Aliyekuwa na uzani wa kilo 500 apungua hadi kilo 174
Mwanamke aliyekuwa
na uzani mzito zaidi duniani atasafirishwa hadi katika milki za kiarabu
UAE baada ya mzozo kuhusu uzani wake katika hospitali ya India ambapo
alikuwa akipatiwa matibabu.
Hospitali ya Saifee mjini Mumbai
ilisema kuwa Eman Abd El Aty alifanyiwa upasuaji wa kupunguza uzani na
sasa alikuwa huru kuondoka kwa sababu ana uzani wa kilo 172 kutoka kilo
500 alizokuwa nazo awali.
Lakini dadake alimshutumu daktari wa
upasuaji huo kwa kudanganya na kumuomba amruhusu dadake aendelee kukaa
katika hospitali hiyo.
Kwa sasa ataelekea katika hospitali ya Burjeel huko Abu Dhabi.
Taarifa
iliotolewa na daktari wa bi Abd El Aty imesema kuwa atapatiwa matibabu
muhimu kwa kuwa hospitali hiyo iko karibu na nyumbani.
Hospitali
ya Saifee imeongezea kwamba ilikuwa fahari kwa juhudi zilizofanywa na
kundi la madaktari wake ikidai kuwa mgonjwa huyo aliwasili kupitia ndege
ya kubebea mizigo na sasa anarudi kama abiri katika ndege ya watu.
Mapema
hospitali hiyo ilikuwa imepinga madai kwamba dadake El Aty, Shaimaa
Selim ambaye alitoa kanda fupi ya video katika mitandao ya kijamii
akidai kwamba dadake aliyekuwa hawezi kuzungumza ama hata kutembea
hajapunguza uzani mkubwa kama hospitali hiyo inavyodai.
Daktari wa upasuaji wa watu walionenepa kupitia kiasi Muffi Lakdawala pia alikana madai hayo katika mtandao wa Twitter.
Post a Comment