Papa Francis ameomba msamaha
Papa Francis katika siku yake ya kwanza ya ziara ya wiki moja katika mataifa ya Amerika ya Kusini ameomba msamaha kutokana na madhara yaliyosababishwa na udhalilishaji kingono nchini Chile.
Matamshi ya Papa Francis yanakuja mnamo wakati idadi ya makanisa ya kikatoliki yaliyoshambuliwa katika kipindi cha wiki iliyopita kupinga ziara yake nchini nchini Chile ikifikia makanisa manane ikiwa ni pamoja na kanisa moja lililochomwa moto katika mkoa wa Auricania ambako Papa Francis aliendesha misa.
Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji mbele ya eneo ambalo Papa Francis alikuwa akiongoza misa katika mji wa Santiago wakipinga ziara ya Papa nchini humo.
Licha ya matukio hayo idadi kubwa ya wananchi wa Chile walijitokeza kumuona Papa Francis katika ziara yake ya kwanza nchini humo ikiwa ni pamoja na watu wanaokadiriwa kufikia 400,000 waliojitokeza katika misa aliyoiongoza.
Taarifa iliyotolewa na makao makuu ya kanisa Katoliki mjini Vatican inasema Papa Francis alikutana na kundi dogo la wahanga waliofanyiwa vitendo vya udhalilishaji wa kingono mjini Chile ambapo alitumia nafasi hiyo kuomba pamoja nao na kushuhudiwa akibubujikwa pia na machozi.
Aidha Papa Francis alisababisha baadhi ya wafungwa kububujikwa machozi alipotembelea gereza la wanawake nchini humo.
Hata hivyo matamshi yake aliyoyatoa katika hotuba yake ya kwanza yalikuwa ni yale ambayo wachile wengi walikuwa wakitarajia kuyasikia
Post a Comment