Header Ads

Maelfu ya watu waandamana kumshinikiza Mugabe kujiuzulu

Maelfu ya Wazimbabwe leo wameandamana katika mitaa ya mji mkuu, Harare, kuunga mkono hatua ya jeshi kuchukua udhibiti wa mamlaka na kumhimiza Rais Robert Mugabe, ambaye amewekwa katika kizuizi cha nyumbani, kujiuzulu. Waandamanaji hao waliojawa furaha huku wengine wakivalia bendera ya Zimbabwe, wamebeba mabango yenye maandishi:


 "Sharti Mugabe aondoke", au "Bob si mjomba wako." Wanaharakati wa Zimbabwe wameunga mkono mkutano huo wa kumshinikiza Mugabe kuondoka madarakani.
 Wengine ambao wameunga mkono wito huo ni Chama cha Maveterani wa Vita pamoja na chama kikuu cha upinzani, Movement for Democratic Change.


 Jeshi limeliambia shirika la habari linalomilikiwa na serikali kuwa mkutano huo umeruhusiwa kufanyika na kutaka uwe wa amani. Jeshi la Zimbabwe lilichukua udhibiti wa mamlaka mnamo Jumatano kwa njia ya amani na bila umwagikaji damu na kumweka Mugabe, mwenye umri wa miaka 93, katika kizuizi cha nyumbani na kuwakamata baadhi ya washirika wake. Rais Mugabe amekuwa madarakani kwa miongo minne


chanzo dw kiswahili

No comments