Header Ads

Yanga yajiokoa SC kombe la shirikisho

  Yanga yajiokoa SC kombe la shirikisho



Klabu ya Yanga imefanikiwa kusonga mbele kwa kuirarua klabu ya Ihefu FC inayoshiriki ligi daraja la pili goli 4-3 kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Ihefu FC ambao walionesha ushindani mkubwa kwenye mchezo huo na ndio waliwatoa Mbeya City katika uwanja huo huo wa Sokoine jijini Mbeya ambao wameutumia leo dhidi ya mabingwa wa Soka Tanzania Bara Yanga SC kutupa karata yao.

Yanga SC walionekana kuelemewa kwenye mchezo huo ambapo walikuwa wanaongozwa mpaka dakika ya 90 kabla ya penati ambayo Obrey Chirwa hakufanya ajuzi na kuisawazishia goli hilo lililodumu dakika 60 .
Kwa matokeo hayo Yanga wanasonga mbele kwenye hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho (ASFC) wakiungana na klabu ya Buseresere na Mbao FC.

No comments