Kuondoka kwa Zuma, kutaleta mabadiliko Afrika Kusini?
Maelfu ya raia wa Afrika Kusini wakiwa wanaandamani kumshinikiza Rais
Jacob Zuma kuachia madaraka, inaleta picha kama vile Zuma ndiyo kikwazo
pekee kinacholizuia taifa hilo kusonga mbele.
"Zuma lazima
aanguke" umekuwa wito maarufu tokea kulipoanza maandamano dhidi ya
rushwa na ukosefu wa ajira mwaka 2015. Hata wanachama wengi wa chama
chake cha African National Congress (ANC) wamembandilikia Zuma.
Kumuondoa Zuma hata hivyo, huenda lisiwe suluhisho la matatizo yote yanayolikabili taifa hilo kwa mujibu wa wachambuzi.
Chama
cha ANC kimejaa wanasiasa wenye mitazamo sawa na Zuma, na matatizo ya
kiuchumi ya Afrika Kusini yameingiliana sana na ukosefu wa usawa
uliorithiwa tokea wakati wa ubaguzi wa rangi, kiasi ya kwamba hata Zuma
akiondolewa madarakani, huenda hatua hiyo isilete mabadiliko makubwa
nchini humo.
Sifa ya Zuma imechafuka kutokana na msururu wa
kashfa za rushwa, ikiwa ni pamoja na ile inayohusu utumiaji wa fedha za
kodi ya umma kuifanyika marekebisho nyumba yake binafsi, na mafungamano
ya karibu na familia ya kibiashara na yenye ushawishi mkubwa.
Wakati
huo huo mamilioni ya Waafrika Kusini wanaishi makaazi yasiyo halali, na
bila ya huduma za msingi, huku ukuaji wa uchumi ukiwa unazorota hadi
kufikia asilimia 0.3 mwaka jana na zaidi ya robo ya idadi yote ya watu
nchini humo imekosa ajira.
Post a Comment