Header Ads

Chanongo amerejea dimbani





Kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa ligi kuu bara mara mbili Mtibwa Sugar, Haruna Chanongo amerejea dimbani baada ya kupona majeraha  na ameanza mazoezi ya pamoja na wenzie.
Chanongo aliyekuwa anasumbuliwa na majeraha ya goti kwa muda mrefu baada ya kukaa nje kwa takribani miezi 6, ameanza mazoezi peke yake aliyopangiwa na jopo la madaktari wa klabu ya Mtibwa Sugar na sasa madaktari wamemruhusu kutumika katika michezo ya kimashindano baada ya kufanya vipimo vya mwisho nakuonekana yupo fiti .
Meneja wa kikosi cha Mtibwa Sugar, Sidy Ibrahim ameuambia mtandao rasmi wa klabu kuwa repoti iliyotolewa na jopo la madakatari wa timu wakiongozwa na Dk.Mussa Juma wamemruhusu Chanongo kucheza
“Chanongo ameruhusiwa kucheza hata michezo ya kimashindano baada ya kufaulu vipimo vya mwisho hivyo hana tatizo lolote .” Amesema Sidy.
Sidy Ibrahim ameongeza “Kafanya mazoezi na wenzake na anaonekana kuwa fiti hivyo hata mchezo ujao dhidi ya Kagera anaweza kutumika kulingana na mahitaji ya kocha.”
Nyota huyo hadi anaumia alikuwa na kiwango bora katika klabu ya Mtibwa Sugar  huku akifunga magoli 7 katika michezo ya ligi kuu aliyokuwa amecheza hadi anaumia katika msimu uliopita.
Kurejea kwa Chanongo kunafanya nyota waliopona majeraha ya muda mrefu kufikia wawili kipindi hiki baada ya Hassan Isihaka kupona na hivyo kuzidi kuimarisha  kikosi  cha wana tam tam.
Wachezaji ambao wanaweza kuukosa mchezo ujao dhidi ya Kagera Sugar siku ya Jumapili kutokana na majeraha ni Henry Joseph Shindika , Salum Kanoni , Shaban Kado, Salum Kihimbwa na Mohamed Issa ataukosa kutokana na kutumikia kadi tatu za njano.

No comments