Ongezeko la vimbunga kanda ya Sahar
Kanda ya jangwa la Sahel barani Afrika imeshuhudia
ongezeko la mara tatu la vimbunga vya mvua vinanoleta taabu na uharibifu
mkubwa badala ya kuleta manufaa tangu 1982.
Kanda ya jangwa la Sahel barani Afrika imeshuhudia ongezeko la mara
tatu la vimbunga vya mvua vinanoleta taabu na uharibifu mkubwa badala ya
kuleta manufaa tangu 1982. Hayo ni kwa mujibu wa utafiti juu ya
mabadiliko ya tabia nchi uliotangazwa hapo siku ya Jumatano 26.04.2017.
Wataalamu waliofanya utafiti huo wamesema iwapo hali ya kuongezeka kwa
joto duniani haitatafutiwa ufumbuzi basi maeneo mengi katika kanda ya
jangwa la Sahel yatakabiliwa na mvua kubwa kupita kiasi na mara kwa mara
maeneo hayo yatakumbwa na mafuriko. Christopher Taylor mtaalamu wa
maswala ya hali ya hewa amesema nchi ambazo zina upungufu wa
miundombinu hazitaweza kupambana na athari hiyo. Taylor na timu yake
walifanya uchunguzi wa mawingu kwa kutumia mitambo ya satellite mnamo
mwaka wa1982-2016 ambapo walifuatilia mageuzi ya ruwaza ya dhoruba
katika eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara, ikiwa ni pamoja maeneo ya,
Mauritania, Mali, Burkina Faso, Niger, Nigeria, Chad, Sudan na Senegal.
Post a Comment