Merkel asikitishwa na viwanda vya magari
Kansela Angela Merkel alijibu maswali ya wapiga
kura katika kipindi cha maswali na majibu cha televisheni,
ambapo aliulizwa kuhusu usalama, wahamiaji na kashfa ya kupima
moshi unaochafua mazingira kwa magari ya VW
Kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Ujerumani mwezi ujao inaendelea. Bibi Markel Anagombea muhula wa nne.
Kansela
Angela Merkel alishiriki katika kipindi cha televisheni cha
kituo cha RTL ambacho kilikuwa kinarushwa moja kwa moja, Jumamosi
jioni. Wapiga kura walimuuliza maswali kansela wakati akiwania
muhula wa nne madarakani katika uchaguzi wa mwezi Septemba.
Uchunguzi
wa maoni ya wapiga kura unaonesha chama cha kansela Merkel
cha Christian Democratic Unioni CDU pamoja na chama ndugu cha
jimbo la Bavaria Christian Social Union , CSU vitakuwa kundi
kubwa la chama bungeni lakini bila ya wingi wa kutosha.
Kutokana na mashambulizi nchini Ujerumani na hivi karibuni kabisa
mjini Barcelona, Merkel aliulizwa hatua gani serikali yake
itachukua kuimarisha usalama.
Merkel alisema kwamba
mchanganyiko wa matumizi ya polisi na matumizi ya teknolojia
inapaswa kutumiwa kuhakikisha usalama. Amesema kwamba wakati kuna
raia wanaokadiriwa kufikia 10,000 ambao wamepata itikadi kali
na kuwa na mawazo ya itikadi kali nchini Ujerumani, ni watu 600
hadi 700 tu wanaonekana kuwa ni hatari.
Merkel amekosoa
matumizi ya Uturuki ya jeshi la polisi wa kimataifa Interpol
kumkamata kwa kutoa waranti na kutaka arejeshwe nchini humo
mwandishi Mjerumani Dogan Akhanli kutoka nchini Uhispania siku ya
Jumatatu kuwa na matumizi mabaya ya shirika hilo la polisi la
kimataifa. "Sio sahihi na nafurahi sana kwamba uhispania
imemuachia huru," Merkel amesema. "Hatupaswi kutumia vibaya
mashirika ya kimataifa kama Interpol kwa madhumini hayo."
Kansela achukizwa na viwanda vya magari
Kansela
amesema atajaribu kuunganisha vifaa vya polisi na utaratibu wa
majimbo 16 nchini Ujerumani. Amedokeza kwamba wengi hawafahamu
upekuzi wa polisi pamoja na uangalizi wa vidio kwamba
unafanyakazi kwa njia tofauti katika majimbo hayo nchini
Ujerumani.
Amesema chama chake cha Christian Democratic ,
kitajaribu kuunganisha mbinu za polisi , akisema : "Pia nitazungumza
tena na mawaziri wakuu wa majimbo binafsi."
Merkel pia
alitetea uamuzi wake wa kufungua mipaka ya Ujerumani kwa mamia
kwa maelfu ya wakimbizi miaka miwili iliyopita. Alipoulizwa iwapo
sasa angefanya tofauti , alisema: "Bado nafikiri uamuzi wangu
ulikuwa sahihi." Ametoa wito wa umoja zaidi katika bara la
Ulaya kusaidia nchi kama Italia na Ugiriki kupambana na idadi
kubwa ya wahamiaji wanaowasili katika mipaka yao.
Mpiga
kura mmoja aliuliza swali kwamba kwanini waombaji hifadhi
hawaruhusiwi kufanyakazi wakati kesi zao zikifanyiwa mapitio
wakati baadhi wakisema wamesubiri kwa miaka kadhaa wakipiewa
fedha za walipa kodi wakati wanataka kufanyakazi.
Merkel
amewaambia wapiga kura kwamba amevunjwa moyo na tasnia ya
makampuni ya kutengeneza magari kufuatia kashfa ya dizeli ya
kampuni ya Vilkswagen. Amesema waziri wa zamani wa mazingira
alifahamu madhara yake. "Nimekasirishwa," Merkel amewaambia
watazamaji. Tasnia ya magari imetishia kujiingiza katika matatizo
makubwa katika kashfa hiyo na makampuni yanapaswa kujisahihisha
kwa kiasi kikubwa kadri wanavyoweza," amedokeza. Amesema program mpya
ipo kwa sasa kuweza kusahihisha makosa hayo.
Mwandishi : Jane Mcintosh / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri: Mohammed Abrul Rahman
No comments:
Post a Comment