vita vya Korea Kaskazini vyanukia
Marekani ikiionya Korea Kaskazini kutoijaribu Kijeshi,utawala wa Korea Kaskazini nao unajibu mapigo kwa jeuri kubwa
Kuongezwa kwa wanajeshi, majibizano ya maneno ya vitisho na kitisho
cha vita vya kinyuklia yanazidi kuongeza wasiwasi kaskazini mashariki
mwa Asia.
Marekani, kwa upande mmoja, inaimarisha juhudi zake
katika eneo la kimkakati na Korea Kaskazini haionekani kusalimu amri
wakati diplomasia na juhudi za kuzuia shambulio la nyuklia zikigongana.
Kimsingi kunashuhudiwa wingu zito limeifunika rasi hiyo ya Korea.
Ikiwa
ni kauli za jeuri na kujiamini zinazotolewa na serikali ya Korea
Kaskazini au upepo wa kishindo unaovuma upande wa Trump au majaribio ya
kawaida ya makombora na mazoezi ya kijeshi, yote yanasababisha wasiwasi
kote ulimwenguni huku hali ikionesha dalili za mambo kuelekea kufikia
katika kiwango kibaya.
Ubabe wa Marekani unapojaribiwa
Makamu
wa Rais wa Marekani, Mike Pence, alitowa hotuba yake wiki iliyopita
akiwa katika ndege ya USS ambayo ilitumiwa na Ronald Reagan huko Japan
na kusema kwamba upanga umeshawekwa tayari.
Kauli
hiyo imeonekana moja kwa moja kulenga kuionya Korea Kaskazini
kutothubutu kuijaribu Marekani kijeshi akiongeza kusema kwamba "Marekani
itajibu kwa kutumia nguvu kubwa ikiwa itashambuliwa."
Siku
chache baadaye, katika hatua za kujibu mazoezi ya kijeshi ya wanamaji
kati ya Marekani na Japan, gazeti rasmi la serikali Korea Kaskazini la
Rodong Sinmun likaandika kwamba vikosi vya kimapinduzi viko tayari
kuizamisha meli ya kubeba ndege za kijeshi za Marekani inayoendeshwa kwa
nguvu za kyuklia kwa kombora moja tu.
Na hiyo ni baada ya
kuripotiwa kwamba meli hiyo ya Marekani ya kundi la USS Carl Vinson
itatia nanga katika bahari ya pwani ya Rasi ya Korea, Korea Kaskazini
ilijibu kwa kusema kwamba kupelekwa kwa zana hizo ni kitendo cha hatari
kabisa kinachofanywa na wale wanaopanga kuanzisha vita vya nyuklia.
Kikosi
hicho cha Vinson kitaungana na USS Michigan, nyambizi iliyosheheni
makombora aina ya 144 Tomahawk ambayo ilishawasili katika bandari ya
Korea Kusini ya Busan tangu Jumanne wiki hii.
Hali isiyoweza kupuuzwa
Hata
hivyo, hadi wakati huu wasiwasi uliopo haujafikia kiwango cha kubadili
mambo yalivyo ingawa kuna kitisho kinachozidi kuongezeka katika kanda
hiyo ambacho hakiwezi kupuuzwa.
Uwezo wa jeshi la Korea Kaskazini
unazidi kuimarika na hakuna ishara yoyote inayoonesha kwamba utawala
huo utabadili msimamo wake wa jazba na mabavu, ambao kimsingi unauona ni
muhimu kwao na unaostahili kuwepo kwa ajili ya kuuwezesha kuendelea
kuwepo.
Wiki
hii pia, nchi hiyo ilionesha nguvu zake za kijeshi wakati ikiadhimisha
miaka 85 tangu kuasisiwa jeshi la nchi hiyo ambapo zana nzito nzito
zilioneshwa.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Korea
Kaskazini, KCNA, hilo lilikuwa ni tukio kubwa kuwahi kufanyika la
maonesho ya nguvu za kijeshi likihusisha mizinga na makombora ya masafa
marefu 300 pamoja na nyambizi zinazoweza kutumiwa katika kushambulia
meli za kivita.
KCNA halikuishia hapo tu, bali lilikwenda mbali
zaidi na kuandika kwamba mazoezi hayo ya kijeshi yameonesha ni kwa jinsi
gani Korea Kaskazini ina uwezo wa kuwamiminia mvua ya makombora bila
hesabu wale lililowaita ''mabeberu'' yaani Marekani na "wafuasi wao
wachafu."
Mwandishi:Saumu Mwasimba/DW English
Mhariri: Mohammed Khelef
Post a Comment