Header Ads

Matukio ya Kisiasa Merkel asikitishwa na viwanda vya magari Kansela Angela Merkel alijibu maswali ya wapiga kura katika kipindi cha maswali na majibu cha televisheni, ambapo aliulizwa kuhusu usalama, wahamiaji na kashfa ya kupima moshi unaochafua mazingira kwa magari ya VW Deutschland Merkel Statement zum Barcelona Anschlag (picture-alliance/dpa/M. Kappeler) Kansela wa Ujerumani Angela Merkel Kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Ujerumani mwezi ujao inaendelea. Bibi Markel Anagombea muhula wa nne. Kansela Angela Merkel alishiriki katika kipindi cha televisheni cha kituo cha RTL ambacho kilikuwa kinarushwa moja kwa moja, Jumamosi jioni. Wapiga kura walimuuliza maswali kansela wakati akiwania muhula wa nne madarakani katika uchaguzi wa mwezi Septemba. USA - Merkel als Malerei: The Art of Leadership in Dallas (picture-alliance/dpa/L. W. Smith) Picha ya kuchora ya kansela wa Ujerumani Angela Merkel Uchunguzi wa maoni ya wapiga kura unaonesha chama cha kansela Merkel cha Christian Democratic Unioni CDU pamoja na chama ndugu cha jimbo la Bavaria Christian Social Union , CSU vitakuwa kundi kubwa la chama bungeni lakini bila ya wingi wa kutosha. Kutokana na mashambulizi nchini Ujerumani na hivi karibuni kabisa mjini Barcelona, Merkel aliulizwa hatua gani serikali yake itachukua kuimarisha usalama. Merkel alisema kwamba mchanganyiko wa matumizi ya polisi na matumizi ya teknolojia inapaswa kutumiwa kuhakikisha usalama. Amesema kwamba wakati kuna raia wanaokadiriwa kufikia 10,000 ambao wamepata itikadi kali na kuwa na mawazo ya itikadi kali nchini Ujerumani, ni watu 600 hadi 700 tu wanaonekana kuwa ni hatari. Merkel amekosoa matumizi ya Uturuki ya jeshi la polisi wa kimataifa Interpol kumkamata kwa kutoa waranti na kutaka arejeshwe nchini humo mwandishi Mjerumani Dogan Akhanli kutoka nchini Uhispania siku ya Jumatatu kuwa na matumizi mabaya ya shirika hilo la polisi la kimataifa. "Sio sahihi na nafurahi sana kwamba uhispania imemuachia huru," Merkel amesema. "Hatupaswi kutumia vibaya mashirika ya kimataifa kama Interpol kwa madhumini hayo." Deutschland Bundeskanzlerin Angela Merkel im ARD-Interview (picture-alliance/dpa/R. Jensen) Kansela Angela Merkel akifanyiwa mahojiano na waandishi habari Kansela achukizwa na viwanda vya magari Kansela amesema atajaribu kuunganisha vifaa vya polisi na utaratibu wa majimbo 16 nchini Ujerumani. Amedokeza kwamba wengi hawafahamu upekuzi wa polisi pamoja na uangalizi wa vidio kwamba unafanyakazi kwa njia tofauti katika majimbo hayo nchini Ujerumani. Amesema chama chake cha Christian Democratic , kitajaribu kuunganisha mbinu za polisi , akisema : "Pia nitazungumza tena na mawaziri wakuu wa majimbo binafsi." Merkel pia alitetea uamuzi wake wa kufungua mipaka ya Ujerumani kwa mamia kwa maelfu ya wakimbizi miaka miwili iliyopita. Alipoulizwa iwapo sasa angefanya tofauti , alisema: "Bado nafikiri uamuzi wangu ulikuwa sahihi." Ametoa wito wa umoja zaidi katika bara la Ulaya kusaidia nchi kama Italia na Ugiriki kupambana na idadi kubwa ya wahamiaji wanaowasili katika mipaka yao. Merkel bei CDA Veranstaltung in Dortmund (picture-alliance/dpa/I.Fassbender) Bibi Angela Merkel Mpiga kura mmoja aliuliza swali kwamba kwanini waombaji hifadhi hawaruhusiwi kufanyakazi wakati kesi zao zikifanyiwa mapitio wakati baadhi wakisema wamesubiri kwa miaka kadhaa wakipiewa fedha za walipa kodi wakati wanataka kufanyakazi. Merkel amewaambia wapiga kura kwamba amevunjwa moyo na tasnia ya makampuni ya kutengeneza magari kufuatia kashfa ya dizeli ya kampuni ya Vilkswagen. Amesema waziri wa zamani wa mazingira alifahamu madhara yake. "Nimekasirishwa," Merkel amewaambia watazamaji. Tasnia ya magari imetishia kujiingiza katika matatizo makubwa katika kashfa hiyo na makampuni yanapaswa kujisahihisha kwa kiasi kikubwa kadri wanavyoweza," amedokeza. Amesema program mpya ipo kwa sasa kuweza kusahihisha makosa hayo. Mwandishi : Jane Mcintosh / ZR / Sekione Kitojo Mhariri: Mohammed Abrul Rahman

1:37:00 AM
Merkel asikitishwa na viwanda vya magari    Kansela Angela Merkel alijibu maswali ya wapiga kura katika kipindi cha maswali n...Read More