Mbinu saba (7) za mafanikio
Mbinu saba (7) za mafanikio
Kama na wewe ni miongoni mwa watu ambao hukata tamaa katika safari yako ya kuelekea mafanikio, naomba nichukue nafasi hii kuweza kukaribisha rasmi hapa Muungwana ambapo katika makala haya tutazungumzia namna sahihi ya kupanga malengo yako hadi kufikia mafanikio.
Wengi hujikuta wakiishia njiani katika safari yao ya mafanikio hii ni kutokana kutokujua namna ya kuzitambua mbinu za kukuza malengo hadi mafanikio.
Zifutazo ndizo mbinu za kupanga malengo ya kimafanikio
1. Malengo ni lazima yaandikwe.
Malengo lazima uyaandike sehemu ambayo inaonekana, hapa ni maana ya kwamba uandike sehemu ambayo inaonekana, kufanya hivi kutakuwa kuna kutakufanya malengo hayo uwe unayakumbuka na kujua namna ya kuayatekeleza.
Unaweza ukayaandika malengo hayo kuyaweka katika simu yako katika (screen saver), kioo ambacho unakitumia kujitazama asubuhi na sehemu nyingine ambayo utayaona malengo hayo.
2. Weka vipaumbele katika malengo yako.
Inawezekana fika ukawa na malengo mengi, yaandike malengo hayo katika makundi matatu.
Kundi la kwanza jua yapi ni malengo ya muhimu yapi si malengo ya muhimu, yapi ni malengo ya haraka na yapi sio malengo, na tatu andika malengo ambayo sio ya muhimu sana.
Endapo utagawa malengo hayo utajua ni kipi kinatakiwa kuanza na kipi kinatakiwa kufuata na kwa muda gani.
3. Anza kwa kuanza na hatua ndogo.
Siku zote kama ilivyo ukuaji Wa kiumbe chochote chenye uhai huanza ukuaji wake katika hali ya chini. Kama ilivyo kwa kiumbe yeyote katika ukuaji hata katika ukuaji wa mafanikio yako huanza katika ngazi za chini.
Kitu cha msingi ni kuweza kupanua wigo mpana kwa ajili ya kupata mafanikio zaidi kwa kila jambo ambalo unalifanya. Na kwa kuwa mafanikio hayana ukomo hakikisha ya kwamba kila iitwayo leo unapata kiu ya kutaka kufanikiwa zaidi.
4. Malengo ni lazima yawe chanya.
Mara kadha watu huwa na ndoto nzuri sana, na pia wengi wao hupanga mambo mazuri kwa ajili ya utekelezaji wa ndoto hizo, ila changamoto kubwa ambayo huwa inakuja ni pale ambapo linakuja suala la utekelezaji wa jambo hilo.
Hapo sasa ndipo utakapoanza kumsikia mtu anasema aaah hivi nitaweza kweli, inatakiwa uondokane na kukata tamaa, vinginevyo kufanikiwa utaendelea kusikia kwa akina Donald Trump.
5.Malengo lazima yawe katika muda maalumu.
Ni lazima uweke muda kamili kwa ajili ya kutekeleza malengo yako, ifike mahali Malengo yako yafananishe na makampuni yanayohusika ujenzi kwani wao kabla ya kuanza kwa mradi huwa wanafanya mahesabu ili kujue mradi huo wa ujenzi utachukua muda gani mpaka ukamilike.
Ukiishi katika utaratibu Wa kuweka mbinu hiyo itakuwa ni rahisi kwako kutekeleza mambo ambayo unataka kutekeza. Kwa mfano lengo lako ni kujenga nyumba unaweza ukaandika katika lengo lako ya kwamba baada ya muda fulani inabidi uwe umekamilisha ujenzi huo.
Kupanga malengo bila kujua muda Wa kutekeleza malengo ni sawa na bure. Hivyo ni vyema ukajua ya kwamba muda ni mali katika kufanikisha malengo yako kwa wakati sahihi.
6. Malengo ni lazima yawe na mbinu za utekelezaji.
Watu wengi wana malengo ya kusema kwa mdomo tu. Lakini nikwambie ya kwamba ukitaka kufa maskini basi endelea na utaratibu huo Wa kuweka malengo mdomoni.
Kama kweli unataka kufanikiwa hakikisha ya kwamba malengo ambayo umejipangia umeyaandika na kuandika mbinu au njia kwa ajili ya utekelezaji wa malengo hayo.
Kufanya hivi kutakusaidia kujua jinsi ambavyo utayatekeleza malengo hayo ili kupata mafanikio. Kwa mfano kama malengo yako ni kujenga nyumba basi huna budi kuandika mbinu ambazo zitakusaidia kutengeza nyumba hiyo, pia hapa huenda sambamba na bajeti ya utekelezaji wa malengo yako.
7. Malengo ni lazima yapimike.
Kila malengo ambayo umejipangia Ni lazima yaweze kupimika. Kama nilivyoeleza hapo awali ya kwamba malengo ni lazima yawe na muda maalum kwa ajili ya utekelezaji.
Hivyo ni lazima upime malengo yako ni wapi ambapo umefikia? Katika muda ambao umepanga kuyatekeza malengo hayo je unahisi utafikia malengo hayo?
Pia uchunguzi yakinifu juu ya malengo yako ni lazima ufanyike ili kujua fursa na changamoto ambazo zimejitokeza katika kuteleza malengo yako.
Post a Comment