Diamond amefunguka kwa mara ya kwanza sababu za kumshirikisha Young Killer katika wimbo wake mpya ambao bado haujatoka.
Diamond amefunguka kwa mara ya kwanza sababu za kumshirikisha Young Killer katika wimbo wake mpya ambao bado haujatoka.
Ni mara nyingi hitmaker huyo wa Marry You, ameonekana kushindwa
kuzizuia hisia zake za kumkubali Msodoki huku mara kadhaa akionekana
kutumia mistari ya rapper huyo katika kuandika katika mitandao yake ya
kijamii.
Akiongea na kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatatu hii, Diamond
amesema,”Nilimuita Young Killer kuja studio, nikamwambia sijawahi
kumshirikisha mtu katika muziki kipindi hiki na nikimshirikisha mtu ni
wa WCB, kuna nyimbo yangu nataka nikushirikishe tufanye. Kwanza alipata
shock kidogo, alipagawa kidogo”
“Nikamwambia usipagawe, hii nyimbo ukifanya verse mbovu nakufuta na
hapa katika ofisi mimi ndio nimekupigania hili swala uingize verse kwa
sababu kila mtu anashangaa kwanini Young Killer? Ile verse imeandikwa
ndani ya siku hizi tatu, akanambia hii nyimbo angekuwa mtu mwingine
ningeshamaliza. Katika intro ya kutafuta kuingilia alitafuta karibuni
hata masaa sita, lakini mwisho wa siku amefanya verse kali sana sana,
imeshaisha bado kushoot video ngoma itoke,” ameongeza.
Bosi huyo wa WCB amesisitiza, “Young Killer mtu ambaye masikini ya
Mungu anajitahidi sana sana kufight na mtu ambaye anaandika, mimi
napenda mtu anavyandika. Nikajua kwanza nikimchukua Young Killer,
nitawaempower vijana wengine wengi wenye ndoto ya kufanya muziki kuona
kwamba kumbe na sisi tunawezekana. Kwasababu wangejua Diamond angefanya
ngoma labda na Fid Q na Joh, wao wanajua hizo ndio atafanya nao, lakini
nimeonyesha kuwa yoyote ninaweza nikafanya naye nyimbo. Na Young Killer
kiukweli anachokifanya ni kitu kikubwa na video tutashoot hapa hapa
Tanzania na ngoma ni kali na yakinyamwezi.”
Post a Comment