Polisi wa Uhispania wa jimbo la Catalonia wamemuua kwa kumpiga risasi
Younes Abouyaqoub, dereva anayeshukiwa kuendesha gari lililokanyaga
watu katika shambulio la kigaidi la Barcelona. Abouyaqoub alipigwa
risasi na kuuwawa kilomita 50 kutoka katika mji wa Barcelona siku nne
baada ya kutokea shambulio hilo la kigaidi. Maafisa wamesema Abouyaqoub,
ambaye ni raia wa Morocco aliyekuwa na umri wa miaka 22, aliendesha
gari hilo na kuvamia kundi wa wapita njia katikati ya mji mkuu wa
Barcelona wiki iliyopita, na kusababisha vifo vya watu 13 na kujeruhi
wengine zaidi ya mia moja. Shambulio sawa na hilo lilitokea katika mji
wa Cambrils, ambapo mwanamke mmoja alipoteza maisha kutokana na majeraha
ya kuchomwa kisu. Kundi linalojiita Dola la Kiislam - IS limedai
kuhusika na mashambulizi yote mawili.
Post a Comment