Uangalizi hafifu wa watoto kutoka kwa wazazi,
Uangalizi hafifu wa watoto kutoka kwa wazazi,
Uangalizi hafifu wa watoto kutoka kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla umetajwa kuwa moja ya sababu ya wimb la upoteaji wa watoto katika maeneo mbalimbali nchni ikiwemo jiji la Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ameyasema hayo wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Fakharia Shomar Khamis aliyetaka kujua sababu zinazopelekea kuongeza kwa tatizo la watoto kupotea na mkakati wa kuondoa tatizo hilo.
Masauni amesema, sababu zingine ni mazingira magumu wanayoshi baadhi ya watoto, imani za kishirikina, visasi kati ya familia na kupotea kwa bahati mbaya. Amesema, Serikali kupitia Jeshi la Polisi imekuwa ikifanya jitihada za kudhibiti matukio ya kupotea kwa watoto kwa kutoa elimu kupitia programu ya Polisi Jamii kwa watoto shuleni na wazazi kupitia mihadhara ya kijamii na vyombo vya habari.
“Jitihada hizo zimekuwa zikizaa matunda kwa kuongeza elimu ya usalama wetu kwanza miongoni mwa jamii na hvyo kuongeza umakini wa kuwalinda watoto,” amesema Masauni. Amesema kuanzia kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka jana kwa mkoa wa Dar es Salaam pekee jumla ya watoto waliopotea ni 184 ambapo kati yao 176 walipatikana na wanane wanaendelea kutafutw
Post a Comment