Wanaume 4 washtakiwa kwa kula nyama ya binadamu Afrika Kusini
Wanaume wanne
wamefikishwa kwenye mahakama ya Afrika Kusini kujibu mashtaka ya ulaji
nyama ya binadamu, baada ya madai kuwa mmoja wao alifika katika kituo
cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama ya binadamu.
Alipohojiwa zaidi mwanamume huyo alionyesha sehemu ya mguu na mkono wa binadamu.
Kisha
polisi wakaandamana na mwanamume huyo hadi kwa nyumba moja iliyo mtaa
wa KwaZulu-Natal, ambapo sehemu zaidi za miili ya binadamu zilipatikana.
Wanaume wanne, wawili kati yao madaktari wa kitamaduni walikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji au kupanga kuua.
Walifikishwa katika mahakama ya Estcourt kilomita 175 kaskazini magharibi mwa mji wa Durban.
Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa kuna uwezekano kuwa wanaume
hao wanne walio na umri wa kati ya miaka 22 na 32 ni sehemu ya genge
kubwa.
Uchunguzi bado unaendelea na polisi wamewashauri watu ambao jamaa zao wametowewa kujitokeza.
Wachunguzi
wa visa vya uhalifu wameitwa kutambua sehemu hizo za binadamu, kwa
kuwa haijulikana ikiwa sehemu hizo ni za mtu mmoja au watu kadhaa.
Mwezi
mmoja uiopita mjini Durban, mwanamume mmoja alikamatwa akiwana na
kichwa cha binadamu ambacho inanamiwa alikuwa na mpango wa kikiuza kwa
daktari ya kitamadunia.
Post a Comment