Ligi kuu nchini Uingereza imeendelea tena leo hii kwa michezo mbalimbali kupigwa katika viwanja tofauti.
Huko Wembley kikosi cha Tottenham kimefanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 2 – 0 dhidi ya Huddersfield Town na hivyo kuwasogelea kwa ukaribu Manchester United inayoshika nafasi ya pili.
Mabao ya Spurs yakifungwa na kiungo wao raia wa Korea Kusini, Son Heung-min dakika ya (27 na 54).
Swansea nao wakiwa katika dimba la Liberty wamefanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 4 – 1 dhidi ya West Ham.
Waliyokuwa mwiba mkali katika mchezo huo kwa upande wa Swansea ni Ki Sung-yueng, Van der Hoon, King na J Ayew wakati bao la West Ham likifungwa na Antonio.
No comments:
Post a Comment