Kikosi cha Simba kilivyowasili uwanja wa ndege wa Kagera
Mapema asubuhi ya leo kikosi cha klabu ya soka ya Simba kimetua mkoani Kagera kwa ajili ya kucheza mechi yao ya ligi kuu Tanzania Bara na Kagera Sugar.
Kikosi cha Simba kilivyowasili uwanja wa ndege wa Kagera
Simba waliondoka alfajiri kwa ndege huku ikiwa na wachezaji wake muhimu ambao jana waliiangamiza Singida United kwa mabao 4-0.
Simba ambao wanaongoza ligi hiyo inatarajiwa kucheza na Kagera Sugar Jumatatu ya wiki ijayo ya January 22 katika uwanja wa Kaitaba.
Post a Comment