August 23, 2017

Polisi yamuua mshambuliaji wa Barcelona Younes Abouyaaqoub




Polisi wa Uhispania wa jimbo la Catalonia wamemuua kwa kumpiga risasi Younes Abouyaqoub, dereva anayeshukiwa kuendesha gari lililokanyaga watu katika shambulio la kigaidi la Barcelona. Abouyaqoub alipigwa risasi na kuuwawa kilomita 50 kutoka katika mji wa Barcelona siku nne baada ya kutokea shambulio hilo la kigaidi. Maafisa wamesema Abouyaqoub, ambaye ni raia wa Morocco aliyekuwa na umri wa miaka 22, aliendesha gari hilo na kuvamia kundi wa wapita njia katikati ya mji mkuu wa Barcelona wiki iliyopita, na kusababisha vifo vya watu 13 na kujeruhi wengine zaidi ya mia moja. Shambulio sawa na hilo lilitokea katika mji wa Cambrils, ambapo mwanamke mmoja alipoteza maisha kutokana na majeraha ya kuchomwa kisu. Kundi linalojiita Dola la Kiislam - IS limedai kuhusika na mashambulizi yote mawili.

Burnley wavunja rekodi yao ya usajili kumnunua Chris Wood

 
 
Chris Wood
 
 
 
od kutoka Leeds United kwa bei iliyovunja rekodi ya klabu hiyo, ambayo inaaminika kuwa takriban £15m .
Mchezaji huyo wa miaka 25 alifunga mabao 44 katika mechi 88 tangu alipojiunga na Leeds kutoka Leicester City Julai 2015.
Raia huyo waNew Zealand alijiondoa kutoka kwa mechi ya Leeds dhidi ya Sunderland katika ligi ya daraja la pili Jumamosi uvumi kuhusu kuhama kwake ulipokuwa umesheheni.
Wood, ndiye mchezaji wa sita kununuliwa na Sean Dyche kipindi hiki.
Ametia saini mkataba wa miaka minne.

Mchezaji huyo alikuwa amefunga bao moja katika mechi tatu alizowachezea Leeds msimu huu, lakini sasa ataanza kujaribu kutikisa nyavu Ligi ya Premia.
Wood anaruhusiwa kuchezea Burnley katika Kombe la EFL kwani alikuwa benchi na hakuchezeshwa mechi waliyolaza Port Vale.
Rekodi ya awali ya usajili wa Robbie Brady waliyemnunua Januari kwa ada inayotarajiwa kufikia £13m.

Matukio ya Kisiasa Merkel asikitishwa na viwanda vya magari Kansela Angela Merkel alijibu maswali ya wapiga kura katika kipindi cha maswali na majibu cha televisheni, ambapo aliulizwa kuhusu usalama, wahamiaji na kashfa ya kupima moshi unaochafua mazingira kwa magari ya VW Deutschland Merkel Statement zum Barcelona Anschlag (picture-alliance/dpa/M. Kappeler) Kansela wa Ujerumani Angela Merkel Kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Ujerumani mwezi ujao inaendelea. Bibi Markel Anagombea muhula wa nne. Kansela Angela Merkel alishiriki katika kipindi cha televisheni cha kituo cha RTL ambacho kilikuwa kinarushwa moja kwa moja, Jumamosi jioni. Wapiga kura walimuuliza maswali kansela wakati akiwania muhula wa nne madarakani katika uchaguzi wa mwezi Septemba. USA - Merkel als Malerei: The Art of Leadership in Dallas (picture-alliance/dpa/L. W. Smith) Picha ya kuchora ya kansela wa Ujerumani Angela Merkel Uchunguzi wa maoni ya wapiga kura unaonesha chama cha kansela Merkel cha Christian Democratic Unioni CDU pamoja na chama ndugu cha jimbo la Bavaria Christian Social Union , CSU vitakuwa kundi kubwa la chama bungeni lakini bila ya wingi wa kutosha. Kutokana na mashambulizi nchini Ujerumani na hivi karibuni kabisa mjini Barcelona, Merkel aliulizwa hatua gani serikali yake itachukua kuimarisha usalama. Merkel alisema kwamba mchanganyiko wa matumizi ya polisi na matumizi ya teknolojia inapaswa kutumiwa kuhakikisha usalama. Amesema kwamba wakati kuna raia wanaokadiriwa kufikia 10,000 ambao wamepata itikadi kali na kuwa na mawazo ya itikadi kali nchini Ujerumani, ni watu 600 hadi 700 tu wanaonekana kuwa ni hatari. Merkel amekosoa matumizi ya Uturuki ya jeshi la polisi wa kimataifa Interpol kumkamata kwa kutoa waranti na kutaka arejeshwe nchini humo mwandishi Mjerumani Dogan Akhanli kutoka nchini Uhispania siku ya Jumatatu kuwa na matumizi mabaya ya shirika hilo la polisi la kimataifa. "Sio sahihi na nafurahi sana kwamba uhispania imemuachia huru," Merkel amesema. "Hatupaswi kutumia vibaya mashirika ya kimataifa kama Interpol kwa madhumini hayo." Deutschland Bundeskanzlerin Angela Merkel im ARD-Interview (picture-alliance/dpa/R. Jensen) Kansela Angela Merkel akifanyiwa mahojiano na waandishi habari Kansela achukizwa na viwanda vya magari Kansela amesema atajaribu kuunganisha vifaa vya polisi na utaratibu wa majimbo 16 nchini Ujerumani. Amedokeza kwamba wengi hawafahamu upekuzi wa polisi pamoja na uangalizi wa vidio kwamba unafanyakazi kwa njia tofauti katika majimbo hayo nchini Ujerumani. Amesema chama chake cha Christian Democratic , kitajaribu kuunganisha mbinu za polisi , akisema : "Pia nitazungumza tena na mawaziri wakuu wa majimbo binafsi." Merkel pia alitetea uamuzi wake wa kufungua mipaka ya Ujerumani kwa mamia kwa maelfu ya wakimbizi miaka miwili iliyopita. Alipoulizwa iwapo sasa angefanya tofauti , alisema: "Bado nafikiri uamuzi wangu ulikuwa sahihi." Ametoa wito wa umoja zaidi katika bara la Ulaya kusaidia nchi kama Italia na Ugiriki kupambana na idadi kubwa ya wahamiaji wanaowasili katika mipaka yao. Merkel bei CDA Veranstaltung in Dortmund (picture-alliance/dpa/I.Fassbender) Bibi Angela Merkel Mpiga kura mmoja aliuliza swali kwamba kwanini waombaji hifadhi hawaruhusiwi kufanyakazi wakati kesi zao zikifanyiwa mapitio wakati baadhi wakisema wamesubiri kwa miaka kadhaa wakipiewa fedha za walipa kodi wakati wanataka kufanyakazi. Merkel amewaambia wapiga kura kwamba amevunjwa moyo na tasnia ya makampuni ya kutengeneza magari kufuatia kashfa ya dizeli ya kampuni ya Vilkswagen. Amesema waziri wa zamani wa mazingira alifahamu madhara yake. "Nimekasirishwa," Merkel amewaambia watazamaji. Tasnia ya magari imetishia kujiingiza katika matatizo makubwa katika kashfa hiyo na makampuni yanapaswa kujisahihisha kwa kiasi kikubwa kadri wanavyoweza," amedokeza. Amesema program mpya ipo kwa sasa kuweza kusahihisha makosa hayo. Mwandishi : Jane Mcintosh / ZR / Sekione Kitojo Mhariri: Mohammed Abrul Rahman



Merkel asikitishwa na viwanda vya magari 

 Deutschland Bundeskanzlerin Angela Merkel im ARD-Interview (picture-alliance/dpa/R. Jensen)

Kansela Angela Merkel alijibu maswali ya wapiga kura katika kipindi cha maswali na majibu cha televisheni, ambapo aliulizwa kuhusu usalama, wahamiaji na kashfa ya kupima moshi unaochafua mazingira kwa magari ya VW
Deutschland Merkel Statement zum Barcelona Anschlag (picture-alliance/dpa/M. Kappeler) Kansela wa Ujerumani Angela Merkel
Kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Ujerumani mwezi ujao inaendelea.  Bibi Markel Anagombea  muhula  wa  nne. 
Kansela  Angela  Merkel  alishiriki  katika  kipindi  cha televisheni cha  kituo  cha  RTL ambacho  kilikuwa  kinarushwa  moja  kwa moja, Jumamosi  jioni. Wapiga  kura  walimuuliza  maswali  kansela wakati  akiwania  muhula  wa  nne  madarakani  katika  uchaguzi  wa mwezi  Septemba.

USA - Merkel als Malerei: The Art of Leadership in Dallas (picture-alliance/dpa/L. W. Smith) Picha ya kuchora ya kansela wa Ujerumani Angela Merkel
Uchunguzi  wa  maoni  ya  wapiga  kura  unaonesha  chama  cha kansela  Merkel  cha  Christian Democratic  Unioni  CDU  pamoja  na chama  ndugu  cha  jimbo  la  Bavaria  Christian Social  Union , CSU vitakuwa  kundi  kubwa  la  chama  bungeni  lakini  bila  ya  wingi  wa kutosha. Kutokana  na  mashambulizi nchini  Ujerumani  na  hivi karibuni  kabisa  mjini  Barcelona, Merkel  aliulizwa  hatua  gani serikali  yake  itachukua  kuimarisha  usalama.
Merkel  alisema  kwamba  mchanganyiko  wa  matumizi  ya  polisi  na matumizi  ya  teknolojia  inapaswa  kutumiwa  kuhakikisha  usalama. Amesema  kwamba  wakati  kuna  raia  wanaokadiriwa  kufikia 10,000   ambao  wamepata  itikadi  kali  na  kuwa  na  mawazo  ya itikadi  kali  nchini  Ujerumani, ni  watu 600  hadi  700  tu wanaonekana  kuwa  ni  hatari.
Merkel  amekosoa  matumizi  ya  Uturuki  ya  jeshi  la  polisi  wa kimataifa  Interpol kumkamata  kwa  kutoa  waranti  na  kutaka arejeshwe  nchini  humo mwandishi Mjerumani  Dogan Akhanli kutoka  nchini  Uhispania  siku  ya  Jumatatu  kuwa  na matumizi mabaya  ya  shirika  hilo  la  polisi  la  kimataifa. "Sio sahihi  na nafurahi  sana  kwamba  uhispania  imemuachia  huru," Merkel amesema. "Hatupaswi  kutumia  vibaya  mashirika  ya  kimataifa kama  Interpol kwa  madhumini  hayo."
Kansela Angela Merkel akifanyiwa mahojiano na waandishi habari
Kansela achukizwa na  viwanda vya magari
Kansela  amesema  atajaribu  kuunganisha  vifaa  vya  polisi  na utaratibu  wa  majimbo  16  nchini  Ujerumani. Amedokeza  kwamba wengi  hawafahamu upekuzi  wa  polisi  pamoja  na  uangalizi  wa vidio kwamba  unafanyakazi  kwa  njia  tofauti  katika  majimbo  hayo nchini  Ujerumani.
Amesema  chama  chake  cha  Christian Democratic , kitajaribu kuunganisha  mbinu  za  polisi , akisema : "Pia  nitazungumza tena na  mawaziri  wakuu  wa  majimbo  binafsi."
Merkel  pia  alitetea  uamuzi  wake  wa  kufungua  mipaka  ya Ujerumani  kwa  mamia  kwa  maelfu ya  wakimbizi miaka  miwili iliyopita. Alipoulizwa  iwapo  sasa  angefanya  tofauti , alisema: "Bado  nafikiri uamuzi  wangu  ulikuwa  sahihi." Ametoa  wito  wa umoja  zaidi  katika  bara  la  Ulaya  kusaidia  nchi  kama  Italia  na Ugiriki  kupambana  na  idadi  kubwa  ya  wahamiaji  wanaowasili katika  mipaka  yao.
Mpiga  kura  mmoja  aliuliza  swali  kwamba  kwanini  waombaji hifadhi  hawaruhusiwi  kufanyakazi  wakati  kesi  zao  zikifanyiwa mapitio  wakati  baadhi  wakisema  wamesubiri kwa  miaka  kadhaa wakipiewa  fedha  za  walipa  kodi wakati  wanataka  kufanyakazi.
Merkel  amewaambia  wapiga  kura  kwamba  amevunjwa  moyo  na tasnia  ya  makampuni  ya  kutengeneza  magari  kufuatia  kashfa  ya dizeli  ya  kampuni  ya  Vilkswagen. Amesema  waziri  wa  zamani wa  mazingira  alifahamu  madhara  yake. "Nimekasirishwa," Merkel amewaambia  watazamaji. Tasnia  ya  magari  imetishia  kujiingiza katika  matatizo  makubwa   katika  kashfa  hiyo na  makampuni yanapaswa  kujisahihisha  kwa  kiasi  kikubwa kadri wanavyoweza," amedokeza. Amesema  program mpya ipo  kwa  sasa  kuweza kusahihisha  makosa  hayo.
Mwandishi : Jane Mcintosh / ZR / Sekione  Kitojo
Mhariri: Mohammed Abrul Rahman

August 22, 2017

Vilabu vya Bundesliga vitafanya vipi katika msimu wa 2017-18?




Nani atashinda Taji la Bundesliga, nani ataingia Kinyang'anyiro cha Mabingwa, nani atafika kwenye Mabingwa wa Uropa na nani atashushwa daraja? Ufuatao ni utabiri wetu jinsi timu 18 za Bundesliga zitakavyochuana 2017-18.
Deutschland Bundesliga | Supercupsieger FC Bayern München (picture alliance/dpa/Revierfoto)

Bayern Munich

Katika ligi ya Bundesliga, timu 18 hucheza mechi 34 kila moja na mara nyingi Bayern Munich huibuka washindi wa taji. Imeshinda mara 27. Baada ya kumnunua Corentin Tolisso kwa kima cha euro milioni 40, ambacho ni juu zaidi katika historia yake, azma ya mabingwa hawa wa Ujerumani inasalia ile ile, kutwaa taji. DW inabashiri kuwa Bayern pekee ndiyo inaweza kutwaa taji la Bundesliga msimu huu

Bundesliga yarejea kwa kishindo




1. Bundesliga | Borussia Mönchengladbach - 1. FC Köln | TOR Mönchengladbach (picture-alliance/dpa/F. Gambarini)

Msimu mpya wa Bundesliga ulianza rasmi kwa kishindo. Borussia Moenchengladbach ilijigamba kwa kushinda mchuano wa watani wa jimbo la Rhine, baada ya kuifunga FC Cologne bao moja kwa bila.
Bao lao lilipatikana mapema katika kipindi cha pili wakati Nico Elvedi alifunga bao safi baada ya kupokea krosi kutoka kwa Ibrahima Traore. Matthias Ginter ni beki wa Gladbach "michuano ya dabi huwa maalum kwa mashabiki na wale wote wanaohusika na klabu. Kuna tofauti. Iwe ni mtu kuja ofisini kesho na kuweka bendera ya Cologne au Gladbach. Hii kawaida huwa michezo maalum na mazingira mazuri na ndio maana tuna furaha kubwa kuwa tumeshinda.
Katika mechi nyingine ya jana, Freiburg na Eintracht Frankfurt zilianza msimu kwa kutoka sare ya bila kufungana. Freiburg ilifunga bao katika kipindi cha kwanza, lakini mfumo wa kutumia video ulifuta bao la Tim Kleindienst baada ya kugundua kuwa mchezaji mwenzake alikuwa ameotea wakati bao hilo lilifungwa.
Mfumo huo wa VAR unafanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza katika ligi ya Ujerumani msimu huu. Ulianza kutumika Ijumaa na Bayern walinufaika kwa kupewa penalti ambayo Robert Lewandowski alifunga na kuwapa mabingwa hao watetezi ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bayer Leverkusen katika mechi ya ufunguzi.
1. Bundesliga FC Freiburg gegen Eintracht Frankfurt Sport (Imago/J. Huebner) Boateng amesaini mkataba miaka mitatu na Frankfurt
Kevin-Prince Boateng arejea Bundesliga
Kiungo wa Ghana Kevin-Prince Boateng alicheza mechi yake ya kwanza na Eintracht Frankfurt baada ya kuwa nje ya Bundesliga kwa miaka miwili alipotupwa nje ya kikosi cha Schalke. Na hapa anauzungumzia mchuano wa jana. "Nadhani tulionyesha mchezo mzuri. Tulikuwa imara kabisa katika ulinzi na ni bao pekee lililokosekana. Tulikuwa na nafasi mbili nzuri ambazo bahati mbaya hatukuzitumia vyema na hivyo hatujaweza kuchukua pointi tatu leo. Lakini nnaridhishwa na mchezo wa timu. Hatujaweza kuacha chochote nyuma.
Boateng mwenye umri wa miaka 30 alikamilisha uhamisho wa haraka haraka kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu na Frankfurt baada ya kuihama klabu ya Las Palmas ya Uhispania akitaja sababu za kibibafsi.
Katika mechi za Jumamosi, Borussia Dortmund iliizidi nguvu VfL Wolfsburg kwa kuilaza tatu bila. Kocha mpya Peter Bosz aliahidi kandanda la kuvutia, la kushambulia na timu yake, ambayo ilimaliza katika nafasi ya tatu msimu uliopita iliidhihirisha hilo. Mabao ya BVB yalifungwa na Christian Pulisic, Marc Bartra na Pierre-Emerick Aubameyang. Msikilize kocha Bosz "unapaswa kuridhika wakati umeshinda mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Wolfsburg na umekuwa na mchezo mzuri. Sehemu kubwa ya mchezo ilikuwa nzuri sana, hatukufungwa bao, lazima uridhike.
Ousmane Dembele anaondoka au anabaki?
Fußball Bundesliga Ousmane Dembele FC Schalke 04 - Borussia Dortmund (picture-alliance/Sport Moments/Paschertz) Dembele anasakwa na Barcelona
Na wakati BVB walishinda bila ya nyota wao Ousmane Dembele, suali ni kuwa je, anaondoka au atabaki? Afisa mkuu mtendaji wa Dortmund Hans-Joachim Watzke anasema klabu hiyo haina nia ya kulegeza msimamo wake kuhusiana na Dembele anayesakwa na Barcelona. Hiyo ina maana kuwa hatua ya kumwondoa Dembele kwenye shughuli za kikosi cha kwanza baada ya kukosa kufika mazoezini itaendelea kutekelezwa. Na Dortmund haitapunguza kiasi cha fedha wanachotaka kupewa kwa ajili ya kumuuza nyota huyo mwenye umri wa miaka 20.

Kwingineko, Schalke ilianza msimu kwa ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya RB Leipzig ambao walimaliza wa pili msimu uliopita. Na kwa matokeo hayo, inaonekana kuwa kocha wao chipukizi Domenico Tedesco amejiandaa kuirejesha klabu hiyo katika kiwango cha juu. Katika matokeo mengine, Hoffenheim walipata ushindi wa moja bila dhidi ya Werder Bremen, Hertha Berlin ikaifunga Stuttgart mbili sifuri. Vladimir Darida ni kiungo wa HSC "nadhani ilikuwa muhimu sana kwetu kujiamini baada ya kupata pointi tatu katika mechi ya kwanza ya msimu. Ni mwanzo mzuri, lakini msimu bado ni mrefu na lazima tuweze kucheza katika kila mtangane kama tilivyocheza leo".
Hanover iliishinda Mainz moja bila wakati Hamburg ambayo ilinusurika kushushwa daraja msimu uliopita, iliifunga Ausburg moja bila, huyu hapa kiungo wa Hamburg, Aaron Hunt. "Unaweza kufikiria nini kingetokea hapa tena kama hatungekuwa tumeshinda. ndio maana timu imekuwa bora zaidi kwa sababu inacheza kwa pamoja tena. Lazima niisifie timu. Imejaribu kucheza vizuri kabisa kwa kujituma. Tumepambana kwelikweli leo na nadhani mwishowe tulistahili kupata ushindi.
Lakini ushindi huo ulikuwa na gharama yake baada ya mfungaji wa bao hilo Nicolai Mueller kuumia wakati akishangilia goli lake na sasa atakuwa mkekani kwa karibu miezi saba

Congo yatolewa katika dimba la CHAN




Burkina Faso iliifunga Ghana mabao mawili kwa moja hapojana kwenye mchuano wa duru ya kufuzu katika dimba la Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani – CHAN.
Mabingwa watetezi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na timu waliyoifunga katika fainali ya 2016, Mali, walibanduliwa nje ya dimba hilo siku ya Jumamosi.
Ghana, makamu bingwa mara mbili katika awamu nne za mwisho za dimba hilo, ilitoka sare ya mabao mawili kwa mawili na Burkinabe katika mechi ya mkondo wa kwanza.
Hivyo Burkina Faso imefuzu kwa jumla ya mabao manne kwa matatu na itajiunga na nchi nyingine 15 katika dimba hilo linalochezwa kila baada ya miaka miwili, na ambalo litaandaliwa Kenya kuanzia Januari 12 hadi Februari 4.
Katika eneo la Afrika Mashariki, Uganda ilifuzu kwa jumla ya mabao matatu kwa mawili baada ya kuiangusha Rwanda licha ya kuzabwa mbili sifuri mjini Kigali katika mchuano wa marudiano.
Aidha Sudan ilifuzu baada ya kuiangusha Ethiopia kwa jumla ya bao moja kwa sifuri. Namibia ilijikatia tikiti kwa mara ya kwanza baada ya kuwafunga Wacomoro mabao mawili kwa bila. Kenya na Guinea ya Ikweta, ambao walifuzu baada ya Gabon kujiondoa, pia watashiriki dimba hilo la CHAN kwa mara ya kwanza.

Duterte aahidi polisi waliomuua kijana wa miaka 17 watakwenda jela



Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte, jana ameuhakikishia umma wake kwamba maafisa wa polisi waliohusika na kifo cha kijana wa kiume aliyekuwa na umri wa miaka 17 wakati wa operesheni ya kupambana na madawa ya kulevya watatumikia kifungo jela, 

wakikutikana na hatia. Duterte ameongeza kwamba Idara ya Sheria tayari imeshaiamuru Ofisi ya Taifa ya Uchunguzi kubaini iwapo maafisa wa polisi walihusika katika kifo cha, Kian Loyd Delos Santos, kilichotokea wiki iliyopita. Masaa machache kabla ya hapo, 

mamia ya watu waliandamana katika mji mkuu wa Manila, kupinga kifo cha Delos Santos, ambaye familia yake na marafiki wamekana kwamba alikuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya. Kampeni ya kupambana na madawa ya kulevya ya Rais Duterte, ambayo imesababisha vifo vya maelfu ya watu ndani ya mwaka mmoja, imekuwa ikishutumiwa sana na makundi ya kutetea haki za binaadamu pamoja na serikali za kigeni.

Grace Mugabe kurejea Zimbabwe



Grace Mugabe  kurejea Zimbabwe

Baada ya kupewa kinga ya kidiplomasia na serikali ya Afrika Kusini, mke wa rais wa Zimbabwe Grace Mugabe alirejea nyumbani siku ya Jumapili, licha ya miito kwamba ashitakiwe kwa madai ya kumshabulia mwanamitindo Jo'berg.
Shirika la utangazaji la Zimbabwe ZBC lilimuonyesha Grace Mugabe akisalimiana na maafisa wa serikali na jeshi katika uwanja wa ndege wa Harare baada ya kushuka kwenye ndege ya shirika la ndege la Zimbabwe pamoja na mume wake, ambaye alihudhuria mkutano wa kilele wa viongozi wa kanda ya kusini mwa Afrika mjini Pretoria. Mugabe na mke wake hawakuhudhuria mazishi ya kitaifa ya afisa mwandamizi wa chama tawala katika mji mkuu wa Zimbabwe; kawaida rais anakuwa mgeni rasmi katika matukio kama hayo.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane, ilimpa kinga ya kidiplomasia Grace Mugabe kupitia taarifa iliyochapishwa katika gazeti la serikali lililochapishwa siku ya Jumapili. Taarifa hiyo iliyosainiwa siku ya Jumamosi, inatambua "kinga na fursa za mke wa rais wa Zimbabwe, Dk. Grace Mugabe."
Awali polisi ya Afrika Kusini ilitoa tahadhari ya kiusalama kwenye maeneo ya mipakani kuhakikisha haondoki bila kutambuliwa, na walisema walikuwa wanasubiri uamuzi wa serikali kuhusu maombi ya kinga.
Model Gabriella Engels zeigt Wunde (picture-alliance/dpa/AP/Debbie Engels) Mwanamitindo Gabriella Engels akionyesha jeraha alilolipata baada ya kupigwa kwa waya na mke wa rais wa Zimbabwe, Grace Mugabe.
Chama kikuu cha upinzani nchini humo, cha Democratic Alliance kimetaka ufanyike uchunguzi wa bunge kuhusu uamuzi wa serikali kumuachia mke wa rais wa Zimbabwe kuondoka na kilisema kupitia ukurasa wake wa twitter, kwamba serikali haikuwa tena na uhalali katika nyanja ya diplomasia ya kimataifa na inaonyesha kupuuza kabisaa utawala wa sheria.
Kisa chalinganishwa na kuachiwa Hassan al-Bashir 2015
John Steenhuisen, afisa mwandamizi wa upinzani, alilinganisha namna serikali ya Afrika Kusini ilivyoshughulikia kesi ya Mugabe na uamuzi wa serikali kumruhusu Rais wa Sudan Omar al-Bashir kuondoka nchini humo mwaka 2015, hata wakati alipotakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa madai ya uhalifu wa kivita, liliripoti shirika la Afrika.
Gabriella Engels, mwanamitindo mwenye umri wa miaka 20, alisema Grace Mugabe alimshambulia Agosti 13, kwa kumchapa na waya wa umeme uliomkata kwenye paji la uso. Likizungumzia habari za kurejea kwa Mugabe nchini Zimbabwe, kundi linalomwakilisha Engels lilisema Jumapili kwamba litakwenda mahakamani kuipinga serikali ya Afrika Kusini kuhusu suala la kinga.
"Tutatumia mkakati wa muda mrefu kuhusu suala hili," alisema Willie Spies, mwakilishi wa kisheria kutoka kampuni ya AfriForum, ambalo ni shirika linalowawakilisha Waafrika Kusini weupe wa jamii ya wachache ya Afrikaner.
"Anaweza kuwa amerudi Zimbabwe, lakini hiyo inaweza kumaanisha kwamba itakuwa vigumu kwake kuja tena Afrika Kusini huko mbeleni," Spies alisema. Vyombo vya habari vya serikali ya Zimbabwe vimekuwa kimya kwa kiasi kikubwa kuhusu kadhia hiyo ya mke wa rais wa Zimbabwe.
Mke huyo wa rais wa Zimbabwe amekosolewa kwa kuwa na hasira za haraka na safari za manunuzi makubwa, lakini nyota yake ya kisiasa inayozidi kupanda imewafanya baadhi wajiulize iwapo anafanya mikakati ya kumrithi mume wake.
Simbabwe Präsident und Gattin Grace Mugabe Präsidentingattin (Getty Images/AFP/J. Njikizana) Grace na mume wake Rais Robert Mugabe.
Hivi karibuni alisema chama tawala cha Zimbabwe kinapaswa kurejesha kipengee kwenye katiba, kinachosema kwamba mmoja wa makamu wa rais anapaswa kuwa mwanamke, alimpa changamoto waziwazi mume wake mwenye umri wa miaka 93 atangaze mrithi.
Pia siku ya Jumapili, mmoja wa makamu wawili wa rais wa Zimbabwe, Phelekezela Mphoko, aliongoza mazishi ya Shuvai Ben Mahofa, mwanachama mwandamizi wa chama tawala cha Zanu-PF aliefariki wiki moja iliyopita.
Kuzuwiliana safari za ndege za mashirika ya serikali
Shirika la ndege la Afrika Kusini wakati huo lilisema Jumapili - saa chache baada ya Mugabe kurejea mjini Harare - kwamba lilikuwa linarejesha safari zake kati ya Afrika Kusini na Zimbabwe, baada ya safari hizo kuzuwiwa na maafisa wa Zimbabwe.
Hatua ya Zimbabwe iliochukuliwa Jumamosi, ilifuatia kuzuwiwa kwa ndege ya shirika la Zimbabwe katika uwanja mkuu wa Johannesburg Ijumaa jioni. Ndege hiyo iliruhusiwa kuruka Jumamosi usiku, walisema maafisa wa usafiri wa anga. HAikuwa bayana iwapo Mugabe alitumia ndege hiyo hiyo kurejea nchini Zimbabwe.
Mataifa yote mawili yalisema yameweka vikwazo kwa sababu ndege zilizoathiriwa hazikuwa na vibali vya operesheni za nje." Willie Spies, wakili anaemwakilisha mwanamitindo aliesema ameshambuliwa, alisema huenda mgogoro huo wa safari za ndege ulikuwa njama iliyosanifiwa kuondoa nadhari kutoka kwenye matatizo ya mke wa rais.
Mwandishi: Iddi Ssessanga/ape
Mhariri: Lilian Motono.

Mshukiwa mkuu wa shambulizi la Barcelona atambuliwa

Mshukiwa mkuu wa shambulizi la Barcelona atambuliwa

 Picha iliyopatikana katika mtandao wa kijamii ya Younes Abouyaaquoub

Polisi nchini Uhispania imemtambua mshukiwa mkuu wa shambulio la Barcelona. Hayo yanajiri huku msako dhidi ya mshukiwa huyo anayeaminiwa kuwa raia wa Morocco ukitanuliwa barani Ulaya kwa jumla.
Polisi nchini Uhispania imethibitisha kuwa imemtambua mshukiwa mkuu wa shambulio la Barcelona lililofanywa mwishoni mwa wiki iliyopita. Hayo yanajiri huku msako dhidi ya mshukiwa huyo anayeaminiwa kuwa ni raia wa Morocco ukitanuliwa barani Ulaya kwa jumla. Wakati huohuo idadi ya watu waliouawa kufuatia shambulizi hilo imefikia 15. Hii ni baada ya polisi kuupata mwili wa mtu aliyedungwa kisu ndani ya gari linaloaminika kutumiwa na mshukiwa kutoroka.
Waziri wa jimbo la Catalonia anayeshughulikia mambo ya ndani Joaquim Fornalisema katika mahojiano na redio ya jimbo hilo kuwa dalili zote zinaashiria kuwa mshukiwa ni Younes Abouyaaqoub, aliye na umri wa miaka 22, raia wa Morocco. Aidha polisi imetoa tahadhari na kusema huenda Abouyaaqoub amejihami na hivyo ni mtu hatari.
Picha iliyopatikana katika mtandao wa kijamii ya Younes Abouyaaquoub Picha iliyopatikana katika mtandao wa kijamii ya Younes Abouyaaquoub
Uchunguzi watanuliwa Ulaya
Maafisa nchini Uhispania, leo wameiarifu polisi ya Ulaya kuhusu utambulisho wa mshukiwa huyo, ili kuwezesha uchunguzi na msako dhidi yake barani Ulaya kwa jumla.
Akizungumza na wanahabari ambapo pia alionesha picha ya mshukiwa huyo mkuu, afisa mkuu wa polisi wa Catalonia Juan Ignacio Zoido alisema: "Hadi sasa juhudi za polisi zimelenga kumkamata mtu huyu, Younes Abouyaaqoub ambaye ametambuliwa kuwa dereva wa lori lilotumiwa katika shambulizi la Barcelona, na ambaye anasakwa na vyombo vya usalama vya taifa pamoja na polisi, na ninafikiri ndiyo itakuwa shughuli kuu katika siku zijazo hadi tumpate."
Inaaminika kuwa Abouyaaqoub ndiye mshukiwa pekee ambaye hajakamatwa miongoni mwa wengine 12 ambao ni wa kundi la kigaidi, na huenda yupo Uhispania au ametorokea nchi nyingine.
Gari la polisi likiondoka na mshukiwa aliyekamatwa baada ya msako mjini Ripoll Gari la polisi likiondoka na mshukiwa aliyekamatwa baada ya msako mjini Ripoll
Misako Ripoll
Forn ameongeza kuwa wachunguzi wanaolenga kundi la kigaidi, wamepiga kambi katika mji wa Ripoll, ambapo misako kadhaa imefanywa katika makaazi ya watuhumiwa, ikiwemo nyumba ya imamu mmoja kutoka Morocco Abdelbaki Es Satty ambaye anasemekana aliwapandikiza itikadi kali vijana wa Ripoll .
Imamu huyo anayeamiwa aliuwawa katika mripuko uliotokea Alcanar siku ya Jumatano wiki iliyopita, aliwahi kufungwa jela kando na kuwa wakati mmoja alikuwa pamoja na mshukiwa mkuu anayesakwa sasa kwa tuhuma za ugaidi. Polisi walipata mitungi 120 ya gesi na vifaa vya kutendeneza milipuko ndani ya nyumba yake.
Maafisa wa polisi wametangaza pia kuwa wameupata mwili wa mtu aliyedungwa kisu ndani ya gari linaloaminika kuwa lilitumiwa na mshukiwa alipokuwa akitoroka kutoka eneo la shambulizi.
Shambulio la Barcelona lilifuatiwa na jingine kama hilo eneo la Cambrils saa kadhaa baadaye ambapo polisi waliwaua washukiwa watano. Hadi sasa Jumla ya watu 15 wameuwawa na 130 kujeruhiwa katika mashambulio hayo ya Barcelona.

Marekani na Korea Kusini zaanza mazoezi ya kijeshi



Südkorea Gemeinsame Militärübung mit der USA (Getty Images/AFP/Jung Yeon-Je)

Wanajeshi wa Marekani na Korea Kusini wameanza mazoezi ya kijeshi ya kila mwaka, baada ya marais wa Marekani na Korea Kaskazini kujibizana maneno ya kuashiria vita na majaribio mawili ya makombora ya Korea Kaskazini.
Mazoezi hayo ya pamoja ya kijeshi ya kila mwaka yajulikanayo kama 'Ulchi Freedom Guardian' ambayo kwa kiasi kikubwa yanaendeshwa kwa kompyuta kwa teknolojia ya kidijitali na kufanyika kila majira ya joto, yamepokewa kwa hasira na upande wa Korea Kaskazini, ambayo inayatazama kama mazoezi ya kujitayarisha kwa uvamizi.

Akizungumza na Baraza lake la mawaziri, Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, amesema leo  kwamba ushirikiano wa kijeshi kati ya Korea Kusini na Marekani haukusudii kuongeza mvutano kwenye rasi ya Korea, na ameionya Korea Kaskazini dhidi ya kulitumia zoezi hilo la kijeshi kama sababu ya kufanya vitendo vya uchochezi.
"Korea Kaskazini inapaswa kufahamu kwamba kutokana na uchokozi wake wa mara kwa mara, zoezi la pamoja kati ya Korea Kusini na Marekani litaendelea. Natumai kuwa maafisa wa serikali zetu pamoja na wanajeshi wapo tayari kujibu uchokozi wowote ule utakaotokana na zoezi la mara hii, na nawataka watu wetu kuwa na mshikamano zaidi kuliko wakati mwengine wowote," amesema Rais, Moon Jae-in, wa Korea Kusini.

Mahakama nchini India yapiga marufuku talaka ya kiislamu

A bride is sitting with her hand covered in henna

Mahakama ya juu nchini India imeamua kuwa talaka ya mara moja katika dini ya kiislamu ni kinyume na katiba, uamuzi ambao umekuwa ni ushindi mkubwa kwa haki wanawake.
India ni moja ya nchi chache ambapo mwanamume muislamu anaweza kumtaliki mkewe kwa kutamka neno talaq mata tatu.
Uamuzi huo wa mahakama unafutia kesi zilizokuwa zikipinga talaka hiyo.
Kesi hizo ziliwasilishwa mahakamani na wanawake watano waislamu waliokuwa wamepewa talaka kwa njia hiyo pamoja na na makundi mawili ya kutea haki.
Miaka ya hivi karibuni visa vingi vimeibuka ambapo wanaume waislamu huwataliki wake zao kwa kutamka neno talaq mara tatu, kwa njia ya simu au kwa kutuma ujumbe ya sms, kupitia WhatsApp na Skype.
Licha ya njia hiyi ya kutaliki kutumiwa kwa miongo kadha hiajatajwa popote pale kwenye Sharia au Koran

Azarenka hatoshiriki michuano ya Marekani

 
Tenesi
Nyota wa tenesi kwa upande wa wanawake Victoria Azarenka hatoshiriki michuano mkubwa ya wazi ya Marekani.





  Nyota wa tenesi kwa upande wa wanawake Victoria Azarenka hatoshiriki michuano mkubwa ya wazi ya Marekani.
Azarenka mwenye umri wa miaka 28 hatoshiriki mashindano hayo yatayoanza kutimua vumbi kuanzia Augost 28, kwa sababu za kifamilia .

"Nasikitika sintoweza kushiriki mashindano ya wazi ya Marekani ya mwaka huu kutokana na hali yangu ya kifamilia inayoendelea kwa sasa," Azarenka alieleza hayo siku ya Jumatatu.
Mchezaji huyu alirejea uwanja mwezi wa sita mwaka huu baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana kuwa mjamzito na alifungua mwanae Leo mwezi Desemba mwaka jana.

Wanaume 4 washtakiwa kwa kula nyama ya binadamu Afrika Kusini


Wanaume wanne wamefikishwa kwenye mahakama ya Afrika Kusini kujibu mashtaka ya ulaji nyama ya binadamu, baada ya madai kuwa mmoja wao alifika katika kituo cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama ya binadamu.
Alipohojiwa zaidi mwanamume huyo alionyesha sehemu ya mguu na mkono wa binadamu.
Kisha polisi wakaandamana na mwanamume huyo hadi kwa nyumba moja iliyo mtaa wa KwaZulu-Natal, ambapo sehemu zaidi za miili ya binadamu zilipatikana.
Wanaume wanne, wawili kati yao madaktari wa kitamaduni walikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji au kupanga kuua.
Walifikishwa katika mahakama ya Estcourt kilomita 175 kaskazini magharibi mwa mji wa Durban.
Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa kuna uwezekano kuwa wanaume hao wanne walio na umri wa kati ya miaka 22 na 32 ni sehemu ya genge kubwa.
Uchunguzi bado unaendelea na polisi wamewashauri watu ambao jamaa zao wametowewa kujitokeza.
Wachunguzi wa visa vya uhalifu wameitwa kutambua sehemu hizo za binadamu, kwa kuwa haijulikana ikiwa sehemu hizo ni za mtu mmoja au watu kadhaa.
Mwezi mmoja uiopita mjini Durban, mwanamume mmoja alikamatwa akiwana na kichwa cha binadamu ambacho inanamiwa alikuwa na mpango wa kikiuza kwa daktari ya kitamadunia.