Header Ads

Ajali ya treni na basi yaua na kujeruhi



Watu 7 wamefariki dunia na wengine 27 wamejeruhiwa vibaya, baada ya basi la Kampuni ya Hamida kugonga treni ya mizigo mkoani Kigoma.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoani Kigoma Martin Otieno, amesema kwamba ajali hiyo imetokea majira ya saa 12:15 asubuhi ya leo katika eneo la Gungu, baada ya basi hilo ambalo linafanya safari zake kutoka Mkoani Kigoma kwenda Tabora, kugonga treni ya mizigo iliyokuwa ikipita kwenye njia yake, licha ya dereva wa treni kupiga honi kumpa tahadhari dereva wa basi.
Dereva wa basi hilo ambaye hajajulikana jina ni miongoni mwa watu waliofariki, huku idadi ya vifo ikitajwa kuweza kuongezeka, kutokana na majeruhi wengi kuwa kwenye hali mbaya.
Kamanda Otieno amesema kwa sasa jeshi la polisi lipo eneo la tukio likiendelea kuokoa miili na majeruhi wengine, na taarifa zingine zitafuata mara baada ya zoezi kukamilika.

No comments