Kocha wa Bayern Münich Carlo Ancelotti amesisitiza ameweka fahamu zake katika kumaliza kazi ya kushinda taji la Bundesliga,
Kocha wa Bayern Münich Carlo Ancelotti amesisitiza
ameweka fahamu zake katika kumaliza kazi ya kushinda taji la Bundesliga,
kabla kuangalia ufanisi wa jumla alioupata katika msimu wake wa kwanza
katika klabu hiyo
Hii ni kufuatia kule kushindwa nyumbani kwao Allianz Arena katika
nusu fainali ya kombe la Ujerumani na mahasimu wao Borussia Dortmund BVB
usiku wa Jumatano.
Mabingwa hao wa Ujerumani walikuwa kifua
mbele 2-1 kabla Dortmund kuwashangaza kwa kutoka nyuma na kutwaa ushindi
wa 3-2. Haya yote yanakuja wiki moja tu baada ya hao the Bavarias,
kubanduliwa kutoka kwenye ligi ya mabingwa barani Ulaya na Real Madrid.
Bayern
lakini bado wanaweza kulishinda taji la ligi kuu ya Ujerumani,
Bundesliga, kwa mara ya tano mfululizo na ndilo jambo lililomfanya
Ancelotti kukataa kuzungumzia ufanisi wake msimu huu, kwa sababu bado
kuna mechi nne za ligi zilizosalia na wamebakisha pointi tano waweze
kutawazwa mabingwa.
Hakuna wasiwasi wa kuachishwa kazi Ancelotti
"Ni mapema sana kwa hilo," alisema Ancelotti. "Tunastahili kuweka mambo wazi katika ligi kuu sasa haraka iwezekanavyo."
Kwa
sasa hakuna wasiwasi wa kuachishwa kazi kwa Ancelotti, ingawa hajapata
ufanisi mkubwa katika msimu wake wa kwanza, akilinganishwa na mtangulizi
wake Pep Guardiola aliyehamia Manchester City. Guardiola aliifikisha
Bayern Munich katika nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya na akashinda
Bundesliga na kombe la shirikisho la Ujerumani, DFB Pokal, katika msimu
wake wa kwanza.
Javi Martinez na Mats Hummels walikuwa wamefunga
magoli mawili katika kipindi cha kwanza na kulifuta lile la mapema
lililowapa Dortmund uongozi na ambalo lilitiwa kimyani na Marco Reus.
Dortmund walizinduka kipindi cha pili na kupata ushindi
Lakini
katika kipindi cha pili, BVB walizinduka kutoka kwenye kile kichapo cha
4-1 walichopewa na hao wapinzani wao hapo Allianz Arena wiki tatu
zilizopita katika mechi ya ligi. Pierre-Emerick Aubameyang alifunga goli
lake la 35 la msimu baada ya kuandaliwa na Ousmane Dembele, kabla
chipukizi huyo kutoka Ufaransa, kufunga goli la tatu na la ushindi la
Dortmund, dakika 16 kabla mechi kukamilika.
Nahodha
wa Bayern Philip Lahm atakayestaafu msimu utakapofikia kikomo alisema,
"Tumeshushwa mabega pakubwa, tulitaka kufika fainali. Tunapokuwa
tunaongoza mechi, inastahili kuwa vigumu kutushinda."
Bayern
wanaweza kushinda taji la Bundesliga, iwapo Leipzig watashindwa kuwalaza
FC Ingolstadt wanaoshikilia nafasi ya 17 na ambao wanapambana
wasishushwe daraja. Ingolstadt ilikuwa timu ya kwanza kuifunga Leipzig
katika mkumbo wa kwanza wa ligi kuu ya Ujerumani msimu huu na kiungo wao
Alfredo Morales ameuambia wavuti wa klabu hiyo kwamba, iwapo wanataka
kuwafunga tena, ni sharti wajizatiti sana.
Post a Comment