Header Ads

Azika watoto hai kisa shamba la mahindi



Mtu mmoja nchini Burundi aliyefahamika kwa jina la Nyandwi Elias wa eneo la Bubanza,anasakwa na jeshi la Polisi kwa kosa la kuwapiga na kuwafukia ardhini watoto wawili, akiwatuhumu kuiba mahindi shambani kwake.
Tukio hilo limetokea January 14, 2018 baada ya majirani kusikia kelele za watoto wakilia, na ndipo walipenda na kukuta watoto hao waliojulikana kwa jina la Egide Bigirimana na Tuyisenge wenye umri wa miaka 10 na 12,  wakiwa wamefukiwa na kuachwa sehemu ya kichwa.
Mwenyekiti wa shirika la kutetea haki za watoto Jacques Nshimirimana, (FENADEB)  amesema kitendo hiko cha ukatili kinadhihirisha ni kwa namna gani watu wa Burundi hawana uelewa wa haki za watoto, kwani vitendo kama hivyo vimekuwa vikitokea mara kwa mara, ambapo watoto wawili walikatwa mikono baada ya kukutwa wakiiba mahindi.
Jeshi la Polisi limesema linaendelea kumtafuta mthuhumiwa huyo ili achukuliwe hatua za kisheria, na kutoa somo kwa wengine.





chanzo eat


No comments