Nani atashinda Taji la Bundesliga, nani ataingia
Kinyang'anyiro cha Mabingwa, nani atafika kwenye Mabingwa wa Uropa na
nani atashushwa daraja? Ufuatao ni utabiri wetu jinsi timu 18 za
Bundesliga zitakavyochuana 2017-18.
Bayern Munich
Katika ligi ya Bundesliga, timu 18 hucheza mechi 34 kila moja na mara
nyingi Bayern Munich huibuka washindi wa taji. Imeshinda mara 27. Baada
ya kumnunua Corentin Tolisso kwa kima cha euro milioni 40, ambacho ni
juu zaidi katika historia yake, azma ya mabingwa hawa wa Ujerumani
inasalia ile ile, kutwaa taji. DW inabashiri kuwa Bayern pekee ndiyo
inaweza kutwaa taji la Bundesliga msimu huu
Post a Comment