Header Ads

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Sigmar Gabriel amerejea nchini Israe

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Sigmar Gabriel amerejea nchini Israel leo, miezi tisa baada ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kufuta mkutano nae kwasababu alikutana na kundi linalopinga ukaliaji wa ardhini ya Wapalestina. 

Gabriel amesisitiza wakati wa ziara hiyo nchini Israel mwezi Aprili mwaka jana kukutana na mashirika yasiyo ya kiserikali, ikiwa ni pamoja na moja ambalo linakusanya ushahidi kutoka kwa wanajeshi wa Israel juu ya shughuli zao katika ardhi inayokaliwa na Israel, baadhi wakidai kutokea vitendo vya kihalifu. Netanyahu alijibu kwa kufuta mkutano huo, akisema hatamkaribisha mtu yeyote ambaye atakutana na kundi ambalo linadhalilisha wanajeshi wa Israel. 

Gabriel anatarajiwa kukutana na Netanyahu kwa mazungumzo, atahutubia katika mkutano wa usalama mjini Tel Aviv, pamoja na kusafiri kwenda Ramallah kwa mazungumzo na kiongozi wa Wapalestina Mahmoud Abbas.

No comments