Azarenka hatoshiriki michuano ya Marekani
Nyota wa tenesi kwa upande wa wanawake Victoria Azarenka hatoshiriki michuano mkubwa ya wazi ya Marekani.
Nyota wa tenesi kwa upande wa wanawake Victoria Azarenka hatoshiriki michuano mkubwa ya wazi ya Marekani.
Azarenka
mwenye umri wa miaka 28 hatoshiriki mashindano hayo yatayoanza
kutimua vumbi kuanzia Augost 28, kwa sababu za kifamilia .
"Nasikitika
sintoweza kushiriki mashindano ya wazi ya Marekani ya mwaka huu
kutokana na hali yangu ya kifamilia inayoendelea kwa sasa," Azarenka
alieleza hayo siku ya Jumatatu.
Mchezaji huyu alirejea uwanja
mwezi wa sita mwaka huu baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana
kuwa mjamzito na alifungua mwanae Leo mwezi Desemba mwaka jana.
Post a Comment