Header Ads

Vigogo wa kampuni ya Six Telecoms kusota rumande


Kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wanne wa Kampuni ya Mawasiliano ya Six Telecoms,akiwemo Wakili Dk Ringo Tenga, imeahirishwa baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa upepezi bado haujakamilika.

Vigogo wa kampuni ya Six Telecoms, mfanyabiashara Peter Noni (kushoto) na Wakili maarufu Dk. Ringo Tenga wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.

Mbali na Dk Tenga, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara Peter Noni, Mhandisi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Hafidhi Shamte, Mkuu wa Fedha wa kampuni hiyo, Noel Odeny Chacha na kampuni  yenyewe ambayo ni Six Telecoms Limited.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka hayo, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Wakili wa Serikali, Leonard Challo ameeleza mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria
Nongwa kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi bado unaendelea.

Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 26, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

No comments