim Choupo-Moting
Kiungo wa kati mwenye miaka 25 Giannelli Imbula, kiungo wa kati mwenye miaka 32 msikochi Charlie Adam, winga raia wa Cameroon mwenye miaka 29 Maxim Choupo-Moting na mlinzi mwenye miaka 33 Geoff Cameron wote wana mpango wa kuondoka Stoke. (Telegraph)
Meneja wa Real Madrid Julen Lopetegui anataka kuongeza mlinzi na mshambuliaji kwenye kikosi chake kabla ya tarehe ya mwisho. (AS)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionJulen Lopetegui a
Bora zaidi kutoka Jumatatu
AC Milan wanamtafuta kiungo wa kati wa Chelsea mwenye miaka 23 Tiemoue Bakayoko kwa mkopo wa msimu wote kabla ya kumpa mkataba wa kudumu. (Sun)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionTiemoue Bakayoko
Barcelona itamwinda Paul Pogba baada ya msimu wa joto wa kununua wachezaji kukamilika tarehe 31 Agosti kufuatia kukubali kuwa Manchester United hawatamuuaza mchezaji huyo mwenye miaka 25 raia wa Ufarasa mwezi huu. (Telegraph)
Kipa wa Liverpool Loris Karius, 25, anawindwa na Besiktas. Klabu hiyo wa Uturuki imekuwa na mpango wa kumsaini Mjerumani huyo kwa mkopo wa msimu wote. (Sun)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionLoris Karius
Beki wa Manchester City mwenye miaka 23 Jason Denayer amekataa kuondoka kwa mkopo kwa kuwa mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ubelgiji anataka kuhamia klabu ya Uturuki ya Galatasaray. (Star)
Cristiano Ronaldo amewashauri Juventus kumuendea kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic. Mchezaji huyo mwenye miaka 23 raia wa Serbia amehusishwa na Manchester United na Chelsea. (Star)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionCristiano Ronaldo
Kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrina Rabiot, 23, amekataa ofa ya kusaini upya mkataka wake na mabingwa hao wa Ligue 1. Mkataba wa kwanza wa Mfaransa huyo unakamilika mwisho wa msimu. (L'Equipe)