Header Ads

Zitambue dalili na za mwanamke anayetaka kuachana nawe katika mahusiano


Kuna tofauti kubwa ya kimaamuzi kati ya mwanaume na mwanamke kwenye suala la kuachana. Inaelezwa kwamba, wanaume ni rahisi kuamua ndani ya dakika moja na kutangaza kuvunja uhusiano, lakini kwa wanawake maamuzi yao mara nyingi hutanguliwa na dalili, ingawa hata wanaume nao wanazo.

Uchunguzi unaonesha kuwa, wanawake wengi hawawezi kuficha sana hisia zao za mapenzi, lakini pia kwenye chuki hawakujaaliwa uvumilivu. Wanasaikolojia wanakiri kwamba, kutambua mawazo yaliyomo ndani ya mwanamke kwa kumtazama muonekano wake usoni ni rahisi kuliko mwanaume ambaye anatajwa kuwa na uwezo wa kuficha mawazo yake.

Muongozo huo wa kitaalamu wa kumtambua mwanamke anayekaribia kukuacha ni kazi rahisi, ambayo inaweza kuanzia kwenye kona ya mazoea ya tabia zake za kila siku kwenye uhusiano wa kimapenzi. Ni imani yangu kuwa kila mwanaume anamfahamu mpenzi wake katika sura mbili za chuki na furaha yake.

Atakuwa mwanaume wa ajabu ambaye atarudi nyumbani kwake na kushindwa kusoma sura ya mkewe na kujua kama ana furaha au amekwazika.

Ninapotazama uwezekano rahisi wa kumtambua mwanamke, nafika mahali pa kuamini kuwa dokezo chache nitakazotoa hapa chini zinaweza kuwa msaada kwa wanaume wengi kujua kama wamekaribia kuwekwa kando kimapenzi.

1. Hupenda kujitenga.
Mwanamke ambaye anapenda kujitenga na mpenzi wake atakuwa kwenye hatua za awali za kuelekea kuachana naye. Tabia ya mwanamke kutopenda kukaa karibu na mumewe au mpenzi wake inatajwa kama ishara ya kuchoka au kukinai penzi. Hoja inabaki pale niliposema yeye kushindwa kuamua haraka na hivyo kutengeneza kwanza hali ya kumpuuza mpenzi wake.

2. Hupoteza hamu ya tendo la ndoa.
Mwanamke ambaye hafurahii tendo la ndoa kwa mumewe au mpenzi wake yuko kwenye hatua za kuacha. Mara zote msisimko wa kimapenzi huashiria utoshelevu wa kihisia ambao ndiyo unaoelezwa kuwa ni muhimu kwenye uhusiano wa kimapenzi kuliko kitu kingine chochote.

Hii ina maana kwamba, mwanamke anayetosheka na kuvutiwa na mwanaume aliyenaye hawezi kukosa hisia za kimapenzi hasa anapokuwa na mwenza wake faragha.

3. Hupenda kukosoa kila kitu.
Kama nilivyosema, kujua historia ya penzi lenu namna lilivyoanza ni jambo muhimu kwa sababu husaidia kujua kama kuna mabadiliko hatari ya tabia za mwanamke.

Ikitokea mpenzi wako ambaye hapo mwanzo alikuwa msikivu na ghafla ukaanza kuona amekuwa mkosaji na mpingaji wa mwenendo wako au kila unachofikiria kukifanya, tambua kuwa hiyo ni ishara kuwa amechoka kilichobaki ni nafasi ya kukuacha.

4. Kutokukutegemea
Mwanamke ambaye ana kusudio la kukuacha huanza kwa kuuondoa utegemezi. Ikiwa alikuwa anakuomba nauli, fedha ya matumizi, ada na huduma nyingine atasitisha bila kukuambia na bado utaona anaendelea kujimudu kama kawaida au kuteseka kimya kimya. Kuacha kukutegemea kama zamani ni dalili za kuweza kuishi bila wewe na hivyo kutafsiri uwezekano wa kukuacha wakati wowote.

5. Kupunguza mawasiliano.
Asikwambie mtu aiseeeh, mapenzi ni mawasiliano bora kati ya mume na mke. Endapo itatokea ya kwamba hakuna mawasiliano thabiti baina yako na mpenzi wako kama ambavyo ilikuwa mwanzo basi tambua fika penzi lenu limefika ukingoni.

Hizo dalili chache kati ya nyingi za mwanamke ambaye anataka kuachana nawe katika muhusiano ya kimapenzi.

No comments