mazito yatolewa kwa Kamishna Uhamiaji
mazito yatolewa kwa Kamishna Uhamiaji
Rais Magufuli amezungumza hayo leo, wakati akizindua Hati ya kusafiria ya kielektroniki jijini Dar es Salaam, ambapo ameipongeza wizara ya Mambo ya Ndani.
“Wizara ya Mambo ya Ndani nawapongeza sana, waziri wa Mambo ya Ndani baada ya kulijua hili kwasababu nilipomteua kupeleka pale nikamwambia kuna mchezo mchafu unachezwa pale ndio bongo land na wizara ya Mambo ya Ndani ina changamoto nyingi sasa immagration mmezitatua hizo changamoto asanteni sana,“ amesema Rais Magufuli.
“Na ndio maana kamishna wa migration alivyoniambia kuwa wanahiotaji nyumba za wafanya kazi wa migration Dodoma sijatoa kwa taasisi nyingine nyumba lakini nilitoa hela serikalini tukatoa nyumba 103 kule Dodoma ni kwasababu ya uzalendo ambao nimeanza kuuona na leo na kwamba hamjaniomba lakini pia mimi nimejiandaa kuja kutoa hela nyingine Makao Makuu mmeshakubali kuhamia Dodoma na hapa palivyokaa kaa hapa hapakai kama makao makuu ya imagration, ninajua kuna baadhi ya wafanyakazi watalaumu kuhamia Dodoma.“
“Lakini ni lazima tuwe na jengo zuri ambalo limekaa kweli kama Makao Makuu ya Imagration lina packing nzuri kwahiyo Dkt. Makakala katafute eneo nitawapa Bilioni 10 wakati wowote mtakapo zihitaji muanze kujenga Makao makuu na ninatoa hivi kwa shukurani unayofanya wewe pamoja na watendaji wako endeleeni kuchapa kazi, endeleeni kubadilisha jina la uhamiaji endeleeni kushughulikia wahamiaji haramu bila kujali bila kumuogopa mtu yoyote,“ ameongeza Rais Magufuli.
Post a Comment