Header Ads

Shirikisho la soka CAF lampiga marufuku ya maisha refa wa Kenya Aden Marwa


Caf ilitoa tangazo hilo baada ya mkutano wa bodi yake ya nidhamu.
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limempiga marufuku ya maisha mpiga kipenga kutoka Kenya Aden Marwa kutoshiriki katika mechi yoyote ya soka.
Uamuzi huo umetolewa baada ya refa huyo kunaswa kwenye video kwenye makala ya uchunguzi akipokea pesa kutoka kwa mwandishi wa habari kabla ya kuanza kwa mashindano ya kombe la Dunia Urusi.
Marwa, alichaguliwa kuismamia mechi katika mashindano hayo , na alitemwa kutoka orodha ya mashindano hayo baada ya uchunguzi huo wa Anas.
Shirikisho la kandanda Barani Afrika CAF pia limechukua hatua dhidi ya marefa wengine 10, waliopigwa marufuku kwa kati ya miaka miwili na miaka 10.
CAF ilitoa tangazo hilo baada ya mkutano wa bodi yake ya nidhamu.
Uchunguzi huo uliofanywa na mwanahabari mpekuzi Anas Aremeyaw Anas kutoka Ghana, ulimuonyesha Refa wa Kenya Aden Marwa akipokea dola 600 kabla ya kusimamia mechi nchini Ghana, kitendo kilichofanyika kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kombe la Dunia Urusi.
Alijiondoa kutoka usimamizi wa mechi katika mashindano hayo chini Urusi, ambapo alichaguliwa kama mmoja wa wapiga kipenga wasaidizi.
Na sasa shirikisho la kandanda barani Afrika CAF limempiga marufuku ya maisha kushiriki shughuli zozote za kandanda.
Aidha wengine kumi na mmoja wamesimamishwa kazi kwa muda wakisuburi vikao vya nidhamu.
Mwandishi wa habari wa Ghana Anas Aremayew Anas akihojiwa na wanahabari kuhusu makala yake ya upelelezi yaliochukua miaka miwili
Image captionMwandishi wa habari wa Ghana Anas Aremayew Anas akihojiwa na wanahabari kuhusu makala yake ya upelelezi yaliochukua miaka miwili
Marefa hao - 10 wa Ghana na mmoja wa Liberia - wanasubiriwa kufika mbele ya bodi ya nidhamu ya CAF Agosti 5.
Refa wa Ivory Coast Denis Dembele, alipigwa marufuku ya miaka 6.
Uchunguzi huo uliopeperushwa na BBC mwezi jana, ulitoa ushahidi wa ufisadi na ushawishi wa matokeo ya mechi katika ulimwengu wa kandanda Afrika Magharibi.
Mkuu wa shirikisho la soka nchini Ghana, Kwesi Nyantakyi alionekana kwenye video akipokea dola 65,000 kama zawadi.
Baada ya kumulikwa alijiuzulu, na serikali ya Ghana ililivunjilia mbali shirikisho hilo la soka.

No comments