Burnley wavunja rekodi yao ya usajili kumnunua Chris Wood
od kutoka Leeds United kwa bei iliyovunja rekodi ya
klabu hiyo, ambayo inaaminika kuwa takriban £15m .
Mchezaji huyo wa miaka 25 alifunga mabao 44 katika mechi 88 tangu alipojiunga na Leeds kutoka Leicester City Julai 2015.
Raia
huyo waNew Zealand alijiondoa kutoka kwa mechi ya Leeds dhidi ya
Sunderland katika ligi ya daraja la pili Jumamosi uvumi kuhusu kuhama
kwake ulipokuwa umesheheni.
Wood, ndiye mchezaji wa sita kununuliwa na Sean Dyche kipindi hiki.
Ametia saini mkataba wa miaka minne.
Mchezaji
huyo alikuwa amefunga bao moja katika mechi tatu alizowachezea Leeds
msimu huu, lakini sasa ataanza kujaribu kutikisa nyavu Ligi ya Premia.
Wood anaruhusiwa kuchezea Burnley katika Kombe la EFL kwani alikuwa benchi na hakuchezeshwa mechi waliyolaza Port Vale.
Rekodi ya awali ya usajili wa Robbie Brady waliyemnunua Januari kwa ada inayotarajiwa kufikia £13m.
Post a Comment