Mahakama nchini India yapiga marufuku talaka ya kiislamu
Mahakama ya juu
nchini India imeamua kuwa talaka ya mara moja katika dini ya kiislamu ni
kinyume na katiba, uamuzi ambao umekuwa ni ushindi mkubwa kwa haki
wanawake.
India ni moja ya nchi chache ambapo mwanamume muislamu anaweza kumtaliki mkewe kwa kutamka neno talaq mata tatu.
Uamuzi huo wa mahakama unafutia kesi zilizokuwa zikipinga talaka hiyo.
Kesi
hizo ziliwasilishwa mahakamani na wanawake watano waislamu waliokuwa
wamepewa talaka kwa njia hiyo pamoja na na makundi mawili ya kutea haki.
Miaka ya hivi karibuni visa vingi vimeibuka ambapo wanaume
waislamu huwataliki wake zao kwa kutamka neno talaq mara tatu, kwa njia
ya simu au kwa kutuma ujumbe ya sms, kupitia WhatsApp na Skype.
Licha ya njia hiyi ya kutaliki kutumiwa kwa miongo kadha hiajatajwa popote pale kwenye Sharia au Koran
Post a Comment