Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro amezungumzia vurugu zilizotokea hivi karibuni katika mkutano
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro
amezungumzia vurugu zilizotokea hivi karibuni katika mkutano uliotakiwa
kufanyike na maeneo ya Mabibo na Chama cha wananchi CUF. Kamanda huyo
amesema kuwa suala hilo na wale waliojeruhiwa upelelezi utasema kama hao
watu ndiyo waliokuja kuvamia au la.
Kamanda Sirro amezungumza na wanahabari na kusema kuwa, mikutano ya
ndani inaruhusiwa hata bila kutoa taarifa Polisi, lakini kwa
waliojeruhiwa amedai kuwa upelelezi utaweka wazi mengi zaidi.
“Kuna hili tukio lililotokea tarehe 22 mwezi wa 4, 2017 majira ya saa
tano karibu na nusu kwenye hotel moja inaitwa Vina Hotel, hii hotel iko
maeneo ya Mabibo kuna wanachama wa Chama cha CUF maana yake Chama kile
kina kundi A na kundi B inaonekana kundi A walikuwa wanafanya mkutano
wao ndani ya ukumbi kwahiyo baadhi ya watu ambao tunafuatilia wakiwa na
magari yapatayo mawili walivamia mkutano huo na wakafanya fujo, kwahiyo
kukawa na vurugu kubwa sana na baadhi ya watu wameumia lakini huyu bwana
Juma Shaban Nkumbi huyu Mwenyekiti wa CUF wanasema wa Kinondoni alikuwa
ameita mkutano kwahiyo kwenye vurugu hizo kuna baadhi ya watu wameumia
suala kubwa ni kujua kwa wale waliokuja kuvamia walikuja kufanya nini ni
suala la upelelezi kwasababu mtu kaumia kakatwa na kitu chenye ncha
kali,” alisema Kamanda Sirro.
“Amefungua jalada lake akieleza kuwa amepigwa mtu fulani na huyo mtu
ndo kamjeruhi kwahiyo je, ni wale waliovamia ni jambo la upelelezi
kwahiyo upelelezi utatuambia kama ni wao waliovamia, nilikuwa nawaambia
pale hata kama wamevamia je kuna uhalali wa kumkata na mapanga? ni suala
la upelelezi kwahiyo kimsingi niseme tu kwamba wale waliokamatwa
nikutokana na yale malalamiko dhidi yao ambapo watu wameandika maelezo
yao wamewatambua wamewataja kwahiyo ndiyo kesi imefunguliwa na hili la
wao kutujulisha ni suala ambalo kwa kawaida wanamjulisha OCD,”
alifafanua Kamanda Sirro.
“OCD wetu ndiyo anaweza kujua hilo lakini nafikiri katika busara ya
kawaida mikutano ya ndani mara nyingi huwa siyo lazima tutoe kibali kwa
hiyo unaweza kuta vyama vingine vya siasa au madhehebu mbalimbali
wanaweza hata wasitupe taarifa kwasababu ni mikutano ya ndani lakini
nafikiri kama walifanya busara zaidi watakuwa walimjulisha OCD kama
mkutano wa namna hiyo ulikuwa unaendelea
Post a Comment