Picha ya Rihanna na Lupita Nyong'o imezua mjadala kwamba huenda wawili hao wanapanga kubuni filamu
Picha ya Rihanna na
Lupita Nyong'o imezua mjadala kwamba huenda wawili hao wanapanga kubuni
filamu hatua ambayo imewashinikiza nyota hao kujitokeza na kusema ndio
wana mpango huo.
Picha hiyo ya 2014 ya mitindo ilisambazwa na
mashabiki wengi na sasa Rihana amesema kuwa ana mpango kama huo katika
mtandao wake wa Twitter.
Mashabiki wamependa sana wazo hilo.
Lupita naye alijibu katika mtandao wa Twitter akisema mimi naunga mkono pendekezo hilo iwapo umeunga mkono.
Zaidi
ya mashabiki 200,000 walilipenda chapisho hilo la Twitter na mapema
siku ya Jumatatu Rihanna alijibu ''I'm Pit'z''-jina la utani katika
filamu yake ya Star Wars.
Watu wengine 99,000 walilipenda chapisho hilo na sasa nyota hao sasa wameunga mkono pendekezo hilo .
Wazo la filamu kutokana na picha hiyo lilionekana
katika mtandao wa Tumblr wakati picha hiyo ilipochapishwa kwa mara ya
kwanza ,lakini sasa wawili hao wamejumuika na sasa inaonekana kwamba
mtandao wa Twitter ulitengeza filamu.
Lakini huku mashabiki wakichangia ni nani anayefaa kupata sifa hizo kwa wazo hilo na kupata faida.
Mashabiki wengi wa Twitter hatahivyo wanegependa wazo hilo kufanikiwa.
Post a Comment