Congo yatolewa katika dimba la CHAN
Burkina Faso iliifunga Ghana mabao mawili kwa moja
hapojana kwenye mchuano wa duru ya kufuzu katika dimba la Kombe la
Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani – CHAN.
Mabingwa watetezi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na timu
waliyoifunga katika fainali ya 2016, Mali, walibanduliwa nje ya dimba
hilo siku ya Jumamosi.
Ghana, makamu bingwa mara mbili katika
awamu nne za mwisho za dimba hilo, ilitoka sare ya mabao mawili kwa
mawili na Burkinabe katika mechi ya mkondo wa kwanza.
Hivyo
Burkina Faso imefuzu kwa jumla ya mabao manne kwa matatu na itajiunga na
nchi nyingine 15 katika dimba hilo linalochezwa kila baada ya miaka
miwili, na ambalo litaandaliwa Kenya kuanzia Januari 12 hadi Februari 4.
Katika
eneo la Afrika Mashariki, Uganda ilifuzu kwa jumla ya mabao matatu kwa
mawili baada ya kuiangusha Rwanda licha ya kuzabwa mbili sifuri mjini
Kigali katika mchuano wa marudiano.
Aidha Sudan ilifuzu baada ya
kuiangusha Ethiopia kwa jumla ya bao moja kwa sifuri. Namibia ilijikatia
tikiti kwa mara ya kwanza baada ya kuwafunga Wacomoro mabao mawili kwa
bila. Kenya na Guinea ya Ikweta, ambao walifuzu baada ya Gabon
kujiondoa, pia watashiriki dimba hilo la CHAN kwa mara ya kwanza.
Post a Comment