macho kwa kwa macho Okolie Vs Chamberlain usiku wa Jumamosi hii
macho kwa kwa macho Okolie Vs Chamberlain usiku wa Jumamosi hii
Zimesalia siku chache kwa wadau na wapenzi wa masumbwi kushuhudia mpambano mkali baina ya Lawrence Okolie dhidi ya Isaac Chamberlain mchezo utakao pigwa usiku wa Jumamosi hii katika dimba la The O2.
Kuelekea katika mpambano huo mabondia wote wawili walipata nafasi ya kuzungumza kupitia chombo cha habari cha Sky Sports.
Kwa upande wake Okolie amesema kuwa “Sote tuna presha, kama mimi kwa upande wangu ndiyo kila dakika hivyo ni sawa na vile ninavyowaza kupata ushindi,”amesema bondia huyo.
Lawrence Okolie ameongeza kuwa “ Mara kwa mara napokea salamu za kunitakia mafanikio katika mchezo huo wa Jumamosi.”
Wakati kwa upande wake Chamberlain amesema “Nadhani Lawrence ndiyo ana presha zaidi kwakuwa yeye ni Olympian, anapaswa kupiga hatua zaidi katika mchezo huo”amesema Chamberlain.
Post a Comment